Ubumuntu
JF-Expert Member
- Oct 21, 2010
- 14,345
- 10,885
Nzi,
Watanzania ni wavivu wa kujisomea na kujiendeleza. Mambo mazuri ya Azimio la Arusha yanapatikana katika documents nyingi duniani. Kwanini tusifunue upeo na kuangalia mambo mengine.
Zakumi. Naomba nikuulize, tatizo lako ni nini katika suala la Azimio la Arusha?! Maana naanza kuamini kana kwamba wewe hiyo document, bila kujali yaliyomo humo ndani hutaki kuisikia. Sasa kama unasema mambo mazuri ya azimio yanapatikana katika documents mbalimbali duniani, tatizo ni nini? Hayo mambo mazuri kuwemo katika azimio au azimio kuchukua mambo mazuri kutoka kwenye documents mbalimbali duniani?Nzi,
Kuhusiana na masuala ya kujitegemea na maendeleo ya walio wengi Azimio isn't a sound guidance. Kumwambia masikini maneno matamu haina kuwa unamsaidia.
Kama msingi wa shida yako upo katika sentensi yangu ya mwisho hapo juu, mimi sioni tatizo lolote kama azimio lilikopi au kuchukua mambo mazuri kutoka kwenye vyanzo mbalimbali. Katika dunia hii ambayo vitu vingi vimeshagundulika na kuandikwa sana, hakuna ubaya wa ku-transfer hiyo knowledge na kui-mould katika mazingira ya nchi husika.
Suala la pili kwenye bluu hapo juu: kama azimio sio sound guidance katika masuala hayo, basi tujadili namna gani ya kuboresha kwa sababu angalau azimio lili-dare kuzungumzia hayo masuala. Ebu, niambie ni mpango au mkakati gani wa serikali ya sasa unaotilia mkazo hayo masuala seriously? Ni mafanikio yake yakoje?!
Kama suala ni utekeleza mbaya wa hayo yaliyo katika azimio, mkuu hiyo inakuwa ni fundisho, sasa tuangalie namna gani ya kutekeleza kwa uhakika na umakini zaidi hayo masuala.
Lakini tukiwa tunakandia azimio bila kuwianisha na "maazimio" yanayotumiwa sasa na taifa, pamoja na mafanikio yake, tutakuwa tunapiga kelele. Kandia huku ukionyesha azimio mbadala limefanikiwa vipi!!
Last edited by a moderator: