Aziz P. Mlima.. Almost ambassador?

Aziz P. Mlima.. Almost ambassador?

Au tuige Morocco ambako nasikia mtu hauwezi kuukana uraia wako wa kuzaliwa. Ukizaliwa mmorocco wewe ni mmorocco hadi kufa. Nasikia na uingereza nako hivyo hivyo.

Amandla......
 
Jmushi1,

Nafikiri ni wanawake tu ambao sio Watanzania na wameolewa na Watanzania wanaruhisiwa kuwa na uraia wa nchi mbili kwa Tanzania. Pia kuna vijana chini ya umri wa miaka 18.

Makundi mengine yeyote, kama wewe una uraia wa nchi nyingine basi kisheria huna uraia wa Tanzania.

Shukran mkuu,kwahiyo basi ina maana Jasusi na Yebo Yebo wako wrong wanapodai kuwa kuna watanzania wenye dual citizenship?
Binafsi nadhani kuna watanzania wenye ku act kama wana dual ie hao ambassadors wa nchi za middle east,lakini ukweli ni kwamba theres nothing as such as a Tanzanian with dual,is that rgt?
 
Wanaiga Marekani na Canada, United Kingdom and Israel ndio unaweza kuwa raia wa Nchi na lile taifa lako la kwanza
 
Hakuna ubaya na kuwa na uraia wa nchi mbili. Lakini pia sitaki raisi wetu, waziri mkuu, mawaziri wetu, wakuu wetu wa usalama wa taifa na wale wa majeshi ya ulinzi na usalama kuwa na uraia wa nchi mbili. Na wengine wanaweza kuongezwa. Iandikwe sheria iliyo wazi na inayoeleweka kwa wengi kwa urahisi. Lakini swala kuwanyima kabisa watu uraia wa nchi mbili kwa visingizio vya kwamba wanaweza kuja kuwa maraisi havina msingi. Mbona sasa hivi tuna sheria zinazoainisha sifa za mtu ambaye anaweza kugombea uraisi? Na mimi hapa nilipo kwa vile sina sifa hizo wala sitajisumbua kugombea huo uraisi. Come on guys....acheni hizo
 
Naomba nitofautiane na wewe kidogo hapa, nijuavyo mimi mteuliwa ndio wakwanza kuelezwa juu ya posting anayotakiwa kupewa. Dr Azziz alijuwa fika kwamba yeye ni raia wa Sweden alitakiwa aseme hilo hata kabla ya process. Tatizo naloliona hapa ni watanzania kutokuwa wakweli hata pale maslahi ya taifa yanapokuwa at stake, na kufikiri kwamba kiujanja ujanja wanaweza kupindisha ukweli.

Yeye angesema tu kwamba kwa Sweden haitawezekana, labda nchi nyingine. Hivi ukweli unauzwa kwa shilingi ngapi?
MgonjwaUkimwi,

Mtu ambaye ameendelea kutumia passport ya Tanzania huku anajua ni makosa, hata ukimwuliza kweli atakwambia kwamba ana uraia wa nchi nyingine?

Wote tumebadilisha passport kuanzia 2005, kama mtu alijaza sio raia wa nchi nyingine huku anajua ana uraia wa nchi nyingine, kweli hata ukimwuliza atakuambia ukweli?

Nafikiri hii kazi ya kuwakamata wanaodanganya ni wajibu wa serikali. Idara husika hapa watakuwa wamechemsha mno na kama tuko serious yaani mhusika wa hiyo idara hata angepoteza kazi.
 
Naomba nitofautiane na wewe kidogo hapa, nijuavyo mimi mteuliwa ndio wakwanza kuelezwa juu ya posting anayotakiwa kupewa. Dr Azziz alijuwa fika kwamba yeye ni raia wa Sweden alitakiwa aseme hilo hata kabla ya process. Tatizo naloliona hapa ni watanzania kutokuwa wakweli hata pale maslahi ya taifa yanapokuwa at stake, na kufikiri kwamba kiujanja ujanja wanaweza kupindisha ukweli.

