Mkuu wangu Jasusi...............
Willliam.
Unarudi kwenye tatizo lile lile la kutojali kabisa kujadili and appreciate '
NIA' ya Sera ya Azimio la Arusha, badala yake unazidi kupotea kwani kwako wewe muongozo wa hoja zako ni '
MCHAKATO' na '
MATOKEO'. Kwa mwendo huo, itakuwa ni vigumu sana kwako kuja na Sound Argument iliyo coherent and that is near the Quality and Character ya Azimio la Arusha. Kwa mfano hapa chini unamjibu Jasusi and I quote:
Unasema hujui kwamba wananchi wengi waliliwa na fisi, baada ya kuachwa maporini kutoka kuhamishwa kwenye miji yao ya asili eti kwenda kupelekwa kwa nguvu kuanzisha vijiji vya ujamaa, I mean vipo wapi sasa hivyo vijiji? Hayo yote yamefanywa under false ideology za Azimio la Arusha, look leo Azimio hakuna wala Vijiji hakuna what a waste?
Kaka William, madhara ya tabia yako ya kutopendelea kujisomea/kufanya utafiti zinazidi kujitokeza hapa. Kwa mfano, kama umesoma historia ya afrika mashariki, wakati wa ujenzi wa Reli ya Kisumu – Mombasa, (waingereza) wazungu wengi pamoja na waafrika waliliwa sana na Simba katika nyika ya Voi. Kuna filamu moja by ‘Michael Douglas' inaitwa ‘Ghost of the Darkness', inaelezea vizuri sana nini kilijiri, lakini maudhui yake sio mchakato au matokeo bali NIA. Kwa vile NIA ya waingereza haikuwa kuwalisha Simba wa Porini nyama za binadamu bali kuleta maendeleo ya miundombinu kama kichocheo cha kujenga uchumi imara, suala la watu kupoteza maisha halikupewa uzito wowote zaidi ya kuchukuliwa kwamba ni suala la ‘ajali kazini'. Inashangaza watu kama wewe kuzidi kung'a'ng'ania hoja ya wananchi kuliwa na ‘Fisi'. Hoja kama hii haitakiwi kutoka kwa mtu mwenye upeo mkubwa kama wewe kaka William.
Unaelewa nini ilikuwa ni Nia ya vijiji vya ujamaa? Nia ilikuwa ni kuvifanya vijiji hivi view the basis of a socialist system of production, ultimate aim ikiwa kuifanya Tanganyika liwe taifa linalojitegemea kutokana na nguvu kazi ya wananchi wake, lakini muhimu zaidi katika mazingira ya people-centered development ambayo yanazingatia a Bottom-Up approach to development badala ya Top-Bottom approach.
Kaka William, kama umewahi kutumia muda wako japo kidogo kujosomea historia ya nchi yetu, by the time tunapata uhuru (mwaka 1961), takibran 85% ya Tanganyika ilikuwa ni vijiji. Pia usisahau kwamba nch yetu mpaka leo hii ni moja ya nchi chache sana duniani ambayo imezungukwa na mbuga za wanyama. Hivi una taarifa kwamba mwaka jana Simba alitokea Mbagala Rangi Tatu na kuleta maafa?
