Aziz Ali wa Gerezani na Mtoni Dar es Salaam

Ila nyerere nae kafanya mengi.kuna mzee kanihadithia baada ya kupigana vita vya kagera wakapelekwa Zanzibar. Wakawekwa sero.wengine wakakimbia.

Mjingamimi
Ukienda YouTube angalia mahojiano ya sheikh Muhsin Barwani ambaye NI mwana historia Na muandishi wa Habari aliye bobea.Alifungwa miaka 10 Na Mwalimu Nyerere
 
Huyo alikuwa mhamiaji mateka wa kivita toka Afrika Kusini, kabila lake ni Mzulu......
Kibaya nikuwa Mohamed Said anamfifisha Cesil Matola kwamba hastahili kupewa jina la mtaa kwakuwa si mdarisalamu lakini hapohapo anajisahau na kumtaja Mzee Azizi Ali ambae ana mtaa kabisa na hakuwa kiongozi wa kisiasa wala harakati, kibaya zaidi hana nasaba za Dar Es Salaam, kwakuwa kwao ni Tanga.

Cesil Matola muyao alikuwa rais wa kwanza wa AA, na mpaka leo hakumbukwi popote katika historia ya Dar wala historia ya CCM....
Yericko tushushie nondo za huyo cesil matola mkuu.jf ni uwanja huru.
 
.............Jukumu la kuandaa nchi hizo kupata uhuru liliratibiwa na shirika hilo la kijasusi kwa ustadi mkubwa bila baadhi ya makoloni kujua, lakini lilikumbana na kikinza hasa kufuatia mnyumbuliko wa kiimani ndani ya ukristu kufuatia nguvu ya Cambrige (Anglikana), mgogoro huo ulikuzwa kwakuwa Anglikana nao tayari walikuwa wameaandaa taasisi yao waliyoiita Fabian Sociaty maalumu kwaajili ya kuwaandaa vijana wa kiafrika kukabidhiwa nchi zao, Barani Afrika Jeisuiti ilibadili mbinu kwakuwa dola la Kiingereza lilikuwa kikwazo kwa sehemu fulani, haikujikita kwenye dola isipokuwa ilisimama katika muundo wa shirika lifanya shughuli zake ndani ya Kanisa. Dhamiri ilikuwa lazima itimie, kama ilivyosemwna huko mwanzo kuwa hawa ndio wabobevu wa elimu ya juu kwa kila nyanja na ndio wanaotawala ulimwengu, hivyo vikwazo havikukwamisha wao kufikia malengo.

Katika Tanganyika chini ya Udhamini wa Jumuiko la Kimataifa, kulikuwa na harakati za hapa na pale za kudai haki za kiraia kwa wenyeji. Ifahamike kuwa vyama vya harakati hizo Tanganyika vilikuwa vingi sana, na vipo vilivyokuwa vikipingana vyenyewe kwa vyenyewe.

Mwaka 1927 hadi 1929 kanisa Katoliki nchini chini Joseph Gabriel Zelger, lilibainika kuingiza siasa katika utendaji kazi zake, kitendo hiki kiliwakwaza wakuu wa mamlaka ya kikoloni na kupelekea majasusi wakikoloni wapendekeze aachishwe uongozi wa kanisa nchini. Ni kweli tarehe 12 februari 1929 Zelger alistaafu wadhifawake kwa lazima. Ni mwaka huohuo wa 1927 ndio Chama cha African Assosiotion (AA) kilianzishwa na Gavana Sir David Cameron maaluma kwaajili ya kuratibu sherehe za watu weusi huko pembeni ya mji huko mtaa wa Stanley (leo Lumumba) na kuwapa ofisi mahali leo wanapojiita TANU ilizaliwa. Lakini historia ya Tanganyika haiwataji waasisi wa AA, Rais wa kwanza Mwalimu Cesil Matola (msomi wa mwanzo kabisa enzi za mjerumani kutoka kabila la Wayao), katibu mkuu wa kwanza Klest Sykes (Mzulu Baba yake alikuwa mateka wa kikoloni toka Afrika Kusini), Mwekahazina Ali Ramadhan (mzaramo na mvuvi maarufu wa pwani la Azania).

Hao ndio mwaka 1927 waliounda Chama cha kwanza kabisa cha kutetea maslahi ya weusi Tanganyika na shughuli zake zilikuwa ni kuratibu sherehe za waafrika tu. (Chama cha walevi kwa lugha nyingine). Mwaka 1933 Mwalimu Cesil Matola alifariki na nafasi yake ikakaimiwa na katibu mkuu wa chama hicho bwana Klest, mpaka ilipofika mwaka 1948 yakatokea mapinduzi yaliyoongozwa na mtoto wa Klest aliyeitwa Abdulwahid Sykes huyu alikuwa ametoka kupigana vita vya pili vya dunia huko Burma, na aliporudi alikuwa na mawazo ya ujana toka vitani, akampindua baba yake kwa kumpiga ngumi puani, mapinduzi yaliyoitwa “ondoa wazee”. Kisha AA ikabadilishwa jina na kuitwa TAA, Rais wake wa Kwanza akawa Dr Vedasto Kyaruzi (Mhaya), huyu ndie dakitari wa binadamu wa kwanza kabisa wa kiafrika Tanganyika, Katibu mkuu akawa Abdulwahid Sykes na Mweka hazina akawa Dosa Azizi, utawala huo ulienda mpaka mwaka 1953 uchaguzi ulipofanyika na Nyerere akashinda pale kwenye ukumbi wa Anautoglo Mnazimoja leo, mwaka 1954 Nyerere akabadili jina la chama na kuwa TANU jina ambalo lilibuniwa na Abdulwahid Sykes, TANU ilikwenda mpaka mwaka 1977 na kisha kikazaliwa chama kiitwacho CCM baada ya Muungano wa ASP na TANU.

