Mkandara,
...Naungana nawe kwenye pointi hizi, na nitafafanua.
kila kitu kinatanguliwa na NIA. La kutazama hapo juu, ni yule anayepeleka punda kwenda kunywa maji mtoni (vijiji vya Ujamaa) huwa ana nia gani, nzuri au mbaya hata kama Punda hawataki kunywa maji wanataka kuendelea kula nyasi hawezi kulazimisha punda wanywe maji. Ni bora wao wafikirie (kama wanaweza kufikiri) ile safari waloichukua toka kwenye nyasi hadi mtoni kabla ya kukataa kabisa kunywa maji na huwezi sema kutokunywa maji basi ni failure ya mtu alowapeleka Punda mtoni.
...Nia ya Baba wa Taifa ilikuwa njema kabisa -kuwawezesha wa-Tanzania wapate maendeleo mapema- ila haikutekelezwa kwa umakini, kwani, kwa nionavyo mimi -with benefit of hindsight- ilibidi wananchi washirikishe kwa kiasi kwenye mipango hiyo, kwa kutoa maoni na ushauri wao.
...Naamini, kungekuwa na mafanikio zaidi kama wananchi wangeshirikishwa, ili kupata kile kinachoitwa "local content". Jambo ambalo ni muhimu sana kwenye community development strategy, plan and execution.
Tatizo la Vijiji vya Ujamaa ni kwamba tulipelekwa kwenye mto wa maji tukakataa kuyanywa. Tukitaka kuendelea kula nyasi hadi shibe. Sawa tulikataa, lakini ile safari ya kurudi kwenye nyasi tulihitaji maji mwilini, hivyo tunarudi kwenye nyasi wakati tuna kiu ya kuua, hivyo tuna mchanganyiko wa njaa na kiu ndio maana tunamalizana kwenye kipande cha nyasi na maji.
...Tatizo halikutokana na wananchi pekee. Mpango huu haukutekelezwa vizuri. Je, tuna uhakika kule walikohamishiwa kulikuwa na vyanzo vya maji, vya kutosha?. Je, wananchi walikuwa na chakula au waliweza kulima from the word go? Ile ardhi ambayo ilibidi iendelezwe, iliwekewa mkakati gani? Ilikuwa bora kama ile waliyokuwa nayo? Ilihitaji muda gani kuanza kuzalisha kama ile ya awali.
...Unajua. Kuna taarifa kwamba, wengi waliliwa na simba au na wanyamapori wakali. Wengine walikufa njaa.
...Zaidi. Wengi walirudishwa nyuma kimaendeleo kutokana na niliyoyasema hapa juu.
Makosa pekee ya Azimio la Arusha ni Ukomunist fulani ulokuwemo, ile kuweka njia zote za uzalishaji chini ya serikali jambo ambalo halipo ktk hata mila na desturi za kiafrika. maana watu walikuwa na mali zao mashamba yao na hata ardhi zao kwa mipaka. Kama tungeweza kuliepuka baada ya kutaifisha mali za wageni wakoloni, kisha mali hizo zingewekwa mikononi mwa wananchi kwa kufuata misingi ya mila na tamaduni zetu pengine ingeleta picha tulitakayo ya U Capitalist, lakini tungeweza vipi kuifanya kazi hiyo ikiwa mali zote zilikuwa za wageni kwanza?
...Ni kweli kulikuwa na makosa katika kutaifisha mali. Lakini, nia ilikuwa nzuri. Nyerere alilenga kuharakisha africanization na kutekeleza miradi kadhaa ya maendeleo ili kuwainua wa-Tanzania.
...Sasa. Tunaweza sema hiyo haikuwa njia sahihi. Lakini, tujiulize ni hali gani ilikuwa inatawala katika philosofia za kimaendeleo wakati huo?
...Mimi nitajenga hoja kwamba, Baba wa Taifa hakuwa amekosea sana, ila alitakiwa kuwa flexible na kupima matokeo ya mipango hii ambayo nia yake ilikuwa njema kabisa.
...Nitarudia ku-hoja kwamba, model ya kifaransa ingetufaa zaidi, na au tungeikumbatia baadae, hasa, ikiendana na hoja yako, kwamba, mali hizi zilikuwa za wageni -na pengine wao ndio walijua namna ya kuzisimamia kwa uzuri zaidi, katika utawala, masoko, malighafi na teknolojia.
Mwaka 1992 ndio ulikuwa mwaka ambao tungeweza yaweka mashirika yote ya serikali ktk wallstreet yetu DSE yakaendeshwa kama mashirika binafsi na watu wakanunua hisa zao. Mwenye uwezo akanunua hadi asilimia 50, lakini sio kuyafilisi kwa kutumia neno la kiingereza Privatization wakati tunayafilisi ili kutajirisha viongozi wale wale waliotaka utajiri huo baada ya Uhuru (kula nyasi). Miiko na maadili kuondolewa ndilo kosa kubwa zaidi ya yuote yaliyotangulia. Uongozi bora hauwezi patikana pasipo miiko na maadili.
...Tusingeweza. Huwezi, katika hali ya kawaida, kuandikisha mashirika yenye madeni makubwa -ambayo mengine thamani yake inafutwa na hayo madeni- katika soko la hisa. Nafahamu kwamba, yapo ambayo yalihitaji kufanyiwa kazi kidogo ili yafae kuwekwa kwenye soko la hisa.
...Tatizo kubwa ambalo tumekuwa nalo hata leo, ni quality ya viongozi kwenye haya mashirika or rather parastatals, na pia uhuru wao wa kufanya maamuzi ya muhimu kwa maendeleo ya mashirika hayo.
...Kama tuna nia ya kuendelea kupitia mashirika haya, lazima tubadili mfumo na aina ya usimamizi unayoyaongoza.
...Lazima viongozi wake wawe bora, wenye sifa -zenye kupimika- za kufanya vyema huko walikotoka, na wasiingiliwe kwenye maamuzi ya utendaji wa shughuli za msingi.
...Pia, wanatakiwa kuwa na uhuru fulani -unaotazamwa- wa kuanzisha, kuendeleza, na kusitisha shughuli zote za uwekezaji kwa manufaa ya mashirika haya na Taifa.