Well said mkuu, Moh anazungumza aliyo yaona na kusikia - mambo mengi/harakati zilianzia hapa Dar kila mtu analijua hilo sasa kama Watanganyika majasiri wakati huo majority walikuwa ni Waislaam, je, mnataka hilo lisisemwe - mbona baadae walikuja wakristo na wapagani mfano: Paul Rupia, Dk.Mtahangarwa, Dk.Kyaruzi nk.
Haya mambo ya kumkandia Moh. eti yuko biased binafsi nashindwa kuelewa hoja za namna hiyo - tatizo kubwa hapa watu wengi utamani Nyerere ndiye ahusishwe kwa kila kitu - wakati yeye alikaribishwa tu na kukriminiwa na Waislaam, waislaam hao hao ndiyo walipedekeza Nyerere aingoze Chama kutokana na Usomi wake, lakini hilo halina maana kwamba wapigania uhuru wengi wa wakati huo walikuwa wasomi sana au nini sijui, waislaam wengeweza kudai uhuru wa Tanganyika bila ya kumshirikisha Nyerere. Haya mambo ya kuchukulia mtu mmoja kama Alpha na Omega hayafahi hata kidogo, kuna,watu wengi tu wakichangia sana katika harakati za kudai uhuru lakini awatajwi kwenye vitabu vya historia ya Taifa letu na ukichunguza sana utakuta ni wale waliopishana kiswahili na Nyerere! Sikatai Nyerere alijitahidi sana pamoja na wenzake kutufikisha tulipo kitu kilicho kuwa kinanishangaza katika mojawapo ya hulka yake ni kuendekeza vinyongo - sikumbuki kama aliwahi kuhudhulia mazishi ya wanaharakati wenzake mfano: Prof. Abdallahaman Babu, Zuberi Mtemvu, Kasela Bantu, Oscar Kambona, Bibi Titi na wengine wengi tu - kitu hiki kilinishangaza sana.