Azimio La Arusha: Why We Were Dead Wrong!

Azimio La Arusha: Why We Were Dead Wrong!

Nzi,

Watanzania ni wavivu wa kujisomea na kujiendeleza. Mambo mazuri ya Azimio la Arusha yanapatikana katika documents nyingi duniani. Kwanini tusifunue upeo na kuangalia mambo mengine.

Nzi,

Kuhusiana na masuala ya kujitegemea na maendeleo ya walio wengi Azimio isn't a sound guidance. Kumwambia masikini maneno matamu haina kuwa unamsaidia.
Zakumi. Naomba nikuulize, tatizo lako ni nini katika suala la Azimio la Arusha?! Maana naanza kuamini kana kwamba wewe hiyo document, bila kujali yaliyomo humo ndani hutaki kuisikia. Sasa kama unasema mambo mazuri ya azimio yanapatikana katika documents mbalimbali duniani, tatizo ni nini? Hayo mambo mazuri kuwemo katika azimio au azimio kuchukua mambo mazuri kutoka kwenye documents mbalimbali duniani?

Kama msingi wa shida yako upo katika sentensi yangu ya mwisho hapo juu, mimi sioni tatizo lolote kama azimio lilikopi au kuchukua mambo mazuri kutoka kwenye vyanzo mbalimbali. Katika dunia hii ambayo vitu vingi vimeshagundulika na kuandikwa sana, hakuna ubaya wa ku-transfer hiyo knowledge na kui-mould katika mazingira ya nchi husika.

Suala la pili kwenye bluu hapo juu: kama azimio sio sound guidance katika masuala hayo, basi tujadili namna gani ya kuboresha kwa sababu angalau azimio lili-dare kuzungumzia hayo masuala. Ebu, niambie ni mpango au mkakati gani wa serikali ya sasa unaotilia mkazo hayo masuala seriously? Ni mafanikio yake yakoje?!
Kama suala ni utekeleza mbaya wa hayo yaliyo katika azimio, mkuu hiyo inakuwa ni fundisho, sasa tuangalie namna gani ya kutekeleza kwa uhakika na umakini zaidi hayo masuala.

Lakini tukiwa tunakandia azimio bila kuwianisha na "maazimio" yanayotumiwa sasa na taifa, pamoja na mafanikio yake, tutakuwa tunapiga kelele. Kandia huku ukionyesha azimio mbadala limefanikiwa vipi!!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Willie,

Kwa yale niliyonayo Azimio la Arusha lilikuja kwa sababu za kisiasa. Lakini kwa mtanzania yoyote mwenye upeo mzuri na akili timamu hawezi kukaa na kulitetea Azimio hilo.

Tanganyika ilipokuwa inapigania uhuru, kulikuwa na mambo mengi ambayo TANU ilitoa ahadi kuyafanya mara baada ya kupata uhuru. Lakini mambo hayo yaliitaji pesa na viongozi wa TANU walikuwa hawajui kuendesha nchi wala bajeti.

Uhuru ulipopatikana, wananchi wakaanza kusubiri kutimiziwa ahadi zao. Lakini kutokana na uhaba wa pesa, TANU ilikuwa nyuma kutekeleza ahadi hizo. Lakini wakati huo huo TANU inashindwa kutimiza ahadi zake, viongozi wa juu walikuwa wanaishi maisha ya kifahari kama wakoloni.

Hivyo TANU kurudisha umaarufu wake kama ule uliopata wakati wa uhuru ilihamua kutangaza Azimio hili. Na vilevile hili serikali ya TANU ipate pesa ya kutimiza ahadi zake, ulihamua kutaifisha mali za wawekezaji. Mfano huu uliigwa kutoka nchi kama Misri iliyoweza kutaifisha Suez Canal hili kujiongezea mapato yake. Hivyo hakuna jipya ambalo Azimio la Arusha lilileta.

Kwenye vipengere vya haki za binadamu, hizo ni haki zilizopo kwenye Tangazo la umoja wa mataifa kuhusu haki za binadamu. Viongozi wa TANU hawakutoa chochote kipya zaidi ya ku-copy and paste.

Na wameshindwa vibaya kwenye haki hizo. Azimio linatoa haki ya kutoa mawazo. Haki za kumiliki mali. Haki ya kushiriki kwenye shughuli za kisiasa. Wakati huo huo viongozi waliotunga Azimio hilo walilazimisha watu kuhamia kwenye vijiji vya Ujamaa bila mapenzi yao na kupoteza mali zao.

Tukurudi kwenye mafanikio ya Azimio la Arusha. Ukweli data zote zinaonyesha kuwa halikuwa na mafanikio yoyote yale. Rasimali zilizotaifishwa kama vile mashamba ya mkonge yalishindwa kuendelea.

Mfanikio ya elimu, afya, na maji hayakuletwa na Azimio la Arusha. Ni mipango ya World Bank, IMF, and donor countries. Hata nchi ambazo hazikuwa na Azimio la Arusha zilipata misaada hiyo. Mojawapo Zambia.

Kuhusiana na viwanda vilivyomilikiwa na serikali, vilevile ni mipangoa ya World Bank, IMF, and donor countries. Zaire, Zambia, Kenya n.k zilikuwa na viwanda vinavyomilikiwa na serikali.

