Aziz Ali wa Gerezani na Mtoni Dar es Salaam

Kadoda,
Wanubi walikuja Tanganyika kwa kuletwa na Wajerumani kama askari.

Ibrahim Hamisi mmoja wa waasisi wa African Association baba yake
aliingia Tanganyika kama askari wa Wajerumani akitokea Daffur.

Wakati wa utoto wangu kulikuwa na Wanubi wengi Gerezani na naikumbuka
famili ya Mzee Johari waliokuwa wakikaa Kirk Street sasa Mtaa wa Lindi.

Hawa wakiishi jirani na nyumba ya Bi. Mluguru biti Mussa mama yake Abdul
Sykes
.

Kulikuwa na Mwalimu Sakina Arab akiishi Mtaa wa Pemba huyu bi. mkubwa
alikuwa Mnubi na allikuwa na kaka yake akiitwa Mustafa.

Mwalimu Sakina alikuwa ni dada wa kuPpnga wa Abdul Sykes na ni mmoja
wa akina mama wa mwanzo kuiunga mkono TANU.

Yeye alikuwa mwalimu Al Jamiatul Islamiyya Muslim School.
Kulikuwa na koo nyingi za Kinubi Chang'ombe, Dar es Salaam na Dodoma.

Katika kitabu cha Abdul Sykes kuna kisa hiki cha Ahmed Adam Mnubi
aliyeishi Mikindani:

''Julius Nyerere, Ali Mwinyi Tambwe na Rajabu Diwani waliwasili
Mikindani kutoka Lindi siku ya Jumamosi.

Kabla ya kuwasili ujumbe huo, kazi kubwa kuliko zote waliyokuwanayo
uongozi wa TANU Mikindani ilikuwa kutafuta mahali pa kumlaza Nyerere.

Walimwendea Ahmed Adam, Mnubi mmoja tajiri na mtu wa makamo,
aliyemiliki nyumba moja ya fahari.

Nyumba hii ilikuwa ya ghorofa moja na ilijengwa kwa mawe na chokaa.
Ahmed Adam aliombwa awe mwenyeji wa Nyerere na ujumbe wake.

Nyumba hii tayari lilikuwa na kisa chake. Ilijengwa na hayati kaka yake
Ahmed Adam baada ya Vita Kuu ya Kwanza.

Kaka yake alikuwa askari wa Kinubi aliyekuwa katika jeshi la Wajerumani.
Huenda alichukuliwa Misri mwishoni mwa mwa karne ya kumi na tisa na
Wajerumani kuja Tanganyika kama mamluki katika jeshi la Wajerumani
wakati wa vita vya Maji Maji.

Baada ya vita alilipwa kiinua mgongo na serikali ya Ujerumani na kwa
kutumia fedha hizo alijenga nyumba hiyo.

Katika Vita Kuu ya Kwanza yeye alipigana katika jeshi la Wajerumani dhidi
ya Waingereza.

Baada ya vita Wajerumani wakiwa wameshindwa vita, Waingereza waliitikadi
nyumba hiyo kama mali ya adui wa himaya ya Kiingereza na kwa hiyo ilibidi
itaifishwe.

Hii ilikuwa ndiyo nyumba pekee iliyokuwa nzuri yenye kumilikiwa na Mwafrika
na kwa ajili hii haikuweza kukosa kuhusudika.

Utawala wa Waingereza ulikuwa katika taratibu ya kuitaifisha nyumba hiyo
wakati ilipofahamika kwamba serikali isingeweza kufanya hivyo kwa sababu ya
kifungu cha sheria ambacho kilisema kuwa mali ya Waafrika waliokuwa wakitumika
katika majeshi ya watawala wao haiwezi kutaifishwa.

Hii ilinusuru nyumba hiyo na hivyo ilibakia mikononi mwa mwenyewe mpaka alipofariki
na nyumba hiyo ikaja kuwa katika miliki ya mdogo wake, Ahmed Adam.

Ahmed Adam alikubali kumpokea Nyerere na ugeni wake nyumbani kwake.
Nyumba hiyo ilikuja kuwa tawi la kwanza la TANU Mikindani.

Siku hiyo hiyo ya Jumamosi, usiku Nyerere aliitisha mkutano na wanachama kama
thelathini hivi walihudhuria.

Nyerere aliwaeleza kwa ufupi juu ya ile safari yake ya UNO na hali ya siasa kwa
ujumla mjini Dar es Salaam.

Nyerere aliwahakikishia waskilizaji wake kuwa kulikuwa na uwezekano mkubwa
sana kuwa Tanganyika itakuwa huru katika uhai wao.
 
 
asante mzee Mohamed Said kwa kupoteza mda wako kuandika article japo fupi,kuhusu wanubi na harakati za kudai Uhuru wa Tanganyika.

kama una kisa kingine kizuri kuhusu hawa wanubi wa kariakoo na kudai Uhuru,basi usisite kutuwekea hapa.

nikipata wasaa wa kutosha,nitarejea na swali lingine.
 
