Mtanganyika...
Sijui ni kitu gani kimekughadhibisha hadi unatukana.
Wala sijui zipi pumba katika haya ninayoandika kwani tumekuwa na mjadala
mzuri tu na wengi wamechangia mengi yenye manufaa.
Kuwa, ''tupo tupo,'' si sawa wala si kweli kusema hivyo.
Sisi tunaishi kama wanavyoishi jamii nyingine katika nchi hii.
Kuhusu kubadilisha kofia tunabadilisha kweli maana ni kivazi chetu kama watu
wa pwani na kama Waislam wala havijabadilika rangi.
Kuna wakati tunavaa kofia na kuna wakati hatuvai kofia.
Nakuwekea kofia hapo chini na hebu onyesha hiyo iliyobadilika rangi:
Ikiwa mimi unaniita ni msomi wa wajinga wewe kwa haya matusi yako na kejeli
unazotoa tukuweke katika kundi gani?
Angalia hapo chini na nionyeshe wajinga katika ya hao waliofungua milango
yao kwangu:
- PUBLICATIONS/RESEARCH PAPERS/ARTICLES
- The Life and Times of Abdulwahid Sykes 1924 –1968 The Untold Story of the Muslim Struggle against British Colonialism in Tanganyika, Minerva Press London, 1998 translated into Kiswahili as Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes 1924-1968 Historia Iliyofichwa Kuhusu Harakati za Waislam Dhidi ya Ukoloni wa Waingereza, Phoenix Publishers, Nairobi, 2002.
- The Torch on Kilimanjaro, Oxford University Press, Nairobi, 2006
- Contributing author for an African anthology: The Mermaid of Msambweni and Other Stories, Oxford University Press 2007, Nairobi.
- Contributing author Dictionary of African Biography (DAB), Oxford University Press 2011, New York.
- Uchaguzi wa Busara, Abantu Publications 2008, Dar es Salaam.
- In Praise of Ancestors (1987) Africa Events (London).
- Abdulwahid Sykes: Founder of Political Movement (1988) Africa Events (London).
- Islam and Politics in Tanzania (1989) Al Haq International (Karachi)
- The Plight of Tanzanian Muslim (1993) Change (Dar es Salaam).
- Tanzania - The "Secular" Unsecular State (1995) Change (Dar es Salaam).
- The Question of Muslim Stagnation in Education in Tanzania - A Muslim Riddle (Paper presented at the Conference of the Global World of the Swahili Intercultural Dialogue on the Indian Ocean Zanzibar, February 20 - 23, 2003).
- Islamic Education and Intellectualism in Eastern Africa ‘Themes from the Pulpit in Tanganyika (Tanzania Mainland) 1800 – 2000’ (Paper presented at International Symposium on Islamic Civilisation in Eastern Africa Kampala, Uganda organised by the Islamic Conference Research Centre for Islamic History, Art and Culture (IRCICA), Istanbul and the Islamic University in Uganda, Mbale December 15th – 17th 2003).
- Sheikh Hassan bin Ameir - The Moving Spirit of Muslim Emancipation in Tanganyika (1950 – 1968) (Paper presented at Youth Camp Organised by Zanzibar University, World Assembly of Muslim Youth (WAMY) and Tanzania Muslim Students Association (TAMSA) 27th February – 4th March 2004).
- Islamic Movement and the Christian Lobby in Tanzania - the Experience of the late Prof. Kighoma Ali Malima (1938 – 1995) (Paper Presented to Tanzania Muslim Students Association (TAMSA) Sokoine University of Agriculture (SUA) Morogoro 11th April 2004).
- Terrorism in East Africa the Tanzanian Experience (Paper Presented at the Conference on Islam, Terrorism and African Development University of Ibadan, Nigeria 8th - 10th February 2006).
- Al Marhum Sheikh Kassim bin Juma bin Khamis (1940 – 1994) and the Pork Riots of 1993. (Paper Presented at the Regional Conference on Islam in Eastern Africa: Islam Encounter with the Challenges of the 21st Century 1st - 3rd August 2006, Kenyatta University, Nairobi.
- 14. Muslim Bible Scholars of Tanzania – The Legacy of Sheikh Ahmed Deedat (1918 – 2005) Paper Presented at the International Symposium on Islamic Civilisation in Southern Africa Organised by The Organisation of Islamic Conference Research Centre for Islamic History, Art and Culture (IRCICA) The National AWQAF Foundation of South Africa (AWQAF SA 1 – 3 September 2006 University of Johannesburg.
- Tanzania: A Nation Without Heroes Seminar Organised by IFRA French Institute for Research in Africa and BIEA British Institute in East Africa 23rd and 24th September 2013 at IFRA Nairobi.
- Awards: Several Awards.
