Azimio La Arusha: Why We Were Dead Wrong!

Azimio La Arusha: Why We Were Dead Wrong!

Azimio la Arusha was a living document iliyobeba dira na 'definition' ya taifa tulilokuwa tunataka kujenga. Iliweka misingi na taratibu za kiutawala pamoja na mahusiaono ya kijamii. Azimio la Arusha lilibeba 'mipaka' na 'barabara' za kupita ili tupate aina ya taifa tulilotaka.

Kwa mtazamo wangu a living document inaweza kufanyiwa update kutokana na mabaliko ya lazima ambayo yanaigusa jamii husika. Lakini sisi tulilifuta Azimio la Arusha kimoja bila mbadala ya maana! Sasa hivi William unaweza kusema Tanzania ni nchi ya aina? Au tuna-aspire kuwa Taifa gani? Na kama unajua aina ya taifa linalojengwa kwa sasa nini misingi ya ujenzi huo?

Ni rahisi sana kuona Azimio la Arusha si chochote kama hujalisoma kwa makini na kuelewa logic yake. Na kwa bahati mbaya au nzuri sasa hivi tunaishi post-Azimio la Arusha, hivyo tunaweza kutofautisha kabisa pande mbili hizi za shilingi. Kulaumu kwamba hali tuliyonayo imesababishwa na Azimio la Arusha ni dalili ya uelewa mdogo wa Azimio lenyewe. With Azimio la Arusha tusengekuwa tunamumunya maneno kuhusu mawaziri wananen waliovurunda!

Azimio la Arusha lilikuwa linahimiza kutafuta majibu ya matatizo yetu kama nchi from within na sio ku-import solutions! Hakuna nchi iliyoendelea kwa kutegemea wawekezeji huku asilimia kubwa ya population yake ikiwa iko outside the system! CCM ya sasa hawatataka kulisikia Azimio la Arusha kwa sababu wamejipa 'hati miliki' ya nchi. Watalisema vibaya kwa ujumla wake bila kuangalia kipengele kimoja kimoja na kufanya marekebisho pale inapobidi. Wanafaidika moja kwa moja na hii nyumba isiyokuwa na msingi na incase inaanguka tayari wameshajiwekea mpango wa dharura kama kuwa na account visiwa ya Jersey huko Uingereza!.

- Living document ni ile Constitution ya USA tu, maana siku zote ina majibu ya maswali magumu ya taifa kila yanapozuka, wanaikimbilia inawapa majibu unajua Why ni kwa sababu ilijikita kwenye Sheria zaidi, kuliko miiiko ya uongozi. A living document inatakwia itoe mwanga panapokuwa giza sio kutoa impossible theories kama za Aazimio la arusha, kwanza haikuweza kufanaya anything muanzilishi wake akiwa hai, sasa hivi kweli kuna aliyetegeema itatusaidia akiwa hayupo?

- I have a lot of respect na Mwalimu, as individual na siku zote ninatenganisha Azimio na yeye kama kiongozi, kwenye maneno ya Azimio la Arusha, hakututendea haki taifa hili na ninasikitika sana kwamba wasomi wanaotakiwa kutusiadia na wao hawana majawabu ya matatizo tuliyonayo sasa wamejikita kujificha kwenye maneno ya Azimio la arusha!

William.
 
Well, heshima mbele sana JF,

- Ninaomba kusema tena na tena, we were Dead wrong na idea za Azimio La Arusha, infact ndilo limetufikisha hapa tulipo yaani tumekwama hili taifa, hatujui tunakokwenda wala tulikotoka. Halafu wanatokea wasomi wanaodai eti turudi kwenye Azimio, hilo Azimio limetushinda mwanzoni kwa nini kuna wanaoamini tutaliweza sasa?

- Recently, nimeona wale wengi walioachwa kwenye uongozi wa juu yaani kwenye mlo, wakililia Azimio, halafu ninachukizwa sana ninapoona media inawapa free lunch hawa waliokosa mlo, sijawahi kuwasikia wakisema Azimio liliwahi kumfunga kiongozi gani wa juu mwizi, sijawasikia wakisema Azimio lilifanya nini cha maaana mpaka wanalilia!

- Mwalimu, yes was the greatest ever, lakini Mwalimu alikuwa na mapungufu makubwa mawili, hakujua;- !. Uchumi 2. Sheria, hivi vitu viwili Mwalimu simply hakuvijua kama alivijiua basi hakuvitilia maanani, na ndivyo vinavyolitafuna taifa letu sasa akiwa hayupo!

