Azimio La Arusha: Why We Were Dead Wrong!

Azimio La Arusha: Why We Were Dead Wrong!

Kwikwikwi,

Even Dickson says that The AD REPRESENTS PHILOSOPHY ... He doesn't say The AD IS A PHILOSOPHY. Anyway, my past time activity is to ready the work of socialist leaders. One common thread about them is everybody tried to write something and everybody was philosopher. Kim Jong Sun, Mao Tse Tung, Nyerere, Sekou Toure, etc.
There are millions of philosophers ...... It doesn't really mean that you are smart or a good leader, it just means you have an idea that is distinguishable.
 
Have you lived there? I lived in Sweden some years ago, and I can tell you that they pay a hell of taxes. In addition, they are very liberal. For example, the prime minister of Sweden can't impose his will upon majority because he or she is educated. They understand human rights and freedom to choose.
And...... they are socialist.
 
JLF,

I have read African history to some extent, and I can tell you that we were just brutal as any civilazation. Take for example Mirambo. He wasn't even a king, but through his business deals and military skills he became one just like Lowassa and JK. So the notion that black forks were innocent doesn't add up.

Brutality katika tamaduni zozote haziwezi kosekana, lakini haileti maana kuwa hazifai. Hapo ndipo tunapojidanganya na ubepari, eti utawala wa sheria na haki za binadamu, wenzetu wameshafikia hatua ya wote kuelimika juu ya demokrasia, sisi tulio wengi hatufahamu hata haki zetu, nitafikiriaje ya kwako? (simaanishi kuunga mkono haki hizo)
Napenda kuugawa ubepari katika sehemu mbili, Internal Capitalism yaani unyonyaji kati ya mtu na mtu ndani ya taifa moja, na ule wa External Capitalism, yaani taifa kunyonya taifa, wenzetu wameshafikia huko, nasi ni waanga wa hilo, je tunategemea siku nasi under ubepari kunyonya nchi za kimagharibi? Au tunataka tuje kumnyonya Mmalawi, au Burundi, unafikiri inawezekana? Tunategemea nini sasa?
Haki za binadamu, demokrasia, dini, na unafiki wetu, vimevisha ubepari ngozi ya kondoo hali ni chui. INAUMA SANA!
Mungu wetu anaita!
 
- Mimi ndiye mleta mada, ninasema hivi ninamuangalia Mwalimu on his policies sio yeye kama binadam, na ninasema hivi Azimio was a failure na ndilo limetufikisha hapa Wa-Tanzania, hatujui tulikotoka!

- Tatizo sio Mwalimu as a human being, tatizo ni policy yake ya Azimio la Arusha, it was not real it was a fake policy ndio maana ilibidi ife!


William.

kaka yangu william
ubepari hata ukikaa miaka 50 na ukawa na athari mbaya kiasi gani wananchihawana option tena kwani kuna vikwazo vingi vya kutokuubali ubepari, hata hivyoubepari kwa muda mfupi tu umeonesha athari kubwa katika jamii kama zifuatazo
matabaka yameongezeka tena kwa kasi ya ajabu na utu umepotea, tunafikamuda hata utamaduni na utambulisho wetu unapotea pia,

rushwa inaongezeka kwa kasi kubwa kwani mianya ni mingi,unyonyaji nadhuluma imekuwa kubwa unyanyasaji wa wananchi na mali za wengi kumilikiwa nawachache imekuwa jambo linalolindwa na tabaka fulani.
ubepari pasipo uzalendo na dira maalumu ni kuisambaratisha jamii nakuleta uadui.
ndicho mwalimu alichokataa kwa wakati ule.ubepari unaweza kukubalika ilaviongozi wetu wawe makini na wawe na limit ya vitu fulani fulani
 
Right !!!!!!!!!! Now you assert that every decration made and signed by a political party is indeed a philosophical document.

i didnt say so!
mind you by that definition i can say AD is a philosophical document.
 
sasa mkuu zakumi utuambie kwa nini wewe waona hiyo siyo ama haina vigezo vya kuwa philosophical document.
 
nimependa mjadala huu hauna mawaa umejaa ubishani wa hoja na sio matusi na kuitana majina ya ajabuajabu haya ndio majadiliano na ubishani wa kiutuuzima busara na kustaarabika. wakija wale wa jazba na uharibifu utawajua tu.
 
Kwikwikwi,

Even Dickson says that The AD REPRESENTS PHILOSOPHY ... He doesn't say The AD IS A PHILOSOPHY. Anyway, my past time activity is to ready the work of socialist leaders. One common thread about them is everybody tried to write something and everybody was philosopher. Kim Jong Sun, Mao Tse Tung, Nyerere, Sekou Toure, etc.

then if it represents philosophy how comes it is not a philosophical document?
zakumi this is your interpretation to say he did not say ad was philosophical document coz he already said it is a philosophical document.

its like i am telling u that bongo flavour represent african beauty this is as same as saying there is african beauty in it.
if it represents philosophy there is philosophy in it and therefore it is philosophical document.
 
Hard work is a personal choice why should it be in a national declaration for greatness. People don't work hard for sake of it. They work hard if there's incentive to do so.

Between 1970-1980 when AA was the rule of the land, productivity in Tanzania was down by more than 50%. If hard work is one of your principle, we should have done better back then.

on bold is where you are wrong mkuu,
in developed countries never started as liberals they are what they are today by working very hard and it was by force to work hard and is was national rule to work hard. there after it when the became liberals. so as we did though it was not succesful to us as it did to others you know the reasons and there are so many.

to a country like ours liberalism and what you call choices are the most enermy of our development.people need to be controled so that later we all enjoy national cake.
freedom,democracy , human rights and all things of their kind work better in developed countries not developing.

in the name of freedom of choice people decide not work, not to protect national resources and do what they feel likedoing. taifa pasipo miongozo yenye nguvu limepotea,
 
Hili nalo neno.

Wrong!!!!!!!
Kwa mfano, falsafa ya nguvu ya umma na itikadi ya mlengo wa kati.
Nguvu ya umma is not a philosophy!!, you have to explain to us people's power in what? How are you going to invest power to the people? Under what philosophy and how did you come up with such a philosophy? Ndiyo maana nasema CDM huwa hawaeleweki unless uwe si mtu makini.
 