Azimio la Arusha ni beneficiary tu wa siasa za kidunia zilizokuwepo miaka ya 60, 70, mwanzoni mwa 80. Na bila kuwepo siasa hizi za kiduani, Azimio la Arusha lisingeweza kuendesha hata kiwanda cha miswaki ya vijiti. Na nashangaa msomi kama Shivji anatoa mfano wa kiwanda cha Urafiki kuonyesha mafanikio ya Azimio la Arusha. Wachina walijenga kiwanda hicho kueneza siasa zao za mambo ya nje. Na matokeo yake wamepata kiti katika baraza la umoja wa mataifa na kura ya veto.

Ni muhimu ukatenganisha NIA, MCHAKATO na MATOKEO when it comes to discussing success and failures za Azimio la Arusha. Katika hoja zako, aidha kwa makusudi au bahati mbaya, umejikita zaidi kwenye MATOKEO huku ukigusia gusia kidogo MCHAKATO. NIA ni suala ambalo haujaligusa kabisa, hivyo kukosesha uzito hoja zako kwanini azimio la arusha was a failure. Kaka yangu William Malecela pia ni victim wa mapungufu haya. Inawezekana hoja zenu zingekubaliwa na wadau wengi humu lakini mnapoanguka ni pale mnapodharau "NIA".
 
Upo sahihi kabisa lakini kwa bahati mbaya sana, nchi yetu ilikuwa inaongozwa na katiba ya CCM kama ndio katiba ya nchi kwa miaka mingi sana mpaka umma/upinzani ulipoanza kuamka. Katiba ya nchi ilikuwa inapuuzwa. isitoshe, Tanzania ilikuwa haina katiba kwa kipindi cha miaka 12 i.e 1964 - 1977, katika kipindi hiki, tulikuwa na katiba ya mpito. Na hata hiyo katiba ya 1977 mara nyingi sana ilikuwa haifuatwi na kuheshimiwa kama katiba katiba ya CCM.

Mchambuzi,

Wakati umefika tubadili haya mambo. Hiko siku tunachagua CUF au CHADEMA kuongoza nchi, na wao wataanza kuchukua manifestos yao na kuyafanya yawe juu zaidi ya katiba au sheria za nchi kwa sababu ya maneno matamu.
 
Ndahani,

You quote my post, but you don't take time to read it. If you had read it, you would have found that I didn't mention Nyerere or his descendants or disciples.

Brain is a terrible thing to waste. Miaka ya utekelezaji ya hizo siasa za Azimio la Arusha, watanzania mmepoteza muda mwingi kujifunza vitu vya kishambashamba na kushindwa kujenga capabilities za kuendesha nchi. Na haichangazi kwa viongozi wa sasa kushindwa kuendesha nchi. Kwani wakati nchi zingine zinafanya juhudi za kujenga capabilities zao, kazi zenu zilikuwa kuandamana na kukimbiza mwenge.

Zakumi,
Naona wewe ndio hujanielewa. Mimi nakubaliana kabisa na wewe kwamba zama zetu hatupo na Tanu wala ASP. Na kama tuna nia ya kusonga mbele basi tuyakabili matatizo yetu ya sasa. Kinachosumbua akili zangu ni mada yenyewe. Azimio la Arusha inawezekana lilikuwa na makosa. Lakini tumefanya jema gani ambalo leo linaweza kutumika kulihukumu Azimio la Arusha? Tunayofanya yanaonyesha wazi lile azimio lilikuwa la maana sana maana imagine wizi huu na matumizi mabaya ya madaraka na mali ya umma yangeanza enzi hizo, leo hili Taifa lingekuwa wapi?
 
- Living document ni ile Constitution ya USA tu, maana siku zote ina majibu ya maswali magumu ya taifa kila yanapozuka, wanaikimbilia inawapa majibu unajua Why ni kwa sababu ilijikita kwenye Sheria zaidi, kuliko miiiko ya uongozi. A living document inatakwia itoe mwanga panapokuwa giza sio kutoa impossible theories kama za Aazimio la arusha, kwanza haikuweza kufanaya anything muanzilishi wake akiwa hai, sasa hivi kweli kuna aliyetegeema itatusaidia akiwa hayupo?

- I have a lot of respect na Mwalimu, as individual na siku zote ninatenganisha Azimio na yeye kama kiongozi, kwenye maneno ya Azimio la Arusha, hakututendea haki taifa hili na ninasikitika sana kwamba wasomi wanaotakiwa kutusiadia na wao hawana majawabu ya matatizo tuliyonayo sasa wamejikita kujificha kwenye maneno ya Azimio la arusha!

William.
Mutuz,

A living document ya Marekani sio Constitution ila ni Decralation of Independence, lazima ufahamu tunazungumzia vitu gani na pengine ndio maana huelewi uwepo wa Azimio la Aruisha. Azimio lao liliandika kutokana na kuelewa walipotoka, wasichataka na wanataka kuwa Tiafa la aina gani na kulinda nini ktk Utaifa wao. Hivyo, kuwa na constitution haina maana zaidi as a living document ikiwa dunia inabadilika kila mara na sheria mpya zinaongezwa kulingana na mahitaji ktk kulinda azma ya Uhuru wao.