Kisa hiki cha kufukuzwa kwa Kasisi huyu Bw. Zelger kinasema, Kanisa lilianzisha mafundisho yenye kuchochea fikra za kimaasi, nalilifanikiwa kuandaa wakufunzi maalumu kwenda katika majimbo yote ya kihuduma Tanganyika, hilo lilipelekea kuleta mtafaruku na dola ya mkoloni wa kiingereza ambapo ilimgharimu kiongozi huyu wa kiroho kuachia madaraka yake. Alipoingia askofu Edger Aristide Maranta mwaka 1930, ikiwa kama vile mwendelezo wa mtangulizi wake, Askofu Maranda alianzisha harakati za kuwashawishi viongozi wengine wa majimbo kuendeleza kutoa mafundisho yenye kumfanya mtanganyika ajitambue na adai uhuru wake, mfano, 23 mei 1938 wakati makanisa saba ya Kilutheri yakiwa kwenye hatua za mwanzo za mchakato wa kuungana, Askofu maranda aliomba kuhudhuria kikao cha tarehe 8 mwezi wa sita kilichofanyika Mjini Arusha, Askofu Maranda aliudokeza mpango ule wa siri wa katoliki katika kikao hicho, japokuwa kulikuwa na hofu ya kutoaminiana, lakini uthabiti wa malengo hayo ulijipembua baadae na kuwa wamafaa, ushahidi wa nyaraka za kumbukumbu za mkutano huo unaeleza.

Juhudi za kanisa kupigania mkataba wa Versailles ziliendelea kushika kasi huku zikiendeshwa kwa siri sana kwamfumo wa neno la kiroho, na ilipofikia miaka ya 1950+ kanisa sasa lilikuwa tayari linanguvu ya ushawishi kufuatia mafanikio ya harakati za kanisa katika nyanja za ukombozi barani afrika. Wakati hayo yakiendelea tayari kanisa kupitia shirika lake la kijasusi lilikuwa limewekeza kwa nguvu kubwa kumtafuta mtu imara mwenye weledi na vipawa atakayejengwa ili aje kuongoza nchi. Mtihani mkubwa kwa kanisa ilikuwa ni namna gani linaweza kuingia rasmi kudai uhuru wa Tanganyika. Katika kipindi hiki tangu harakati za kanisa zianze, Askofu Maranta pamoja na mapadre wa baadhi ya mikoa, walikuwa tayari ameshafanya juhudi kadhaa za kukutana na Mashehe waliokuwa na ushawishi mkubwa, mfano 05/02/1948, Askofu Maranda alikutana Shehe Issa bin Amir kiongozi wa kiroho katika msikiti wa Ilala - mchikichini.

Shehe Issa Bin Amir alizaliwa 1846 katika viunga vya Mzizima, mchikichini na kuhudumu katika wadhifa wa shekhe katika msikiti uliokuwa hapohapo viwanja vya nyumbani kwake na alifariki mwaka 1953 akiwa na umri 107, Shehe Issa Bin Amir kwa kabila alikuwa Mzaramo na akiishi hadi kifo chake Mchikichini pale nyuma ya kilipo kiwanda cha bia leo (TBL). Shehe Issa Bin Amir rafiki kipenzi wa Padre Maranta na mzee wa hekima za kilele cha zama hizo, mtu aliyekuwa kiungo muhimu kati ya uislamu na ukristu, Mtu ambae Mwalimu Cesil Matola rais wa kwanza wa AA na Klest Sykes katibu mkuu wakwanza wa AA, na wanachama wengine waliokuwa AA walimheshimu sana kwa hekima zake na mmoja wa wasisi wa Jumuiko la Uislamu Afrika Mashariki (EAMWS) Mazungumzo yao yalihusu harakati za ukombozi, Shehe Issa alimshauri Askofu kuwa ikiwa makanisa na misikiti yanapigwa marufuku na mkoloni kujihusisha na siasa za ukombozi basi watafute baadhi ya vyama vya harakati za ukombozi na waviunge mkono, wazo hilo lilimvutia Askofu lakini akajenga hofu kama je ndani ya vyama hivyo watapata vijana wasomi?.
Siku chache baada ya makutano yake na Shehe Issa, Askofu Maranta aliletewa mapendekezo kutoka kwa Attilio Beltramino kasisi wa katoliki aliyehudumu kule Iringa, mapendekezo ya kasisi huyu yalikuwa ni, Umishonari makao makuu uruhusu udurufu wa biblia zisomeke kwa makabila ya wahusika wa eneo, ndani ya biblia hizo yaongezwe mafundisho ya haki ya kujitambua na kujitawala wenyewe. Pendekezo hili lilimvutia sana Maranta hivyo akalipa baraka zake, kwa hakika lilifanikiwa na ndio lilizaa hisia kali za mwamko wa kudai uhuru, mfano biblia ya lugha ya kihehe ilikuwa inaeleza wazi athari za kutawaliwa.

Harakati za Ukombozi za Mwalimu Nyerere akiwa na nguvu mpya ya kifikra toka Chuo kikuu, zililivutia kanisa na uungaji mkono ukachagizwa, mfano mwaka 1953 wakati TAA kikiwa chama chenye nguvu kufuatia mabadiliko ya 1948 toka AA kwenda TAA. Askofu Maranta alimwalika ofisini kwake Mwalimu Nyerere, walizungumza mengi lakini kubwa nikuwa alimsifu kwa juhudi za kujipambanua bila kuwaogopa wakoloni, akamweleza jinsi kanisa linavyounga mkono juhudi za ukombozi wa Tanganyika, kisha akamshauri kuwa ajaribu kuvishawishi baadhi ya vyama vya harakati za kiraia viungane ili kuvipa nguvu ya kudai uhuru na kanisa litasaidia.

Wazo la Askofu Maranta lilimkaa Mwalimu Nyerere na mwaka 1954, alianza juhudi za kuwaunganisha vijana wenzake wa kariakoo ambao walikuwa ndani ya TAA na wenye nguvu ya ushawishi lakini wakikabiliwa na matatizo makubwa mawili katika lengo lao ambayo ni Elimu na Woga. Ikumbukwe kuwa mwaka 1953 baada ya harakati za ukombozi kupamba moto na kamata kamata ya wanaukombozi, Askofu Edger Aristide Maranta alihamishiwa Zanzibar na nafasi yake ikachukuliwa na Vicar Apostolic, lakini bado aliendelea kuwa mshauri imara wa Mwalimu Nyerere. Jambo la kushangaza kama si kufurahisha, mwaka huohuo mwezi wa 8, Edger Aristide Maranta alirudishwa tena Dar es Saalam, na sasa mbinyo dhidi ya ukoloni ukashika mkondo wake.

