Mkuu ungejua ajenda zake ungeelewa... Huyo ni mmoja Wa watu anaotaka kuwaweka katika history ya Uhuru yaani anaanzia kwenye kizazi cha kwanza hadi cha mwisho.
Duduwasha,
Huna haja ya kunitilia maneno kinywani kwangu.
Hilo la kuwa mimi nina agenda hakika agenda ninayo nayo ilikuwa
ni kusahihisha historia ya TANU.
Hayo mengine usemayo mimi si yangu.
Ila nitakufahamisha kuwa
Aziz Ali hakuwa mwanasiasa ingawa
alikuwa rafiki kipenzi na
Kleist Sykes na alikuwa hapungui kwake.
Historia hii niliyoandika mimi binafsi imeninyanyua sana kabisa.
Kitabu kimependwa sana kinakwenda sasa toleo la nne.
Si hivyo tu kutokana na kitabu hicho nimealikwa vyuo kadhaa Afrika,
Ulaya na Marekani kuzungumza.
Halikadhalika kitabu kufanyiwa pitio na mabingwa wa African History.
Juu ya haya kitabu hiki kimevuruga akili wengi sana.
Prof. Haroub Othman alikuwa mwalimu wangu lakini akili ilimruka
aliposoma historia ya
Abdul Sykes na kuasisiwa kwa TANU kiasi
alitaka kusikia kauli ya
Mwalimu Nyerere mwenyewe achilia mbali kuwa
alinihoji na kisha kwenda kwa
Ahmed Rashad Ali kupata ukweli zaidi.
Mohamed Said: Ahmed Rashad Ali Bingwa wa Propaganda za Ukombozi wa Afrika Sehemu ya Tatu
Kwa hiyo utaiona kuwa wewe si mtu wa kwanza kuchomwa na historia hii
na hautakuwa wa mwisho.
Kila siku hapa JF akinisoma mtu kwa mara ya kwanza lazima atapigwa na
mshangao na mnakasha utaanza upya.
Nimeweka rekodi hapa JF ya kufanya mjadala kwa takriban miezi sita.
Unaweza kuingia hapa ujionee mwenyewe vipi mjadala ulivyokuwa moto:
Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa
Wote hao wamelikimbia jamvi wameniacha sasa niko pweke natoa darsa
kwa mtu mmoja mmoja kama wewe.
Duduwasha,
Ungependa kusikia nini likitokea baada ya
Abdul Sykes na nduguye
Ally
kufutwa katika historia ya TANU?