Mkuu wangu wee mshikaji wangu sana lakini sasa naona umechanganyikiwa. Sielewi sababu aidha kutokana na maisha magumu Bongo au unataka kuvuka daraja kuingia upande ulokuwa ukupiga vita. Bongo, mkuu wangu shule na watui wanachukua Phd hapo kwa ugumau wa maisha tu hivyo endelea kuchukua darasa... hahaha! hahaha!! Mimi simung'unyi maneno, sina unafiki wala sipendi mtu anayejifanya ana uchungu sana na Taifa lakini kumbe ndani ya roho yake amejizatiti kutumaliza. Huyu sii Mutuz nimjuaye hata kidogo.

Please be who u are, The Baharia niliyemjua kwa miaka mingi sana usije danganyika na kundi la EL kwa sababu unafikiria he is the next President. He will never be! hilo chukua toka kwangu. Kama wewe hukubaliani na Azimio la Arusha kwa fikra za maslahi yako binafsi hutaelewa nini hasa maana ya Utaifa. Na wale wote wanaopingana na Azimio la Arusha ni wale ktk kundi la Mabauncer yaani wanaojipendekeza kwa matajiri ama watawala kama tulivyowaona enzi za utumwa kina Tiputipu, ama Ukoloni dhidi ya mashujaa wetu kina Mkwawa.

Mtanzania halisi, unaweza kupingana na baadhi ya sheria ktk Azimio hilo lakini huwezi pingana na ukweli mkubwa uloshinikiza kuandikwa kwa Azimio la Arusha na nakuhakikishia kama sii Azimio la Arusha, Tanzania hii isingekuwa huru na amani. Tumefika hapa tulipo kutokana na watu kama nyie mnaopenda sana kupingana na Azimio la Arusha na mmeliongoza Taifa hili kwa miaka 20 sasa lakini hakuna zuri hata moja. Nimeishi Tandale wakati wa Nyerere haikuwa Uwanja wa Fisi na wala hakuna Mtanzania aliyekuwa akilala ktk nyumba za kutengenezwa na makarati ya Plastic, watoto maskini wanaokula masaza wakitifua majalala enzi zile walikuwa vichaa peke yake. Mutuz, nini kimekupata ndugu yangu?
 
I think tatizo halikua Azimio la arusha, tatizo kama kawaida ilikua ni ile process management

Mimi mara nyingi huwa najiangalia kama mtanzania na tabia yetu ya "easy way out" or "easy does it"

Ukichunguza hata ubepari ulipokuja, asilimia kubwa yetu ilikomalia yaliyo rahisi, this could a mindset, vizazi vilivyotangulia au hata genetic... haiwezekani wachagga wajue pesa halafu directly tuwaone wana tamaa na mmakua awe bize kwenye ngoma, ngono na majungu, then tusingizie ujamaa... KAMWE

As always, we tend to put blames on someoen else, and in many cases anakua either mtoto mdogo, marehemu au siyekuwepo

HII MADA NI NZURI, ILA IMEANZA NA BLAME GAME, DEAD END ETC!!! WE COULD USE IT POSITIVELY KAMA MCHAMBUZI NA WENGINE WANAVYOJARIBU KUTUSAIDIA

HATA UNGEKUA UBEPARI NDIYO SERA YA 1967, BADO WATANZANIA TUNGEISHIA KUULAANI, KUUTUKANA NA KUUKASHIFU, WE HAVE THAT CURSE SOMEHOW
Asante mkuu kwa kuweka sawa hii hoja. Hatuna uhalali wa kulilaani Azimio la Arusha kama leo tunalifuja taifa. Why do we think we are better?
 
Zakumi,
Naona wewe ndio hujanielewa. Mimi nakubaliana kabisa na wewe kwamba zama zetu hatupo na Tanu wala ASP. Na kama tuna nia ya kusonga mbele basi tuyakabili matatizo yetu ya sasa. Kinachosumbua akili zangu ni mada yenyewe. Azimio la Arusha inawezekana lilikuwa na makosa. Lakini tumefanya jema gani ambalo leo linaweza kutumika kulihukumu Azimio la Arusha? Tunayofanya yanaonyesha wazi lile azimio lilikuwa la maana sana maana imagine wizi huu na matumizi mabaya ya madaraka na mali ya umma yangeanza enzi hizo, leo hili Taifa lingekuwa wapi?
Ndahani. Mkuu hapo ndipo umegonga penyewe. Sasa Zakumi na W. J. Malecela waje wajibu hoja.
 
Last edited by a moderator:
Zakumi. Naomba nikuulize, tatizo lako ni nini katika suala la Azimio la Arusha?! Maana naanza kuamini kana kwamba wewe hiyo document, bila kujali yaliyomo humo ndani hutaki kuisikia. Sasa kama unasema mambo mazuri ya azimio yanapatikana katika documents mbalimbali duniani, tatizo ni nini? Hayo mambo mazuri kuwemo katika azimio au azimio kuchukua mambo mazuri kutoka kwenye documents mbalimbali duniani?

Kama msingi wa shida yako upo katika sentensi yangu ya mwisho hapo juu, mimi sioni tatizo lolote kama azimio lilikopi au kuchukua mambo mazuri kutoka kwenye vyanzo mbalimbali. Katika dunia hii ambayo vitu vingi vimeshagundulika na kuandikwa sana, hakuna ubaya wa ku-transfer hiyo knowledge na kui-mould katika mazingira ya nchi husika.

