Azim Dewji awatuliza Simba kuhusu viongozi

Azim Dewji awatuliza Simba kuhusu viongozi

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Mfadhili wa zamani wa Simba Azim Dewji amewatuliza mashabiki wa timu hiyo kuacha kuendelea kuwashurutisha viongozi wao kujiuzulu akisema hatua hiyo itaibomoa timu yao.

Dewji ameyasema hayo leo kufuatia malumbano ya uongozi yanayoendelea ndani ya klabu hiyo.

Amewashauri viongozi wa Simba kujitokeza hadharani haraka kuwatuliza mashabiki wao huku akiwataka pia kuhakikisha wanasimamia vizuri usajili wa dirisha kubwa sambamba na kutafuta kocha ambaye atakaa kwa muda mrefu badala ya kuwa na mabadiliko ya mara kwa mara ambayo yamekuwa yakiiathiri timu hiyo.
 
Mfadhili wa zamani wa Simba Azim Dewji amewatuliza mashabiki wa timu hiyo kuacha kuendelea kuwashurutisha viongozi wao kujiuzulu akisema hatua hiyo itaibomoa timu yao...
Wacha watwangane
 
Tatizo viongozi ni wadwanzi sana, badala ya kutoka hadharani watoe taarifa rasmi ya klabu ili kuzima kelele na uvumi wao wamejifungia afu wanajiuzulu kimya kimya
 
Huyu Dewji kila siku yupo kwaajili ya kuwatetea waliofeli, mara amtetee mama Abdul sasa anamtetea mdogo wake.

Kama hataki waliotufelisha wote waondoshwe maana yake anataka tuendelee kuwaacha wazidi kutuharibia?

Huyu gabachori mkubwa nae hajielewi. Kwanza amwambie mdogo wake atuwekee mezani zile bilioni 20 alizotudanganya kwa hundi feki..

Akishindwa kutuonesha wapi mzigo ulipo yeye na mdogo wake wafungashe, ile Simba Sc ni brand kubwa sana haiwezi kukosa wadhamini hata watatu.
 
Back
Top Bottom