Duduwasha,
Usitukane tufanye tu mjadala wa kiungwana.
Nitakupa majibu ya mkasa mzima wa wapi hitilafu ilitokea katika uandishi ya historia ya TANU.
Yaelekea wewe ni mgeni hapa jamvini kwani hili nishalieleza huko nyuma.
Niwie radhi niko njiani.
Duduwasha,
Nakuwekea hapo chini niliyoandika katika kitabu cha
Abdul Sykes ili uone
chanzo cha matatizo ya historia ya TANU:
''Kwa mara ya kwanza historia ya TANU ilitaka kuandikwa na
Abdulwahid
mwenyewe.
Baada ya kupatikana kwa uhuru mwaka 1961 na TANU ilipokuwa sasa
inataka kujiimarisha kama chama cha umma, inasemekana
Nyerere wakati
ule Waziri Mkuu alimuomba
Abdulwahid aandike historia ya harakati ya
Waafrika wa Tanganyika dhidi ya ukoloni wa Waingereza.
Hii kwa hakika ndiyo historia ya TANU.
Dr Wilbert Kleruu ambae ndiyo kwanza alikuwa ametoka masomoni Amerika
alichaguliwa na TANU asaidiane na
Abdulwahid katika utafiti na uandishi wa
historia ile.
Abdulwahid alirudi kwenye ofisi za TANU makao makuu; kwenye ofisi yake
ya zamani aliyokuwa akiitumia kama rais wa TAA.
Nyaraka zake binafsi, za baba yake nyingine kuanzia mwaka wa 1929 wakati
wa enzi za African Association zililetwa pale kwa utafiti kama ushahidi wa yale
yaliyopitika zama hizo.
Maelezo ya
Abdulwahid katika kuanzishwa kwa African Association bila ya
kutegemea inasemekana hayakumpendeza
Nyerere, kwa kuwa mwanzo wa
harakati dhidi ya ukoloni jinala baba yake
Abdulwahid,
Mzee Kleist Sykes,
lilikuwa likitawala.
Halikadhalika ilipofika kueleza namna TAA ilivyokujabadilishwa kuwa TANU
watotowake wote watatu -
Abdulwahid, Ally na
Abbas wakiongozwa na
kaka yao mkubwa
Abdulwahid wakawa wanatawala harakati zile.
Historia hii inasemekana haikumpendeza
Nyerere na baadhi ya viongozi
wa TANU.
Haukupita muda
Abdulwahid akatambua kuwa viongozi wapya walioshika
nafasikatika TANU kwa kweli hawakuwa na nia hasa ya kutafiti na kuandika
historia yaTanganyika bali nia na azma yao ilikuwa na kumjenga
Nyerere
na kumkuza kwa sifa ambazo hazikumstahili.
Abdulwahid alipong’amua hili haraka akajitoa katika kazi ile.
Hata hivyo
Dr. Kleruu aliendelea na utafiti na akaandika historia ya TANU.
Historia hii inasemekana ilifuta mchango wa akina
Sykes na wazalendo
wengine katika kuunda African Association na baadae kuasisi TANU.
Hata hivyo baada ya kazi hii kukamilika haikuchapishwa na ikabaki katika
maktabaya TANU, Mtaa wa Lumumba, Dar es Salaam.
Lakini baadae kazi ile ilitoweka na ikachapishwa baada ya ‘’mwandishi,’’
kufanya mabadiko kadhaa katika mswada ule ili usitambulike chanzo chake.
Hata hivyo TANU iligundua kuwa ile ilikuwa historia yao iliyoandikwa na
Dr.
Kleruu na wakafanya bidii kuzuia isichapishwe.
Kimya kimya TANU ikafanya juhudi ya kuzuia kitabu hicho kisitoke toleo la
pili.
Lakini hili halikuwezekana na kitabu hicho kimechapishwa sasa mara kadhaa.
Uandishi wa kitabu kile haukutofautiana sana na kitabu cha TANU kilichotoka
mwaka 1981 kilichoandikwa na Chuo cha TANU cha Kivukoni.''
Duduwasha,
Nakuomba ruksa nisimame hapa kisha In Shaa Allah tutaendelea na mkasa
huu wa kuandika historia ya TANU.
Sasa ukisema kuwa kulikuwa na wazee wakati ikiandikwa historia ya TANU
na wakaikubali historia iliyoandikwa ni muhimu pia ukajua hao waz ni wazee
gani.
Nakueleza haya kwa kuwa hao wazee ninaowajua mie waliokuwa katika
Baraza la TANU walipigwa marufuku kufika Ofisi ya TANU na Baraza la
Wazee wa TANU likavunjwa kwa kushutumiwa kuchanganya dini na siasa.
Haya yalitokea mwaka wa 1963.
Wakati huo mwenyekiti wa Baraza hilo alikuwa
Mzee Idd Tulio aliyechukua
uongozi mwaka wa 1958 baada ya
Sheikh Suleiman Takadir aliyekuwa
mwenyekiti wa Baraza la Wazee kufukuzwa chama baada ya ugpmvi na
Mwalimu Nyerere kuhusu Kura Tatu.
Huu ni muhtasari tu.
Yako mengi.