Suala la pili kwenye bluu hapo juu: kama azimio sio sound guidance katika masuala hayo, basi tujadili namna gani ya kuboresha kwa sababu angalau azimio lili-dare kuzungumzia hayo masuala. Ebu, niambie ni mpango au mkakati gani wa serikali ya sasa unaotilia mkazo hayo masuala seriously? Ni mafanikio yake yakoje?!
Kama suala ni utekeleza mbaya wa hayo yaliyo katika azimio, mkuu hiyo inakuwa ni fundisho, sasa tuangalie namna gani ya kutekeleza kwa uhakika na umakini zaidi hayo masuala.

Lakini tukiwa tunakandia azimio bila kuwianisha na "maazimio" yanayotumiwa sasa na taifa, pamoja na mafanikio yake, tutakuwa tunapiga kelele. Kandia huku ukionyesha azimio mbadala limefanikiwa vipi!!

Kwanza ni lazima tuamini kuwa the best of the country is ahead of us. Siku zote kizazi kilichopo kinajaribu ku-shape maisha ya kizazi kinachokuja. Lakini siku zote kizazi kipya kinachagua maisha yake.

Chukua mfano wa Azimio la Uhuru wa Marekani na Katiba yao. Katika documents hizo mbili hakuna sehemu inayosema Marekani ni nchi ya wakulima. Na hakuna sehemu inayosema Marekani ifanye juhudi kuwa nchi ya viwanda au kusaidia wengi vijijini.

Azimio la Arusha is so specific kana kwamba Tanzania itakuwa nchi ya wakulima na wafanyakazi milele. Je mfuga nyuki au ng'ombe sio mtanzania. Je mvuvi, mfanyabiashara sio watanzania. Je watunzi wa vitabu, wasanii sio watanzania?

Watanzania wanahama vijijini na hatuwezi kuzuia mass migration. Azimio linafikiri kuwa uti wa mgongo ni kilimo, ukweli wa mambo sekta ya utalii na madini zinazidi sekta ya kilimo.

Kuhusu mbadala wa Azimio la Arusha, ukweli wa mambo Tanzania ni nchi ya vyamba vingi. Utawala wa kikatiba na kisheria ndio mwelekeo uliobaki.
 
Zakumi,
Naona wewe ndio hujanielewa. Mimi nakubaliana kabisa na wewe kwamba zama zetu hatupo na Tanu wala ASP. Na kama tuna nia ya kusonga mbele basi tuyakabili matatizo yetu ya sasa. Kinachosumbua akili zangu ni mada yenyewe. Azimio la Arusha inawezekana lilikuwa na makosa. Lakini tumefanya jema gani ambalo leo linaweza kutumika kulihukumu Azimio la Arusha? Tunayofanya yanaonyesha wazi lile azimio lilikuwa la maana sana maana imagine wizi huu na matumizi mabaya ya madaraka na mali ya umma yangeanza enzi hizo, leo hili Taifa lingekuwa wapi?

Ndahani,

Matatizo yetu ya sasa hayatokani na Azimio la Arusha. Matatizo yetu yanatokana kuwa kwa miaka mingi hatujafuata utawala wa sheria. Na kuthibitisha maneno yangu nenda kwenye magereza. Wafungwa wengi ni wezi wa kuku.

Wakati wa harakati za uchaguzi wa 1995, tuliambiwa kuwa Lowassa mwizi. Kama ni mwizi kwanini aliachiwa kuwa mbunge au waziri? Wizi wake unajulikana pale alipotaka kuwa rais wa nchi.

Tume ya Warioba ilifanya kazi nzuri. Je matokeo yake yalikuwa ni nini? Walisema watazuia rushwa kisayansi. Matokeo mzuiaji rushwa kisayansi naye ana kashfa ya wizi.
 
Kwanza ni lazima tuamini kuwa the best of the country is ahead of us. Siku zote kizazi kilichopo kinajaribu ku-shape maisha ya kizazi kinachokuja. Lakini siku zote kizazi kipya kinachagua maisha yake.

Chukua mfano wa Azimio la Uhuru wa Marekani na Katiba yao. Katika documents hizo mbili hakuna sehemu inayosema Marekani ni nchi ya wakulima. Na hakuna sehemu inayosema Marekani ifanye juhudi kuwa nchi ya viwanda au kusaidia wengi vijijini.

Azimio la Arusha is so specific kana kwamba Tanzania itakuwa nchi ya wakulima na wafanyakazi milele. Je mfuga nyuki au ng'ombe sio mtanzania. Je mvuvi, mfanyabiashara sio watanzania. Je watunzi wa vitabu, wasanii sio watanzania?

Watanzania wanahama vijijini na hatuwezi kuzuia mass migration. Azimio linafikiri kuwa uti wa mgongo ni kilimo, ukweli wa mambo sekta ya utalii na madini zinazidi sekta ya kilimo.