Mnamo tarehe 07/07/1954, Vijana (wazee wa kariakoo) wakiongozwa na Julius Kambarage Nyerere, walikubaliana wazo la kuhuisha chama kutoka TAA kwenda TANU, chini ya uratibu wa karibu wa Wajeisut (Askofu Maranta) na Waislamu (Shehe Issa bin Amir) ijapokuwa alikuwa amefariki mwaka mmoja nyuma, lakini hekima za Shehe huyu zilisaidia. Na zaidi ni kuwa safari ya kwanza ya Mwalimu Nyerere ya kwenda UNO 05/03/1955 Kanisa Katoliki lilitoa msaada kwa chama cha TANU wa tiketi ya ndege ya kwenda na kurudi, lilifanya hivyo kupitia shirika lake la Maryknoll Sisters la New York Marekani,

Si hivyo tu bali katika moja ya utani wa Mwalimu wenye ukweli ndani yake aliwahi kusema kuwa makasisi Walsh na Art Wille wa Shirika la Maryknoll ni maboss wake, akikumbuka malipo ya shilingi 600 angali ameacha kazi ya ualimu akiwa kijijini Butiama.Kuna ushahidi wa kihistoria pia unaochagiza habari hizi kwamba majasusi wa Kanisa walimuandaa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kuja kuwa kiongoza Tanganyika mpya................

Kutoka kwenye kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi.

Unaweza kupakua hapa www.simgazeti.com
 
safi yericko,nitarudi kuisoma zaidi baadaye nikipata mda wa kutosha.
 
.............(Nukta tatu tu) Jukumu la kuandaa nchi hizo kupata uhuru liliratibiwa na shirika hilo la kijasusi kwa ustadi mkubwa bila baadhi ya makoloni kujua, lakini lilikumbana na kikinza hasa kufuatia mnyumbuliko wa kiimani ndani ya ukristu (Ukristu) kufuatia nguvu ya Cambrige (Cambridge)(Anglikana), mgogoro huo ulikuzwa kwakuwa Anglikana nao tayari walikuwa wameaandaa taasisi yao waliyoiita Fabian Sociaty (Society: soma historia ya Fabian Society haina uhusiano wowote na Kanisa lolote na baadhi ya waasisi wake kama Bernad Shaw hatu Mungu alikuwa haamini) maalumu kwaajili (kwa ajili) ya kuwaandaa vijana wa kiafrika (Kiafrika) kukabidhiwa nchi zao, Barani Afrika Jeisuiti ilibadili mbinu kwakuwa (kwa kuwa) dola la Kiingereza lilikuwa kikwazo kwa sehemu fulani, haikujikita kwenye dola isipokuwa ilisimama katika muundo wa shirika lifanya shughuli zake ndani ya Kanisa. Dhamiri ilikuwa lazima itimie, kama ilivyosemwna huko mwanzo kuwa hawa ndio wabobevu wa elimu ya juu kwa kila nyanja na ndio wanaotawala ulimwengu, hivyo vikwazo havikukwamisha wao kufikia malengo.

Katika Tanganyika chini ya Udhamini wa Jumuiko la Kimataifa, kulikuwa na harakati za hapa na pale za kudai haki za kiraia kwa wenyeji. Ifahamike kuwa vyama vya harakati hizo Tanganyika vilikuwa vingi sana, na vipo vilivyokuwa vikipingana vyenyewe kwa vyenyewe.

Mwaka 1927 hadi 1929 kanisa Katoliki nchini chini Joseph Gabriel Zelger, lilibainika kuingiza siasa katika utendaji kazi zake, kitendo hiki kiliwakwaza wakuu wa mamlaka ya kikoloni na kupelekea majasusi wakikoloni wapendekeze aachishwe uongozi wa kanisa nchini. Ni kweli tarehe 12 februari 1929 Zelger alistaafu wadhifawake kwa lazima. Ni mwaka huohuo wa 1927 ndio Chama cha African Assosiotion (AA) kilianzishwa na Gavana Sir David Cameron maaluma kwaajili ya kuratibu sherehe za watu weusi huko pembeni ya mji huko mtaa wa Stanley (leo Lumumba) na kuwapa ofisi mahali leo wanapojiita TANU ilizaliwa. Lakini historia ya Tanganyika haiwataji waasisi wa AA, Rais wa kwanza Mwalimu Cesil Matola (msomi wa mwanzo kabisa enzi za mjerumani kutoka kabila la Wayao), katibu mkuu wa kwanza Klest Sykes (Mzulu Baba yake alikuwa mateka wa kikoloni toka Afrika Kusini), Mwekahazina Ali Ramadhan (mzaramo na mvuvi maarufu wa pwani la Azania).

Hao ndio mwaka 1927 waliounda Chama cha kwanza kabisa cha kutetea maslahi ya weusi Tanganyika na shughuli zake zilikuwa ni kuratibu sherehe za waafrika tu. (Chama cha walevi kwa lugha nyingine). Mwaka 1933 Mwalimu Cesil Matola alifariki na nafasi yake ikakaimiwa na katibu mkuu wa chama hicho bwana Klest, mpaka ilipofika mwaka 1948 yakatokea mapinduzi yaliyoongozwa na mtoto wa Klest aliyeitwa Abdulwahid Sykes huyu alikuwa ametoka kupigana vita vya pili vya dunia huko Burma, na aliporudi alikuwa na mawazo ya ujana toka vitani, akampindua baba yake kwa kumpiga ngumi puani, mapinduzi yaliyoitwa “ondoa wazee”. Kisha AA ikabadilishwa jina na kuitwa TAA, Rais wake wa Kwanza akawa Dr Vedasto Kyaruzi (Mhaya), huyu ndie dakitari wa binadamu wa kwanza kabisa wa kiafrika Tanganyika, Katibu mkuu akawa Abdulwahid Sykes na Mweka hazina akawa Dosa Azizi, utawala huo ulienda mpaka mwaka 1953 uchaguzi ulipofanyika na Nyerere akashinda pale kwenye ukumbi wa Anautoglo Mnazimoja leo, mwaka 1954 Nyerere akabadili jina la chama na kuwa TANU jina ambalo lilibuniwa na Abdulwahid Sykes, TANU ilikwenda mpaka mwaka 1977 na kisha kikazaliwa chama kiitwacho CCM baada ya Muungano wa ASP na TANU.

