Azimia kwa kulipa kodi miaka 15 nyumbani kwa mkewe

Azimia kwa kulipa kodi miaka 15 nyumbani kwa mkewe

We uoni kafanya jambo la maendeleo.
Bila kumwambia mwenzake, acheni kujitoa ufahamu kuweni na uhuruma.
Utakuta hapo:

1.Hela ya kula anatoa yeye.
2.Hela ya ada analipa yeye.
3.Mahitaji ya mke anatimiza yeye na unaweza ukakuta mpaka ndugu zake jamaa anasaidia.
4.Huduma nyingine za kijamii na afya anatimiza huyo mwanaume.

Sasa ww ulitaka uyo mwanaume afanyeje?

Ila nikwambie sisi wanaume tumeumbwa kwa roho ya tofauti isiyo na ubinafsi, ila nyinyi ndugu zangu........
 
Unagawana mali na mwanamke kama wewe sio mpambanaji,kama umezaa nae unamuachia tu unaanza upya.Unaziweka urithi watoto then unapeleka document government custod kwa wosia maalumu mali za watoto wakabidhiwe ikifika umri fulani,mama yao ni msimamizi haziruhusiwi kuuzwa hadi unaweka specific umri ambao watoto watakuwa wamejitambua.
Atakaeuza na atakae nunua imekula kwake.
Neno “mpambanaji” unalichukulia simple sana, kuunga unga tena mpaka ifike million 90, sio leo wala kesho mzee, labda uingie kwenye ngada
 
Kwani nyumba walitengeneza pamoja wakiwa kwenye ndoa mpaka aombe 50 50?
Ok nijibu hili swali, tufanye mume alkuwa ana nyumba pembeni akamficha mke wake, siku ikatokea wameachana, mke ana haki kwenye ile nyumba ambayo hawakutengeneza pamoja??
 
Ukiona una mwanamme haeleweki ni bora ufanye mambo yako,mfano unakuta limwanaume linawaza kununua gari ya kutembelea huku halina nyumba au biashara nyingine(wengine wananunua magari ya biashara ye ananunua la kutambia kwa ndugu zake) unaona mipango yake ni ya kijingajinga kazi yake kutaka kuwafurahisha watu my friend kama we ni mwanamke badala ya kugombana naye kwamba kwa nini hafanyi vitu vya maendeleo we endelea kuwekeza kivyako,utanishukuru badae
 
Huyo mwanamke ana akili hao ndio wanawake wa kuoa kaona mmewe hana akili ya maisha ye kajitahidi kujenga nyumba. Na usikute hizo pesa za pango zote zipo fixed account miaka 15 ni milioni 90.

Mme unapewa ukafanyie biashara.
Wapo wanaume wapumbavu wengi wameokolewa na wake zao wao ni ulevi tu
Wengi watakupinga yaani unakuta mwanamme anapata hela afu haionekani bora mwanamke ujiongeze
 
Ukistaajabu ya mussa utayaona ya firauni, yamemkuta Mwanaume mmoja huko nchini Zambia amejikuta anapoteza fahamu baada ya kugundua kuwa mke wake ndiye mwenye nyumba aliyokuwa analipia kodi kwa miaka 15.

Nyieee hahaha wanawake mnasiri kubwa daah,Mwanaume huyo aliyefahamika kwa jina la Martin Stampa amepata na maswahibu hayo baada ya kumtambia mke wake kuwa anatafuta mwanamke mwengine mwenye akili na atakaye mpa mawazo ya kimaendeleo zaidi (kuliko mke wake)

Baada ya kauli hiyo mke wake akamwambia kuwa yeye ndiye hana akili maana amekaa kwenye nyumba hiyo kwa miaka 15 akilipa kodi zaidi ya Laki 5 kwa mwezi bila kugundua kuwa alikua anamlipa mke wake (mmiliki wa nyumba).

Unaambiwa kwa miaka yote hiyo mzee baba Stampa alikua akimkabidhi mke wake pesa ili alipe kodi kwa mwenye nyumba kumbe nyumba ni ya mke wake.

Taarifa hiyo ilimshtua sana Stampa jambo ambalo lilipelekea apoteze fahamu.

Daaaah wanaume nahitaji comment zenu hapa juu ya hili nyieeee wanawake mtakuja kuwaua wenza wenu hahaha.

Source: Mwananchi Scoop
 
Ukiona una mwanamme haeleweki ni bora ufanye mambo yako,mfano unakuta limwanaume linawaza kununua gari ya kutembelea huku halina nyumba au biashara nyingine(wengine wananunua magari ya biashara ye ananunua la kutambia kwa ndugu zake) unaona mipango yake ni ya kijingajinga kazi yake kutaka kuwafurahisha watu my friend kama we ni mwanamke badala ya kugombana naye kwamba kwa nini hafanyi vitu vya maendeleo we endelea kuwekeza kivyako,utanishukuru badae
Kwangu hii ni comment bora kabisa kwa mwaka huu.

Japo sitataka kumdharau kwa kuwa akidharaulika ntaumia kupita maelezo.

So nikufanya vitu bila show off na kuweka documents vizuri maana yajayo yanaweza yasieleweke.
 
Back
Top Bottom