Yeye angesema tu kwamba kwa Sweden haitawezekana, labda nchi nyingine. Hivi ukweli unauzwa kwa shilingi ngapi?

Iwapo hili hapa chini lilitokea sioni sababu ya kumlaumu Dr Aziz...

Yebo Yebo,
Alipewa nafasi ya kuukana uraia huo akakataa. That is the issue! He wants to have his cake and eat it too. Yaani atumikie Tanzania, afaidike na baadaye anapostaafu anarudi kwao.

Kwa mujibu wa Jasusi, Dr Aziz hakuficha kuwa ana-uraia wa nchi hiyo nyingine hivyo wa kulaumiwa tena wanastahili kuathibiwa kiofisi ni hao waliofanya uamuzi wa kupeleka jina kwa Rais.
 
Hakuna ubaya na kuwa na uraia wa nchi mbili. Lakini pia sitaki raisi wetu, waziri mkuu, mawaziri wetu, wakuu wetu wa usalama wa taifa na wale wa majeshi ya ulinzi na usalama kuwa na uraia wa nchi mbili. Na wengine wanaweza kuongezwa. Iandikwe sheria iliyo wazi na inayoeleweka kwa wengi kwa urahisi. Lakini swala kuwanyima kabisa watu uraia wa nchi mbili kwa visingizio vya kwamba wanaweza kuja kuwa maraisi havina msingi. Mbona sasa hivi tuna sheria zinazoainisha sifa za mtu ambaye anaweza kugombea uraisi? Na mimi hapa nilipo kwa vile sina sifa hizo wala sitajisumbua kugombea huo uraisi. Come on guys....acheni hizo

Julius.. usielewe vibaya mkuu. Binafsi sina tatizo kabisa na kuruhusu Watanzania kuweza kuwa na uraia wa zaidi ya nchi moja (sielewi kwanini lazima uwe wa nchi mbili tu!) lakini kama unavyosema lazima tuweke wazi exceptions kwa sababu.. nakumbuka Fujimori kilipomuungulia kule Peru akakimbia nchi ya asili ya wazazi wake (Japani!) akidai uraia wa kule.

Leo hii tunaona jinsi Wahaiti wenye uraia wa Marekani kilipoungua kule Haiti walivyokimbia kuonesha passport zao kuwa wao ni raia wa Marekani. Tumeliona hili hata kule Lebanon wakati mgongano kati ya Israel na Hezbollah. Tanzania itakuwa hivyo hivyo (tayari in some cases with some people in the Asian communities).

Tusipoweka mambo vizuri.. watawala wetu watakuwa ni raia wa nchi nyingine huku wakifanya mambo bila ya kujali maslahi ya nchi yetu hii kwani wanajua tukitaka kuwatia pingu wanaonesha passport zao au zile za watoto wao na kutimka kwenda "kwao"!

so.. tunaporuhusu uwezekano wa mtu kuwa na uraia wa nchi zaidi ya moja ni lazima wakati huo huo tuainishe vizuri kabisa mipaka ya jambo hilo. Sasa kama wakati huu ambapo hatuna sheria hiyo na tunajua kuwa mtu akiwa na uraia wa nchi nyingine anakuwa ameuakana uraia wetu inakuwaje katika akili timamu tunampendekeza kutuwakilisha kwenye nchi nyingine wakati siyo raia wetu!?

Kuna watu ambao walikuwa karibu sana na serikali yetu kwa miaka mingi baada ya mambo kutulia kwenye nchi zao wakafunga virago na kurudi "kwao" a.k.a Wanyarwanda tuliowadhania ni Waangaza!
 
Radosław Sikorski (born 23 February 1963 in Bydgoszcz, Poland.

Martial law in Poland refers to the period of time from December 13, 1981 to July 22, 1983, he fled to Britain, which granted him asylum the following year.
He then worked as a freelance journalist. In 1984, he took British citizenship. In the mid-1980s, Sikorski worked as a war correspondent in Afghanistan and Angola.