Kuhusu mbadala wa Azimio la Arusha, ukweli wa mambo Tanzania ni nchi ya vyamba vingi. Utawala wa kikatiba na kisheria ndio mwelekeo uliobaki.
Mkuu wangu Marekani ni Marekani wao walipitia historia ya mambo tofauti kabisa na sisi, kwanza walikuwa wazungu waingereza waliotawaliwa na Malkia na hawakupenda kuwa chini ya Malkia na utawala wake. Pengine naweza kusema kama leo sisi tukiazimia kuiangusha CCM na utawala wake tukaandika Azimio jipya dhidi ya CCM, ndivyo unaweza linganisha kwa uchache na Decralation of Independence. Again, kila nchi ina WATU na MAZINGIRA tofauti hivyo wanakabiriana na maswala tofauti na hata kuweka malengo tofauti.

Tatizo lenu mnachanga sana vitu, Marekani halikuwa Taifa la kilimo ama wafanyakazi hata siku moja isipokuwa ni watu waliovamia nchi ya watu na wakaazimia kuifanya nchi yao waliyopewa na Mungu na kuanza kuinvest ktk nyanja tofauti..Uhalali wa Marekani hauwezi kulinganishwa na Uhalali wa wananchi wazawa wa Tanzania kudai Uhuru wao na kuweka malengo yao iwe sawa na yale ya Marekani, Pleaseeee..

Na pengine nikwambie tu kwamba hata Azimio letu haliwezi kufanana na Kenya ambao hadi leo Wakikuyu wanadai ni nchi yao, hivyo maadam tulipopata Uhuru tulijua wazi nguvu kubwa ya kuupata Uhuru wetu ilitokana na WAKULIMA na WAFANYAKAZI na hao ndio watakuwa wamiliki wa Taifa letu haijalishi mabadiliko yoyote ya mbele. Leo hii hao Wakulima na wafanyakazi wakiwa ndio wafanyabiashara haiwezi kuondoa maana ya kusudio la Ujenzi wa Taifa hili kulingana na mazingira tulokuwa nayo. Hata Bakhresa alianza kama fundi mshona viatu na aliweka malengo yake kufikia hapa alipo - haibadilishi who he was..
 
----Ninaomba kusema tena na tena, we were Dead wrong na idea za Azimio La Arusha, infact ndilo limetufikisha hapa tulipo yaani tumekwama hili taifa, hatujui tunakokwenda wala tulikotoka. Halafu wanatokea wasomi wanaodai eti turudi kwenye Azimio, hilo Azimio limetushinda mwanzoni kwa nini kuna wanaoamini tutaliweza sasa?

Ebu twende hatua kwa hatua Hili azimo "Bovu" Arusha limetufukisha hapa kivipi
  • Assume hakuna hata jambo moja chanya kuhusu Azimio la arusha kitaifa ebu elezea ni vipi azimio la arusha chanzo cha ubovu
  • Then chukulia mfano simple wa Jirani zetu Kenya,Uganda,Rwanda, Burundi. Walikuwa wana maazimio gani kiasi amabcho yametuacha mbali kama ndivyo unavyodhani.? Kwama hatuna tofauti sana na Uganda na kenyank je zaidi yaazimio la arusha nini tatizo.....?

Ukilichmbua azimio la Arusha au kitu chochote jaribu kuangalia Prons and Cons kabla ya kufanya conclusion. Wewe umejikita kwenye mapungufu tu.

.........Recently, nimeona wale wengi walioachwa kwenye uongozi wa juu yaani kwenye mlo, wakililia Azimio, halafu ninachukizwa sana ninapoona media inawapa free lunch hawa waliokosa mlo, sijawahi kuwasikia wakisema Azimio liliwahi kumfunga kiongozi gani wa juu mwizi, sijawasikia wakisema Azimio lilifanya nini cha maaana mpaka wanalilia!

William @ Darcity

Wanaolilia Azimio la arusha wapo wengi Zaidi ya waliochwa kwenye mlo.Mfano Yupo Sabodo Yupo Issa shivji. etc Nasikia Wengine wanakataa mpaka milo ya kuwa wajumbe wa katiba . So usi -generalise . Ukiwasikia watu makini wanaotetea azimi lo la Arusha ni wazi wanasema CCM ubepari ingeweza kuliboresha wa manufa ya taifa na tungekuwa mbali zaidi.

Alafu mkuu hivini kweli hujui hata azimio lilifanya nini au unajaribu kuwa kipofu. ? Nitakupa mfano ukitaka.
 
Kwanza ni lazima tuamini kuwa the best of the country is ahead of us. Siku zote kizazi kilichopo kinajaribu ku-shape maisha ya kizazi kinachokuja. Lakini siku zote kizazi kipya kinachagua maisha yake.

Chukua mfano wa Azimio la Uhuru wa Marekani na Katiba yao. Katika documents hizo mbili hakuna sehemu inayosema Marekani ni nchi ya wakulima. Na hakuna sehemu inayosema Marekani ifanye juhudi kuwa nchi ya viwanda au kusaidia wengi vijijini.

Azimio la Arusha is so specific kana kwamba Tanzania itakuwa nchi ya wakulima na wafanyakazi milele. Je mfuga nyuki au ng'ombe sio mtanzania. Je mvuvi, mfanyabiashara sio watanzania. Je watunzi wa vitabu, wasanii sio watanzania?