Kobello embu jisome kwanza mwenyewe, kabla ya jibu langu maana nyie washabiki wa hili AA mmekazana na kuwaambia wenzenu hawalifahamu halafu wenyewe kila saa mnaji-contradict na implemention za AA. Chini hapa mnasema misingi ilikuwa ni kujikomboa na soko la dunia.
The Arusha Declaration represents the philosophy developed by Nyerere and the Tanganyika African National Union as they worked to bring economic and social development to their impoverished country and navigate the complex global economic and political arena.

Halafu hapa tena unasema (tatizo kubwa) ni hao hao wasimamizi wa soko la dunia waliwatema, mkuu mi naanza kuona hili AA kwako lipo kiimani zaidi kuliko ukweli wenyewe kwenye implemention. Maana ni kitu ambacho ni impossible kwenye dunia ya sasa, kufanya economical activities bila ya external trade.
The biggest of all (there are many) was "political", by leaning left, we were isolated by the international community in things like trade, international financing eg. IMF,WB etc.
We were also too pan Africanist (at least labeled as), fighting for our brothers down south, supporting polisario, not recognizing Taiwan, South Korea and Israel. It was of course an uphill battle compared to puppet nations like Kenya.

Maana amna hata sababu za kwenda kuchambua the challenges of production efficiency kwenye hili Azimio Uchwara, hili kuweza kuja kuelezana matatizo ya mistari ya kununua bidhaa na upungufu wa bidhaa yalipoanzia na huko ndio mimi sikupendi kabisa kuhusu hili Azimio.

Inabidi watetezi sasa mje na ubishi imara lakini si hizi hadithi za maandishi embu mjadala ueleke kisayansi na si haya mambo ya utu.
 
...Hii kazi sio ilifanywa na Deng?

...Mao si ndiye aliyekuja na cultural revolution? I think, he was a sadist of the highest degree. ...True. ...Ok. ...Kwanza, nadhani tatizo au rather chanzo ni africanization. Pili, vijiji vya ujamaa si China au Urusi tu. Hii ilikuwa au na hata sasa -inategemea tafsiri yako- ilikuwa almost kote Ulaya -ili kuweza leta maendeleo kwa haraka na kujilinda. Makes me remember Kibbutzim. ...True. ...You can say this, again!


Chairman Mao mwenyewe alifanya normalization. Alimwalika Richard Nixion.
 
There are millions of philosophers ...... It doesn't really mean that you are smart or a good leader, it just means you have an idea that is distinguishable.

So I won't commit crime if I say the authors of AD weren't smart and good leaders.

Z-10
 
i didnt say so!
mind you by that definition i can say AD is a philosophical document.

sasa mkuu zakumi utuambie kwa nini wewe waona hiyo siyo ama haina vigezo vya kuwa philosophical document.


You didn't say so but you have imply so. As it stands, the AD is a political party declaration, and it's not a work of a philosopher.

Now concerning the second party, the word philosophy was used to elevate Ujamaa and AD to international prominence. In 50, 60 and 70, there was a desire within African continent and in the west to promote home grown African philosophies. However, those philosophies didn’t stand the test of time and generations because they were ill-conceived. It’s simple us that.

In case of AD, the authors were the subjects of their own philosophical experiments. They used their own personal experiences as the baseline of what should come. For example, Tanzania is diverse country. But the authors, who spent majority of their teen years and adult lives in colonial boarding schools or colonial system, thought that we were just the same people. They got that wrong.
 
Siasa ni lazima izingatie maadili, mifumo, falsafa, imani, itikadi, mitazamo, nk. Kwetu waafrika msingi mkuu wa mambo hayo ni UTU. Ni unafiki na usaliti mkubwa kushadadia siasa ikiukayo values zetu, kisa mzungu kasema ndio usasa.

Mzungu huwa ajisemei tu kaka in most cases anachokisema mara nyingi kesha kifanyia uchunguzi wa kina na atapokisema ujue kwamba atakitetea kwa nguvu zote lakini hakulazimishi na wewe ukichukue. Kwa maneno ya mzungu mmoja msomi mwenye miakili alivyosema (John Stuart Mill), ' the general or prevailing opinion in any subject is rarely or never the whole truth; it is only by the collusion of adverse opinions that the remainder of the truth has any chance of being supplied.

Sasa wewe uwezi kutumia neno utu tu kama kigezo cha umuhimu wa AA. kwanza utu wenyewe pekee unapatikana/tolewa kwa njia nyingi na huwa na tafsiri nyingi kwa watenda na watendewa pia. Fukara mmoja anaweza ona sawa akihakishiwa mkate kila siku, mwingine anaona yeye bora hawezeshwe kuweza kuutengeneza mkate hili asijione mtegemeaji.

Na siasa pia ni hivyo hivyo kuna watu wanataka vitu vingi au hata vile vile lakini wakapingana na njia za kufikia hapo. Sasa nyinyi mmekazana na utu tu as if AA la ndio njia pekee ya kuleta utu: kisa eti akina JK na wenzake wana haribu taifa leo. For god sake huyo huyo aliyewaandikia upuuzi wa AA ndiye yule yule alieibariki katiba inayosema raisi asishitakiwe. Kama yeye alikuwa anataka utu kwanza angeelewa yeye kapewa dhamana na raia watanzania na yeye ni raia kama wengine isipokuwa amepewa dhamana tu. Kwa maana hiyo katiba inayotoa sheria inayomfanya kibaka wa mataani aingie lupango itoe na sheria za raisi anae haribu kupewa adhabu hili hile huo ndio utu na sasa JK kama anakesi tungekuwa tushamfikisha mitaa Kisutu.

Leo kila kitu ni Azimio la Zanzibar tu ndio chanzo, sipingi limeruhusu njia za wizi kwenye kutafuta mwelekeo mpya. Lakini ukweli wenyewe tatizo lenyewe lilianzia kwenye katiba mbovu iliyotengenezwa wakati wa azimio bovu na leo hii kuruhusu uovu kutendeka kirahisi. [/QUOTE]

Unajua demokrasia ya ancient Greece, ilikuw ni Direct, mazingira yao yaliruhusu. Mabepari wa leo wakaja na ya kwao makusudi, Representative(indirect),

Kwanini mnapenda kupotosha watu, Greece miaka hiyo aikuwa na population ya hivyo na waliokuwa waki-participate kwenye hii michakato ni wanaume pekeyao tena wale waliokuwa na haki za kigiriki na watu wazima. Kwa maana hiyo makundi mengi ya watu hayakushiriki katika michakato hii ukizingatia vijana, wanawake, watumwa waliokuwa wengi walikuwa hawashirikishwi it was possible to practise direct democracy.