Returning to Poland, in 1992 he briefly became deputy defence minister in the Jan OlszewskiJan Olszewski

During the latter appointment, Sikorski became notorious in the Polish expatriate community, Polonia.

Currently he is the Minister of Foreign Affairs of the Republic of Poland.

Poland kwa sasa wanaruhusu mtu kuchukua uraia wa nchi mbili.

Ila huyo bwana Sikorski alikuwa na wa British na Poland na alipochaguliwa kushika nyadhifa kubwa, ilibidi wamnyan'ganye uraia wa British. Maana ingelikuwa kichekesho kama leo hii alivyo, Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Poland na pia ni Raia wa Uingereza.

Poland wanakitu kimoja kuwa kila raia wao anapewa Identity Card. Nilikutana na Mmoja ambaye kachukua uraia wa Tanzania na hivyo alirudisha passport ya Poland ila bado ana Kadi yake ambayo akiingia tu ndani ya Schengen, basi anaweza kuficha Pass ya Tanzania na akawa anatesa na hiyo Kadi yake.

Kwa faida ya WAZAWA, mtu anayerudisha Passport, anaweza kupewa Kadi ambayo itaruhusiwa kutumika mpakani mwa Tanzania. Hivyo, kama mtu anataka kwenda kuchakalika, basi anaweza kuchukua Passport mpya na kurudisha ya Tanzania. Akichoka kuishi huko, anaweza kurudi na kuomba Passport yake upya na ile ya ugenini wanaichukua na kuirudisha kwa wenyewe.
Mie walininyang'anya Driving Licence ya Tanzania na kuipeleka Berlin. Sijui iko pale au walishairudisha Tanzania? Unakuta wakati mwingine hata hawafahamu waifanye nini pale ubalozini. SIntashangaa nikisikia walilitupa maana hata muda wake umeisha.
 
Shukran mkuu,kwahiyo basi ina maana Jasusi na Yebo Yebo wako wrong wanapodai kuwa kuna watanzania wenye dual citizenship?
Binafsi nadhani kuna watanzania wenye ku act kama wana dual ie hao ambassadors wa nchi za middle east,lakini ukweli ni kwamba theres nothing as such as a Tanzanian with dual,is that rgt?
jmushi1
Hapana. Sijakosea. Kuna Watanzania wana uraia wa nchi mbili kama si zaidi. Shida inakuja kwenye sheria zetu na udhibiti wake. Either hatuna uwezo wa kuwashughulikia au basi tu hatuna ari ya kuhakikisha sheria inafuatwa. Tena wamejaa serikalini. Hata waziri mmoja inashukiwa ni dual citizen. Lakini usinichokonoe zaidi.
 
Membe atakuwa London kwenye mkutano wa diaspora wiki chahce zijazo.Nadhani itakuwa fursa nzuri akiulizwa kuhusu huo mchakato usio na mwisho about dual citizenship.
 
Nadhani Mkjj amesimama kidete kuupinga uDC...kila la heri Mkjj lakini ujue Watanzania wa 2010 ni tofauti sana na wale wa mwaka 47 ambao walikuwa wakipata bahati ya kupata kazi nchi za nje kutokana na kuwa na vyeti vya nguvu asilimia 99% bado walifikiria kurudi nyumbani ili wakasukume "gurudumu la maendeleo". Hawa wa 2010 hawalazi damu wakipata tu opportunity ya kuuchangamkia uraia, basi hufanya hivyo haraka sana bila kujali Tanzania kama itaruhusu uDC au la.
 
Iwapo hili hapa chini lilitokea sioni sababu ya kumlaumu Dr Aziz...

