Azimio La Arusha: Why We Were Dead Wrong!

There are millions of philosophers ...... It doesn't really mean that you are smart or a good leader, it just means you have an idea that is distinguishable.
 
And...... they are socialist.
 

Brutality katika tamaduni zozote haziwezi kosekana, lakini haileti maana kuwa hazifai. Hapo ndipo tunapojidanganya na ubepari, eti utawala wa sheria na haki za binadamu, wenzetu wameshafikia hatua ya wote kuelimika juu ya demokrasia, sisi tulio wengi hatufahamu hata haki zetu, nitafikiriaje ya kwako? (simaanishi kuunga mkono haki hizo)
Napenda kuugawa ubepari katika sehemu mbili, Internal Capitalism yaani unyonyaji kati ya mtu na mtu ndani ya taifa moja, na ule wa External Capitalism, yaani taifa kunyonya taifa, wenzetu wameshafikia huko, nasi ni waanga wa hilo, je tunategemea siku nasi under ubepari kunyonya nchi za kimagharibi? Au tunataka tuje kumnyonya Mmalawi, au Burundi, unafikiri inawezekana? Tunategemea nini sasa?
Haki za binadamu, demokrasia, dini, na unafiki wetu, vimevisha ubepari ngozi ya kondoo hali ni chui. INAUMA SANA!
Mungu wetu anaita!
 

kaka yangu william
ubepari hata ukikaa miaka 50 na ukawa na athari mbaya kiasi gani wananchihawana option tena kwani kuna vikwazo vingi vya kutokuubali ubepari, hata hivyoubepari kwa muda mfupi tu umeonesha athari kubwa katika jamii kama zifuatazo
matabaka yameongezeka tena kwa kasi ya ajabu na utu umepotea, tunafikamuda hata utamaduni na utambulisho wetu unapotea pia,

rushwa inaongezeka kwa kasi kubwa kwani mianya ni mingi,unyonyaji nadhuluma imekuwa kubwa unyanyasaji wa wananchi na mali za wengi kumilikiwa nawachache imekuwa jambo linalolindwa na tabaka fulani.
ubepari pasipo uzalendo na dira maalumu ni kuisambaratisha jamii nakuleta uadui.
ndicho mwalimu alichokataa kwa wakati ule.ubepari unaweza kukubalika ilaviongozi wetu wawe makini na wawe na limit ya vitu fulani fulani
 
Right !!!!!!!!!! Now you assert that every decration made and signed by a political party is indeed a philosophical document.

i didnt say so!
mind you by that definition i can say AD is a philosophical document.
 
sasa mkuu zakumi utuambie kwa nini wewe waona hiyo siyo ama haina vigezo vya kuwa philosophical document.
 
nimependa mjadala huu hauna mawaa umejaa ubishani wa hoja na sio matusi na kuitana majina ya ajabuajabu haya ndio majadiliano na ubishani wa kiutuuzima busara na kustaarabika. wakija wale wa jazba na uharibifu utawajua tu.
 

then if it represents philosophy how comes it is not a philosophical document?
zakumi this is your interpretation to say he did not say ad was philosophical document coz he already said it is a philosophical document.

its like i am telling u that bongo flavour represent african beauty this is as same as saying there is african beauty in it.
if it represents philosophy there is philosophy in it and therefore it is philosophical document.
 

on bold is where you are wrong mkuu,
in developed countries never started as liberals they are what they are today by working very hard and it was by force to work hard and is was national rule to work hard. there after it when the became liberals. so as we did though it was not succesful to us as it did to others you know the reasons and there are so many.

to a country like ours liberalism and what you call choices are the most enermy of our development.people need to be controled so that later we all enjoy national cake.
freedom,democracy , human rights and all things of their kind work better in developed countries not developing.

in the name of freedom of choice people decide not work, not to protect national resources and do what they feel likedoing. taifa pasipo miongozo yenye nguvu limepotea,
 
Hili nalo neno.