Kisa hiki cha kufukuzwa kwa Kasisi huyu Bw. Zelger kinasema, Kanisa lilianzisha mafundisho yenye kuchochea fikra za kimaasi, nalilifanikiwa kuandaa wakufunzi maalumu kwenda katika majimbo yote ya kihuduma Tanganyika, hilo lilipelekea kuleta mtafaruku na dola ya mkoloni wa kiingereza ambapo ilimgharimu kiongozi huyu wa kiroho kuachia madaraka yake. Alipoingia askofu Edger Aristide Maranta mwaka 1930, ikiwa kama vile mwendelezo wa mtangulizi wake, Askofu Maranda alianzisha harakati za kuwashawishi viongozi wengine wa majimbo kuendeleza kutoa mafundisho yenye kumfanya mtanganyika ajitambue na adai uhuru wake, mfano, 23 mei 1938 wakati makanisa saba ya Kilutheri yakiwa kwenye hatua za mwanzo za mchakato wa kuungana, Askofu maranda aliomba kuhudhuria kikao cha tarehe 8 mwezi wa sita kilichofanyika Mjini Arusha, Askofu Maranda aliudokeza mpango ule wa siri wa katoliki katika kikao hicho, japokuwa kulikuwa na hofu ya kutoaminiana, lakini uthabiti wa malengo hayo ulijipembua baadae na kuwa wamafaa, ushahidi wa nyaraka za kumbukumbu za mkutano huo unaeleza.

Juhudi za kanisa kupigania mkataba wa Versailles ziliendelea kushika kasi huku zikiendeshwa kwa siri sana kwamfumo wa neno la kiroho, na ilipofikia miaka ya 1950+ kanisa sasa lilikuwa tayari linanguvu ya ushawishi kufuatia mafanikio ya harakati za kanisa katika nyanja za ukombozi barani afrika. Wakati hayo yakiendelea tayari kanisa kupitia shirika lake la kijasusi lilikuwa limewekeza kwa nguvu kubwa kumtafuta mtu imara mwenye weledi na vipawa atakayejengwa ili aje kuongoza nchi. Mtihani mkubwa kwa kanisa ilikuwa ni namna gani linaweza kuingia rasmi kudai uhuru wa Tanganyika. Katika kipindi hiki tangu harakati za kanisa zianze, Askofu Maranta pamoja na mapadre wa baadhi ya mikoa, walikuwa tayari ameshafanya juhudi kadhaa za kukutana na Mashehe waliokuwa na ushawishi mkubwa, mfano 05/02/1948, Askofu Maranda alikutana Shehe Issa bin Amir kiongozi wa kiroho katika msikiti wa Ilala - mchikichini.

Shehe Issa Bin Amir alizaliwa 1846 katika viunga vya Mzizima, mchikichini na kuhudumu katika wadhifa wa shekhe katika msikiti uliokuwa hapohapo viwanja vya nyumbani kwake na alifariki mwaka 1953 akiwa na umri 107, Shehe Issa Bin Amir kwa kabila alikuwa Mzaramo na akiishi hadi kifo chake Mchikichini pale nyuma ya kilipo kiwanda cha bia leo (TBL). Shehe Issa Bin Amir rafiki kipenzi wa Padre Maranta na mzee wa hekima za kilele cha zama hizo, mtu aliyekuwa kiungo muhimu kati ya uislamu na ukristu, Mtu ambae Mwalimu Cesil Matola rais wa kwanza wa AA na Klest Sykes katibu mkuu wakwanza wa AA, na wanachama wengine waliokuwa AA walimheshimu sana kwa hekima zake na mmoja wa wasisi wa Jumuiko la Uislamu Afrika Mashariki (EAMWS) Mazungumzo yao yalihusu harakati za ukombozi, Shehe Issa alimshauri Askofu kuwa ikiwa makanisa na misikiti yanapigwa marufuku na mkoloni kujihusisha na siasa za ukombozi basi watafute baadhi ya vyama vya harakati za ukombozi na waviunge mkono, wazo hilo lilimvutia Askofu lakini akajenga hofu kama je ndani ya vyama hivyo watapata vijana wasomi?.
Siku chache baada ya makutano yake na Shehe Issa, Askofu Maranta aliletewa mapendekezo kutoka kwa Attilio Beltramino kasisi wa katoliki aliyehudumu kule Iringa, mapendekezo ya kasisi huyu yalikuwa ni, Umishonari makao makuu uruhusu udurufu wa biblia zisomeke kwa makabila ya wahusika wa eneo, ndani ya biblia hizo yaongezwe mafundisho ya haki ya kujitambua na kujitawala wenyewe. Pendekezo hili lilimvutia sana Maranta hivyo akalipa baraka zake, kwa hakika lilifanikiwa na ndio lilizaa hisia kali za mwamko wa kudai uhuru, mfano biblia ya lugha ya kihehe ilikuwa inaeleza wazi athari za kutawaliwa.

Harakati za Ukombozi za Mwalimu Nyerere akiwa na nguvu mpya ya kifikra toka Chuo kikuu, zililivutia kanisa na uungaji mkono ukachagizwa, mfano mwaka 1953 wakati TAA kikiwa chama chenye nguvu kufuatia mabadiliko ya 1948 toka AA kwenda TAA. Askofu Maranta alimwalika ofisini kwake Mwalimu Nyerere, walizungumza mengi lakini kubwa nikuwa alimsifu kwa juhudi za kujipambanua bila kuwaogopa wakoloni, akamweleza jinsi kanisa linavyounga mkono juhudi za ukombozi wa Tanganyika, kisha akamshauri kuwa ajaribu kuvishawishi baadhi ya vyama vya harakati za kiraia viungane ili kuvipa nguvu ya kudai uhuru na kanisa litasaidia.