Kwa mujibu wa Jasusi, Dr Aziz hakuficha kuwa ana-uraia wa nchi hiyo nyingine hivyo wa kulaumiwa tena wanastahili kuathibiwa kiofisi ni hao waliofanya uamuzi wa kupeleka jina kwa Rais.
Yebo Yebo,
Sikusema kuwa the said official hakuficha. Kilichotokea ni kwamba ile nchi aliyokuwa aende kuwa balozi ndio waliofichua kuwa huyu mbona ni raia wetu? Na ili kuokoa jahazi wapakendekeza akane uraia wao. Akakataa. That is what I said. He wanted to have his cake and eat it too. Talk about loyalty!
 
Nadhani atakuwa ameonewa kama loyalty yake ikipimwa kwa level hii,kwasababu first si nafasi ya urais ama hizo nyinginezo za usalama,jeshi nk....Pili sidhani kama ali apply,nadhani majina yanapendekezwa na watu flani...Ofcourse inaonyesha serikali haijali kwani iko mguu ndani mguu nje,hii ni kama habari za kuwapeleka mabalozi wasiokuwa raia wa Tanzania kwenye nchi zisizouliza kama Saudi nk.
 
inadaiwa yeye ni raia wa huko huko tayari.. sasa nchi inampendekezaje raia wa nchi nyingine kuwa balozi wake?

Wenzetu system zao zinafanya kazi huyu jamaa wanamfahamu zaidi ya Tanzania tunavyomfahamu inawezekana ni jangili flani hivi kwa hiyo hawawezi kuafiki umafia wake kwenye nchi yao ambayo inafuata utawala wa sheria. Tena ni aibu kubwa kwa Tanzania. Stupidity of the highest degree in the highst office.

Labda hili suala la dual citizenship inabidi tulifikiria jinsi litakavyofanya kazi kwa public servants wetu isije kutokea yale ya Fujimori kule Peru!

Thanks ka nzi!

Wanaotaka kuwa raia wa nchi nyingine kwa nini bado wanatamani kazi za wabongo? Haiingii akilini kuukana uraia wako lakini unatamani fweza za walipa kodi wake.

Swala la dual lazima liwe exception tu kwa watoto waliozaliwa na wazazi nje ya Tanzania kwa sababu by right kule walikozaliwa wanaweza kudai uraia na hawatanyimwa kama wanafuata utaratibu.

Mzee Mwanakijiji,

..nahisi jamaa yako kaingizwa mjini huyo.

.kama anautaka ubalozi aombe na ang'ang'anie apelekwe Middle East ambako hawana longolongo/hawachunguzi kama wanavyofanya jamaa wa European Union.

Kwani hakuna Watanzania wengine walio na sifa? Hii Ikulu imejaa majambazi.

kwa hiyo unafikiri tunaweza kuwa na Rais ambaye si Mtanzania? sijazungumzia tatizo la kuwa na mtu ambaye si Mtanzania kushika nafasi mbalimbali hata Zanzibar waliwahi kukopa Jaji Mkuu kutoka Nigeria???

Marekani haina uraia wa nchi mbili kama watu wanavyoamini; Marekani inatambua uraia wake tu.

Zamani tulikuwa hatuna wasomi wa kutosha hivyo kama unakumbuka tulikuwa hata na askari utoka Nigeria miaka ya 1960's sio sasa hivi wakati wabongo wengi wanahitaji hizo kazi.

Pamoja na haya yote kutokea sidhani kama kuna kimburu yoyote atawajibishwa tumezoea uozo na uozo huo ndio unaendelea. Sijui kama tulikuwa tunafahamu tunawaweka pimbi wa aina gani pale Magogoni.
 
Tusipoweka mambo vizuri.. watawala wetu watakuwa ni raia wa nchi nyingine huku wakifanya mambo bila ya kujali maslahi ya nchi yetu hii kwani wanajua tukitaka kuwatia pingu wanaonesha passport zao au zile za watoto wao na kutimka kwenda "kwao"!