 
Kobello embu jisome kwanza mwenyewe, kabla ya jibu langu maana nyie washabiki wa hili AA mmekazana na kuwaambia wenzenu hawalifahamu halafu wenyewe kila saa mnaji-contradict na implemention za AA. Chini hapa mnasema misingi ilikuwa ni kujikomboa na soko la dunia.

Halafu hapa tena unasema (tatizo kubwa) ni hao hao wasimamizi wa soko la dunia waliwatema, mkuu mi naanza kuona hili AA kwako lipo kiimani zaidi kuliko ukweli wenyewe kwenye implemention. Maana ni kitu ambacho ni impossible kwenye dunia ya sasa, kufanya economical activities bila ya external trade.

Maana amna hata sababu za kwenda kuchambua the challenges of production efficiency kwenye hili Azimio Uchwara, hili kuweza kuja kuelezana matatizo ya mistari ya kununua bidhaa na upungufu wa bidhaa yalipoanzia na huko ndio mimi sikupendi kabisa kuhusu hili Azimio.

Inabidi watetezi sasa mje na ubishi imara lakini si hizi hadithi za maandishi embu mjadala ueleke kisayansi na si haya mambo ya utu.
 


Chairman Mao mwenyewe alifanya normalization. Alimwalika Richard Nixion.
 
There are millions of philosophers ...... It doesn't really mean that you are smart or a good leader, it just means you have an idea that is distinguishable.

So I won't commit crime if I say the authors of AD weren't smart and good leaders.

Z-10
 
i didnt say so!
mind you by that definition i can say AD is a philosophical document.

sasa mkuu zakumi utuambie kwa nini wewe waona hiyo siyo ama haina vigezo vya kuwa philosophical document.


You didn't say so but you have imply so. As it stands, the AD is a political party declaration, and it's not a work of a philosopher.

Now concerning the second party, the word philosophy was used to elevate Ujamaa and AD to international prominence. In 50, 60 and 70, there was a desire within African continent and in the west to promote home grown African philosophies. However, those philosophies didn’t stand the test of time and generations because they were ill-conceived. It’s simple us that.

In case of AD, the authors were the subjects of their own philosophical experiments. They used their own personal experiences as the baseline of what should come. For example, Tanzania is diverse country. But the authors, who spent majority of their teen years and adult lives in colonial boarding schools or colonial system, thought that we were just the same people. They got that wrong.
 
Siasa ni lazima izingatie maadili, mifumo, falsafa, imani, itikadi, mitazamo, nk. Kwetu waafrika msingi mkuu wa mambo hayo ni UTU. Ni unafiki na usaliti mkubwa kushadadia siasa ikiukayo values zetu, kisa mzungu kasema ndio usasa.

Mzungu huwa ajisemei tu kaka in most cases anachokisema mara nyingi kesha kifanyia uchunguzi wa kina na atapokisema ujue kwamba atakitetea kwa nguvu zote lakini hakulazimishi na wewe ukichukue. Kwa maneno ya mzungu mmoja msomi mwenye miakili alivyosema (John Stuart Mill), ' the general or prevailing opinion in any subject is rarely or never the whole truth; it is only by the collusion of adverse opinions that the remainder of the truth has any chance of being supplied.

Sasa wewe uwezi kutumia neno utu tu kama kigezo cha umuhimu wa AA. kwanza utu wenyewe pekee unapatikana/tolewa kwa njia nyingi na huwa na tafsiri nyingi kwa watenda na watendewa pia. Fukara mmoja anaweza ona sawa akihakishiwa mkate kila siku, mwingine anaona yeye bora hawezeshwe kuweza kuutengeneza mkate hili asijione mtegemeaji.