Lakini kwa sasa ni impossible kwanza vyama vingi vinasimamia njia tofauti za kuleta maendeleo, population ni kubwa na washiriki ni wengi ndio sababu za indirect-democracy si eti mzungu kajitungia tu, kisa unatetea uonevu uliotokana na Azimio Bovu.

Tanzania haikuwa kama Urusi au China, ndio maana Nyerere alikuj na AA, ambalo ni zao la mazingira na nyakati zetu halisi "African Socialism", kibaya kipi?
Tulishazikwa hai kwa ukaidi na usaliti wetu, tusiache iwe kwa watoto wetu!
Mungu wetu anaita!

Tanzania ni Tanzania and nothing else na dunia ni dunia. Sasa ulimwengu mzima hupo kwenye global economy, wasomi wa wenzetu wanaumiza vichwa kutengeneza namna ya kupigana na challenges the world market kwa manufaa ya mataifa yao. Sisi tumekazana na kurudi nyuma, how about creativity for once on how to face the world challenges. kama utaweka waziri kama mkullo na raisi kama tulienae na katiba kama hiliyopo halafu unategemea maendeleo then you dont live in the real world.

We need to go back, get accountabilty and checks right before anything. Halafu vyama vya siasa vianze kutunadia njia mbadala za kutuletea maendeleo wenye kutaka AA ni haki yao vile vile lakini si kwenye katiba yetu huko huko vyamani. Katiba yetu inataka kujua limitations za viongozi na uhakika kwa wataliwa, misingi yao ambayo wanajua hawevunjiwa na heshima ya kutambua tuna haki zilezile walizonazo viongozi.
 
Inzi,
The problem you guys are having is to try to convert us and accept that Azimio Arusha is a fabulous document and all Tanzanians should rally behind it. That's a tall order to achieve because majority in your camp don't read and understand Azimio la Arusha in its entirety. They don't know what is Ujamaa and what's AD. So instead of looking for new converts, you need to educate your own supporters.

In addition, we have two sold philosophical camps here. Probably this is the best outcome of Azimio la Arusha, a political spectrum. Those who support should go to the left (wajamaa) and those who don't should go to the right (wabepari).

Cau

Z10
Mkuu hapa ndipo uliponigusa haswaaa. Sababu kubwa ya kuwepo demokrasia ktk nchi ni kuruhusu itikadi nyingine pinzani nafasi sawa ya kuweza kutawala pindi wananchi watakapozichagua. Ni mfumo unao ondoa Udikteta hivyo maadam tulianza na TANU yenye siasa za Ujamaa na Kujitegemea ilitakiwa vyama pinzani vinatokana na upinzani wa kiitikadi hii, badala yake sisi tulifanya upinzani wa WATU wale wasiokubaliana na Nyerere ktk resolutions zilizofikiwa.
Watu kama Kambona waliporudi nchini kuanzisha vyama pinzani na CCM walikuta tayari CCM chenyewe hakifuati siasa za Ujamaa na Kujitegemea, CUF, Chadema na hata TLP vyote hivi vilipingana kutokana na vichwa vya viongozi walioko upande wa pili na mara zote mabadiliko ama misuguano ndani ya chama haikuhusiana na sera au itikadi bali watu wenyewe kutoaminiana.

Hivyo basi. swala langu mimi halipo hata ktk Itikadi ya TANU au CCM kwa kuchukua mlengo wa kushoto, hapana hoja yangu mmi ni kwamba hata ukichukua mrengo wa kushoto au kulia, NIA yetu ni kufanya na kulinda nini? Ukisoma declaration of Independence huwezi kuona kuna Uhafidhina au Usosialist kwa sababu hizi ni nyezo za maono tofauti kufikia NIA ya taifa walilotaka kulijenga. Nasi wakati tunapata Uhuru wetu tulitakiwa kuwa na NIA sio tu ya kujitawala ama kumweka kiongozi mweusi, kufuata siasa za TANU ambao hadi 1967 hawakuwa na siasa zaidi ya kuupata Uhuru wetu. Hatukuwa na dira zaidi ya kuweka malengo ya kuupata Uhuru wetu toka mikononi mwa Wakoloni thats it. sasa from there tunakwenda wapi?.. ndipo Azimio la Arusha lilikuja tupa mwanga huo japokuwa liliambatana na itikadi ya chama ambayo ilitambua nafasi yetu kimataifa na kuorodhesha maadui wetu. How to deal with them hapa ndipo tulitakiwa kutofautiana kiitikadi lakini sio kufuta kabisa DIRA yetu kwa sababu tu Azimio zima halikuwapendeza baadhi ya watu.

Ninachounga mkono mimi ktk Azimio la Arusha ni kwamba lilikuwa na madhumuni, nia na malengo. Kisha likatupa njia gani itakayotuwezesha kufika kule tunakotaka kwenda tofauti kabisa na siasa za vyama vyote nchini ambavyo havitazami WATU bali VITU. Azimio la Arusha linajieleza wazi kwamba nchi hii ni ya WAKULIMA na WAFANYAKAZI hii haina mlengo iwe Ujamaa au Ubepari ni kutambua who we are, na likajieleza wazi serikali italinda maslahi ya watu hawa.

Azimio la Arusha lilitambua maadui wetu kuwa ni umaskini, Ujinga na maradhi na ktk kutambua huko wakatoa resolution ambazo zinapambana na maadui hawa. Sasa tunaweza bishana na maamuzi ya silaha zilizotumika lakini haina maana kuazimia kwamba nchi yetu ni ya wakulima na wafanyakazi, maadui wetu ni umaskini, Ujinga na maradhi ni makosa kwa sababu vipo vitu universal kama haki za binadamu hapo ndipo mnaponiacha hoi. Maana hata waislaam na wakristu wanakubaliana ktk vitu Universal, wanakubaliana ktk kujenga maisha ya hapa dunia na Akhera lakini wanatofautiana ktk itikadi na mbinu za kufikia huko.

Na ndio maana tunarudi nyuma na kusema leo hii hatuiti Umaskini, Ujinga na maradhi kuwa maadui wetu ndio maana tumechukua mfumo wa nchi zilizoendelea ambao hawana maadui hawa na kuzitumia kuendeleza VITU badala ya kutaqmbua kwamba niu WATU wanaoweza kubadilisha mazingira. Matokeo yake tuna umaskini, ujinga na maradhi kuliko hata wakati wa Azimio la Arusha. Hivyo utaweza vipi kupambana na Umaskini ikiwa watu wake ni wajinga na nguvu kazi wenyewe asilimia kubwa wanakumbwa na maradhi.

