inadaiwa yeye ni raia wa huko huko tayari.. sasa nchi inampendekezaje raia wa nchi nyingine kuwa balozi wake?
Astaghfirullah
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
inadaiwa yeye ni raia wa huko huko tayari.. sasa nchi inampendekezaje raia wa nchi nyingine kuwa balozi wake?
hapa ndiyo tatizo la uraia wa nchi mbili labda pia litaonekana. Je, tuko tayari rais wetu awe ni raia wa Tanzania na Kenya at the same time? au wa Rwanda na TZ at the same time au nchi nyingine yoyote? Vipi kuhusu Ubunge, Uwaziri, Ukuu wa Jeshi, vyombo vya usalama n.k?
acha uongo umekuwa muongo kama Membe? Dr.Sharrifu aliteuliwa kuwa balozi wa Tanzania nchini Uingereza sio Saudia. na alikuwa akifundisha University of London. hajawahi kuwa balozi wetu nchi Saudia acha uongo.na alikaa kwa muda mrefu sana Uingereza kama Balozi.Mwanakijiji,
..isije ikawa wamependekeza jina la Dr.Mlima kwa nchi ambayo wanajua atakataliwa.
..kuna jamaa aliniambia Dr.Sherrif alishaukana uraia wa Tz, lakini akateuliwa balozi wa Tanzania Saudia, na hakuwekewa kikwazo chochote.
..labda kwa huyu Dr.Mlima wangeanza na kumpeleka nchi kama Saudia,Oman,au UAE, ambako hawaulizi maswali mengi.
NB:
..haya mambo yalishamkuta Balozi Bandora[alikuwa balozi wetu Lagos] baada ya Rwanda kumteua kuwa mwakilishi wao Ujerumani.
wengine hadi uraia wa nchi tatu.jMushi1
Mkuu usibishe kitu ambacho hufahamu. Mimi binafsi nawafahamu wabongo wengi tu wana uraia wa UK, South Afrika, USA nk. hao wote bado wana passport za bongo na wanadunda tu tena usifikirie ni watu wenye hadhi za ubalozini au mawaziri etc. watanzania wa kawaida kabisa na wewe ukiambiwa utabisha. Dunia tambala bovu halikawii kuchanika.
Hili la Fujimori ni tofauti kidogo. Sidhani kama alikuwa na uraia wa nchi mbili alipokuwa rais wa Peru. Nchi nyingi tu zinatumia utaratibu wa uraia wa jus sanguinis, yaani mtu yeyote ambaye ana damu ya nchi hiyo ana haki ya kuishi nchini humo na akifuata utaratibu kupata uraia baadaye. Nchi hizi ni kama Ujerumani, Ugiriki, Japan, Estonia, Rwanda n.k. Baadhi ya nchi hizi (Rwanda n.k.) zinatoa uraia kwa yeyote yule atakayerudi. nyumbani. Fujimori kutokana na uzawa wake alikuwa na haki ya kuishi Japan na angetaka baadae kuchukua uraia. Kwa hali hiyo la Fujimori si suala la double citizenship bali mfumo wa uraia huko walikotoka wazazi wetu. Kwetu sisi, tukitaka kuzuia hiyo ni pengine kupitisha sheria kuwa mtu yeyote ambaye ana damu ya Rwanda asiwe na haki ya kutumikia nchi yake katika sehemu kadhaa! Hata kama ni babu zake ndiyo waliotoka Rwanda. Huu utakuwa ni ubaguzi wa hali ya juu.
Amandla........
Kusema tu kuwa kutakufa na faida za kiuchumi kama wengi wanavyojenga hoja sidhani kama inatosha.
Mkjj kwa maoni yangu sioni kasoro zozote hasa ukitilia maanani kwamba Tanzania inafikiria kwanza kuwapa uDC Watanzania ambao ni wazawa wa Tanzania kabla ya kuruhusu kwa wale ambao si wazawa wa Tanzania. Kama unaona faida za kiuchumi hazitoshi basi tuwekee mapungufu ambayo wewe unayaona.
inadaiwa yeye ni raia wa huko huko tayari.. sasa nchi inampendekezaje raia wa nchi nyingine kuwa balozi wake?
Mimi binafsi sidhani kama hiyo hoja ya faida za kiuchumi ina nguvu. Ila Mwanakijiji wewe unadhani wangetoa hoja gani ambayo kwa mtazamo wako unaona itakuwa na nguvu na itatosha?
iko hoja moja tu ambayo inanifanya niunge mkono uraia wa nchi mbili.
Ya kwamba mtu asilazimishwe kuukana uraia wake wa kuzaliwa kwa vile tu kachukua uraia wa nchi ingine?
Ya kwamba mtu asilazimishwe kuukana uraia wake wa kuzaliwa kwa vile tu kachukua uraia wa nchi ingine?
basi sio hoja moja tu ,kuna nyingine pia ndani ya hiyo hoja. From other side of the coin jiulize swali hili
kwa nini mtu ajilazimishe kuwa na uraia wa nchi nyingine wakatai tayari ni raia wa Tanganyika soory Tanzania ?
jokaKuu,
Akena alitoka Uganda. Na hiyo ilifahamika. Hakimu Mkuu Georges ambaye alitoka Trinidad and Tobago aliajiriwa ikifahamika kuwa si raia lakini baada ya uhuru hatukuwa na wanasheria wa kutosha kujaza nafasi muhimu kwa hiyo wengi walichukuliwa kutoka nchi za Commonwealth wakiwemo Waghana na Wanigeria. Katika suala hili tofauti ni kwamba huyu ni Mtanzania aliyekwishachukua uraia wa kigeni na kwa bahati mbaya akateuliwa kuwa balozi wa nchi hiyo hiyo ya kigeni. Inavyoonekana Watanzania walikuwa hawajui kuwa mwenzetu kishajilipua na alipopewa uteuzi huo hakusema kuwa tayari ni raia wa kule. Sasa wenyeji wakastukia wakasema hatuwezi kumchukua raia wetu awe balozi wa nchi yenu wakampa ofa ya kukana uraia ule akakataa. Hapo ndipo utamu ulipo!
Hatufuati nchi yoyote ile Mkuu Mkjj bali ni kwenda na wakati. Nchi nyingi sana zinaona faida kubwa ya kuwashirikisha katika ujenzi wa nchi zao raia wanaoishi nchi za nje ambao tayari wana uraia wa nchi nyingine, hivyo sioni sababu zozote zile za Tanzania kusubiri kuwa nchi ya mwisho katika Afrika kufanya hivyo. Wenzetu wa Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi etc wameshafanya hivyo sijui sisi tunangoja nini!
.
Ya kwamba mtu asilazimishwe kuukana uraia wake wa kuzaliwa kwa vile tu kachukua uraia wa nchi ingine?
Kwanini tusifuate mtindo wa India ambao Katiba yao inakataza kabisa dual citizenship lakini wakati huo huo wanawatambua wananchi wao walio nje ya nchi?
Wanawatambua kivipi kama Taifa, tunaomba fafanua kidogo.