Na siasa pia ni hivyo hivyo kuna watu wanataka vitu vingi au hata vile vile lakini wakapingana na njia za kufikia hapo. Sasa nyinyi mmekazana na utu tu as if AA la ndio njia pekee ya kuleta utu: kisa eti akina JK na wenzake wana haribu taifa leo. For god sake huyo huyo aliyewaandikia upuuzi wa AA ndiye yule yule alieibariki katiba inayosema raisi asishitakiwe. Kama yeye alikuwa anataka utu kwanza angeelewa yeye kapewa dhamana na raia watanzania na yeye ni raia kama wengine isipokuwa amepewa dhamana tu. Kwa maana hiyo katiba inayotoa sheria inayomfanya kibaka wa mataani aingie lupango itoe na sheria za raisi anae haribu kupewa adhabu hili hile huo ndio utu na sasa JK kama anakesi tungekuwa tushamfikisha mitaa Kisutu.

Leo kila kitu ni Azimio la Zanzibar tu ndio chanzo, sipingi limeruhusu njia za wizi kwenye kutafuta mwelekeo mpya. Lakini ukweli wenyewe tatizo lenyewe lilianzia kwenye katiba mbovu iliyotengenezwa wakati wa azimio bovu na leo hii kuruhusu uovu kutendeka kirahisi. [/QUOTE]

Unajua demokrasia ya ancient Greece, ilikuw ni Direct, mazingira yao yaliruhusu. Mabepari wa leo wakaja na ya kwao makusudi, Representative(indirect),

Kwanini mnapenda kupotosha watu, Greece miaka hiyo aikuwa na population ya hivyo na waliokuwa waki-participate kwenye hii michakato ni wanaume pekeyao tena wale waliokuwa na haki za kigiriki na watu wazima. Kwa maana hiyo makundi mengi ya watu hayakushiriki katika michakato hii ukizingatia vijana, wanawake, watumwa waliokuwa wengi walikuwa hawashirikishwi it was possible to practise direct democracy.

Lakini kwa sasa ni impossible kwanza vyama vingi vinasimamia njia tofauti za kuleta maendeleo, population ni kubwa na washiriki ni wengi ndio sababu za indirect-democracy si eti mzungu kajitungia tu, kisa unatetea uonevu uliotokana na Azimio Bovu.


Tanzania ni Tanzania and nothing else na dunia ni dunia. Sasa ulimwengu mzima hupo kwenye global economy, wasomi wa wenzetu wanaumiza vichwa kutengeneza namna ya kupigana na challenges the world market kwa manufaa ya mataifa yao. Sisi tumekazana na kurudi nyuma, how about creativity for once on how to face the world challenges. kama utaweka waziri kama mkullo na raisi kama tulienae na katiba kama hiliyopo halafu unategemea maendeleo then you dont live in the real world.

We need to go back, get accountabilty and checks right before anything. Halafu vyama vya siasa vianze kutunadia njia mbadala za kutuletea maendeleo wenye kutaka AA ni haki yao vile vile lakini si kwenye katiba yetu huko huko vyamani. Katiba yetu inataka kujua limitations za viongozi na uhakika kwa wataliwa, misingi yao ambayo wanajua hawevunjiwa na heshima ya kutambua tuna haki zilezile walizonazo viongozi.
 
Mkuu hapa ndipo uliponigusa haswaaa. Sababu kubwa ya kuwepo demokrasia ktk nchi ni kuruhusu itikadi nyingine pinzani nafasi sawa ya kuweza kutawala pindi wananchi watakapozichagua. Ni mfumo unao ondoa Udikteta hivyo maadam tulianza na TANU yenye siasa za Ujamaa na Kujitegemea ilitakiwa vyama pinzani vinatokana na upinzani wa kiitikadi hii, badala yake sisi tulifanya upinzani wa WATU wale wasiokubaliana na Nyerere ktk resolutions zilizofikiwa.
Watu kama Kambona waliporudi nchini kuanzisha vyama pinzani na CCM walikuta tayari CCM chenyewe hakifuati siasa za Ujamaa na Kujitegemea, CUF, Chadema na hata TLP vyote hivi vilipingana kutokana na vichwa vya viongozi walioko upande wa pili na mara zote mabadiliko ama misuguano ndani ya chama haikuhusiana na sera au itikadi bali watu wenyewe kutoaminiana.