Watanzania wanahama vijijini na hatuwezi kuzuia mass migration. Azimio linafikiri kuwa uti wa mgongo ni kilimo, ukweli wa mambo sekta ya utalii na madini zinazidi sekta ya kilimo.

Kuhusu mbadala wa Azimio la Arusha, ukweli wa mambo Tanzania ni nchi ya vyamba vingi. Utawala wa kikatiba na kisheria ndio mwelekeo uliobaki.

Duh! Mkuu Zakumi, naona wewe hutaki kuelewa au huelewi kweli. Mimi sijasema kama azimio halina mapungufu, linalo. Lakini vile vile lina mazuri pia ambayo yanatufaa, ni kiasi cha ku-mould hayo mazuri ili yaweze kuendana na hali ya sasa. Sasa ukiwa unang'ang'ania hoja yako kwa kutumia maneno kama hayo, nakushangaa. Hivi huwezi kuona zaidi ya ulivyoona katika hayo? Vile vile wakati linaandikwa, wafanyakazi na wakulima ndiyo walikuwa uti wa mgongo wa taifa. Wao ndiyo walikuwa walipa kodi na chanzo kikubwa cha mapato; hivyo lengo likawa katika kuhakikisha wanapewa kipaumbele ili waweze kusaidia katika gurudumu la maendeleo. Ila kama azimio lilikuwa so specific, kuna ubaya gani sasa, tukilirekebisha na kuzingatia makundi mbalimbali ya watanzania?

Kwenye suala la pili, mzee hata hilo nalo huelewi? Hivi asimilia kubwa ya watanzania wapo katika sekta gani? Jibu ni kilimo, hivyo azimio lilitilia mkazo katika sekta ambayo watanzania wengi wapo na wanaitegema kwa maisha yao na maendeleo ya taifa kiujumla. Ulitaka liseme madini ndio uti wa mgongo wakati watanzania wengi sio wachimba madini?!
Vile vile tukija katika hali ya sasa, ambapo misingi kama hiyo ya azimio imetupiliwa mbali, hizo sekta ulizozisema (utalii na madini) licha ya kuwa zinaongoza katika pato la taifa, sekta hizo hazijaweza kuleta tija ya moja kwa moja kwa watanzania walio wengi. Wawekezaji wa nje na "wenye mamlaka" ndiyo wananufaika. Si ajabu kuona takwimu zikisema uchumi wa nchi unakuwa, wakati mifuko ya watanzania wengi inazidi kutoboka.
Mkuu tutazunguka na kumaliza dunia yote, mwishowe tutarudi pale pale, kwamba taifa limepoteza dira na mwelekeo toka lilipoamua kulitupilia mbali Azimio la Arusha.
 
Last edited by a moderator:
Zakumi
Watanzania wanahama vijijini na hatuwezi kuzuia mass migration. Azimio linafikiri kuwa uti wa mgongo ni kilimo, ukweli wa mambo sekta ya utalii na madini zinazidi sekta ya kilimo.
Mkuu wangu unaona sasa ulivyopotea. Hizo sekta za Utalii na Madini zinaajiri watu wangapi?..Hivi kweli Utaifa kwako unatokana na pato la nchi hata kama pato hilo ni dogo kiasi gani maadam ndilo linaongoza?... ama unatokana na ukweli kwamba hawa wazawa ni watu wa aina gani. Ikiwa asilimia 80 ya nguvu kazi yetu ni wakulima na wafanyakazi unafikiri wakiwezeshwa hawa watazidiwa na huo Utalii wa wanyama pori na madini ambayo mmeshawakabidhi wazungu hadi yaishe?..

Waarabu kwa asili ni merchant - Wafanyabiashara, sii wakulima na wanaifanya biashara toka enzi za Abraham, hivyo kuwepo mafuta ni sehemu ya ujuzi wao kuweza kutumia rasilimali walizonazo kuendesha biashara hiyo na wamefanikiwa. Leo hii Ukienda Saudia, Dubai au UAE utakuta biashara za kila aina na ndiko asilimia kubwa ya wananchi wake wamejikita japokuwa pato kubwa la Taifa ni mafuta ambayo 35 years ego yalimilikiwa na wageni. Je, hii iliondoa ukweli wao kutambua who they are?
 
Kiukweli sijui sana kuhusu Azimio la Arusha ila ninachojua ni kuwa kwa mujibu wa Mzee Nyerere halikuwa na mawaa kiasi hicho kama ambavyo Willy anataka tuamini. Ninapomsoma Willy napata picha kuwa kuna mambo kaambiwa (in a wrong way) na watu fulani kuwa Azimio lilikuwa si sawa. Ningemwelewa kama aheweka hoja za msingi kama ambavyo Mchambuzi ameainisha, tena kwa upeo sana ni jinsi gani ya kupangua dhana, hoja ama jambo fulani na ukaonekana wa maana kuliko kutumia jazba katika kupingana na jambo ambalo huna utafiti nalo wala data za kukusaidia kuwasilisha hoja yako.

