Azzan Zungu ataka uwepo wa kodi ya uzalendo itakayokatwa kwenye Mitandao ya simu kwa kila Mtanzania

Azzan Zungu ataka uwepo wa kodi ya uzalendo itakayokatwa kwenye Mitandao ya simu kwa kila Mtanzania

kama nimemsikia vizuri 30,000,000x50=540,000,000,000!
na 30,000,000x100=1,800,000,000,000!
Naomba kusahihishwa kama nimekosea
 
Nngekumuona ni mzalendo kweli kama angeshauri yafuatayo;
  1. Posho zote za wabunge zikatwe kodi kama wanavyofanywa wananchi wengine.
  2. Mafao yao wanayolipwa kila baada ya miaka 5 nayo yakatwe kodi
Hiki ndicho kipimo chao cha uzalendo kitakavyopimwa.
 
Wamebaki wenyewe sasa wanabwabwaja tu ndo urithi aliotuachia Magu mitano tena
 
Mbunge wa Ilala, Azzan Zungu ametaka kuwepo na kodi ya uzalendo itakayokatwa katika mitandao ya simu kwa kila Mtanzania kwa siku kama chanzo kipya cha mapato kwa Serikali.
Huyu naye ni hamnazo kabisaaa!!! Kwakuwa yeye na familia yake wanakula wanashiba basi anafikiri kumkamua mwananchi wa chini, ningemwona wa maana angeanza yeye na familia yake, kisha awashawishi magabachori wenzake, mjinga kabisa hajui kuna watu hawana hata sh. 200 ya kununua majani ya chai!!! shame on him!!!
 
Huyu bwanyenye pumbavu sana anataka kurudisha kodi ya kichwa
Ni kweli ndiyo maana kila mwananchi sasa hivi amewadharau, ningemwona wa maana angetangaza kuishi bila mshahara wala posho kwa miezi 6 ili ajifunze wananchi wa chini wanatesekaje ndipo aje na hoja zake
 
Isitoshe uzalendo haulazimishwi kwa matakwa ya gabachori
 
Haya ndo yale mabunge ambayo hayanaga point za msingi bungeni litakalokuja kichwani linalopoka tu bila kuangalia nyuma na mbele.
Usishangae kuna cku tena litasema watanzania walipe kodi ya nguo wanazovaa. Lipo limelunda mwili bungeni bila kujali kuna watanzaia maskin jinga hili
 
Yeye analipa kodi kiasi gani?
Wabunge hawalipi kodi, waanze kukatwa ikijumuishwa na posho zao. Wabunge wengi ndio wamiliki wa mabasi, daladala, bajaj, malori, masoko maalum (supermarkets), ubia na viwanda binafsi, wamiliki wa vituo vya mafuta, maduka ya kuuza magari nk.

Wanatunga sheria za kujipendelea lakini wanakwepa kutunga sheria za kulinda wenye vipato vya chini ili wawanyonye vizuri wakati wakijua hakuna mtetezi.

Kama ubunge na biashara vikitenganishwa akili zitawaijia na kuwatetea wananchi na taifa kwa dhati bila hivyo WATANZANIA POLENI SANA mtaendelea kuumia huku wakiwapulizia maneno matamu yasiyolambwa hata siku moja.