Wakoloni walipokuja walikuta mazingira ya Tanganyika ni pori kwa kiasi kikubwa sana. Fahamu tu kwamba hawakujenga miji huko porini na badala yake waliwafuata watanganyika huko huko na kuwatumikisha katika kilimo cha mazao ya biashara. Nadhani unatambua kwamba wakoloni hawakuwa na mkakati wowote wa kuwahamishia watanganyika mijini au kuwajengea industrial centres. Je, katika mazingira ya mwaka 1961, Mwalimu ilitakiwa afanye nini kama njia yaku ‘transform' jamii hizi? Kumbuka kwamba ilikuwa ni miaka sita tu tokea uhuru na nchi ilikuwa haina fedha za kutosha kuwa na options nyingi za kufikishia wananchi huduma, wananchi ambao asilimia 90 walikuwa hawajui kusoma na kuandika, hawana huduma za afya, hawana ajira, na wanaishi mazingira ya porini and in a very sparse manner. Kaka William, nadhani una ufahamu mzuri kwamba nchi yetu hata leo, population yake imetapakaa sana, kwani ni sehemu chache tu ndio zenye concentration kubwa ya watu. Je, ulitegemea Mwalimu afanye nini ili kuwafikishia wananchi huduma muhimu, wananchi ambao walikuwa na kiu ya maendeleo baada ya miaka mingi ya colonial exploitation, wananchi ambao walishapewa ahadi nyingi sana wakati wa harakati za ukombozi? Mwalimu angezitimizaje ahadi za matunda ya uhuru in terms of kuwapatia wananchi
huduma za kijamii pamoja na ajira? Inawezekana una mawazo tofauti juu ya nini Mwalimu angefanya, huu ni wasaa wako kutueleza ili tujue tulikosea wapi na tusonge vipi mbele.
Vinginevyo kwa mtazamo wangu ambao unaweza kuwa finyu – kwa kifupi tu – Njia sahihi ilikuwa kuja na mkakati/sera ambayo ingepelekea watanganyika kuishi kwa pamoja na kwa wingi katika maeneo kadhaa ili iwe rahisi kuwafikishia huduma za kijamii pamoja na kuwapatia mazingira ya kujishughulisha kiuchumi ili kujipatia kipato. Kwa maana hii, ilibidi vijiji vya ujamaa vinazishwe kwa wingi ili kuwaondoa wananchi kutoka maeneo ambayo mengi yalikuwa na watu wachache kwani
Economies of Scale zisingewezekana huko walipo. More importantly, a system of production inayokidhi level ya maendeleo ya wakati ule pamoja na mazingira ilibidi iwe devised, so by default it had to be Kilimo. Kumbuka, jamii zote zilianza na Kilimo kwani huo ndio msingi wa kukupelekea kwenye Mapinduzi ya Viwanda. Ukipunguza uvivu wa kufanya utafiti utalibaini hilo mapema sana.
Unasema umulike madhambi yanayofanywa toka Azimio liuliwe kule Zanzibar, lakini husemi kwamba madhambi against Azimio yalianzia the very Awamu ya kwanza iliyotuletea hilo janga la taifa, Viongozi walioliunga mkono waliruhusiwa kuiba as much they wanted bila kuulizwa, lakini waliolipinga wakasingiziwa majungu mengi, ukiona nyumba ina matatizo muhimu ni kwenda kuchungulia msingi wake, utakuta matatizo yalipoanzia, ukweli ni kwamba Azimio wa s a myth, na infact it was a complete lie nido maana halikuwa na njia zaidi tu ya kufa!
If one reads between the lines, atabaini kwa upesi tu kwamba inaonyesha ‘inside information' kuhusu viongozi Fulani Fulani
kuruhusiwa kuiba mali ya umma wakati wa Ujamaa. Kwa vile sisi hatuna hizo taarifa na hapa JF We Dare to Speak Openly, please speak up ili hoja yako iache kupepesuka na badala yake iwe na mashiko.
Kuhusu hoja yako juu ya Kifo cha Azimio la Arusha, nakushauri jaribu kufanya utafiti japo kidogo kuhusu
internal and external factors zilizopelekea kifo chake kwani kwa haraka sana utagundua kwamba, ni kweli partially ilikuwa ni poor implementation ya sera lakini kwa kiasi kikubwa sana ilitokana na juhudi za makusudi on part of viongozi waliopewa dhamana ya kulitekeleza kum ‘black mail' Mwalimu. Viongozi wengi walikuwa wanashirikiana na wahindi pamoja na mabepari wa nje kuharibu uchumi wa nchi yetu, na wengi wa hawa ndio waliopewa dhamana kusimamia mashirika ya umma. Kama William, unafahamu kwamba nchi yetu ina rasilimali nyingi sana na wazungu walikuwa wanatafuta kila njia ya kuhakikisha Ujamaa haufanyi kazi ili waweze pata nafasi ya kuja kutufilisi kupitia ubepari chni ya soko huria holela lisilojali maslahi ya Watanzania, jambo ambalo sasa wamefanikiwa chini ya Structural Adjustment Policies na Azimio la Zanzibar.
