Unarudi kwenye tatizo lile lile la kutojali kabisa kujadili and appreciate
NIA ya Sera ya Azimio la Arusha, badala yake unazidi kupotea kwani kwako wewe muongozo wa hoja zako ni
MCHAKATO na
MATOKEO. Kwa mwendo huo, itakuwa ni vigumu sana kwako kuja na Sound Argument iliyo coherent and that is near the Quality and Character ya Azimio la Arusha. Kwa mfano hapa chini unamjibu Jasusi and I quote:
Kaka William, madhara ya tabia yako ya kutopendelea kujisomea/kufanya utafiti zinazidi kujitokeza hapa. Kwa mfano, kama umesoma historia ya afrika mashariki, wakati wa ujenzi wa Reli ya Kisumu Mombasa, (waingereza) wazungu wengi pamoja na waafrika waliliwa sana na Simba katika nyika ya Voi. Kuna filamu moja by Michael Douglas inaitwa Ghost of the Darkness, inaelezea vizuri sana nini kilijiri, lakini maudhui yake sio mchakato au matokeo bali NIA. Kwa vile NIA ya waingereza haikuwa kuwalisha Simba wa Porini nyama za binadamu bali kuleta maendeleo ya miundombinu kama kichocheo cha kujenga uchumi imara, suala la watu kupoteza maisha halikupewa uzito wowote zaidi ya kuchukuliwa kwamba ni suala la ajali kazini. Inashangaza watu kama wewe kuzidi kungangania hoja ya wananchi kuliwa na Fisi. Hoja kama hii haitakiwi kutoka kwa mtu mwenye upeo mkubwa kama wewe kaka William.
Unaelewa nini ilikuwa ni Nia ya vijiji vya ujamaa? Nia ilikuwa ni kuvifanya vijiji hivi view the basis of a socialist system of production, ultimate aim ikiwa kuifanya Tanganyika liwe taifa linalojitegemea kutokana na nguvu kazi ya wananchi wake, lakini muhimu zaidi katika mazingira ya people-centered development ambayo yanazingatia a Bottom-Up approach to development badala ya Top-Bottom approach.
Kaka William, kama umewahi kutumia muda wako japo kidogo kujosomea historia ya nchi yetu, by the time tunapata uhuru (mwaka 1961), takibran 85% ya Tanganyika ilikuwa ni vijiji. Pia usisahau kwamba nch yetu mpaka leo hii ni moja ya nchi chache sana duniani ambayo imezungukwa na mbuga za wanyama. Hivi una taarifa kwamba mwaka jana Simba alitokea Mbagala Rangi Tatu na kuleta maafa?
Wakoloni walipokuja walikuta mazingira ya Tanganyika ni pori kwa kiasi kikubwa sana. Fahamu tu kwamba hawakujenga miji huko porini na badala yake waliwafuata watanganyika huko huko na kuwatumikisha katika kilimo cha mazao ya biashara. Nadhani unatambua kwamba wakoloni hawakuwa na mkakati wowote wa kuwahamishia watanganyika mijini au kuwajengea industrial centres. Je, katika mazingira ya mwaka 1961, Mwalimu ilitakiwa afanye nini kama njia yaku transform jamii hizi? Kumbuka kwamba ilikuwa ni miaka sita tu tokea uhuru na nchi ilikuwa haina fedha za kutosha kuwa na options nyingi za kufikishia wananchi huduma, wananchi ambao asilimia 90 walikuwa hawajui kusoma na kuandika, hawana huduma za afya, hawana ajira, na wanaishi mazingira ya porini and in a very sparse manner. Kaka William, nadhani una ufahamu mzuri kwamba nchi yetu hata leo, population yake imetapakaa sana, kwani ni sehemu chache tu ndio zenye concentration kubwa ya watu. Je, ulitegemea Mwalimu afanye nini ili kuwafikishia wananchi huduma muhimu, wananchi ambao walikuwa na kiu ya maendeleo baada ya miaka mingi ya colonial exploitation, wananchi ambao walishapewa ahadi nyingi sana wakati wa harakati za ukombozi? Mwalimu angezitimizaje ahadi za matunda ya uhuru in terms of kuwapatia wananchi
huduma za kijamii pamoja na ajira? Inawezekana una mawazo tofauti juu ya nini Mwalimu angefanya, huu ni wasaa wako kutueleza ili tujue tulikosea wapi na tusonge vipi mbele.