1. FAO la KUJITOA lirejeshwe mara moja kama kweli wabunge waliopo bungeni wako kwa maslahi ya wananchi bila hivyo ukurasa wao unapaswa kufutwa (PESA zilizohifadhiwa kwenye mifuko ya kijamii ni mali ya mchangiaji SIO ya serikali wala umma kwa hiyo SIO hisani kudai irejeshwe kwa wanufaika)
2. UBUNGE na BIASHARA vitenganishwe haraka ili kulinda maslahi ya wananchi na umma
3. ELIMU UJUZI (Kawaida, kati na wa Juu) ufundishwe kwa VITENDO (asilimia 85%) kuanzia sekondari hadi chuo/chuo kikuu badala ya elimu NADHARIA na elimu TAALUMA ambazo hazisaidii mhitimu kujiajiri mwenyewe maana hakuna serikali yoyote duania iliyofaulu kuajiri kila anayehitimu/shule/chuo/chuo kikuu
4. Wajasiriamali wadogo (mama lishe, bodaboda, bajaj, machinga) watengewe maeneo maalumu rafiki kuendesha shughuli zao bila bughudha huku vitambulisho vyao vikiboreshwa kwa kuongezewa taarifa nyingi zilizounganishwa na kitambulisho cha taifa ikiwemo (picha, namba ya simu, makazi, wazazi wake, tarehe kuzaliwa nk). Walipo kwenye kitambulisho hicho yawe TZS 35,000/= kwa mwaka ambayo atalipia kwa muda wa miaka mitatu kwa mfululizo, baada ya hapo biashara yake ifanyiwe tathimini kwenda daraja jingine ili kuhimiza ushindani na kuongeza kipato kwa pande zote mbili bila kuumia (nchi inamhudumia kila raia kwa gharama sawa na mwenye kipato cha chini kama ulizni na usalama, huduma za jamii, miundo mbinu, nishati na maji nk)
5. Wafanyabiashara wenye mitaji mikubwa wasaidiwe kuwa na mazingira yasiyozongwa na biashara ndogondogo mbele yao maana hapo pana hujuma mbili (mfanyabiashara mkubwa kukosa kuuza bidhaa zake kwa wingi na muda mchache hivyo kuingia hasara za uendeshaji la pili ni ukwepaji wa kodi mfanyabiashara mkubwa kwa kuamua kumpa mjasiriamali mdogo kuuza bidhaa zake kwa mapatano ya kupewa kamisheni ya kiwango cha mauzo maana anajua hakuna kodi anayodaiwa) Serikali itaendelea kuona maduka makubwa yamejaa bidhaa lakini wamiliki wakijitetea kushindwa kufanya biashara kwa kuwa machinga wamehodhi soko;
6. Vinywaji vikali ndio viongezwe kodi
7. Wamiliki wa nyumba warasimishwe na kupewa hati halali za serikali ili kodi kulingana na matumizi,eneo, na thamani yake yatozwe kodi bila bughudha kama inavyoendelea kwa sasa kuna uonevu mkubwa sana
8. Utalii wa miji, vijiji, hifadhi, misitu, utamaduni na miundombinu uhimizwe kwa watanzania wote kwa gharama nafuu na bila ukiritimba usiokuwa na tija, (kwa mfano mtu anatoka Ifakara, Kilosa au Iringa anataka kutembelea mbuga ya wanyama Mikumi akifika kwa wakala waliopo hapo Mikumi anaambiwa aende kulipia gharama za kuingia hifadhini Morogoro mjini yapata kilomita 132 hivi kisha ajiandikishe kwenye usafiri wa Coaster au kama ana gari binafsi ni sharti liwe na 4Drive hata kama gharama za usajili huo ni kidogo lakini hizo za nyongeza zinapandisha gharama kwa msingi huo hakuna mwananchi wa chini atakayeweza kumudu kutembela hifadhi hizo hadi anazeeka hii ni aibu kwa serikali
9. Maeneo mengi ambayo kwa kweli laiti kama utalii wa ndani ungehimizwa bila kuhodhiwa na matajiri ungeleta neema kwa wananchi na taifa kwa ujumla. Mji wa Mikindani Mtwara bado haujawekewa kipaumbele cha kutosha hata kwenye kwenye ramani vizuri ili watu wafunge safari kwenda kujifunza kwa kuona na majumba kongwe yalivyo hadi sasa. Mji wa Lindi kwa maoni yangu ndio ungeteuliwa kuwa mji mkongwe na unaobeba utamaduni halisi wa wenyeji wa kanda ya kusini maana hakuna maghorofa makubwa yaliyojengwa kubadilisha uhalisia uliokuwepo tangua miaka ya 1925-1961 (Lindi landscape lying aong the Indian ocean coast is beautiful decoarated by mangrove trees, coral reeves and ancient building structures is unforgatable to recommend for as many as possible local and foreign tourists to enjoy the entertaining natural features). Nawahimiza watanzania wote unapopata nafasi tembela Mtwara (Masasi, Mikindani, Shangani, Msanga mkuu nk), Lindi (mjini na Kilwa masoko/kivinje) na Ruvuma (mjini ambako chifu Songea alizikwa, Mbamba bay, Tunduru) . Kumbuka Korosho inayopatikana Mtwara ndiyo bora sana kwa maandalizi, ladha na thamani yake usisahau supu ya samaki kama ilivyo huko kanda ya ziwa kwa supu ya sato (very delicious and nutrient for health improvement).
10. Viwanda vinavyotengeneza vifaa vya ujenzi (simenti, bati, na rangi vipunguziwe kodi) hivyo kuhalalisha kushushwa kwa bei iliyo himilivu kwa watumiaji (wananchi wa kawaida) wamuda ujenzi na kuondokana na kupanga miaka yote
 
Wife: How much do you love me?
Husband: My heart is a mobile and you are the sim of it.
Wife: OMG! I'm so lucky you love me so much.

She really don't know that her Husband is a dual sim.
 

Kodi ya Uzalendo Ianze Sasa kwa Wabunge Wetu​


image.png

Na Nkwazi Mhango

Kwenye kikao cha bunge kinachoendelea, Mbunge wa Ilala, mheshimiwa Musa Azzan Zungu (CCM) alitoa wazo zuri la namna ya kukuza wigo wa kodi kwa ajili ya mapato ya taifa. Alipendekeza kuanzishwa kwa kodi ya uzalendo ambapo kila mtumia simu anapaswa kutozwa angalau shilingi mia. Hili wazo, kama nilivyosema hapo juu ni zuri. Ila katika utekelezaji wake tunapaswa kuwabana wale wanaopata fedha nyingi kama mishahara au marupurupu. Hivyo, kuanzia, tuanzie na wabunge ambao mishahara na marupurupu yao ni makubwa ukiachia mbali kutokatwa kodi. Kama tutalenga kweli kupanua wigo wa mapato, basi waheshimiwa wabunge wakatwe kodi kwenye mishahara na marupurupu yao ambavyo ni vikubwa ikilinganishwa na wale wanaosema wanawawakilisha.
Natoa pendekezo hili la kuanza na wabunge kutokana na sababu zifuatazo:

Kwanza, wanapata mishahara mikubwa na marupurupu makubwa ikilinganishwa na wananchi wa kawaida wanaowawakilisha. Kwanini wawakilishwa wakatwe kodi lakini watumishi wao ambao ni wabunge wasikatwe kodi?