Utaweza vipi kuibadilisha nchi yetu kuwa ya Technologia ikiwa hatutambui uwezo wa wakuilima wenyewe matumizi ya vifaa hivyo na tutawawezesha vipi hawa watu waweze kuviutumia badala yake tunafikiria kukiwezesha kilimo chenyewe. Utaweza vipi kuzalisha kazi ikiwa hutambui nafasi ya wananchi wako kama wengi ni wajinga na kwa asili ni wafanyakazi sio wafanyabiashara, na kutokana na umaskini na ujinga wao ni muhimu kuwawezesha ktk ujuzi na ufanisi mbele ya uzalishaji wa ajira zenyewe. Yote haya hayana Ujamaa wala Ubepari bali ni kuelewa unataka kulijenga Taifa gani na una rasilimali zipi mkononi kisha vyama vya siasa vinatafuta mbinu za kutumia rasilimali ktk maendeleo ya jamii ili tutoke hata ktk hali ya Umaskini, Ujinga na maradhi.

Leo hii sidhani kama tunakubali umaskini, kinachoaminiwa ni kwamba umaskini wetu ni wa kujitakia kwa sababu mali tunazo, msemo wa Kawawa kwamba Uchumi tunao tumeukalia. Na kwamba umaskini wetu unatokana na uongozi mbaya maana tunayo madini na rasilimali za kutosha kuitwa matajiri.

Nami nasema sii kweli maana Mmasai ni maskini kwa sababu kaamua kuishi maisha ya ufugaji anayojua zaidi maana akiingia ktk biashara wakati hajui michezo yake atafilisika mapema zaidi..Na ndivyo tulivyofanya sisi tumeondoa miiko na maadili yetu kwa kuiga ile ya wale waliokuwa na ujuzi na biashara. Tukaweka mikataba mibovu japokuwa kabla ya mwaka 1992 ilikuwa mwekezaji yeyote anayetaka kuwekeza nchini lazima atoe asilimia 50 au 51 kwa mwananchi. Kwa mgeni hakuweza kuwekeza nchini pasipo Ubia na mwananchi iwe madini au shirika lolote lakini tukaja yaondoa haya yote tukalegeza miiko yetu.

Azimio la Zanzibar likaondoa mambo mengi tu tukaingia kuitafuta MALI kutazama maendleo ya vitu kwa sababu nchi matajiri hawashughuliki na umaskini maana ni asilimia chini ya 10 ktk Utaifa wao wakati sisi hawa maadui tunalala nao tunaamka nao kila siku ya Mungu - hatuwezi kufanikiwa pasipo kutambua sisi ni nani, tunapambana na nini na tuna uwezo gani..Andikeni vitabu vyoote mtakavyo lakini pasipo kujimbabua sisi kwanza mbele ya itikadi halafu tukatazama sayansi na Technologia itaweza vipi kutumika kutusaidia kuondokana na vita hii basi tutaendelea kubishana hadi Kiyama..
 
Ndugu Eric...
(natumia mchina dat why nashindwa reply directly, hata likes pia)
>Nani kakudanganya kuwa kila kilichosemwa na mzungu, kwa kuwa unahisi amefanyia uchunguzi, basi ndo principles dunia yote! Matokeo yake ndio yale kuvaa kaoshi Makambako! Mzungu hayupo kwa maslahi ya watu wote duniani, ila kwao wenyewe tu!
>Unakosea tena, kuwa mzungu hatulazimish kufuata anachoamini, unafahamu neno "propaganda", "shinikizo" je? Fika mbali sana, fikiria beyond the reality, Tv stations zao zinatoonesha nin kwa malengo gani, is it for just pleassure? Lumumba yuko wapi? Gaddafi je? UN imesimama kwa ajili ya nani? The ICC nayo? NATO? Military bases? Puppets? Mitaala ya elimu yetu je? US dollor? Vyote hivyo ni kwa ajili ya ustawi wetu? Au unavichukulia juu juu tu?
>Fukara kuomba mkate na kuridhika, je sio wewe uliyepindisha mantiki yake, na kumdanganya kuwa una haki ya kuwa na mikate 5 hali ye hana?
>Nyerere hakuwa malaika, katiba ya leo kutoka kwake, si kigezo cha kupinga fikra zilizokuwemo AA, kwanza hazikutolewa naye pekee, ni jopo!
>Kwanini ushangae uozo wa JKM, kutochukuliwa hatua, hali unajua kipi kimemsimika, na unakiafiki? Mzungu mweu mkuu, taka usitake, wakimchoka wanamtimua hata leo!
>Unasema uchache wa wagiriki, na "only men participation" yao. Ndicho kilichowaongoza kwenye mila, imani, itikadi, falsafa, mitazamo, nk. Ndio maana hakukuwa na complications!
>Unazungumzia wasomi wa wenzetu kuumiza kichwa kupigania nchi zao, nikukumbushe kuwa, miongoni mwa vitu vinavyowaumiza vichwa ni namna gani wataendelea kushika akili zetu, kutufunga tusione hila zao juu yetu! Wasomi wetu wao wanasubiri wasomi wa kizungu waseme nini, ili watufundishe. Nasi kwa upuuzi na unafiki wetu tunasubiri msomi wetu aseme nini ili tusikie, aoneshe nini ili tuone, hali wanaendelea kutuonesha sura ya kondoo hali ni chui waliyooneshwa na mzungu.
Bob alinena hivi "imancipate yourself from mental slavery, none but ourselves can free our minds, have no fear for atomic energy, coz none of them can stop the time"
Nikimuona mtu mweusi, naiona Afrika na Mungu!
Mungu wetu anaita.
 