Vinginevyo kwa mtazamo wangu ambao unaweza kuwa finyu kwa kifupi tu Njia sahihi ilikuwa kuja na mkakati/sera ambayo ingepelekea watanganyika kuishi kwa pamoja na kwa wingi katika maeneo kadhaa ili iwe rahisi kuwafikishia huduma za kijamii pamoja na kuwapatia mazingira ya kujishughulisha kiuchumi ili kujipatia kipato. Kwa maana hii, ilibidi vijiji vya ujamaa vinazishwe kwa wingi ili kuwaondoa wananchi kutoka maeneo ambayo mengi yalikuwa na watu wachache kwani
Economies of Scale zisingewezekana huko walipo. More importantly, a system of production inayokidhi level ya maendeleo ya wakati ule pamoja na mazingira ilibidi iwe devised, so by default it had to be Kilimo. Kumbuka, jamii zote zilianza na Kilimo kwani huo ndio msingi wa kukupelekea kwenye Mapinduzi ya Viwanda. Ukipunguza uvivu wa kufanya utafiti utalibaini hilo mapema sana.
If one reads between the lines, atabaini kwa upesi tu kwamba inaonyesha inside information kuhusu viongozi Fulani Fulani
kuruhusiwa kuiba mali ya umma wakati wa Ujamaa. Kwa vile sisi hatuna hizo taarifa na hapa JF We Dare to Speak Openly, please speak up ili hoja yako iache kupepesuka na badala yake iwe na mashiko.
Kuhusu hoja yako juu ya Kifo cha Azimio la Arusha, nakushauri jaribu kufanya utafiti japo kidogo kuhusu
internal and external factors zilizopelekea kifo chake kwani kwa haraka sana utagundua kwamba, ni kweli partially ilikuwa ni poor implementation ya sera lakini kwa kiasi kikubwa sana ilitokana na juhudi za makusudi on part of viongozi waliopewa dhamana ya kulitekeleza kum black mail Mwalimu. Viongozi wengi walikuwa wanashirikiana na wahindi pamoja na mabepari wa nje kuharibu uchumi wa nchi yetu, na wengi wa hawa ndio waliopewa dhamana kusimamia mashirika ya umma. Kama William, unafahamu kwamba nchi yetu ina rasilimali nyingi sana na wazungu walikuwa wanatafuta kila njia ya kuhakikisha Ujamaa haufanyi kazi ili waweze pata nafasi ya kuja kutufilisi kupitia ubepari chni ya soko huria holela lisilojali maslahi ya Watanzania, jambo ambalo sasa wamefanikiwa chini ya Structural Adjustment Policies na Azimio la Zanzibar.
Hivi nikuulize - Kwanini Ujamaa wa Sweden ulifanikiwa? Tusidanganyake kwamba Ujamaa hauwezekani. Ujamaa unawezekana, hivyo Azimio la Arusha bado lina nafasi katika Tanzania yetu ya leo, lakini linahitaji kufanyiwa marekebisho. Kwa mtazamo wangu, huo ndio uwe msingi wa mjadala wetu kubaini success and failures za Azimio la Arusha, iwapo kweli tuna nia nzuri na taifa letu changa.
Kama dira ya taifa haikuwepo toka awamu ya kwanza, haiwezi kuwa ajabu kama haipo leo, wizi haukuanza leo umeanzia awamu ya kwanza, we were here, mpaka siku hili taifa kwa pamoja tutakapo kubali kwamba Azimio na maazimio mengi ya awamu ya kwanza ndio yametufikisha hapa tumekwama, ndio tutaanza kusonga mbele, maana taifa lisilojua linakotoka, haliwezi kujua linapokweda! /quote]
Kwa kweli inasikitisha kuona kwamba, licha ya wadau wengi hapa kujaribu kukuelezea jinsi gani taifa letu lilikuwa na dira huko nyuma, wewe bado unazidi kupingana na hilo. Lakini ukiulizwa je, dira ya sasa ni nini? Majibu hauna zaidi ya kuleta hoja zinazoelwa juu ya ubepari na utawala wa kisheria. Na ni nani anaesema kwamba wizi unaweza kudhibitiwa kwa asilimia mia moja? Hakuna nchi inayoweza kuzuia hilo, lakini nchi makini zinaweza kuja na leadership code na mambo kama hayo kupunguza tatizo husika. Na hivyo ndivyo alivyofanya Mwalimu chini ya Azimio La Arusha. Leo hii we are facing a major social evil UFISADI, and this is a by-product ya hatua ya kuachana na azimio la arusha. Sidhani kama utapingana na hili. Azimio la Arusha served as an orbit ya kisiasa, kijamii na kiuchumi; Chini ya Azimio la Arusha, na katika mazingira ya nchi changa iliyokuwa na umri wa miaka sita tu ya uhuru (1961 1967), ajira ndio ilikuwa ni kipato halali kwa kila mtanzania; lakini leo hii chini ya azimio la Zanzibar, equation imepanuliwa na sasa Rushwa na Ubadhirifu pia vimekuwa sehemu halali ya viongozi kujipatia kipato. Hii ndio nature of leadership that we have nurtured chini ya azimio la Zanzibar. Viongozi wameacha kuwa watumishi wa umma, sasa wanashindana kwa utajiri and lifestyle huku wale waliowapa dhamana wakizidi kudidimia.