Ni sawa na mshabiki kulalama kuwa mchezaji fulani kapewa 'red card'. Utakapomhoji ni kwa vipi asipewe utasikia akisema, ,ah! Refa kanunuliwa!' Hayo ndio mapungufu ya Willy. Ningependa ajibu na kuleta mada yake kwa namna ambayo Mchambuzi kaainisha, ndipo tuwe na ujasiri wa kuungana nae ama la
 
Duh! Mkuu Zakumi, naona wewe hutaki kuelewa au huelewi kweli. Mimi sijasema kama azimio halina mapungufu, linalo. Lakini vile vile lina mazuri pia ambayo yanatufaa, ni kiasi cha ku-mould hayo mazuri ili yaweze kuendana na hali ya sasa. Sasa ukiwa unang'ang'ania hoja yako kwa kutumia maneno kama hayo, nakushangaa. Hivi huwezi kuona zaidi ya ulivyoona katika hayo? Vile vile wakati linaandikwa, wafanyakazi na wakulima ndiyo walikuwa uti wa mgongo wa taifa. Wao ndiyo walikuwa walipa kodi na chanzo kikubwa cha mapato; hivyo lengo likawa katika kuhakikisha wanapewa kipaumbele ili waweze kusaidia katika gurudumu la maendeleo. Ila kama azimio lilikuwa so specific, kuna ubaya gani sasa, tukilirekebisha na kuzingatia makundi mbalimbali ya watanzania?

Kwenye suala la pili, mzee hata hilo nalo huelewi? Hivi asimilia kubwa ya watanzania wapo katika sekta gani? Jibu ni kilimo, hivyo azimio lilitilia mkazo katika sekta ambayo watanzania wengi wapo na wanaitegema kwa maisha yao na maendeleo ya taifa kiujumla. Ulitaka liseme madini ndio uti wa mgongo wakati watanzania wengi sio wachimba madini?!
Vile vile tukija katika hali ya sasa, ambapo misingi kama hiyo ya azimio imetupiliwa mbali, hizo sekta ulizozisema (utalii na madini) licha ya kuwa zinaongoza katika pato la taifa, sekta hizo hazijaweza kuleta tija ya moja kwa moja kwa watanzania walio wengi. Wawekezaji wa nje na "wenye mamlaka" ndiyo wananufaika. Si ajabu kuona takwimu zikisema uchumi wa nchi unakuwa, wakati mifuko ya watanzania wengi inazidi kutoboka.
Mkuu tutazunguka na kumaliza dunia yote, mwishowe tutarudi pale pale, kwamba taifa limepoteza dira na mwelekeo toka lilipoamua kulitupilia mbali Azimio la Arusha.

Nzi,

Unapotea. Maazimio au katiba zinazoendesha nchi zinatakiwa kuweka misingi ya kumwezesha mtu kuchagua na kuendesha maisha yake bila kuvunja sheria. Hayapo kuchagua professions za watu au professions gani ziongoze nchi.

Kuhusiana na uti wa mgongo, ni zile sekta zenye kuletea taifa kipato kikubwa. Na unaowaita wakulima Tanzania, wengi wao wanajikimu. Na shughuli zao haziwezi kulipa hata gharama za mishahara ya huduma watoto wao wanazopata mashuleni. Hivyo kuwaita wakulima ni kuwapendelea.
 
Upo sahihi kabisa lakini kwa bahati mbaya sana, nchi yetu ilikuwa inaongozwa na katiba ya CCM kama ndio katiba ya nchi kwa miaka mingi sana mpaka umma/upinzani ulipoanza kuamka. Katiba ya nchi ilikuwa inapuuzwa. isitoshe, Tanzania ilikuwa haina katiba kwa kipindi cha miaka 12 i.e 1964 - 1977, katika kipindi hiki, tulikuwa na katiba ya mpito. Na hata hiyo katiba ya 1977 mara nyingi sana ilikuwa haifuatwi na kuheshimiwa kama katiba katiba ya CCM.

- Interesting, unasema katiba ilikuwa inaapuuzwa, ok nani aliyekwua anaipuuuza wakati the author wa katiba na Azimio alikuwepo, tena kwenye power ni kwasababu hata yeye mwenyewe aliona ameunda something that is imaterial, I mean ni vyema kama na wewe unakubali kwamba katiba na Azimio vilikuwa vinapuuzwa hata the author alipokuwepo, sasa tutaliweza leo akiwa hayupo?

William.
 
Ni muhimu ukatenganisha NIA, MCHAKATO na MATOKEO when it comes to discussing success and failures za Azimio la Arusha. Katika hoja zako, aidha kwa makusudi au bahati mbaya, umejikita zaidi kwenye MATOKEO huku ukigusia gusia kidogo MCHAKATO. NIA ni suala ambalo haujaligusa kabisa, hivyo kukosesha uzito hoja zako kwanini azimio la arusha was a failure. Kaka yangu William Malecela pia ni victim wa mapungufu haya. Inawezekana hoja zenu zingekubaliwa na wadau wengi humu lakini mnapoanguka ni pale mnapodharau "NIA".

- Mkuu sana muhimu ni matokeo sio nia, matokeo ndio haya unayaona taifa limekwama sasa nawashangaa sana Viongozi wanaolilia turudi kwenye Azimio tena na huku matokeo yapo tayari, inashangaza sana nia bila technical know how ya kutekeleza nia ni waste na ni unproductive na that is what happened na Azimio!

William.