Wazo la Askofu Maranta lilimkaa Mwalimu Nyerere na mwaka 1954, alianza juhudi za kuwaunganisha vijana wenzake wa kariakoo ambao walikuwa ndani ya TAA na wenye nguvu ya ushawishi lakini wakikabiliwa na matatizo makubwa mawili katika lengo lao ambayo ni Elimu na Woga. Ikumbukwe kuwa mwaka 1953 baada ya harakati za ukombozi kupamba moto na kamata kamata ya wanaukombozi, Askofu Edger Aristide Maranta alihamishiwa Zanzibar na nafasi yake ikachukuliwa na Vicar Apostolic, lakini bado aliendelea kuwa mshauri imara wa Mwalimu Nyerere. Jambo la kushangaza kama si kufurahisha, mwaka huohuo mwezi wa 8, Edger Aristide Maranta alirudishwa tena Dar es Saalam, na sasa mbinyo dhidi ya ukoloni ukashika mkondo wake.

Mnamo tarehe 07/07/1954, Vijana (wazee wa kariakoo) wakiongozwa na Julius Kambarage Nyerere, walikubaliana wazo la kuhuisha chama kutoka TAA kwenda TANU, chini ya uratibu wa karibu wa Wajeisut (Askofu Maranta) na Waislamu (Shehe Issa bin Amir) ijapokuwa alikuwa amefariki mwaka mmoja nyuma, lakini hekima za Shehe huyu zilisaidia. Na zaidi ni kuwa safari ya kwanza ya Mwalimu Nyerere ya kwenda UNO 05/03/1955 Kanisa Katoliki lilitoa msaada kwa chama cha TANU wa tiketi ya ndege ya kwenda na kurudi, lilifanya hivyo kupitia shirika lake la Maryknoll Sisters la New York Marekani,

Si hivyo tu bali katika moja ya utani wa Mwalimu wenye ukweli ndani yake aliwahi kusema kuwa makasisi Walsh na Art Wille wa Shirika la Maryknoll ni maboss wake, akikumbuka malipo ya shilingi 600 angali ameacha kazi ya ualimu akiwa kijijini Butiama.Kuna ushahidi wa kihistoria pia unaochagiza habari hizi kwamba majasusi wa Kanisa walimuandaa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kuja kuwa kiongoza Tanganyika mpya................

Kutoka kwenye kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi.

Unaweza kupakua hapa www.simgazeti.com

Hivi hiki kweli kinaweza kuwa kitabu?
Nimesahihisha sehemu ndogo tu kuonyesha kichekesho hiki.

Hajui, ''facts,'' mathalan daktari wa kwanza Mwafrika ni Dr. Joseph Mutahangarwa, AA ilibadili jina 1948 na wakati huo Dr. Kyaruzi hata hiyo siasa kwake bado.

Siwezi kusahihisha kila kitu inachosha.
MS

Wanamajlis,
Bandiko hili limeshawahi kuletwa hapa na nilieleza kuwa kuna makosa mengi.
Inaelekea mwandishi hakubali kuwa kuna makosa.

Kazi ya kisomi inahitaji rejea ili kuthibitisha kinachoelezwa.

Walimu wetu siku zile Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam wakituasa kutoandika
''barua,'' yaani kuandika mada ya kisomi bila rejea.

Hicho hapo juu ni ''barua,'' siyo mada ya kisomi.
African Association haikuasisiwa 1927 bali 1929.

Anaweza kufanya rejea katika, ''Modern Tanzanians,'' John Iliffe (Ed) makala
ya Daisy Sykes Buruku, ''Kleist Sykes The Townsman,'' akipenda hata amsome
Mohamed Said, ''The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924-1968)...''Kleist
Sykes:
Pioneer and Man of Ideas 1894 - 1949.''

Akipenda zaidi anaweza kuingia katika Dictionary of Africa Biography, Oxford
University Press 2011, aangalie Kleist Sykes.

Anasema African Association iliassisiwa Stanley Street si kweli kwani wakati huo
1920s hiyo nyumba ya harakati za siasa ya Kleist hapo mtaani ilikuwa bado kabisa
haijajengwa.

Nyumba hiyo ilijengwa 1942.

AA iliasisiwa Mission Quarter nyumbani kwa Cecil Matola Mtaa wa Masasi, nyumba
hii baadae ilinunuliwa na John Rupia.

Kuna mengi ya kutunga mfano wa Nyerere kukusanya ''vijana wenzake wa Kariakoo,''
nk. nk. hakuna ukweli wowote Nyerere hakupatapo kuishi Kariakoo ila kwa muda
mfupi sana 1955 alipokaa nyumbani kwa Abdul Sykes Stanley Street baada ya kuacha
kazi ya ualimu.

Atakae kujua TANU iliasisiwa vipi sharti kwanza aijue Kamati ya Siasa katika TAA.

Waliokuwa katika kamati ya ndani ya kuasisi TANU ni wajumbe wa TAA Political Subcommittee
wajumbe walikuwa Mufti Sheikh Hassan bin Amir, Sheikh Said Chaurembo, Abdulwahid
Sykes, Dr. Vedasto Kyaruzi, Steven Mhando, Hamza Mwapachu
na John Rupia.

Safari ya Mwalimu Nyerere ya kwanza 1955 ilighariimiwa na TANU yenyewe na mratibu
wa safari ile aliyekuwa akikusanya fedha alikuwa Idd Faiz Mafongo aliyekuwa mweka
hazina wa TANU na Al Jamiatuli Islamiyya fi Tanganyika.

Hebu kwanza tusimame hapa.