Tangia mwaka 1995, wanasiasa wote wenye nia ya kuongoza nchi hii hawafanyi hivyo kwa maslahi ya umma bali maslahi binafsi na ushahidi ulio wazi juu ya hili ni jinsi gani wanatumia mamilioni ya pesa kununua wajumbe wa mkutano mkuu wa taifa. Wengi wa hawa wanakamatwa na pesa hizo chafu wakati wa michakato ya kupata mgombea wa Urais kupitia CCM, lakini kwa vile Azimio La Zanzibar linakamata wengi zaidi, masuala kama haya yanapotezewa. Je, hii ndio Tanzania yako ya sasa yenye Dira?
Mchambuzi
Mark my words Nostalgia isn't a sound guide to economic and social policies. Premises and variables ambazo zilitumika kutunga Azimio la Arusha hazipo sasa. Hivyo huwezi kurudisha Azimio la Arusha na kutegemea matokeo mazuri.
Kwa bahati nimetembea katika nchi zilizokuwa za kijamaa za ulaya mashariki. Nchi nyingi hizi zinaongeza katika masuala ya rushwa na uzembe kama vile Tanzania. Hiyo tunaweza kuita, post communism syndrome. Hili nchi hizi zirudi katika hali ya kawaida ni lazima zijenge taasisi za kiraia ambazo zitasimamia haki za binadamu, sheria, na uwajibikaji. Inachukua miaka mingi na nguvu nyingi kujenga taasisi hizi.
Tanzania haijajenga au kuziimalisha taasisi hizi. Kwa mfano katiba bado ni hilehile ya chama kimoja. Bunge bado ni rubber stamp. Mahakama bado zinaingiliwa. Kamati kuu ya CCM bado ina sauti.
Kushindwa kwa taasisi hizi kumetufanya watanzania tushindwa mambo mengi. Hivyo hata kama utamfufua Nyerere na kumpa urais na kulirudisha Azimio la Arusha, bado Tanzania inaboronga. Hii ni kwa sababu hatuna taasisi za kiraia zenye ufanisi.
Ndugu Mkandara saa zote anakazania declaration of independence. Ukweli wa mambo kuna taasisi inazozilinda hilo Azimio. Na hizo taasisi zimekuwepo toka mwanzo wa uhuru.
Chukua mfano, makao makuu ya serikali ya Marekani. Makao makuu ya kwanza yalikuwa Philadelphia. Lakini walipohamua kuhamishia Washington DC, walihama mara moja hata kabla majengo kumalizika. Hivyo mji wa Washington DC unakuwa kama alama ya uhuru wao. Wameweza kumadilisha msitu kuwa mji wa nchi yao huru.
Huu ni mwaka wa 40 toka Dodoma itangazwe kuwa makao makuu ya nchi. Marais wote toka Nyerere wameongoza nchi kwa kutumia remote kutoka DSM. Kila mtu anasubiri mpaka Dodoma iwe kama New York ndipo wahamie. Hivyo hakuna maazimio yanayokuja kwa vitendo. Cha kusikitisha hata waNigeria walioiga kutoka kwetu tayari wamehamia Abuja.
Azimio la Arusha linazungumza kuinua maisha vijijini. Ni kazi nyepesi kuwaambia wakulima na watu wasio na uwezo wafanye nini. Lakini kuwawezesha ni kitu kigumu. Inashukua zaidi ya miaka mitano kwa mtu kujijengea nyumba ya maana na kuwa na shamba la kuweza kutoa manufaa. Lakini viongozi wa serikali wanafikiri kuwa katika kipindi cha mwaka mmoja bila matayarisho yoyote mtu anaweza kuhamia kwenye kijiji cha ujamaa na kuwa productive. Hata Pro. Issa Shivji anasema huu ndio mwanzo wa kuua Azimio lenyewe.
Mpaka sasa sijaona kiongozi yoyote aliyepitisha Azimio la Arusha ambaye alijaribu kufanya yale wanavijiji waliyotakiwa kuyafanya. Kwenye makaratasi vitu vinaonekana vyepesi, kuna complexities zake. Na mpaka sasa sijaona watu wanaozungumzia complexities za kuinua maisha kwa kutumia maazimio.
Kuhusiana na Ujamaa wa Sweden. Sweden ni nchi ndogo na highly educated. Wanayo private sector iliyo nzuri sana na Ujamaa wao hupo kwenye huduma za jamii. Watu wanalipa tax kubwa sana hili serikali itoe huduma kwa jamii.
Azimio la Arusha linataka serikali imiliki njia za uzalishaji na litoe huduma za jamii bila watu kulipa tax directly. Kwa nchi kama Tanzania mfumo huu unaifanya nchi iwe ya watu wavivu na kutegemea sana misaada kutoka nje.
Cau
Z10.