Hivi nikuulize - Kwanini Ujamaa wa Sweden ulifanikiwa? Tusidanganyake kwamba Ujamaa hauwezekani. Ujamaa unawezekana, hivyo Azimio la Arusha bado lina nafasi katika Tanzania yetu ya leo, lakini linahitaji kufanyiwa marekebisho. Kwa mtazamo wangu, huo ndio uwe msingi wa mjadala wetu – kubaini success and failures za Azimio la Arusha, iwapo kweli tuna nia nzuri na taifa letu changa.
Kama dira ya taifa haikuwepo toka awamu ya kwanza, haiwezi kuwa ajabu kama haipo leo, wizi haukuanza leo umeanzia awamu ya kwanza, we were here, mpaka siku hili taifa kwa pamoja tutakapo kubali kwamba Azimio na maazimio mengi ya awamu ya kwanza ndio yametufikisha hapa tumekwama, ndio tutaanza kusonga mbele, maana taifa lisilojua linakotoka, haliwezi kujua linapokweda!
Kwa kweli inasikitisha kuona kwamba, licha ya wadau wengi hapa kujaribu kukuelezea jinsi gani taifa letu lilikuwa na dira huko nyuma, wewe bado unazidi kupingana na hilo. Lakini ukiulizwa je, dira ya sasa ni nini? Majibu hauna zaidi ya kuleta hoja zinazoelwa juu ya ubepari na utawala wa kisheria. Na ni nani anaesema kwamba wizi unaweza kudhibitiwa kwa asilimia mia moja? Hakuna nchi inayoweza kuzuia hilo, lakini nchi makini zinaweza kuja na leadership code na mambo kama hayo kupunguza tatizo husika. Na hivyo ndivyo alivyofanya Mwalimu chini ya Azimio La Arusha. Leo hii we are facing a major social evil – UFISADI, and this is a by-product ya hatua ya kuachana na azimio la arusha. Sidhani kama utapingana na hili. Azimio la Arusha served as an ‘orbit' ya kisiasa, kijamii na kiuchumi; Chini ya Azimio la Arusha, na katika mazingira ya nchi changa iliyokuwa na umri wa miaka sita tu ya uhuru (1961 – 1967), ajira ndio ilikuwa ni kipato halali kwa kila mtanzania; lakini leo hii chini ya azimio la Zanzibar, equation imepanuliwa na sasa Rushwa na Ubadhirifu pia vimekuwa sehemu halali ya viongozi kujipatia kipato. Hii ndio nature of leadership that we have nurtured chini ya azimio la Zanzibar. Viongozi wameacha kuwa watumishi wa umma, sasa wanashindana kwa utajiri and lifestyle huku wale waliowapa dhamana wakizidi kudidimia.
Tangia mwaka 1995, wanasiasa wote wenye nia ya kuongoza nchi hii hawafanyi hivyo kwa maslahi ya umma bali maslahi binafsi na ushahidi ulio wazi juu ya hili ni jinsi gani wanatumia mamilioni ya pesa kununua wajumbe wa mkutano mkuu wa taifa. Wengi wa hawa wanakamatwa na pesa hizo chafu wakati wa michakato ya kupata mgombea wa Urais kupitia CCM, lakini kwa vile Azimio La Zanzibar linakamata wengi zaidi, masuala kama haya yanapotezewa. Je, hii ndio Tanzania yako ya sasa yenye Dira?