Lakini kwa kulisaidia jamvi lau kwa ukumbusho kwa kuwa mada hii ilishajadiliwa miaka mingi
iliyopita nawaomba waingie hapo chini wasome niliyopata kuandika kuhusu historia ya
Tanganyika:
Mohamed Said: LIWALI AHMED SALEH NA SHEIKH SAID CHAUREMBO
Mohamed Said: KUTOKA JF: MAMA DAISY NA HISTORIA YA CHIEF DAVID KIDAHA MAKWAIA
Mohamed Said: KUMBUKUMBU ZA IDDI TOSIRI MWANACHAMA WA TANU KADI NO. 24
Mohamed Said: LAMECK BUGOHE MUASISI WA TANU 1954 KAFARIKI NA KUZIKWA KIMYA KIMYA
Mohamed Said: ZUBERI MWINSHEHE MANGA MTEMVU MZALENDO ALIYEKUWA NA MSIMAMO MKALI WA “AFRIKA KWA WAAFRIKA”
Mohamed Said: Abbas Kleist Sykes 1929 -
Mohamed Said: Idd Faiz Mafongo Mweka Hazina wa Safari ya Nyerere UNO 1955
Mohamed Said: MCHANGO WA MUFTI SHEIKH HASSAN BIN AMEIR KATIKA KUPIGANIA UHURU WA TANGANYIKA MAHOJIANO KATI YA SHEIKH RASHID SALIM NA MOHAMED SAID RADIO NUR ZANZIBAR
Mohamed Said: KUTOKA FB: VITUKO VYA YERICKO ''NYERERE''
Mohamed Said: KUTOKA JF: HISTORIA YA TANU - DK. VEDASTO KYARUZI, KASELLA BANTU NA JULIUS NYERERE
Mohamed Said: Ijue Historia ya Kweli ya Kuasisiwa kwa TANU
Mohamed Said: KUMBUKUMBU YA MASHUJAA WA UHURU WA TANGANYIKA RASHID ALI MELI
Mohamed Said: AZAM TV KIPINDI MAALUM CHA MASHUJAA WA UHURU WA TANGANYIKA
Mohamed Said: KUTOKA JF: SHEIKH HASSAN BIN AMIR ALIVYOIONGOZA TANU KUWA CHAMA CHA KISEKULA
Mohamed Said: KLEIST SYKES (1894 - 1949) KATIKA DICTIONARY OF AFRICAN BIOGRAPHY (DAB) OXFORD UNIVERSITY PRESS, NEW YORK
Wanamajlis,
Hizo hapo juu ni zaidi ya kurasa 100 za kusoma pamoja na audio za kusikiliza
na video za kuangalia.

Si lazima upitie zote chagua moja mbili tatu utakuwa ushajifunza kitu.

Waswahili tuna msemo na Mzee Ali Hassan Mwinyi akipenda kuutumia,
''Muongo muongoze.''

Chembelecho Maalim Faiza: Elimu bila Khiyana.

Huyu Jonathon Glassman ni professor wa historia Northwestern University
Evanston, Chicago alinialika nikazungumze chuoni kwake juu ya historia ya
TANU na uhuru wa Tanganyika.

Nilizungumza katika Ukumbi wa Eduardo Mondlane.

Glassman alifanya pitioa la kitabu changu katika Cambridge Journal of African
History Vol. 42 Issue 1 March 2001 halikadhalika John Iliffe.
 
Huyo alikuwa mhamiaji mateka wa kivita toka Afrika Kusini, kabila lake ni Mzulu......
Kibaya nikuwa Mohamed Said anamfifisha Cesil Matola kwamba hastahili kupewa jina la mtaa kwakuwa si mdarisalamu lakini hapohapo anajisahau na kumtaja Mzee Azizi Ali ambae ana mtaa kabisa na hakuwa kiongozi wa kisiasa wala harakati, kibaya zaidi hana nasaba za Dar Es Salaam, kwakuwa kwao ni Tanga.

Cesil Matola muyao alikuwa rais wa kwanza wa AA, na mpaka leo hakumbukwi popote katika historia ya Dar wala historia ya CCM....
Yericko,
Kabla hujaandika kwanza fanya utafiti lau mchache.
Aziz Ali hajapewa jina la mtaa si yeye wala mwanae Dossa.

Ikiwa una habari za kueleza za Cecil Matola itapendeza ikiwa utaziandika
nasi tuzisome.

Mimi sijamfifllisha Cecil Matola na sina sababu ya kufanya hivyo.
Kleist alizaliwa Pangani na akakulia Dar es Salaam hakuwa mhamiaji.

Vita vya kwanza alipigana katika jeshi la Wajerumani dhidi ya Waingereza
chini ya Von Lettow Vorbeck akiwa mpambe wake na alitekwa na majeshi
ya Waingereza.

Katika vita ile alikuwa pamoja na nduguye Schneider Abdillah Plantan ambae
alipigwa risasi ya mguu aliomuachia athar ya kuchechemea maisha yake yote.

Schneider yupo katika picha ya ufunguzi wa Ofisi ya AA New Street.

Picha hii ipo katika nyaraka za akina Sykes waliojenga hiyo ofisi na nimeitumia
katika kitabu cha Abdul Sykes.

Schneider ndiye aliyesaidia kuiweka madarakani uongozi wa Abdul Sykes na Dr.
Vedasto Kyaruzi
1950 uliopelekea kuundwa kwa TANU 1954.

Wazalendo hawa mimi nimewaona kwa macho yangu na nazijua historia yao wala
si kwa sababu ya kusoma au nini la hasha ila kwa kuwa hawa mimi ni wazee wangu.

Mohamed Said: KUTOKA JF: HISTORIA YA TANU KAMA ILIVYOANDIKWA NA YERICKO NYERERE
 
Yericko tushushie nondo za huyo cesil matola mkuu.jf ni uwanja huru.
Kadoda,
Hata mimi ningependa kusoma habari za Cecil Matola.

Nilifanya utafiti wa wazalenso wa Mission Quarters habari nilizopata
zilikuwa za Erika Fiah na Mwalimu Thomas Saudtz Plantan peke yao.

Sikupata maisha ya Cecil Matola labda kwa kuwa alikufa mwaka 1933
mapema kiasi cha kutoweza kufanya mengi.

Hata katika nyaraka za Sykes, Cecil Matola hakutokeza ila akina Plantan
wote, Thomas, Schneider na mdogo wao Ramadhani wamo.
 
Hivi hiki kweli kinaweza kuwa kitabu?
Nimesahihisha sehemu ndogo tu kuonyesha kichekesho hiki.

Hajui, ''facts,'' mathalan daktari wa kwanza Mwafrika ni Dr. Joseph Mutahangarwa, AA ilibadili jina 1948 na wakati huo Dr. Kyaruzi hata hiyo siasa kwake bado.

Siwezi kusahihisha kila kitu inachosha.
MS

Wanamajlis,
Bandiko hili limeshawahi kuletwa hapa na nilieleza kuwa kuna makosa mengi.
Inaelekea mwandishi hakubali kuwa kuna makosa.