Hapa tupo pamoja asilimia 100. Ni lazima kuweka mambo sawa. Na hili si jambo la kukurupukia. Ni jambo ambalo itabidi tuchukue muda wetu kulijadili na kulifanyia kazi kwa kuangalia mifano kama ya kina Alberto Fujimori. Hata Marekani kama Mmarekani hajakaa Marekani kwa miaka 13 mfululizo (kama sijakosea idadi ya miaka) hawezi kugombea uraisi. Unaona wenzetu walivyo wajanja? Na uzuri wa sheria unaweza ukazibadilisha, ukaongeza na kupunguza vipengele kwa kadri ya mahitaji. Sasa baada ya Fujimori kuwageuzia kibao Peru sijui kama walibadili sheria yao kuhusu jambo hilo.

so.. tunaporuhusu uwezekano wa mtu kuwa na uraia wa nchi zaidi ya moja ni lazima wakati huo huo tuainishe vizuri kabisa mipaka ya jambo hilo. Sasa kama wakati huu ambapo hatuna sheria hiyo na tunajua kuwa mtu akiwa na uraia wa nchi nyingine anakuwa ameuakana uraia wetu inakuwaje katika akili timamu tunampendekeza kutuwakilisha kwenye nchi nyingine wakati siyo raia wetu!?

Hili la kumpendekeza huyu jamaa ni moja ya mifano mingi tu ya jinsi gani serikali yetu ilivyo dysfunctional. And the dysfunction starts at the very top and sadly it trickles all the way down to the bottom. It's lunacy.

Kuna watu ambao walikuwa karibu sana na serikali yetu kwa miaka mingi baada ya mambo kutulia kwenye nchi zao wakafunga virago na kurudi "kwao" a.k.a Wanyarwanda tuliowadhania ni Waangaza!

Yeah hili ni tatizo dogo katika picha kubwa ya ukosefu wa utawala wa sheria. Rule of law ni kitu muhimu sana. Sijui kama watu wanalitambua hilo.
 
Nadhani Mkjj amesimama kidete kuupinga uDC...kila la heri Mkjj lakini ujue Watanzania wa 2010 ni tofauti sana na wale wa mwaka 47 ambao walikuwa wakipata bahati ya kupata kazi nchi za nje kutokana na kuwa na vyeti vya nguvu asilimia 99% bado walifikiria kurudi nyumbani ili wakasukume "gurudumu la maendeleo". Hawa wa 2010 hawalazi damu wakipata tu opportunity ya kuuchangamkia uraia, basi hufanya hivyo haraka sana bila kujali Tanzania kama itaruhusu uDC au la.

BAK.. unanielewa vibaya kabisa. Mimi sipingi uraia wa nchi mbili at all.. napinga kanuni zinazopendekezwa. Hatuwezi kubadilisha nature ya uraia wetu kwa sababu ya rangi, nasaba, hali ya kiuchumi, kufuata mtindo n.k.. we have to articulate proper arguments why we have to change.. siyo nchi zote duniani zinaruhusu uraia wa nchi mbili hata zile za kiafrika au za kimagharibi. Sielewi kwanini tuonekane tunafuata zile za nchi fulani na zile za nchi nyingine tuone hazifai.
 
Serikali iko bias hapa,ni kama inautambua urai wa nchi mbili na wakati huo huo haiutambui.
 
jmushi1
Hapana. Sijakosea. Kuna Watanzania wana uraia wa nchi mbili kama si zaidi. Shida inakuja kwenye sheria zetu na udhibiti wake. Either hatuna uwezo wa kuwashughulikia au basi tu hatuna ari ya kuhakikisha sheria inafuatwa. Tena wamejaa serikalini. Hata waziri mmoja inashukiwa ni dual citizen. Lakini usinichokonoe zaidi.

Si kweli,i beg to differ,nadhani watanzania wenye uraia wa nchi mbili ni hao mabalozi wanaoiwakilisha nchi huko middle east,nje ya hapo si watanzania tena,rather ni "waliokuwa watanzania" ambao sasa ni raia wa nchi nyingine,mfano huyo wa nchi ya Scandnavia,yeye si mtanzania tena,however angeweza kuwa mtanzania kama angepelekwa huko middle east ama kama sheria ingebadilishwa.
 
Back
Top Bottom