- WA-TANZANIA, KAMA TUNATAKA KUSONGA MBELE NA KIJIREKEBISHA TUACHANE NA MANENO YA AZIMIO LA ARUSHA, KWA SABABU NDILO HASA LIMETURUDISHA NYUMA SANA, LISIRUDI, LIENDE ZAKE, NA TUSILIJADILI MAANA NI SHETANI LILILOTURUDISHA NYUMA SANA, SASA TWENDE MBELE NA UBEPARI NA UTAWALA UNAOHESHIMU SHERIA NDIO THE BEST WAY MBELE!

RESPECT PEOPLE!

Mr. Willie @DSM City!

Naomba soma hapa chini ili uone umuhimu wa azimio la arusha

Shivji: Azimio la Zanzibar liliporomoa maadili ya uongozi

12 April 2010
Gazeti la Mwananchi


NI miaka 43 tangu lilipoanzishwa Azimio la Arusha na mwasisi wa Taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere. Pamoja na misingi iliyowekwa na Azimio hilo kuwa na nia njema kwa maendeleo ya nchi yetu, wapo viongozi walioliona kama kero kwa upande mwengine hata wakafikia hatua ya kubadilisha misingi hiyo na kuanzisha Azimio la Zanzibar.

Katika mahojiano na mwandishi ELIAS MSUYA, Profesa wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere, Issa Shivji anatetea misingi ya Azimio la Arusha na kusema kuwa lilipotoshwa.

Swali: Viongozi wengi wa serikali wanasema kuwa Azimio hilo limekufa kwa sababu halitekelezeki. Hiyo inaonekana hata kwa nchi nyingine duniani kama vile Urusi na China ambazo zimejiingiza kwenye ubepari. Unadhani bado Azimio hilo linalosisitiza siasa za ujamaa na kujitegemea lina nafasi katika kumwendeleza Mtanzania?

Jibu: Ingawa ujio wa sera za uliberali mambo leo katika Afrika kuanzia miaka ya 1980 umedhoofisha sana uwezo wa makundi ya wakulima na wafanyakazi wa kupambana dhidi ya mfumo wa unyonyaji wa kibeberu, bado hakujawa na mfumo mbadala na endelevu ulioweza kuwapa matumaini watu wanyonge ambao ndio wengi.

Watanzania wengi waishio mijini na vijijini wamekata tamaa hasa katika kipindi ambacho siasa ya Ujamaa na Kujitegemea imepuuzwa. Kupuuzwa kwa siasa ya Ujamaa na Kujitegemea kumetokana na upotoshwaji wa makusudi uliofanywa na maadui wa ujamaa wa ndani na nje. Pamoja na upotoshwaji huo ujamaa bado haujashindwa kwa sababu Ujamaa ni imani; imani katika utu wa binadamu.

Hata dhana ya kujitegemea imekuwa ikipotoshwa. Kujitegemea kwa jamii ya watu wanyonge hakuna maana ya kujitosheleza bali ni ile hali ya kutambua na kuamini kwamba ni jukumu la wanyonge wenyewe kubadilisha hali yao kwa kutumia vipaji na rasilimali zao kupanga na kuamua kuhusu hatima yao.

Siamini kwamba Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea haitekelezeki. Kuamini hivyo ni sawa na kuamini kwamba siasa ya ubepari ambayo msingi wake ni unyonyaji inatekelezeka. Ni sawa na kuamini kwamba maendeleo ya wanyonge yataletwa kwa njia ya hisani na ufadhili.

Naamini kwamba Ubepari wa kibeberu ni unyama na unyama ni adui wa utu. Kwa maneno mengine ubepari wa kibeberu ambao ndio unatawala dunia hivi sasa ndio hautekelezeki kwa sababu watu wanaonyonywa na kudhalilishwa huwa na kawaida ya kuasi na kupinga unyonyaji kwa nguvu zao zote. Uasi na mapambano dhidi ya ukoloni katika bara la Afrika viliendeshwa na wanyonge waliokuwa wakipinga unyonyaji, udhalilishaji, ukandamizaji na dhuluma. Kwa hiyo ujamaa hauwezi kufa kama mfumo wa unyonyaji na udhalimu bado upo.

Swali: Kama kweli Mwalimu Nyerere aliyeasisi Azimio la Arusha alilisimamia vizuri, kwanini utekelezaji wake ulikuwa mgumu? Huoni kwamba tukilirudisha tena halitatekelezeka?