Kazi ya kisomi inahitaji rejea ili kuthibitisha kinachoelezwa.

Walimu wetu siku zile Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam wakituasa kutoandika
''barua,'' yaani kuandika mada ya kisomi bila rejea.

Hicho hapo juu ni ''barua,'' siyo mada ya kisomi.
African Association haikuasisiwa 1927 bali 1929.

Anaweza kufanya rejea katika, ''Modern Tanzanians,'' John Iliffe (Ed) makala
ya Daisy Sykes Buruku, ''Kleist Sykes The Townsman,'' akipenda hata amsome
Mohamed Said, ''The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924-1968)...''Kleist
Sykes:
Pioneer and Man of Ideas 1894 - 1949.''

Akipenda zaidi anaweza kuingia katika Dictionary of Africa Biography, Oxford
University Press 2011, aangalie Kleist Sykes.

Anasema African Association iliassisiwa Stanley Street si kweli kwani wakati huo
1920s hiyo nyumba ya harakati za siasa ya Kleist hapo mtaani ilikuwa bado kabisa
haijajengwa.

Nyumba hiyo ilijengwa 1942.

AA iliasisiwa Mission Quarter nyumbani kwa Cecil Matola Mtaa wa Masasi, nyumba
hii baadae ilinunuliwa na John Rupia.

Kuna mengi ya kutunga mfano wa Nyerere kukusanya ''vijana wenzake wa Kariakoo,''
nk. nk. hakuna ukweli wowote Nyerere hakupatapo kuishi Kariakoo ila kwa muda
mfupi sana 1955 alipokaa nyumbani kwa Abdul Sykes Stanley Street baada ya kuacha
kazi ya ualimu.

Atakae kujua TANU iliasisiwa vipi sharti kwanza aijue Kamati ya Siasa katika TAA.

Waliokuwa katika kamati ya ndani ya kuasisi TANU ni wajumbe wa TAA Political Subcommittee
wajumbe walikuwa Mufti Sheikh Hassan bin Amir, Sheikh Said Chaurembo, Abdulwahid
Sykes, Dr. Vedasto Kyaruzi, Steven Mhando, Hamza Mwapachu
na John Rupia.

Safari ya Mwalimu Nyerere ya kwanza 1955 ilighariimiwa na TANU yenyewe na mratibu
wa safari ile aliyekuwa akikusanya fedha alikuwa Idd Faiz Mafongo aliyekuwa mweka
hazina wa TANU na Al Jamiatuli Islamiyya fi Tanganyika.

Hebu kwanza tusimame hapa.

Lakini kwa kulisaidia jamvi lau kwa ukumbusho kwa kuwa mada hii ilishajadiliwa miaka mingi
iliyopita nawaomba waingie hapo chini wasome niliyopata kuandika kuhusu historia ya
Tanganyika:
Mohamed Said: LIWALI AHMED SALEH NA SHEIKH SAID CHAUREMBO
Mohamed Said: KUTOKA JF: MAMA DAISY NA HISTORIA YA CHIEF DAVID KIDAHA MAKWAIA
Mohamed Said: KUMBUKUMBU ZA IDDI TOSIRI MWANACHAMA WA TANU KADI NO. 24
Mohamed Said: LAMECK BUGOHE MUASISI WA TANU 1954 KAFARIKI NA KUZIKWA KIMYA KIMYA
Mohamed Said: ZUBERI MWINSHEHE MANGA MTEMVU MZALENDO ALIYEKUWA NA MSIMAMO MKALI WA “AFRIKA KWA WAAFRIKA”
Mohamed Said: Abbas Kleist Sykes 1929 -
Mohamed Said: Idd Faiz Mafongo Mweka Hazina wa Safari ya Nyerere UNO 1955
Mohamed Said: MCHANGO WA MUFTI SHEIKH HASSAN BIN AMEIR KATIKA KUPIGANIA UHURU WA TANGANYIKA MAHOJIANO KATI YA SHEIKH RASHID SALIM NA MOHAMED SAID RADIO NUR ZANZIBAR
Mohamed Said: KUTOKA FB: VITUKO VYA YERICKO ''NYERERE''
Mohamed Said: KUTOKA JF: HISTORIA YA TANU - DK. VEDASTO KYARUZI, KASELLA BANTU NA JULIUS NYERERE
Mohamed Said: Ijue Historia ya Kweli ya Kuasisiwa kwa TANU
Mohamed Said: KUMBUKUMBU YA MASHUJAA WA UHURU WA TANGANYIKA RASHID ALI MELI
Mohamed Said: AZAM TV KIPINDI MAALUM CHA MASHUJAA WA UHURU WA TANGANYIKA
Mohamed Said: KUTOKA JF: SHEIKH HASSAN BIN AMIR ALIVYOIONGOZA TANU KUWA CHAMA CHA KISEKULA
Mohamed Said: KLEIST SYKES (1894 - 1949) KATIKA DICTIONARY OF AFRICAN BIOGRAPHY (DAB) OXFORD UNIVERSITY PRESS, NEW YORK
Wanamajlis,
Hizo hapo juu ni zaidi ya kurasa 100 za kusoma pamoja na audio za kusikiliza
na video za kuangalia.

Si lazima upitie zote chagua moja mbili tatu utakuwa ushajifunza kitu.

Waswahili tuna msemo na Mzee Ali Hassan Mwinyi akipenda kuutumia,
''Muongo muongoze.''

Chembelecho Maalim Faiza: Elimu bila Khiyana.

Huyu Jonathon Glassman ni professor wa historia Northwestern University
Evanston, Chicago alinialika nikazungumze chuoni kwake juu ya historia ya
TANU na uhuru wa Tanganyika.

Nilizungumza katika Ukumbi wa Eduardo Mondlane.

Glassman alifanya pitioa la kitabu changu katika Cambridge Journal of African
History Vol. 42 Issue 1 March 2001 halikadhalika John Iliffe.
Nakushuru kwa kusahihisha makosa ya kiherufi...

Juu ya rejea sina sababu ya kuzisoma kwakuwa zote ni mkusanyiko wa mawazo yako jambo ambalo mimi nakupinga siku zote.
 