HITIMISHO

1. Kinyume cha UTU Huru wa MTU sio hali ya Unyama kama wengi wanavyotaka kutusadikisha. Si sahihi kumuita mtu aliyesaliti uasili wake ambao ni Utu wake kuwa, kwa kuukosa Utu sasa ana unyama. Mnyama hakusaliti uasili wake ili kuufikia Unyama ambao ndio asili yake, mnyama hajafanya kosa lolote ili kuwa mnyama. Mtu kuusaliti na kutelekeza uasili wake ambao ndio utu wake kafanya kosa, na sasa anathamani ya chini kabisa kuliko ya mnyama asiyefanyia mzaha uasili wake ambao ndio unyama wake. Kwa kuwa tunamuongelea MTU kujipambanisha na MAZINGIRA yake ili kujistawisha na kujiendeleza, lazima kuzingatia makundi haya mawali ambayo kwa muonekano wa machoni, watu wote wa makundi haya wanaonekana ni sawa, kumbe sio sahihi. Kosa hili lilifanyika mwaka 1967 lisirudiwe tena. Itamkwe dhahiri kuwa kuna "MTU-MWENYE UTU" na "MTU-MPINGA UTU" ambao watakuwa na miingiliano na makabiliano TOFAUTI kwenye MAZINGIRA yao ili kujipatia Maendeleo.

2. Mtu mwenye UTU kwa mfano akisukumwa na Utu wake, ataona kuwa tupambane na mazingira yetu kupitia Ardhi tufanye Kilimo, Ufugaji na kufanya kazi ili kupata rizki na ustawi wa jamii kama hatua ya mwanzo ya kujenga Taifa changa kwani ndicho kinachoweza kuwafikia wananchi wake wengi kwa wakati huo. Lakini Mpinga Utu atasukumwa Kibinafsi na Kupinga Hoja hiyo na kuona tufanye biashara nk ambayo si muafaka kwa wakati husika. Mpinga UTU anayetawaliwa na ubinafsi ulio kithiri, kwani ndio utambulisho wake, anapopewa kundi la watu kuwaongoza ili kukabiliana na Mazingira yao, atapelekea madhara makubwa, hivyo lazima KU/Azimia namna ya kuwadhibiti Wapinga UTU kabla ya kuanza mchakato wowote kustawisha na kuendeleza jamii! Azimio La UTU lililoasisiwa Arusha, haliko ili likubalike kwa namna yeyote na wapinga UTU, bali liko ili kuwakabili na kurejesha heshima na usawa wa utu kwenye Maendeleo ya Jamii HURU na yanye KUHESHIMIANA katika ujenzi wa Taifa.

3. UTU Huru wa MTU unahitaji kulindwa, kujengwa, kurutubishwa na kusimamiwa ili kumsukuma MTU kikamilifu kujipambanisha na Mazingira yake ambayo ndio rasilimali, mali ya asili, mitaji, ardhi, bahari na kila lile lililoko kwenye mazingira yake ili kumjegea maendeleo yake. UTU wa MTU ni "RASILIMALI MAMA" na Mazingira yake yanakuwa ni "RASILIMALI MAZINGIRA" ambazo zote kwa pamoja vinatupelekea kwenye Maendeleo ya Mtu kwenye Mazingira yake.

4. Isipokuwa kwa Mpinga Utu peke yake, hakuna mtu mwingne asiyejua kuwa bila rasilimali mama, rasilimali mazingira peke yake hugeuka na kuwa vyanzo vya magonjwa, vita, ufukara, ukandamizaji, ufisadi nk. Bila rasilimali mama (Utu wa Mtu kushika hatamu ya Jamii/Taifa) ambao ni ujulma wa utu wa jamii, "Mazingira yanabadilika na kuwa chombo cha kumuadhibu Mt". Ni Mpaka Mbegu ya utu kifamilia na Kitaifa, itawale jamii husika ndipo Mazingira na rasilimali zake zote zinaweza kumuendeleza na Kumneemesha Mtu. Rasilimali mazingira na Madini yote ya thamani chini ya Utawala Usiozingatia UTU ambayo ndio rasilimali mama, Madini hayo yanakuwa vyanzo vya kustawisha wachache na pengine kuzua machafuko na vita kati ya "walikowa nacho" na wale "waliodhulumiwa" hivyo kubomoa na kuangamiza maendeleo kwa kila hali. Kunahitajika Azimio La UTU lililo IMARA kabisa na "linaloendana na wakati kila wakati" ili Kunusuru UTU WA TAIFA usifanyiwe mzaha na kuchezewa na wapinga Utu, katika michakato yote ya kijamii ili kufikia maendeleo na ustawi wa jamii ya Kitanzania.

5. Kuwadhibiti wapinga Utu, ambao wakifanikiwa "kusoma" na "kuhodhi fedha" wanaweza kabisa kusambaratisha UTU Huru wa mtu kwenye jamii, Lazmia SASA Katiba ya nchi, Sheria za nchi, Miiko ya nchi, Maadil na Elimu ya nchi vione ukweli huu na vitamke rasmi kwa kuazmia, kama Taifa kuwapinga na kuwachukulia hatua zote za kuwatokomeza Wapinga UTU wa Taifa, ili kusitiri na kustawisha Utu wa familia, jamii na Taifa kwa ujumla! Nani haoni kwa sasa UTU wa jamii ulivyoshuka na Wapinga UTU (Magugu MTU) walivyoshika Hatamu? Taifa sasa liamke na kutambua kwa undani unapotoka msukumo hasi wa kijamii unaodiriki kupinga kwa hali na mali thamani ya Utu huru kwenye jamii! Hii itatoa mwanga wa kutokufanyia mzaha Azimio Lolote La Utu litakalokuwepo kwenye WAKATI HUSIKA!

6. UTU HURU wa MTU uliokuwa ndio lengo letu la mwaka 1961, haupitwi na wakati, Ulikuwepo, Upo na Utakuwepo wakati wowote atakapokuwepo Mtu na Mazingira yake Tanzania na duniani. Kwa kuwa UTU unajieleleza kupitia kauli, fikra na matendo ya mtu ili kijipamabanisha na mazingira yake, ni hakika basi muoenekano wa nje wa dhana ya Utu utakuwa unabadilika kwa vipindi mbalimbali kama ilivyo kweli kwa mabadiliko ya fikra, kauli , matedo na mabadiko ya mazingira ya Mtu, LAKINI KATU UTU NA THAMNI YAKE KAMWE HAVITABADILIKA NI ULE ULE NA UNAHITAJI UANGALIZI makini kupitia azimio sahihi dhidi ya wapinga Utu wakati wote.