Naam hapo ndipo atalipata chimbuko la Azizi Alli
 
Wewe basi nawe ni Shida inamaana hujasoma tokea mwanzo nini kilichofanya huyu mzee abishiwe ukiwa mvivu Wa kusoma basi utaamini kilichoandikwa ni sawa.. So bora usome alichoandika huyu na nilochopinga na maswali aliyoulizwa na member humu hadi akaanza madharau baada ya kuonwa hawezi kikubali kukanusha uongo... Na pia kasome maandiko yake yote ni udini as if anataka kuonesha Uhuru Wa Tanganyika umeletwa na Uislam kitu hicho asahau... Record zipo uingereza na Dunia inajua Nyerere ndie na sio wauza kahawa wabulundi hawa
 
Duduwasha,
Mimi nimetiwa moyo sana na ujasiri wako kuwa ingawa una tatizo katika
kuandikalakini hilo halikuzuii kufanya mjadala na mimi.

Nakupongeza.

Umeandika fikra zako ila kasoro umehamaki na ndiyo unakuja na hizo lugha
za, ''huyu mzee,'' ''wauza kahawa,'' na ''Waburundi,''

Muhimu sana utie juhudi ujifunze kuandika vyema.
 
Ila nyerere nae kafanya mengi.kuna mzee kanihadithia baada ya kupigana vita vya kagera wakapelekwa Zanzibar. Wakawekwa sero.wengine wakakimbia.
 
Tatizo historia amesimuliwa.ila wewe ulikuwepo.haujasimuliwa,ilo ndo tatizo.
 
Mmmmh.imechezewa Bible. Sembuse historia.
 
Haha ndio hoja yako ati utasababisha tuache kuona madhaifu yaki ??? Eti sijui kuandika so what? OK sijui kuandika lakini umeelewa jinsi nilivyokuanika na uongo wako... Hizo reds ulizo mark zingine zimesababishwa na simu nayotumia haswa kwenye harufi kubwa mwanzo so huna hoja zaidi sasa unaleta viroja mnafiki akizeeka huwa mcha.w.i ndipo uelekeo... Na pia kiswahili kisha kuwa proved hakina faida zaidi ya kumfanya mtu abakie level ya chini kimaendeleo...

Wewe unayejua kuandika hapo nilipo mark ni neno moja hilo? Naweza pitia nukuu zako humu nikakuonesha kila ulilokosea ..lete story za kweli na uache kujaza uongo usio hitajika.. Watu wanapenda kupata Elimu haswa za Historia lakini sio kuchonekea na mambo yasiyohusu..
 
Hata Koran zilikuwa na waandishi wawili ikachaguliwa ya muandishi mmoja.
Tatizo lako wewe kiumbe nimeshaanza kuliona,kumbe yote haya yanatokana na chuki zako tu kwa dini ile eeh!

Hujajishtukia tu kua umegeuka kituko kwenye hii thread?
Badilika Mkuu,sio kwa vile uko nyuma ya key board au kwa vile unajibizana na watu usio wajua ndio utumie lugha za kashfa,
usifikiri kua watu hawajui kutukana kama wewe ila hii ni forum tunajifunza na hatuko hapa ili kutukanana,

Mzee wa watu anakujibu kwa busara na uvumilivu wa hali ya juu lakini umeshindwa kuheshimu wenzako, Badilika mkuu,
 
Duduwasha,
Umehamaki.
Unatukana.

Tukubali kuwa mimi naandika uongo.
Sasa hebu lete ukweli usomwe kama ninavyosomwa mimi.
 

Maalim Mohamed Saidi
Namuomba MwenyeziMungu anijaalie niwe Na HIKMA ZAKO japo kidogo.
Uzidishiwe baraka,Hikma Na kila la kheri
 

CleverKING
huyo duduwasha ana hasira Kwa sababu Maalim Mohamed anatufungua macho na historia ambayo wengi wetu tulikuwa hatujui.
Nimesoma historia ya Tanganyika nilipokuwa shule ambazo Sasa naziona zilikuwa nusu kweli.Labda Alikuwa miongoni mwa waandishi
 
Hivi huyo Kleist Sykes alilitoa wapi hilo jina?

Kwa sababu naona kama vile ni jina la kigeni hivi....
Huyo alikuwa mhamiaji mateka wa kivita toka Afrika Kusini, kabila lake ni Mzulu......
Kibaya nikuwa Mohamed Said anamfifisha Cesil Matola kwamba hastahili kupewa jina la mtaa kwakuwa si mdarisalamu lakini hapohapo anajisahau na kumtaja Mzee Azizi Ali ambae ana mtaa kabisa na hakuwa kiongozi wa kisiasa wala harakati, kibaya zaidi hana nasaba za Dar Es Salaam, kwakuwa kwao ni Tanga.

Cesil Matola muyao alikuwa rais wa kwanza wa AA, na mpaka leo hakumbukwi popote katika historia ya Dar wala historia ya CCM....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…