-
 
Kiukweli sijui sana kuhusu Azimio la Arusha ila ninachojua ni kuwa kwa mujibu wa Mzee Nyerere halikuwa na mawaa kiasi hicho kama ambavyo Willy anataka tuamini. Ninapomsoma Willy napata picha kuwa kuna mambo kaambiwa (in a wrong way) na watu fulani kuwa Azimio lilikuwa si sawa. Ningemwelewa kama aheweka hoja za msingi kama ambavyo Mchambuzi ameainisha, tena kwa upeo sana ni jinsi gani ya kupangua dhana, hoja ama jambo fulani na ukaonekana wa maana kuliko kutumia jazba katika kupingana na jambo ambalo huna utafiti nalo wala data za kukusaidia kuwasilisha hoja yako.

Ni sawa na mshabiki kulalama kuwa mchezaji fulani kapewa 'red card'. Utakapomhoji ni kwa vipi asipewe utasikia akisema, ,ah! Refa kanunuliwa!' Hayo ndio mapungufu ya Willy. Ningependa ajibu na kuleta mada yake kwa namna ambayo Mchambuzi kaainisha, ndipo tuwe na ujasiri wa kuungana nae ama la

- Ni rahisi sana kudai wengine hawana hoja kama huna hoja, ukiwa na hoja unaweka hoja hapa wachambuzi ndio wataamua kama unazo au la, lakini hulazimishi hoja kwa nguvu sana, ninachosema ni kwamba Azimio la Arusha ndilo limetufikisha hapa tulipo yaani tumekwama, sihitaji takwimu wala sensa kujua kwamba viwanda vyetu vilikufa kwa sababu ya uzembe ulioletwa na Azimio, sasa ninawashangaa sana wanaosema Azimio lilikwua sawa ila utekelezaji tu!

- Hapana everything was wrong na Azimio ndio maana lilikuwa haliwezekani kutekelezeka!

William.
 
- Interesting, unasema katiba ilikuwa inaapuuzwa, ok nani aliyekwua anaipuuuza wakati the author wa katiba na Azimio alikuwepo, tena kwenye power ni kwasababu hata yeye mwenyewe aliona ameunda something that is imaterial, I mean ni vyema kama na wewe unakubali kwamba katiba na Azimio vilikuwa vinapuuzwa hata the author alipokuwepo, sasa tutaliweza leo akiwa hayupo?

William.
Mkuu wangu kuna mengi ambayo Thomas Jefferson mwandishi wa Declaration of Independence hakuweza kuyamaliza wala kuyafanya wakati akiwa madarakani au uhai wake, lakini mengi leo yamefikiwa. Slave trade iliekuwepo na weusi hawakuchukuliwa kama raia wa nchi ile lakini maudhui ya Azimio hili bila kupindishwa yamewaweka weusi kuwa katika kundi la Azimio hilo. Hili ni swla la kiimani zaidi na sio technical ila ni kama unavyoamini juu ya YESU ktk utawala wa mbinguni, hapa pia una uzima wako kama mwananchi mzawa kiutawala.

Zile haki zote walizodai Waamerika imepita karne nyingi kuweza kuyafikia lakini muhimu Waamerika hawakupoteza dira wala hawakufikia kudharau Azimio lile na wamefika hapa walipo sii kwa sababu ya miaka mingi ndani ya Uhuru wao isipokuwa waliweka malengo na wanaendelea kuifanya kazi hiyo wakijitambua wao ni Taifa la watu gani. Hii imekuwa sifa kubwa ya Azimio lile na hata nchi kibao zime copy baadhi ya imani zile wakati Jefferson hayupo duniani. Bado tu huelewi?
 
- Interesting, unasema katiba ilikuwa inaapuuzwa, ok nani aliyekwua anaipuuuza wakati the author wa katiba na Azimio alikuwepo, tena kwenye power ni kwasababu hata yeye mwenyewe aliona ameunda something that is imaterial, I mean ni vyema kama na wewe unakubali kwamba katiba na Azimio vilikuwa vinapuuzwa hata the author alipokuwepo, sasa tutaliweza leo akiwa hayupo?

William.
Hakuna anaesema kwamba utawala wa Nyerere haukuwa na mapungufu, lakini sio sahihi kusema Azimio la Arusha halikuwa na mazuri. Hoja ya msingi hapa ya kuijadili ni je, Yepi yalikuwa ni mazuri na yepi yalikuwa na mapungufu when it comes to Azimio La Arusha? More importantly, tukijaribu kujadili separately kabla ya kuyajumuisha masuala matatu - NIA, MCHAKATO na MATOKEO YA SERA YA AZIMIO LA ARUSHA, ili kujenga msingi mzuri wa kutuongoza katika mjadala huu.

Ninaamini kabisa kwamba hivyo ndivyo sote kwa pamoja tutaweza kubaini ni mambo gani bado tunayahitaji na yepi yamepitwa na wakati hivyo tuachane nayo 'kama taifa'.

Kwa mfano, katika suala la 'leadership', binafsi naamini kabisa kuna baadhi ya values na principles ndani ya azimio la arusha ambazo tukiziweka kama terms of reference katika mjadala wa katiba mpya, itatusaidia kupata viongozi ambao ni ethical, patriotic, honest and loyal to their country.
 
Back
Top Bottom