Jibu: Kama nilivyosema awali Ujamaa ni imani. Kwa hiyo ujenzi wa ujamaa unahitaji kuendeshwa na watu wanaoamini katika utu na wenye uthubutu wakupambana dhidi ya mfumo wa kinyonyaji. Ujenzi wa Ujamaa si lelemama, ni kazi ngumu na yenye vikwazo vingi. Kwa bahati mbaya viongozi wenye imani katika utu na wenye uthubutu wa kutekeleza sera za maendeleo kwa mujibu wa Azimio la Arusha kwa kiwango cha Mwalimu Nyerere hawakuwa wengi. Wengi wa viongozi wa kisiasa wakati wa uongozi wa Mwalimu walikuwa na imani ndogo katika utu na hawakuwa na uthubutu wa kueleza waziwazi kwamba hawakuamini misingi ya Azimio la Arusha. Ni viongozi wachache sana waliopinga wazi wazi mawazo ya Mwalimu na kuamua kuachia madaraka. Hali hii ilisababisha kazi ya kujenga ujamaa kuwa ngumu.

Azimio la Arusha bado lipo na hivyo kazi inayopaswa kufanyika siyo ya kulirejesha bali kuhuisha mijadala juu ya falsafa na misingi yake. Kazi hii sio ya wanasiasa na wanazuoni peke yao bali ni kazi ya kila Mtanzania anayeamini katika utu na hasa yule anayepinga udhalilishaji, unyonyaji na dhuluma.

Swali: Unakitafsirije kitendo cha wana CCM waliokutana Zanzibar mwaka 1991 na kuanzisha kile kinachoitwa sasa Azimio la Zanzibar?

Jibu: Baada ya kuanzishwa kwa Azimio la Zanzibar, maadili ya viongozi wa umma yameporomoka kutokana na kuondolewa kwa miiko ya uongozi iliyobainishwa katika Azimio la Arusha. Katika kipindi cha utekelezaji wa Azimio la Zanzibar, rasilimali za umma zimekosa mlinzi kutokana na tabia iliyoota mizizi ya baadhi ya watumishi wa umma katika ngazi za kitaifa ya kujilimbikizia mali kwa kutumia nyadhifa zao.

Nyumba za serikali zimeuzwa kwa bei ya kutupa na ubinafsishaji wa mashirika ya umma umegubikwa na kashfa za kifisadi zinazowahusisha watumishi wa umma. Hali hii imesababisha manung'uniko miongoni mwa Watanzania na hivi sasa tunashuhudia migogoro ya kila aina katika jamii yetu. Hata imani ya wananchi katika utendaji wa taasisi za umma imeshuka kiasi cha kuathiri mahusiano baina ya wananchi na serikali yao.

Swali: Kuna taarifa kuwa hadi sasa asilimia 90 ya uchumi wa Watanzania unamilikiwa na wageni, je hayo ndiyo matokeo ya kutelekezwa kwa Azimio la Arusha? Waafrika wafanye nini ili nao wapate uwezo wa kumiliki njia kuu za uchumi?

Jibu: Azimio la Arusha linasisitiza kwamba uchumi wa taifa usimamiwe na dola kwa niaba ya wakulima na wafanyakazi. Hivi sasa inasisitizwa kwamba dola lina jukumu la kuweka mazingira bora ya kuiwezesha sekta binafsi ili iwe injini ya maendeleo.

Kwa bahati mbaya sekta ya kilimo ambayo ndiyo iliyokuwa ikitoa mchango mkubwa katika uchumi wa taifa kwa mda mrefu haijapewa msukumo wala haihesabiwi kuwa ni sehemu ya sekta binafsi inayoweza kuchangia pato la taifa. Matokeo ya mabadiliko haya ya kisera ni kukua kwa sekta za fedha, madini na utalii ambazo ushiriki wa Watanzania ni mdogo.

Swali: Pamoja na kulitelekeza Azimio la Arusha, serikali imekuwa katika jitihada za kufufua kilimo kwa kuanzisha mkakati maalum unaojulikana kama "Kilimo kwanza". Unadhani mkakati huo utafanikiwa nje ya misingi ya Azimio la Arusha?

Jibu: Kama msisitizo utawekwa katika kuhamasisha wakulima wadogo kuzalisha kwa tija, mkakati wa kilimo kwanza utafanikiwa. Kilimo chetu kimeendelea kutegemea wakulima wadogo kwa muda mrefu. Wakulima hawa ndio wamebeba mzigo mkubwa wa uendeshaji wa serikali pamoja na kuzalisha chakula cha kulisha watu waishio mijini. Hata hivyo hali za wakulima zimeendea kuwa mbaya kutokana na mazingira magumu ya kazi ya kilimo. Kwa hiyo walengwa wakuu wa mkakati wa kilimo kwanza wanapaswa kuwa wakulima wadogo. Wakaluma wadogo wanahitaji ulinzi dhidi ya watu wanaovamia ardhi yao, wanahitaji nyenzo za kisasa na masoko na pia huduma za ugani na umwagiliaji. Pia mkakati wa kilimo kwanza utafanikiwa iwapo mkakati wa kuboresha maisha na miundombinu vijijini utabuniwa na kutekelezwa. Wakulima wanaotajwa katika Azimio la Arusha si wakulima wakubwa kutoka nje bali ni watanzania waishio vijijini ambao maisha yao yanategemea kilimo ili kupata chakula na pesa za kubadilisha maisha yao. Vilevile sera ya maendeleo ya viwanda nayo inapashwa kuangaliwa upya ili pembejeo mhimu za kilimo zizalishwe hapa nchini na mazao ya kilimo yasindikwe na kuogezewa thamani