- Visiting Scholar: (2011)
- University of Iowa, Iowa City, USA
- Northwestern University, Chicago, Illinois, USA
- Zentrum Moderner Orient (ZMO), Berlin.
- OTHER COUNTRIES VISITED
- Zambia, Ethiopia, Swaziland, Msumbiji, Zimbabwe, Sudan, Egypt, Saudi Arabia, United Arab Emirates, Oman, Yemen, Uganda, Switzerland, Iran, France, Netherlands, Turkey and Abu Dhabi.
Mtanganyika...
Utakumbuka nilikuambia kuwa kuna mtu aliniomba ruksa akutukane nami
nikamkataza.
Baada ya wewe kurejea tena hapa Majlis na matusi mara ya pili na mie kukupa
jibu hilo hapo juu karejea tena na ombi lile lile...
.
Nimemkatalia lakini nimemuahidi kukuandika na kukupa maelezo lao kwa ufupi
kuhusu
Hamza Mwapachu.
Ikiwa umefuatilia darsa langu kuhusu tatizo lililotokea katika kuandika historia ya
TANU ndani ya wana TANU wenyewe akiwemo
Abdul Sykes, Julius Nyerere,
Saadan Abdu Kandoro na
Mwalimu Kihere utaona kuwa ilifika mahali
Abdul
Sykes jina lake liliondolewa kabisa katika historia ya TANU na likawa halitajwi wala
kuhusishwa na siasa za kupigania uhuru wa Tanganyika.
Ikawa hata ilipoandikwa historia ya TANU na Kivukoni College mwaka wa 1981
haikuelezwa
Nyerere alichukua uongozi wa TAA 1953 kutoka kwa nani.
Lakini mimi nilipoandika kitabu cha
Sykes nilieleza kwa kirefu uchaguzi wa 1953
wa urais wa TAA kati ya
Abdul Sykes na
Nyerere uliofanyika Ukumbi wa Arnautoglo
tarehe 17 April, uchaguzi ambao ndiyo ilikuwa ngazi ya
Nyerere ya kwanza kupanda
na kuwa kiongozi wa watu wa Tanganyika.
Katika kitabu cha
Sykes nimeeleza vipi
Nyerere alishinda uchaguzi ule dhidi ya
Abdul.
Kitu ambacho sikueleza na sababu ni kuwa ilikuwa sikijui ni mazungumzo aloyofanya
Abdul Sykes na
Hamza Mwapachu Nansio, Ukerewe ambako Hamza alikuwa anafanya
kazi.
Agenda ya mazungumzo yale ilikuwa
Nyerere.
Katika mazungumzo haya alikuwapo pia
Ali Mwinyi Tambwe aliyekuwa Katibu wa Al
Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika.
Abdul alikwenda kwa
Hamza kutaka ushauri na neno lake la mwisho kuhusu
Nyerere
kuachiwa kiti cha rais wa TAA na
Abdul 1953 na mwaka unaofuatia waunde TANU.
Hamza alimwambia
Abdul kuwa yeye hajabadili mawazo na alimtaka
Abdul amsaidie
Nyerere kushinda uchaguzi ule.
(Habari hizi kaziandika
Juma Mwapachu miaka ya hivi karibuni baada ya kusoma makala
yangu moja).
Hivi ndivyo
Nyerere alivyokuja kuingia katika uongozi wa TAA 1953 na viongozi wake
ni hawa hapo chini:
J. K. Nyerere, Rais,
Abdulwahid Sykes, Makamu wa Rais;
J. P. Kasella Bantu, Katibu
Mkuu;
Alexander M. Tobias na
Waziri Dossa Aziz, Katibu wa pamoja wa muhtasari;
Wajumbe wa kamati:
Dr Michael Lugazia, Hamisi Diwani, Tewa Said Tewa, Denis
Phombeah, Z. James, Dome Okochi, C. Ongalo na
Patrick Aoko.
Katika historia hii ndipo unapokuja umuhimu wa
Hamza Mwapachu na
Abdul Sykes
katika historia ya uhuru wa Tanganyika na maisha ya
Nyerere.
Mtanganyika...
Nakuhitimishia kwa kukueleza kuwa moja ya sababu kubwa ya
Hamza kutaka
Nyerere
achukue uongozi ni kuwa alimwambia
Abdul kuwa Waingereza hawatakuwa na hofu
kujadili uhuru wa Tanganyika na
Nyerere kwa kuwa ni Mkristo.
Mimi nimemjua
Juma Mwapachu toka 1967 angalia picha tuliyopiga pamoja miaka hiyo
wa kwanza kulia ni
Mwandishi, William Mfuko, Juma Mwapachu, Andrew Gordon,
Edward Makwaia (sasa mmoja wa machifu Usukuma), Huyo Bi. Mkubwa ni mama yake
Edward, Mama Mary Mackeja na nyuma yake ni
Wendo Mwapachu: