Aziz P. Mlima.. Almost ambassador?


Nafikiri U.S. approach imetulia hasa kwenye suala la urais. Katiba yao inaweka wazi kama wewe si 'mzawa' yaani ujazaliwa kwenye nchi ya marekani huwezi kuwa rais. Hii issue ya dual nationality ni nzuri lakini lazma kuwepo na mipaka ili tusije kupata viongozi mamluki. Lazima tutizame katiba na sheria nyinginezo ambazo zitasaidia katika kufanikisha ustawi wa taifa na huku zikizuia na kuondoa nafasi za 'hawa mamluki wa kisiasa n.k' katika kutaka kubaka uchumi na nafasi za kisiasa.
 
acha uongo umekuwa muongo kama Membe? Dr.Sharrifu aliteuliwa kuwa balozi wa Tanzania nchini Uingereza sio Saudia. na alikuwa akifundisha University of London. hajawahi kuwa balozi wetu nchi Saudia acha uongo.na alikaa kwa muda mrefu sana Uingereza kama Balozi.
 
wengine hadi uraia wa nchi tatu.
 

FM,

To refresh your memory,rekodi zaonyesha huyu jamaa alipata uraia wa Japan baada ya wazazi wake kumwombea kwenye consulate ya Japan hapo Lima. Yaonyesha nchi hizo mbili zinautambua uraia wa nchi zaidi ya moja(dual nationality).

Birthplace
According to government records, Fujimori was born on July 28, 1938, in [ame="http://en.wikipedia.org/wiki/Miraflores_District"]Miraflores[/ame], a district of [ame="http://en.wikipedia.org/wiki/Lima"]Lima[/ame].[22] His parents, Naoichi Fujimori (1897–1971) and Mutsue Inomoto de Fujimori (1913–2009), were natives of [ame="http://en.wikipedia.org/wiki/Kumamoto"]Kumamoto[/ame], [ame="http://en.wikipedia.org/wiki/Japan"]Japan[/ame] who emigrated to Peru in 1934.[23][24] He holds dual Peruvian and Japanese [ame="http://en.wikipedia.org/wiki/Citizenship"]citizenship[/ame], his parents having secured the latter through the Japanese Consulate. Source:[ame]http://en.wikipedia.org/wiki/Alberto_Fujimori[/ame]
 
Kusema tu kuwa kutakufa na faida za kiuchumi kama wengi wanavyojenga hoja sidhani kama inatosha.

Mimi binafsi sidhani kama hiyo hoja ya faida za kiuchumi ina nguvu. Ila Mwanakijiji wewe unadhani wangetoa hoja gani ambayo kwa mtazamo wako unaona itakuwa na nguvu na itatosha?
 

BAK..

a. Ili kuwekeza Tanzania huitaji kuwa raia wa Tanzania.
b. Mazingira sasa hivi nchini yalivyo yanapendelea wawekezaji wa kigeni zaidi kuliko wa ndani. Hivyo, Mtanzania mwenye uraia wa nje ya nchi ataangaliwa kama Mtanzania mwingine tu hata akionesha pasi yake ya nje au itakuwaje? Au atakuwa ni wa nje kama anaishi nje lakini akiwa ndani ni Mtanzania mkazi?
c. Ukiwa raia wa nje na unawekeza nchini una haki ya kuhamisha faida yako (hata asilimia 100) kupeleka kwenye nchi yako hasa kama kuna uwezekano wa kupata faida zaidi kule kuliko huku au kuna usalama zaidi wa fedha yako. Hivyo, bado inafaa zaidi kuwa mgeni kuliko Mtanzania asiye na uraia mwingine.
d. Nchi mbalimbali ambazo zimepokea wawekezaji hakuna masharti ya kuwabana wasio raia. Wawekezaji wanaowekeza China si lazima wawe wa China lakini hawaogopi kuwekeza ati kwa sababu siyo Wachina.
e. Hadi hivi sasa Watanzania wanatuma fedha nyingi bila kujali kama ni raia bado wa Tanzania au la. Kutuma fedha nyumbani haiitaji uwe raia wa Tanzania na wala hakuna advantage yoyote isipokuwa moyo wa mtu tu kutuma fedha nyumbani au kusaidia nyumban.
 
inadaiwa yeye ni raia wa huko huko tayari.. sasa nchi inampendekezaje raia wa nchi nyingine kuwa balozi wake?


Huyo Aziz sio wa kwanza kukataliwa. wako wengi walipitishwa waende balozi mbali mbali hasa Ulaya na Marekani na majina yao yakakataliwa.SIO SABABU YA DUAL NATIONALITY KUNA VIGEZO VINGI.