Swali: Tofauti na Azimio la Arusha, mfumo wa soko huria uliopo sasa umesaidia upatikanaji wa bidhaa kwa urahisi. Huoni kwamba tukirudisha Azimio lile kutakuwa na uhaba wa bidhaa na huduma hasa kutokana na kuzibwa kwa nafasi za wawekezaji wa ndani na wa nje?

Jibu: Lengo la Azimio la Arusha ni maendeleo ya watu sio maendeleo ya vitu. Watu wanapaswa kuwa na nyenzo za maendeleo yao. Azimio la Arusha linahimiza kufanya kazi kwa bidii na maarifa ili kuongeza tija katika shughuli za uzalishaji. Azimio la Arusha linasisitiza ujenzi wa uchumi wa kitaifa ambapo wakulima na wafanyakazi wanatoa mchango wao na kuishi kwa jasho lao.

Ujenzi wa ujamaa unalenga kuondoa unyonyaji na kutoa fursa kwa watu wote kufaidi matunda ya jasho lao. Kwa hali iliyopo sasa wingi wa bidhaa madukani hauna maana kama watu wengi hawana uwezo wa kuzinunua bidhaa hizo. Vile vile wingi wa wawawekezaji nao hauna maana ikiwa uwekezaji huo unawaneemesha wachache.
 
- Living document ni ile Constitution ya USA tu, maana siku zote ina majibu ya maswali magumu ya taifa kila yanapozuka, wanaikimbilia inawapa majibu unajua Why ni kwa sababu ilijikita kwenye Sheria zaidi, kuliko miiiko ya uongozi. A living document inatakwia itoe mwanga panapokuwa giza sio kutoa impossible theories kama za Aazimio la arusha, kwanza haikuweza kufanaya anything muanzilishi wake akiwa hai, sasa hivi kweli kuna aliyetegeema itatusaidia akiwa hayupo?

- I have a lot of respect na Mwalimu, as individual na siku zote ninatenganisha Azimio na yeye kama kiongozi, kwenye maneno ya Azimio la Arusha, hakututendea haki taifa hili na ninasikitika sana kwamba wasomi wanaotakiwa kutusiadia na wao hawana majawabu ya matatizo tuliyonayo sasa wamejikita kujificha kwenye maneno ya Azimio la arusha!

William.

Wasomi waikaanga Serikali

* SHIVJI ASHANGAA CCM KUTAKA KUREJESHA AZIMIO LA ARUSHA

Elias Msuya | Mwananchi
01 May 2011


WASOMI na wanasiasa mbalimbali wameilaumu Serikali ya CCM kwa kuua Azimio la Arusha na kuanzisha Azimio la Zanzibar lililoua mwelekeo wa taifa. Wakizungumza katika Kongamano la kujadili Azimio la Arusha lililoandaliwa na Chama cha Sauti ya Vijana cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kufanyika katika chuo hicho jana, wasomi na wanasiasa hao walionyesha nia ya kutaka azimio hilo lirudishwe na kuwa moja ya misingi ya mabadiliko ya Katiba.

Awali akitoa mada kuhusu Azimio la Arusha, Mwenyekiti wa Kigoda cha Kitaaluma cha Mwalimu Nyerere, Profesa Issa Shivji, alisema kuwa dalili za kufa kwa Azimio la Arusha zilianza kujionyesha kabla ya Azimio la Zanzibar. Profesa Shivji alizitaja dalili hizo kuwa ni pamoja na utaifishwaji wa rasilimali za umma, operesheni vijiji iliyotokea mwanzoni mwa miaka ya 1970, vuguvugu la wafanyakazi na hatua ya CCM kushika hatamu. Profesa Shvji ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alisema pamoja na kufa kwa azimio hilo bado mzimu wake utaendelea kusumbua.

