Nimeelewa wewe na
FaizaFoxy kwanini mna ugomvi na Nyerere mna mahusiano baina ya hao wazee so its time for and her to revange oi. Pengine hao watu walikuwa ni matreita against him au walikuwa wanatoa siri kwa waingereza au uchonganishi au majivuno ya kijinga n.k ni very easy kuwa wipe kuliko assassination
Duduwasha,
Hili suala la kuvuruga historia utalikuta kila nchi Afrika.
Kenya kwa muda mrefu sana walimpuuza
Dedan Kimathi, Bildad
Kaggia na wapigania uhuru wengine.
Historia ya uhuru wa Zanzibar hadi leo hakuna kiongozi anaitaka wao
ni mapinduzi tu.
Hata hayo mapinduzi yenyewe wahusika wakuu hazikuandikwa historia
zao hadi
Dr. Harith Ghassany alipoandika kitabu maarufu, ''Kwaheri
Ukoloni, Kwaheri Uhuru.''
Hakuna usaliti wowote katika historia ya TANU uliowahusisha hao wote
niliowataja katika kitabu cha
Abdul Sykes.
Ukiwa unataka taarifa za usaliti katika harakati za kudai uhuru katika
utafiti wangu nimekutana na kesi tatu tu.
Kuna kisa cha
Alexander Thobias, Martin (sina jina la pili) na cha
huyu ambae sitamtaja kwa sasa.
Alexander Thobias yeye huyu alichukua majalada ya TAA aliyopewa
na
Abdul Sykes akawapa Special Branch.
Alexander alifukuzwa chama.
Martin alimchoma
Dome Budohi kwa Waingereza kuwa alikuwa na
uhusiano na Mau Mau.
Budohi alikamatwa na kufungwa Kenya kisiwani Lamu.
Budohi kadi yake ya TANU ni no. 6.
Umezungumza kuhusu majivuno na fitna.
Abdul Sykes hadi anaingia kaburini hakupata kusema kuwa yeye ndiye
aliyeasisi TANU au ofisi ya TANU ilijengwa na baba yake juu ya kuwa
kulikuwa na kejeli kuwa TAA kilikuwa, ''chama cha starehe,'' nk. nk.
ingawa rafiki zake wengi kama
Ahmed Rashad Ali walimtaka aeleze
vipi TANU iliundwa.
Duduwasha,
Mimi hawa watu ni sehemu ya maisha yangu wengine wamenibeba
nikiwa mtoto mdogo pale Kipata Street (Sasa Mtaa wa Kleist).
Mzee Shebe aliyenipiga picha yangu ya kwanza nikiwa na umri labda
wa miaka 2 ndiye alikuja kuwa mpiga picha wa TANU na
Nyerere 1955.
Unazungumza habari za ''assasination,'' kwa lipi hadi watu wauane?
Jitulize na niulize chochote kuhusu TANU na watu hawa nitakupa majibu.
Mohamed Said: HISTORIA YA JOMO KENYATTA NA ABDULWAHID SYKES 1950