Mwalimu Nyerere aliwahi kumpromise MUSTAFA NYANG'ANYI kuwa ataongea na wamarekani ili wakubali awe balozi wa Tanzania nchini Marekani.na kweli itaja kutokea KUWA NYANGANYI AKAWA BALOZI MAREKANI.KUNA MAMBO MENGI SANA HADI JINA LIKUBALIWE KWENYE NCHI HUSIKA.
 
Mimi binafsi sidhani kama hiyo hoja ya faida za kiuchumi ina nguvu. Ila Mwanakijiji wewe unadhani wangetoa hoja gani ambayo kwa mtazamo wako unaona itakuwa na nguvu na itatosha?


iko hoja moja tu ambayo inanifanya niunge mkono uraia wa nchi mbili.
 
Ya kwamba mtu asilazimishwe kuukana uraia wake wa kuzaliwa kwa vile tu kachukua uraia wa nchi ingine?

basi sio hoja moja tu ,kuna nyingine pia ndani ya hiyo hoja. From other side of the coin jiulize swali hili

kwa nini mtu ajilazimishe kuwa na uraia wa nchi nyingine wakatai tayari ni raia wa Tanganyika soory Tanzania ?
 
basi sio hoja moja tu ,kuna nyingine pia ndani ya hiyo hoja. From other side of the coin jiulize swali hili

kwa nini mtu ajilazimishe kuwa na uraia wa nchi nyingine wakatai tayari ni raia wa Tanganyika soory Tanzania ?

Mtu hajilazimishi kuwa una uraia wa nchi nyingine bana. Mtu anaomba kwa hiari yake uraia wa nchi nyingine.
 

Kweri hiri rishakuwa tumwa la kufa mtu, rinatupa nchi yake na kungángánia kwa watu!
 

BAK.
Ilikuwa hakuna haja ya kuongeza kipengele cha pili kama cha kwanza kinajitosheleza. sasa inaoneka kumbe tunafuata nchi zingine🙂
 
Kwanini tusifuate mtindo wa India ambao Katiba yao inakataza kabisa dual citizenship lakini wakati huo huo wanawatambua wananchi wao walio nje ya nchi?
 
Ya kwamba mtu asilazimishwe kuukana uraia wake wa kuzaliwa kwa vile tu kachukua uraia wa nchi ingine?

Hii hoja imeenda shule hadi imepitiliza..!!

Hoja nyingine zote zingejengwa juu ya hoja hii kama hoja mama. Sasa kinachofanyika ni kinyume, tunaifanya hoja hii ndogo na kuzipa hoja nyingine kibaumbele kwa kulazimisha.
 
Fundi Mchundo: Celine Dion ambaye ni mzaliwa wa Canada, alishaimbia Switzerland kwenye mashindano ya Eurovision mwaka 1988 na akashinda. Na cha ajabu ni kuwa ameendelea kuwa Mcanada hadi leo ingawa sijui kwa sasa anaishi Canada au USA.

Hakuna kitu kibaya kama kwenda kwenu na kuambiwa ulipie viza. Hii ndiyo inawauma watu wengi. Ni sawa na urudi kwenu na kukuta mama wa kambo kashatawala na watoto wake na wewe unaambiwa na wadogo zako muende banda la nyuma mkalale na kushinda huko.

JULIUS: Naungana na maneno yako kuwa kumnyang'anya mtu uraia wakati anataka kuchakalika nchi za watu sidhani kama ni wazo zuri. Akifanikiwa, watakuwa wa kwanza kusema "mtoto wetu huyo...." Mie nina imani kuwa Mtanzania mwenye asili ya Tanzania atakuwa muwekezaji mzuri kuliko mfanyabiashara. Serikali inaweza kukataa kutoa uraia wa nchi mbili ila ikatoa nafasi kwa wazawa kurudi nyumbani muda wowote na hata kuishi ila awe na Passport moja na tuseme kitambulisho cha uraia wa Tanzania.
 
Wanawatambua kivipi kama Taifa, tunaomba fafanua kidogo.

Inasemekana wanaangalia sura. Ila ninafikiri kuwa hawa watakuwa ni kama walivyo Wayahudi. Mambo yote yanapitia kwa Rabin/sinagogi. Huko ndiko wanatunza data zao zote (kwa wahindi ni Jamatini??) na hii iliwasaidia Waizrael kuja kuwachukua ndugu zao Ethiopia.
Wakati huyu Malikia Sheba (queen Sheba) ameenda kukutana na Mfalme Suleiman (King Solomon), huyu Malikia alipata mimba na wakati anaondoka kurudi Ethiopia, Mfalme akampa askari 300 na familia zao ili wamlinde mtoto. Hivi ndiyo walivyoanza kuishi huko hawa Wayahudi. Ila ukweli ni kuwa wakati wanarudi Izrael, kuna Waethiopia wengine walidandia kwani siyo rahisi kuwafahamu wote. India itakuwa hilohilo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…