"Walijitokeza watu wenye jazba ndani ya chama na kuhoji uhalali wa Serikali kutaifisha hata maduka, vituo vya kuuzia mafuta. Kwa kawaida Serikali haiwezi kumiliki maduka, lakini walitaka kuichanganya tu ili nao wamiliki," alisema Profesa Shivji. Akizungumzia kuhusu CCM kushika hatamu kama hatua mojawapo iliyovunja Azimio la Arusha, Profesa Shivji alisema kuwa chama hicho ndiyo kilichoshika mwongozo huku Bunge likiwa mtendaji tu.

"Chama kiliposhika hatamu, kilikuwa chama dola, Bunge lilikuwa na kazi ya kutekeleza tu, viongozi nao walishika ‘utamu'," alisema.

Kuhusu vyama vya siasa, Profesa Shivji alikumbusha kauli ya Mwalimu Julius Nyerere aliyewahi kusema kuwa angependa nchi iwe na vyama viwili vikubwa vya upinzani vinavyofuata mfumo wa ujamaa, lakini mpaka sasa karibu vyama vyote vinafuata ubepari.

"Hadi sasa hakuna hata chama kimoja kinachofuata ujamaa na kuwajali wananchi, vyama vyote vinafuata mrengo wa kulia. Hata wakipata matatizo wanakimbilia kwenye balozi za nchi za kibepari," alisema.

Kuhusu Azimio la Arusha katika mchakato wa Katiba, Profesa Shivji alisema katiba mpya siyo suluhisho, bali maoni ya wananchi pekee ndiyo yanapaswa kuangaliwa zaidi.

Shivji alitanabaisha: "Katiba mpya siyo mwarobaini au kikombe cha Babu wa Loliondo kinachotibu maradhi yote. Kitu cha muhimu ni mchakato, wananchi watatoa malalamiko yao, manung'uniko kulingana na mahitaji yao."

Akichangia mjadala huo, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alikiri umuhimu wa Azimio la Arusha na kuhimiza vijana kujitokeza na kulirudisha.

"Leo huwezi kuzungumza historia ya nchi yetu bila kutaja Azimio la Arusha
. Kwa kuwa Profesa Shivji amesema kuwa haiwezekanai kulirudisha ila tunaweza kuirejesha misingi yake, basi vijana tujifunge mikanda na kufanya hivyo ili tutoke hapa tulipo," alisema Nnauye.

Hata hivyo, akihitimisha kongamano hilo, Profesa Shivji alimkosoa Nape akihoji kuwa CCM itawezaje kulirudisha Azimio la Arusha wakati ilishindwa kulitetea?

"Sijui kama bado Nape yupo, lakini alizungumzia kuhusu kulirudisha azimio. Ni kweli sasa CCM wafikirie kulirudisha azimio. Lakini watalirudishaje wakati walishindwa kulisimamia? Ni swali tu najiuliza," alisema Profesa Shivji.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku alisahihisha dhana iliyojengeka kuwa kulikuwa na Azimio la Zanzibar akisema, "Hakuna Azimio la Zanzibar, ndiyo maana nikasema fanyeni utafiti, siyo mnasimama hapa chuo kikuu na kusema kuwa kulikuwa na Azimio la Zanzibar. Kile kilikuwa ni kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM kilichofanyika Zanzibar," alisema Butiku.

Alifafanua kuwa kikao hicho kilipokea maombi ya waliokuwa viongozi wa CCM ambao walilalamika kuwa miiko ya Azimio la Arusha ilikuwa inawafanya kuwa ombaomba, ndipo wakaomba masharti yalegezwe.

Hata hivyo, alisema baada ya kuruhusiwa, ndipo matajiri walipopata mwanya wa kujilimbikizia mali.

Butiku alifahamisha kuwa miiko ya Azimio la Arusha ilikuwa migumu mno kuifuata.

"Miiko ya Azimio la Arusha ilikuwa migumu. Nyie tukiwaletea miiko hiyo mtaimudu?" alihoji Butiku.

Naye Balozi Ibrahim Kaduma, aliyewahi kuwa Waziri wakati wa Mwalimu Nyerere, alisisitiza juu ya umuhimu wa maadili ya uongozi kama njia ya kukomesha ufisadi nchini.

Hata hivyo, Kaduma alimkosoa Profesa Shivji katika suala la maadili aliposema kuwa maadili hayafundishwi darasani bali yanaigwa tu.
"Inawezekana kweli miiko ya Azimio la Arusha haikuwa maadili, lakini lengo lake lilikuwa ni kujenga maadili. Kwa hiyo maadili yanafundishika, yakikomaa yanakuwa utamaduni wa nchi. Mmomonyoko wa maadili ndiyo umeleta rushwa, wizi na ufisadi," alisema Kaduma.