Hivyo basi. swala langu mimi halipo hata ktk Itikadi ya TANU au CCM kwa kuchukua mlengo wa kushoto, hapana hoja yangu mmi ni kwamba hata ukichukua mrengo wa kushoto au kulia, NIA yetu ni kufanya na kulinda nini? Ukisoma declaration of Independence huwezi kuona kuna Uhafidhina au Usosialist kwa sababu hizi ni nyezo za maono tofauti kufikia NIA ya taifa walilotaka kulijenga. Nasi wakati tunapata Uhuru wetu tulitakiwa kuwa na NIA sio tu ya kujitawala ama kumweka kiongozi mweusi, kufuata siasa za TANU ambao hadi 1967 hawakuwa na siasa zaidi ya kuupata Uhuru wetu. Hatukuwa na dira zaidi ya kuweka malengo ya kuupata Uhuru wetu toka mikononi mwa Wakoloni thats it. sasa from there tunakwenda wapi?.. ndipo Azimio la Arusha lilikuja tupa mwanga huo japokuwa liliambatana na itikadi ya chama ambayo ilitambua nafasi yetu kimataifa na kuorodhesha maadui wetu. How to deal with them hapa ndipo tulitakiwa kutofautiana kiitikadi lakini sio kufuta kabisa DIRA yetu kwa sababu tu Azimio zima halikuwapendeza baadhi ya watu.

Ninachounga mkono mimi ktk Azimio la Arusha ni kwamba lilikuwa na madhumuni, nia na malengo. Kisha likatupa njia gani itakayotuwezesha kufika kule tunakotaka kwenda tofauti kabisa na siasa za vyama vyote nchini ambavyo havitazami WATU bali VITU. Azimio la Arusha linajieleza wazi kwamba nchi hii ni ya WAKULIMA na WAFANYAKAZI hii haina mlengo iwe Ujamaa au Ubepari ni kutambua who we are, na likajieleza wazi serikali italinda maslahi ya watu hawa.

Azimio la Arusha lilitambua maadui wetu kuwa ni umaskini, Ujinga na maradhi na ktk kutambua huko wakatoa resolution ambazo zinapambana na maadui hawa. Sasa tunaweza bishana na maamuzi ya silaha zilizotumika lakini haina maana kuazimia kwamba nchi yetu ni ya wakulima na wafanyakazi, maadui wetu ni umaskini, Ujinga na maradhi ni makosa kwa sababu vipo vitu universal kama haki za binadamu hapo ndipo mnaponiacha hoi. Maana hata waislaam na wakristu wanakubaliana ktk vitu Universal, wanakubaliana ktk kujenga maisha ya hapa dunia na Akhera lakini wanatofautiana ktk itikadi na mbinu za kufikia huko.

Na ndio maana tunarudi nyuma na kusema leo hii hatuiti Umaskini, Ujinga na maradhi kuwa maadui wetu ndio maana tumechukua mfumo wa nchi zilizoendelea ambao hawana maadui hawa na kuzitumia kuendeleza VITU badala ya kutaqmbua kwamba niu WATU wanaoweza kubadilisha mazingira. Matokeo yake tuna umaskini, ujinga na maradhi kuliko hata wakati wa Azimio la Arusha. Hivyo utaweza vipi kupambana na Umaskini ikiwa watu wake ni wajinga na nguvu kazi wenyewe asilimia kubwa wanakumbwa na maradhi.