7. Ni wendawazimu kufikiri kuwa Azimio la Utu, utafika wakati likatapitwa na wakati na kutotahitajika kabisa huku magugu Mtu yapo wakati wote katika jamii hiyohiyo. Hiyo itakuwa ni kweli tu wakati mwanadamu atakuwa ametoweka duniani. Kama ilivyo mimea shambani inayoshambuliwa na magugu wakati wote na kuhitaji palizi la mara kwa mara, ndivyo Azimio La Utu litakavyohitajika wakati wote na kila wakati likija na makali yanayolingana na aina ya magugu yaliyopo, kwani magugu nayo pia ni viumbe vinavyopambana na mazingira yake ili kujisitiri na kunedeleza vizazi vyao na kutokukubali kushindwa na kutoweka kirahisi kwenye uso wa dunia.

8. Mchunguze kwa makini MTU mwenye msukomo wa kupinga UTU wake, wa wenzake na wataifa lake. Kwa kuwa utu ndio msingi wa Uhai na maisha ya mtu, katika kuishi yaani "LIVE" na mpinga UTU anapinga KUISHI basi aitwe jina hili hili la "LIVE" lakini, spell it backward and what do you get!? Yes you r right ant humans are not animals they are "LIVE" spelled backwards! Ingawa wengi wanapenda kutumia neno Fisadi, lakini utagundua kuwa jina la hawa watu linakwenda na wakati au vipindi na mazingira yao! Wakiwa urusi watakuwa na jina lao, wakiwa Kenya jina lao, wakiwa Tanzania jina lao wakiwa uingereza jina lao na jina linaweza kubadilika kulingana na nyakati jamii inapojikuta na kupitia!

9. Mjadala huu hautatupatia muafaka wa pamoja ni hakika! Na sifikiri kuwa ndio lengo lake. ILA Utafanikiwa kutupembulia Makundi haya mawili muhimu ambayo yako kwenye jamii wakati wote na ambayo KUSIGANA KWAKE ndiko kuna "define" ustawi na maendeleo ya jamii ya Tanzania. Na kiuwkeli kabisa yangetakiwa yawe ndio chimbuko la Vyama Vya Upinzani na michaato muhimu ya kijamii.

10. Ni vema tuwe wakweli kabisa na kuona hatari ya Wapinga UTU wanapozidi kushamiri kama uyoga na kuiteka jamii. Hivyo lazima tuazimie bila kubabaisha na hatua za haraka zichukuliwe na bila mzaha kurejesha UTU WA TAIFA kwenye mikono salama. Tunahitaji Azimio La Utu Huru wa Mtu katika kukabiliana na mazingira yake katika "mtizamo mpya" Kwani ni kweli halipingiki Ili kuipata Tanzania tunayoikusudia!!!

Azimio la Arusha was the right blue print of this nation. Wanaopinga hilo wana haki kufanya hivyo lakini cha ajabu ni kwamba kila ukiwasikia wakitoa hoja zao juu ya jinsi gani tumepotea kama nchi - kiuchumi, kiutawala na kijamii, wanajisahau kwamba mengi ya wanayo ongelea yaliwekewa misingi mizuri ndani ya azimio la arusha. Lakini muhimu zaidi ni kwamba wameamua ku 'work backwards': Wanaanza kwa 'kushambulia' MATOKEO YA SERA kutokana na kuwa na mtazamo na msimamo wao usio yumba kwamba 'development is path-dependent' (njia iliyotumiwa na mataifa tajiri kama marekani, UK n.k ndio njia pekee ya kuweza kuletea maendeleo binadamu), hivyo moja kwa moja wanajikita zaidi katika kukosoa na kutafuta madhambi ya MCHAKATO, na kuhitimisha kwa kukejeli na kutusi NIA YA AZIMIO LA ARUSHA. Kilichoshanganza wengi ni kwamba mtoa mada alikiri mwenyewe kwamba hajalisoma azimio la arusha na hakuona sababu ya kufanya hivyo. Sina uhakika kama yeye ni muumini wa dhana ya 'dont judge a book by its cover' au he has some reservations on that concept.

Vinginevyo Lets Agree to Disagree kwamba since the 'demise' of Azimio La Arusha, nchi yetu imepoteza mwelekeo na itakuwa vigumu sana kwa nchi yetu kuweza kujitambua tena kiutawala, kiuchumi na kijamii. It remains to be seen nini itakuwa source ya 'true emancipation' ya watanzania walio wengi chini ya Sera ya Azimio la Zanzibar, hasa walio vijijini, Azimio ambalo limekuwa likitekelezwa kwa miaka 20 sasa (1992-2012) na kuwa endorsed na wenzetu wanaolipinga Azimio la Arusha ambao in their humble opinion,Hatimaye Tanzania (ya watanzania wengi, hasa vijijini) sasa ipo kwenye njia sahihi ya kujipatia maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Mwisho, ni muhimu tu wakatambua kwamba mambo yafuatayo bado yataendelea kuwa muhimu katika harakati zetu za kutukomboa kiuchumi, kiutawala na kijamii: "ARDHI", "WATU", "SIASA/SERA SAFI", na "UONGOZI BORA".

Unofficially nitatumia nafasi kuelezea sababu za kushindwa kwa Azimio la Arusha.

1./ Tanzania ni jamuhuri. Na Jamuhuri inaongozwa na vitu viwili muhimu. Katiba na sheria za nchi. Hii ni mikataba kati ya wananchi na serikali yao. Azimio la Arusha ni document iliyotumbukizwa lakini haina uhalali wowote wa kisheria. Halmashauri ya TANU iliyopitisha Azimio hili iliwakilisha chama cha kisiasa cha TANU ambao walichaguliwa na wanachama wenye kadi za TANU. Document ya Taifa ni lazima ipitishwe na bunge ambalo limechaguliwa na wananchi wenye sifa za kupiga kura.

Tukumbuke pia kuwa wakati Azimio hili linapita, idadi ya wanachama wa TANU ilikuwa ndogo kuliko idadi ya watanzania. Na hata sasa idadi ya wanachama wa vyama vya siasa ni ndogo kuliko ya watanzania. Hivyo wanasiasa ni lazima wakumbuke kuwa taifa ni kubwa kuliko imani ya vyama vyao.

2./ Pili kurudishwa kwa mfumo wa vyama vingi, kuanza kurudisha katiba na sheria kwa wananchi. Katiba ya nchi na sheria za nchi hazikatazi mtanzania kuvunja baadhi ya kanuni muhimu ya Azimio la Arusha. Kwa mfano mtanzania anaweza kuwa mkurugenzi wa kampuni binafsi na akagombea ubunge kwa kupitia chama chochote cha siasa kisicho na kanuni za Azimio la Arusha.