Tofauti na makongamano ya kujadili mchakato wa kupata Katiba mpya yanayofanyika katika ukumbi huo na kutawaliwa na vurugu, kongamano hilo lilitawaliwa na utulivu huku watu wakisikiliza hoja kwa makini. Hili ni kongamano la pili kufanyika chuoni hapo siku za hivi karibuni baada ya lile la katiba mpya lililowafanya washiriki kujadili kwa jazba.
 
Mimi naona kwa sababu ya azimio lile wfanyakazi walikuwa waadilifu sana kuliko leo. Maoni yangu ni kwamba lingerekebiswa tu na siyo kufutwa.
Kubinafsisha njia kuu za uchumi ndiyo sababu kubwa ya kufa kwa viwanda vyetu vingi na hii sera ya ubinafsishaji imechangia unataka kusema hata ile siasa ya ujamaa na kujitegemea haifai?
 
- Prof. Shivji ndio wale wale hana hoja hana jipya, toka enzi za Mwalimu kazi yake ni kilalamika tu sijawahi kusikia akitoa hoja za kisasa zinaendana na maisha ya sana, Mwalimu alipokuwepo alikuwa kaimponda sana, sasa amegeuka kwua mtetezi wa siasa zake, ukweli ni kwamba hana jipya!

- Azimio limetufikisha hapa tulipo, lime-create tabaka katika jamii yetu, limetufanya tumekuwa wanafiki wa kutupwa hatuna msimamo, kazi kulia lia tu bila kusema what is the alternative, huwezi kujenga uchumi na miiiko ya uongozi, unajenga uchumi kwa regulate wanaosimamia uchumi. na huwezi ku-regulate uchumi kama huna sheria kali.

- Wa-Tanzania mpaka tutakapokubali kwamba Azimio ndilo limetumaliza ndio tutaanza kufikiria kuendelea, ama sivyo tutakuwa tunazunguka hapa hapa tulipo!

William.
 
- Prof. Shivji ndio wale wale hana hoja hana jipya, toka enzi za Mwalimu kazi yake ni kilalamika tu sijawahi kusikia akitoa hoja za kisasa zinaendana na maisha ya sana, Mwalimu alipokuwepo alikuwa kaimponda sana, sasa amegeuka kwua mtetezi wa siasa zake, ukweli ni kwamba hana jipya!

- Azimio limetufikisha hapa tulipo, lime-create tabaka katika jamii yetu, limetufanya tumekuwa wanafiki wa kutupwa hatuna msimamo, kazi kulia lia tu bila kusema what is the alternative, huwezi kujenga uchumi na miiiko ya uongozi, unajenga uchumi kwa regulate wanaosimamia uchumi. na huwezi ku-regulate uchumi kama huna sheria kali.

- Wa-Tanzania mpaka tutakapokubali kwamba Azimio ndilo limetumaliza ndio tutaanza kufikiria kuendelea, ama sivyo tutakuwa tunazunguka hapa hapa tulipo!

William.

vipi kuhusu Nape Maana nae analihitaji azimio hilo lirudi,unamweka ktk kundi la Prof Shivji?

lakini mwalimu alisema

kaeni chini na mlisome vyema azimio la arusha na mseme wapi panatatizo ili pafanyiwe kazi,cha kushangaza mkakimbila Zanzibar na kuanzisha azimio la zanzibar ambalo liliwapa mwanya wa kugawana kile kilicho anzishwa na azimio la arusha,uchumi ukamilikiwa na wachache,kikundi cha watu kika anza kunyonya waliowengi

sijui kama unayaona hayo mkuu
 
vipi kuhusu Nape Maana nae analihitaji azimio hilo lirudi,unamweka ktk kundi la Prof Shivji?

lakini mwalimu alisema

kaeni chini na mlisome vyema azimio la arusha na mseme wapi panatatizo ili pafanyiwe kazi,cha kushangaza mkakimbila Zanzibar na kuanzisha azimio la zanzibar ambalo liliwapa mwanya wa kugawana kile kilicho anzishwa na azimio la arusha,uchumi ukamilikiwa na wachache,kikundi cha watu kika anza kunyonya waliowengi

sijui kama unayaona hayo mkuu

- Mkuu wangu please with all due respect, naomba tuongelee marekebisho ya katiba mpya sio Azimio la Arusha, tumekwama kwa sababu hatujui sheria, hatujui uchumi tulifikiri Serikali ndio inatakwia kufanya kila kitu, kumbe sio zile zilikua dead theories za Azimio la Arusha, sasa tunatka mapinduzi ili twende wka mbele lazima tucahane na mambo ya kizamani.