Utaweza vipi kuibadilisha nchi yetu kuwa ya Technologia ikiwa hatutambui uwezo wa wakuilima wenyewe matumizi ya vifaa hivyo na tutawawezesha vipi hawa watu waweze kuviutumia badala yake tunafikiria kukiwezesha kilimo chenyewe. Utaweza vipi kuzalisha kazi ikiwa hutambui nafasi ya wananchi wako kama wengi ni wajinga na kwa asili ni wafanyakazi sio wafanyabiashara, na kutokana na umaskini na ujinga wao ni muhimu kuwawezesha ktk ujuzi na ufanisi mbele ya uzalishaji wa ajira zenyewe. Yote haya hayana Ujamaa wala Ubepari bali ni kuelewa unataka kulijenga Taifa gani na una rasilimali zipi mkononi kisha vyama vya siasa vinatafuta mbinu za kutumia rasilimali ktk maendeleo ya jamii ili tutoke hata ktk hali ya Umaskini, Ujinga na maradhi.

Leo hii sidhani kama tunakubali umaskini, kinachoaminiwa ni kwamba umaskini wetu ni wa kujitakia kwa sababu mali tunazo, msemo wa Kawawa kwamba Uchumi tunao tumeukalia. Na kwamba umaskini wetu unatokana na uongozi mbaya maana tunayo madini na rasilimali za kutosha kuitwa matajiri.

Nami nasema sii kweli maana Mmasai ni maskini kwa sababu kaamua kuishi maisha ya ufugaji anayojua zaidi maana akiingia ktk biashara wakati hajui michezo yake atafilisika mapema zaidi..Na ndivyo tulivyofanya sisi tumeondoa miiko na maadili yetu kwa kuiga ile ya wale waliokuwa na ujuzi na biashara. Tukaweka mikataba mibovu japokuwa kabla ya mwaka 1992 ilikuwa mwekezaji yeyote anayetaka kuwekeza nchini lazima atoe asilimia 50 au 51 kwa mwananchi. Kwa mgeni hakuweza kuwekeza nchini pasipo Ubia na mwananchi iwe madini au shirika lolote lakini tukaja yaondoa haya yote tukalegeza miiko yetu.

Azimio la Zanzibar likaondoa mambo mengi tu tukaingia kuitafuta MALI kutazama maendleo ya vitu kwa sababu nchi matajiri hawashughuliki na umaskini maana ni asilimia chini ya 10 ktk Utaifa wao wakati sisi hawa maadui tunalala nao tunaamka nao kila siku ya Mungu - hatuwezi kufanikiwa pasipo kutambua sisi ni nani, tunapambana na nini na tuna uwezo gani..Andikeni vitabu vyoote mtakavyo lakini pasipo kujimbabua sisi kwanza mbele ya itikadi halafu tukatazama sayansi na Technologia itaweza vipi kutumika kutusaidia kuondokana na vita hii basi tutaendelea kubishana hadi Kiyama..
 