Hivyo demise ya Azimio la Arusha haitokani na Azimio la Zanzibar. Inatokana na kuwa waliotunga Azimio la Arusha walitegemea chama kushika utamu daima na kusahau kulifanya Azimio hilo sheria ya nchi au extension ya katiba.

3./ Azimio halina walinzi. Nchi kama Iran au North Korea zinye kufuata itikadi zao zina watu walio tayari kutoa damu kulazimisha wengine au kulinda. Watu wengi ambao walisaidiwa na Azimio hili, ndio wao wa kwanza kuli-molest. Huwezi kujenga itikadi ukiwa huna wafuasi.

4./ Kila binadamu ana matamanio yake na hiyo ni haki aliyopewa na muumba wake. Azimio la Arusha linakiuka msingi huu na kufikiri kuwa serikali inaweza au mafundisho ya itikadi ya chama yanaweza kuwafanya binadamu wafikiri sawa sawa. Kilichotakiwa kuwaachia wananchi watimize matamanio yao mazuri bila kuvunja sheria.

5./ Utekelezaji wa mambo mengine ya azimio la Arusha ulikuwa advance kwa watanzania hata kwa mwandisi mkuu wa Azimio hilo. Kama kulikuwa na watanzania 12 wenye elimu ya juu wakati tunapata uhuru, nina uhakika namba haikuwa nzuri miaka ya 70 kusema kuwa tuendeshe viwanda vyetu au mabenki yetu. Kufanya hivyo ilikuwa ni kukataa education na kutumia ignorance.

6./Azimio liliongeza regulations ambazo zinazuia innovation and creativity.

7./ Leadership that bring results is an art form. You have it or you don't, and you don't need Azimio la Arusha to make things better.

Cau

Z10

Just to add to the point. Kweli tulipolitupa azimio la Arusha kule Zanzibar tulisema kuwa nchi yetu sasa ni uwanja wa fisi. Sasa hivi hata hiyo tunayoita Ardhi yetu inakuwa vigumu kuuita ardhi yetu, kwa kuwa inauzwa siku hizi, inawezekana akaja kaburu akasema ni ardhi yake na sisi tukakosa la kusema, siasa safi(sera) naweza kusema in papers tunazo nzuri labda hata kuliko za Marekani, lakini kitekelezaji ni 0 kabisa, ukisikia viongozi wanasema "maisha bora kwa kila mtanzania" utaona kuwa ni fix fix tu,no one is working to that end, kila mtu is working on fattening his bank account, hakuna kitu ambacho serikali inaweza kusema inafanya zaidi ya uendeshaji wa siku hadi siku, Uongozi bora hili siwezi hata kusema we see it day in day out. Sasa hakuna uongozi Tanzania, tuna viongozi lakini hakuna uongozi, hata viongozi wenyewe wanatia shaka kama kweli ni viongozi.

Unless we go back to Azimio la Arusha, unless we go back to the core principles or the main guiding principle of this country, we will still be in mess. Hatuwezi kuendesha nchi bila miiko ya uongozi na bila kuwa na guiding principle yeyote.

Najua mjadala ni mrefu!

Summaries zitatusadia kwani finally we have to postulate AZIMIO LA ARUSHA in a way it fits our modem times and We wish the other side do the same come out with something which YOU think can substitute/compliment the New Azimio!

We have had this discussion when it was Jambo Forums and many more times in Jamii forums, this time We have to produce working document, not mare discussion ... YES We have mjadala kwa Katiba Mpya and here we are starting Mjada kwa Azimio la Arusha JIPYA!!
 
Mkuu hapa ndipo uliponigusa haswaaa. Sababu kubwa ya kuwepo demokrasia ktk nchi ni kuruhusu itikadi nyingine pinzani nafasi sawa ya kuweza kutawala pindi wananchi watakapozichagua. Ni mfumo unao ondoa Udikteta hivyo maadam tulianza na TANU yenye siasa za Ujamaa na Kujitegemea ilitakiwa vyama pinzani vinatokana na upinzani wa kiitikadi hii, badala yake sisi tulifanya upinzani wa WATU wale wasiokubaliana na Nyerere ktk resolutions zilizofikiwa.
Watu kama Kambona waliporudi nchini kuanzisha vyama pinzani na CCM walikuta tayari CCM chenyewe hakifuati siasa za Ujamaa na Kujitegemea, CUF, Chadema na hata TLP vyote hivi vilipingana kutokana na vichwa vya viongozi walioko upande wa pili na mara zote mabadiliko ama misuguano ndani ya chama haikuhusiana na sera au itikadi bali watu wenyewe kutoaminiana.

Hivyo basi. swala langu mimi halipo hata ktk Itikadi ya TANU au CCM kwa kuchukua mlengo wa kushoto, hapana hoja yangu mmi ni kwamba hata ukichukua mrengo wa kushoto au kulia, NIA yetu ni kufanya na kulinda nini? Ukisoma declaration of Independence huwezi kuona kuna Uhafidhina au Usosialist kwa sababu hizi ni nyezo za maono tofauti kufikia NIA ya taifa walilotaka kulijenga. Nasi wakati tunapata Uhuru wetu tulitakiwa kuwa na NIA sio tu ya kujitawala ama kumweka kiongozi mweusi, kufuata siasa za TANU ambao hadi 1967 hawakuwa na siasa zaidi ya kuupata Uhuru wetu. Hatukuwa na dira zaidi ya kuweka malengo ya kuupata Uhuru wetu toka mikononi mwa Wakoloni thats it. sasa from there tunakwenda wapi?.. ndipo Azimio la Arusha lilikuja tupa mwanga huo japokuwa liliambatana na itikadi ya chama ambayo ilitambua nafasi yetu kimataifa na kuorodhesha maadui wetu. How to deal with them hapa ndipo tulitakiwa kutofautiana kiitikadi lakini sio kufuta kabisa DIRA yetu kwa sababu tu Azimio zima halikuwapendeza baadhi ya watu.

Ninachounga mkono mimi ktk Azimio la Arusha ni kwamba lilikuwa na madhumuni, nia na malengo. Kisha likatupa njia gani itakayotuwezesha kufika kule tunakotaka kwenda tofauti kabisa na siasa za vyama vyote nchini ambavyo havitazami WATU bali VITU. Azimio la Arusha linajieleza wazi kwamba nchi hii ni ya WAKULIMA na WAFANYAKAZI hii haina mlengo iwe Ujamaa au Ubepari ni kutambua who we are, na likajieleza wazi serikali italinda maslahi ya watu hawa.