William.
 
- Living document ni ile Constitution ya USA tu, maana siku zote ina majibu ya maswali magumu ya taifa kila yanapozuka, wanaikimbilia inawapa majibu unajua Why ni kwa sababu ilijikita kwenye Sheria zaidi, kuliko miiiko ya uongozi. A living document inatakwia itoe mwanga panapokuwa giza sio kutoa impossible theories kama za Aazimio la arusha, kwanza haikuweza kufanaya anything muanzilishi wake akiwa hai, sasa hivi kweli kuna aliyetegeema itatusaidia akiwa hayupo?

- I have a lot of respect na Mwalimu, as individual na siku zote ninatenganisha Azimio na yeye kama kiongozi, kwenye maneno ya Azimio la Arusha, hakututendea haki taifa hili na ninasikitika sana kwamba wasomi wanaotakiwa kutusiadia na wao hawana majawabu ya matatizo tuliyonayo sasa wamejikita kujificha kwenye maneno ya Azimio la arusha!

William.

Kwenye red: Ni wazi huelewi nini maana hasa ya a 'living document', na hapo ndipo pa kuanzia. Tofautisha na 'biblical' document.
 
Mkuu William Malecela,

Unaposema Azimio la Arusha ndio kiini cha matatizo yanayotukabili leo kama taifa, una maana gani hasa, kwani azimio la arusha per se ni pana sana. Ungefunguka kidogo tungeweza pata mjadala mzuri zaidi.

Kamanda, jamaa huwa anchukua maneno bar na kwenye vijiwe na kuleta bila fact wala research

Muulize amelisoma azimio la arusha?? na chanzo ni document au implementation au change of our own policies??
 
William,

Not all the principles of Azimio la Arusha were bad.
Not all principles of Azimio la Arusha were good.

However, most of the principles of AD are outdated and we will be cheating ourselves to go back to Arusha declaration.
The present cries of going back to Arusha declaration are caused by some greedy leaders with insatiable desire for accumulating for themselves.

The present cries for AD is one way of addressing this problem
 
Kwenye red: Ni wazi huelewi nini maana hasa ya a 'living document', na hapo ndipo pa kuanzia. Tofautisha na 'biblical' document.

- Does it matters kama ninajua kwamba Azimio la Arusha ndilo limetudumaza kimaendeleo Tanzania? ha! ha! ha!

William.
 
Kamanda, jamaa huwa anchukua maneno bar na kwenye vijiwe na kuleta bila fact wala research

Muulize amelisoma azimio la arusha?? na chanzo ni document au implementation au change of our own policies??

- sihitaji kusoma anything, ninahitaji kuangalia tu kwa macho yangu na kuamua kwamba Azimio was dead kabla hata halijaanza, wewe soma halafu njoo hapa useme tulifikaje hapa tulipo hili taifa kama sio Azimio lilokufa!

William.
 
Mkuu wangu baharia mbona unaturudisha nyuma kiasi hicho.. Wewe Azimio la Arusha ndilo limekusomesha bure na ukajisifia kwa kumpa sifa zote Nyerere leo unaliponda.. Nyerere hakujuja Uchumi vipi?..Ni Azimnio la Arusha lilojenga reli ya Tazara, Azimio la Arusaha lkililojenga viwanga vya matairi General tyre, UFI, viwanda vya nguo, saruji, nguvu za umeme ukayarudi disco la Mbowe hata siku moja umeme haukukatika, leo unaliponda wakati ndio kwanza tulijenga vitu hivyo tukashindwa kuviendesha sisi wenyewe kama walivyoshindwa China na Russia..

Au mwenzetu una maana tofauti ya Uchumi? maana kuwa na wazo zuri ukashindwa kufanikiwa haina maana hata wazo lenyewe halikuwa na maana. Leo hii umetaka kugombea Ubunge wa EA na ukashindwa je tuseme wewe huna maana tena kwa sababu umeshindwa huko..Tafadhali mkuu wangu Azimio la Arusha lilikuwa na mapungufu yake kimfumo hasa pale tulipochagua serikali kumiliki uchumi lakini haina maana hakuna kitu hicho ktk somo la Uchumi. Asiyejua Uchumi atafanya jambo ambalo halipo ktk somo la Uchumi lakini ukifanya ikashindikana haina maana hujui uchumi..

Na unaposungumzia Sheria ni sheria gani?..ati kwa nini Nyerere aliendelea kuwatumia viongozi wabovu, hivi nikuulize tulikuwa na wasomi wangapi? angembadilisha mzee Malecela akamweka nani ikiwa wote walikuwa wabovu. Wewe hapo ulipo nambie mtu hata mmoja ambaye wewe ulimwoina kingozi mzuri Nyerere angemtumia na hakumtumia. Haya leo hii pamoja na kuwa nao kibao na tumebadilisha mfumo mbona ndio kwanza tunatokomea zaidi shimoni tuna excuse gani?