Ndugu Eric...
(natumia mchina dat why nashindwa reply directly, hata likes pia)
>Nani kakudanganya kuwa kila kilichosemwa na mzungu, kwa kuwa unahisi amefanyia uchunguzi, basi ndo principles dunia yote! Matokeo yake ndio yale kuvaa kaoshi Makambako! Mzungu hayupo kwa maslahi ya watu wote duniani, ila kwao wenyewe tu!
>Unakosea tena, kuwa mzungu hatulazimish kufuata anachoamini, unafahamu neno "propaganda", "shinikizo" je? Fika mbali sana, fikiria beyond the reality, Tv stations zao zinatoonesha nin kwa malengo gani, is it for just pleassure? Lumumba yuko wapi? Gaddafi je? UN imesimama kwa ajili ya nani? The ICC nayo? NATO? Military bases? Puppets? Mitaala ya elimu yetu je? US dollor? Vyote hivyo ni kwa ajili ya ustawi wetu? Au unavichukulia juu juu tu?
>Fukara kuomba mkate na kuridhika, je sio wewe uliyepindisha mantiki yake, na kumdanganya kuwa una haki ya kuwa na mikate 5 hali ye hana?
>Nyerere hakuwa malaika, katiba ya leo kutoka kwake, si kigezo cha kupinga fikra zilizokuwemo AA, kwanza hazikutolewa naye pekee, ni jopo!
>Kwanini ushangae uozo wa JKM, kutochukuliwa hatua, hali unajua kipi kimemsimika, na unakiafiki? Mzungu mweu mkuu, taka usitake, wakimchoka wanamtimua hata leo!
>Unasema uchache wa wagiriki, na "only men participation" yao. Ndicho kilichowaongoza kwenye mila, imani, itikadi, falsafa, mitazamo, nk. Ndio maana hakukuwa na complications!
>Unazungumzia wasomi wa wenzetu kuumiza kichwa kupigania nchi zao, nikukumbushe kuwa, miongoni mwa vitu vinavyowaumiza vichwa ni namna gani wataendelea kushika akili zetu, kutufunga tusione hila zao juu yetu! Wasomi wetu wao wanasubiri wasomi wa kizungu waseme nini, ili watufundishe. Nasi kwa upuuzi na unafiki wetu tunasubiri msomi wetu aseme nini ili tusikie, aoneshe nini ili tuone, hali wanaendelea kutuonesha sura ya kondoo hali ni chui waliyooneshwa na mzungu.
Bob alinena hivi "imancipate yourself from mental slavery, none but ourselves can free our minds, have no fear for atomic energy, coz none of them can stop the time"
Nikimuona mtu mweusi, naiona Afrika na Mungu!
Mungu wetu anaita.
 
HITIMISHO





Najua mjadala ni mrefu!

Summaries zitatusadia kwani finally we have to postulate AZIMIO LA ARUSHA in a way it fits our modem times and We wish the other side do the same come out with something which YOU think can substitute/compliment the New Azimio!

We have had this discussion when it was Jambo Forums and many more times in Jamii forums, this time We have to produce working document, not mare discussion ... YES We have mjadala kwa Katiba Mpya and here we are starting Mjada kwa Azimio la Arusha JIPYA!!
 

I admit your post above is impressive.

I have no doubts that that during the struggles for independences, the intent to fight for freedom was there, crystal and clear. For instance in Tanganyika the common thread was around development levy, number of Tanganyika students in universities, self-rule, land reforms, etc. As such freedom wasn't a partisan issue, and people from various backgrounds were united for common course.

However, as it happened in other African countries, the top leaders of various freedom movements had their own hidden motives: power, greedy, ideology, and status. These motives, some are noble in their outlook, have hijacked our intents. In Africa we fought independence for something else, but as free people, we are subjected to power struggle, greedy, ideology orientation, and status.

For example, in some interviews, Nyerere admitted that he envisioned Ujamaa well before we got independence. Nonetheless, he didn't introduce it during the independent struggles because it was a lightning rod that could have divided TANU. He kept it to himself. However, there were ample signs to suggest that Ujamaa was the path he has chosen for us. Take for example Kivukoni College.

It was the first education institution Nyerere engineered. It was foundered in July 1961, 5 months before independence, and its main objective was to teach left leaning ideology. This example alone refutes the claim that Nyerere took some preemptive actions because we didn't have enough educated personnel. The truth is if somebody has already chosen your path, he or she won't consult you for your opinions.

Taking into consideration the world politics of 50s, and 60s, one could understand why Nyerere was swayed to follow that route. Socialism and communism were winning audience worldwide in large number. Even the liberal and leftists in the West didn't anticipate the triumph of capitalism in late 80s and early 90s. It was inconceivable that the USSR will cease to exist.

Simply put, the triumph of capitalism left Tanzania or for that matter many countries which has spent considerable amount of time denouncing the west unprepared. In Tanzania those who support Ujamaa have everything at their disposal such as school of thought and institutions. But they don't have courage and guts. On other hand those who support the right (capitalism) don't have school of thought, institutions, and ideas. They want to be part of something they don't know.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…