Azimio la Arusha lilitambua maadui wetu kuwa ni umaskini, Ujinga na maradhi na ktk kutambua huko wakatoa resolution ambazo zinapambana na maadui hawa. Sasa tunaweza bishana na maamuzi ya silaha zilizotumika lakini haina maana kuazimia kwamba nchi yetu ni ya wakulima na wafanyakazi, maadui wetu ni umaskini, Ujinga na maradhi ni makosa kwa sababu vipo vitu universal kama haki za binadamu hapo ndipo mnaponiacha hoi. Maana hata waislaam na wakristu wanakubaliana ktk vitu Universal, wanakubaliana ktk kujenga maisha ya hapa dunia na Akhera lakini wanatofautiana ktk itikadi na mbinu za kufikia huko.

Na ndio maana tunarudi nyuma na kusema leo hii hatuiti Umaskini, Ujinga na maradhi kuwa maadui wetu ndio maana tumechukua mfumo wa nchi zilizoendelea ambao hawana maadui hawa na kuzitumia kuendeleza VITU badala ya kutaqmbua kwamba niu WATU wanaoweza kubadilisha mazingira. Matokeo yake tuna umaskini, ujinga na maradhi kuliko hata wakati wa Azimio la Arusha. Hivyo utaweza vipi kupambana na Umaskini ikiwa watu wake ni wajinga na nguvu kazi wenyewe asilimia kubwa wanakumbwa na maradhi.

Utaweza vipi kuibadilisha nchi yetu kuwa ya Technologia ikiwa hatutambui uwezo wa wakuilima wenyewe matumizi ya vifaa hivyo na tutawawezesha vipi hawa watu waweze kuviutumia badala yake tunafikiria kukiwezesha kilimo chenyewe. Utaweza vipi kuzalisha kazi ikiwa hutambui nafasi ya wananchi wako kama wengi ni wajinga na kwa asili ni wafanyakazi sio wafanyabiashara, na kutokana na umaskini na ujinga wao ni muhimu kuwawezesha ktk ujuzi na ufanisi mbele ya uzalishaji wa ajira zenyewe. Yote haya hayana Ujamaa wala Ubepari bali ni kuelewa unataka kulijenga Taifa gani na una rasilimali zipi mkononi kisha vyama vya siasa vinatafuta mbinu za kutumia rasilimali ktk maendeleo ya jamii ili tutoke hata ktk hali ya Umaskini, Ujinga na maradhi.

Leo hii sidhani kama tunakubali umaskini, kinachoaminiwa ni kwamba umaskini wetu ni wa kujitakia kwa sababu mali tunazo, msemo wa Kawawa kwamba Uchumi tunao tumeukalia. Na kwamba umaskini wetu unatokana na uongozi mbaya maana tunayo madini na rasilimali za kutosha kuitwa matajiri.

Nami nasema sii kweli maana Mmasai ni maskini kwa sababu kaamua kuishi maisha ya ufugaji anayojua zaidi maana akiingia ktk biashara wakati hajui michezo yake atafilisika mapema zaidi..Na ndivyo tulivyofanya sisi tumeondoa miiko na maadili yetu kwa kuiga ile ya wale waliokuwa na ujuzi na biashara. Tukaweka mikataba mibovu japokuwa kabla ya mwaka 1992 ilikuwa mwekezaji yeyote anayetaka kuwekeza nchini lazima atoe asilimia 50 au 51 kwa mwananchi. Kwa mgeni hakuweza kuwekeza nchini pasipo Ubia na mwananchi iwe madini au shirika lolote lakini tukaja yaondoa haya yote tukalegeza miiko yetu.

Azimio la Zanzibar likaondoa mambo mengi tu tukaingia kuitafuta MALI kutazama maendleo ya vitu kwa sababu nchi matajiri hawashughuliki na umaskini maana ni asilimia chini ya 10 ktk Utaifa wao wakati sisi hawa maadui tunalala nao tunaamka nao kila siku ya Mungu - hatuwezi kufanikiwa pasipo kutambua sisi ni nani, tunapambana na nini na tuna uwezo gani..Andikeni vitabu vyoote mtakavyo lakini pasipo kujimbabua sisi kwanza mbele ya itikadi halafu tukatazama sayansi na Technologia itaweza vipi kutumika kutusaidia kuondokana na vita hii basi tutaendelea kubishana hadi Kiyama..

I admit your post above is impressive.

I have no doubts that that during the struggles for independences, the intent to fight for freedom was there, crystal and clear. For instance in Tanganyika the common thread was around development levy, number of Tanganyika students in universities, self-rule, land reforms, etc. As such freedom wasn't a partisan issue, and people from various backgrounds were united for common course.

However, as it happened in other African countries, the top leaders of various freedom movements had their own hidden motives: power, greedy, ideology, and status. These motives, some are noble in their outlook, have hijacked our intents. In Africa we fought independence for something else, but as free people, we are subjected to power struggle, greedy, ideology orientation, and status.

For example, in some interviews, Nyerere admitted that he envisioned Ujamaa well before we got independence. Nonetheless, he didn't introduce it during the independent struggles because it was a lightning rod that could have divided TANU. He kept it to himself. However, there were ample signs to suggest that Ujamaa was the path he has chosen for us. Take for example Kivukoni College.

It was the first education institution Nyerere engineered. It was foundered in July 1961, 5 months before independence, and its main objective was to teach left leaning ideology. This example alone refutes the claim that Nyerere took some preemptive actions because we didn't have enough educated personnel. The truth is if somebody has already chosen your path, he or she won't consult you for your opinions.

Taking into consideration the world politics of 50s, and 60s, one could understand why Nyerere was swayed to follow that route. Socialism and communism were winning audience worldwide in large number. Even the liberal and leftists in the West didn't anticipate the triumph of capitalism in late 80s and early 90s. It was inconceivable that the USSR will cease to exist.

Simply put, the triumph of capitalism left Tanzania or for that matter many countries which has spent considerable amount of time denouncing the west unprepared. In Tanzania those who support Ujamaa have everything at their disposal such as school of thought and institutions. But they don't have courage and guts. On other hand those who support the right (capitalism) don't have school of thought, institutions, and ideas. They want to be part of something they don't know.
 
Back
Top Bottom