- Bob with all due respect, mambo ya EALA mambo ya baba hayahusu hapa, siwezi kujadili hoja za taifa kwa kumuongelea baba yako wala wa mtu yoyote humu ni kukosa hoja, wewe na mimi ni watu huru we think for ourseleves, na tuna haki ya kutofautiana sio kwa sababu ni marafiki basi tuwekenae vikwazo kwenye kujadili taifa!

- Azimio limejengea viwanda vingi vibovu visivyo na tija wka taifa, ndio maana imebidi viuzwe tena wka bei poa sana, infact Azimio limejengea nyumba kama za bonde la Msimbazi, mvua ikija na zenyewe zinaondoka, Azimio limenisomesha bure, lakini ukweli ni kwamba hapa Duniani hakuna free lunch, so tunalipia sasa na ndio maana ninasema Azimio limetuletea matatzio makubwa sana kwenye hili taifa nashangaa sana wasomi wanapodai lirudi, hapana hatulihitaji tena lifie huko huko!

- Tuanze upya na utawala wa sheria na uchumi mbele, that is all! hakuna short cut!

William.
 
- sihitaji kusoma anything, ninahitaji kuangalia tu kwa macho yangu na kuamua kwamba Azimio was dead kabla hata halijaanza, wewe soma halafu njoo hapa useme tulifikaje hapa tulipo hili taifa kama sio Azimio lilokufa!

William.


William,

hawa viongozi wetu si walikwenda kule Zanzibar kufuta AD?
na si ndio maana leo kuna viongozi wanautajiri usioelezeka?
wanagawa pesa kama njugu makanisani?
Out of frustration ndio maana watu wanataka kurudi kwenye AD.
Ni Mwenendo wa baadhi ya viongozi wa CCM ndio unachochea mawazo ya kwenda kwenye AD
 
- Tuanze upya na utawala wa sheria na uchumi mbele, that is all! hakuna short cut!

William.
Only and if only, this is possible....!!!!!????

The question is how?

Viongozi wanaingia madarakani kwa njia zisizo halali.

The state machinery protects the interest of the government leaders and not the interests of the state!!
Africans are very funny!!!.
No wonder people are frustrated.
 
- Mkuu wangu please with all due respect, naomba tuongelee marekebisho ya katiba mpya sio Azimio la Arusha, tumekwama kwa sababu hatujui sheria, hatujui uchumi tulifikiri Serikali ndio inatakwia kufanya kila kitu, kumbe sio zile zilikua dead theories za Azimio la Arusha, sasa tunatka mapinduzi ili twende wka mbele lazima tucahane na mambo ya kizamani.

William.

kaka

nachokisema hapa ni kwamba,serikali ilitakiwa kumiliki njia kuu za uchumi,kama ni wawekezaji ilitakiwa kuandaa mazingira ya uwekezaji kama walivyofanya uchina na sio kuuza viwanda vyote na serikali kujitoa ktk umilikaji wa viwanda hivyo

juzi tu nimesikia tena kiwanda cha urafiki kinatakiwa kubinafsishwa,yaani tunazidi kupeleka vyanzo vya uchumi kwa wawekezaji.

nadhani tulitakiwa si kulitupa azimio la arusha bali kufanya marekebisho ktk kile tunachokiona hakifai,tatizo ni kwamba baada ya kuona azimio hilo limeziba mianya ya ulaji tukaliondoa.

nataka uelewe kitu kimoja

hata hiyo katiba mpya kama viongozi hawataichukulia kwa dhamila ya dhati kabisa ya kutaka katiba itakayo jibu dukuduku za wananchi bado haitosaidia,kwani bado itahitaji kupita ktk mikono ya wazarendo wenye nia ya dhati kufanya na kuheshimu maoni ya wananchi

maana tangu awali waziri anayehusika na katiba hakuwa tayari kufanya badaliko haya,je waki amuwa iwe tunaweza kupata kile tunachokitegemea?
 
- sihitaji kusoma anything, ninahitaji kuangalia tu kwa macho yangu na kuamua kwamba Azimio was dead kabla hata halijaanza, wewe soma halafu njoo hapa useme tulifikaje hapa tulipo hili taifa kama sio Azimio lilokufa!

William.

hebu tuambie faida ya azimio la zanzibar tunalo lifanyia kazi sasa hivi?
 
Back
Top Bottom