YERICO NYERERE HAUNA MZIGOO KAKA ..KASOMEE ACHAA KUIGAA FANI YA MZEE HUYOO UTAUMBUKAA NA UNAENDELEAA KUUMBUKAA ........MSOMI GANI HAUNA REJEA ..AU UNAREJEA KWA MZEE MOHAMMAD SAID...[emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15]
 
Katika andiko ili udini uliwekwa mbele upo wapi tuache kufikiria kikaburu jamani mbona hivyo

Tatizo ni kuwa waliaminishwa kila kitu ni Rambo pekee. Jeshi la mtu mmoja.

Wanapokuja kuona kumbe jeshi lilikuwa kubwa na wapiganaji haswa ni wengi tena ni wale wale walioaminishwa kuwa si chochote si lolote, hapo lazima mioyo iungulike.

Ni maradhi tu yalio mioyoni mwao, hakuna zaidi.
 
Nakushuru kwa kusahihisha makosa ya kiherufi...

Juu ya rejea sina sababu ya kuzisoma kwakuwa zote ni mkusanyiko wa mawazo yako jambo ambalo mimi nakupinga siku zote.

Weka rejea zako uzijuazo, au chanzo ni wewe mwenyewe na ulikuwepo 1920s?

Barua.

Msalimie technically
 
Wajing Wa humu wamekazia kumtetea mtu muongo na hatari ujinga na uongo anao uandika humu ni hatari sana kihistoria na nilijua keshashikwa atakwepa majibu mwishowe atatoa matusi ndio formula ya mtu muongmuongo... Ati Aziz Ali ndie mwafrica Wa kwanza au mtanganyika kununua gari na kujenga nyumba ya vigae! nilikuwa namsubiri ataje mwaka nimuumbue kakwepa kujibu hivyo thread yake hii ni hizo mtupu haiwezi kuwa history yenye uongo ndani... Tusiwe wapumbavu kumtetea mtu muongo

Una kichwa kizito sana na huyo mwenzako sjui usichoelewa ni nini na hiko ni kiswahili cha kawaida tu na sio mara ya kwanza kutumika neno muafrika katika historia ya tanzania tunaambiwa raia waligawanya kwenye matabaka matatu wazungu waarabu na waafrika wewe kichwa kilivyo kizito unauliza km hao waarab ni hadi wale wa saudia au unauliza kuwa hao waafrika ni mpaka wale wale wa ghana wakati unajua historia inayoongelewa ni tanzania usimlaumu mtu mwingine kwa ufinyu wako wa kuelewa mambo
 
Nakushuru kwa kusahihisha makosa ya kiherufi...

Juu ya rejea sina sababu ya kuzisoma kwakuwa zote ni mkusanyiko wa mawazo yako jambo ambalo mimi nakupinga siku zote.
Yericko kuwa nä mawazo kinzani ni jambo jema linalojenga na kuongeza elimu.

Muhimu kuwasoma wengine.

Laiti nisingekusoma singeweza kuandika niliyoandika hapo juu.
 
Una kichwa kizito sana na huyo mwenzako sjui usichoelewa ni nini na hiko ni kiswahili cha kawaida tu na sio mara ya kwanza kutumika neno muafrika katika historia ya tanzania tunaambiwa raia waligawanya kwenye matabaka matatu wazungu waarabu na waafrika wewe kichwa kilivyo kizito unauliza km hao waarab ni hadi wale wa saudia au unauliza kuwa hao waafrika ni mpaka wale wale wa ghana wakati unajua historia inayoongelewa ni tanzania usimlaumu mtu mwingine kwa ufinyu wako wa kuelewa mambo
Viroba ni hatari sana acha kuvinywa akili zako zirejee... Nani kasema sielewi au unachanganya hoja za wengine unanipa Mimi na pia hujaulizwa wewe na aliyemuuliza ni mwingine acha uvivu Wa kusoma Mada huku ndio maana unakurupuka... Aliyeulizwa mleta Mada kashindwa kujibu wewe ndio unajua majibu kuliko yeye aliyetunga story ya uongo? Mimi namuweka sawa asiweke vikorombezo kwenye mambo ya history even history za dini ujinga ujinga mwingi ulifutwa maana vinaleta upuuzi na history haitokubalika katu... Huyu huwezi mtetea zaidi nawe unajionesha kuwa ni bwege Wa ushabiki tu mbululaz kitu kielezea wazi na Dunia wakisoma wanaona Mwafrica Wa kwanza kujenga nyumba ya Vigae aliishi Tanganyika period
 
Tatizo ni kuwa waliaminishwa kila kitu ni Ramb ino pekee. Jeshi la mtu mmoja.

Wanapokuja kuona kumbe jeshi lilikuwa kubwa na wapiganaji haswa ni wengi tena ni wale wale waliaminishwa kuwa si chochote si lolote, hapo lazima mioyo iungulike.

Ni maradhi tu yalio mioyoni mwao, hakuna zaidi.
Huyo Wa kutuaminisha mpiganaji hakuwa Rambo pekee ndio huyu bwanako?
 
Ni historia nzuri kabisa na nimefurahi sana kuisikia kwani mimi nimewahi kuishi Mtoni National Housing na nailikuwa sijui historia hii ya Mtoni kwa Aziz Ali. Lakini kilichonifurahisha zaidi ni kuhusu mtoto wa huyu bwana ambaye alikuwa contractore enzi hizo za niaka ya 50 hence he was rich lakini I quote ''Aziz Ali yeye alinunua karabai kwa kila msikiti na ikifika Maghrib mwanae Hamza alikuwa akizitia mafuta na kuziwasha kisha akizipeleka kila msikiti tayari kwa sala ya Maghrib. Inapomalizika sala ya Isha alikuwa anapita tena katika ile misikiti kukusanya karabai zake na kurudi nazo nyumbani kwao Mtaa wa Mbaruku na Kongo' I am so humbled kwa kweli. Hili ndio wenzetu matajiri wanalotushinda kuwafundisha watoto humbleness, big up Marehemu Aziz Ali May your Soul Rest in Peace! Huyu Hamza nayeye yuko wapi?
 
Back
Top Bottom