Pili, wabunge––––ambao ni kioo cha jamii kama viongozi na wawakilisha wa umma kama kweli wanauwakilisha na siyo kujiwakilisha–––wanapaswa kuonyesha mfano mzuri wa kuchangia kupanua wigo wa mapato kwa taifa lao kwa ajili ya maendeleo na ufanisi wa waajiri wao na taifa kwa ujumla.
Tatu, wabunge wetu ni wengi kuliko idadi inayohitajika kulingana na uwezo wetu wa kiuchumi kama taifa. Kimsingi, majimbo yetu mengi yameanzishwa kisiasa na si kiuchumi wala kiuhalisia. Hata baadhi ya mikoa nayo kadhalika imeanzishwa kisiasa hasa tukizingatia kuwa tokana na kuwa na miundo mbinu mizuri kwa sasa, tuna haja ya kuipunguza. Hivyo, sehemu nyingine ya kupanua wigo wa mapato ya serikali ni kubana matumizi ambapo mojawapo ya njia inanaweza kuwa kupunguza majimbo ya uchaguzi. Mfano, ukiangalia wabunge watokao visiwani na idadi ya watu wanaowakilisha, unashangaa mantiki ya jumla ya kufanya hivi. Katiba ya Tanzania inatamka wazi kuwa watanzania wote ni sawa. Je ni usawa gani iwapo wabunge mfano, toka Visiwani wanawakilisha idadi ndogo ya wapiga kura na wananchi wakati watokao Bara wanawakilisha idadi kubwa? Lazima tukiri. Hapa kuna tatizo la kimfumo ambalo lisiposhughulikiwa, linaweza kuleta malalamiko baadaye.

Nne, kama ilivyodokezwa hapo juu, mishahara na marupurupu ya wabunge ni makubwa. Kwanini wananchi wenye mishahara kiduchu–––tena ambayo haijapandishwa kwa miaka mingi–––wakatwe kodi lakini wabunge wasikatwe kodi wala kuwa na mishahara inayolinga au kufanana au kukaribia na ile ya wale wanaowawakilisha? Kazi ya serikali siyo kuhudumiwa wanasiasa huku ikiwaminya wananchi wa kawaida.

Ukiachia mbali na kuwakata kodi wabunge–––na hata ikiwezekana kupunguza marupurupu yao na hata majimbo–––kuna haja ya kubana matumizi kwa kupunguza nafasi za kisiasa zisizo na ulazima zaidi ya kuwapo kwa sababu za kisiasa kama utititiri wa majimbo. Kwa kumbukumbu ni kwamba Hayati John Pombe Magufuli alipunguza mshahara wake na ile ya wakurugenzi waliokuwa wakipata mishahara mikubwa kuliko hata rais na mawaziri ili kuleta uwiano wa kipato na usawa. Je kwanini mantiki haya yasitumike hata kwa wabunge ambao kimsingi, ni matajiri ikilinganishwa na wananchi wa kawaida wanaodai kuwawakilisha. Ukitaka kujua kuwa ubunge ni sehemu ya kutajirikia, angalia namna watu wanavyoacha hata taaluma zao na kujiunga na siasa ili kupata hii fedha na kutajirika haraka. Watu wako tayari kutoa hata rushwa ili waupate ubunge kwa vile unalipa sana. Wengine wanaacha hata makanisa yao ili kwenda kuchuma fedha hii kubwa inayowafanya si wawe matajiri tu bali hata wawe na ushawishi katika jamii. Hivyo, njia mojawapo inayoweza kuongeza mapato ya serikali ni ku-decolonise ubunge na nafasi nyingine za kisiasa ambazo zinatoa mishahara mikubwa isiyolingana uhalisia wa taifa kiuchumi.

Suala jingine ni kuachana na mfumo wa kikoloni ambapo uchumi ulitumikia siasa badala ya siasa kutumikia uchumi. Tangu tupate uhuru, tulishindwa kuliona hili. Tulisahau kuwa wakoloni walikuwa wakipeana mishahara mikubwa kama njia ya kutudhoofisha ili waendelee kutunyonya na kutusikinisha ili tuwategemee kama ilivyo sasa. Sioni mantiki ya mbunge ambaye, kimsingi, hana ulazima wala hatoi huduma inayohitajika sana kuwa na mshahara mkubwa kuliko daktari au profesa. Ubunge hausomewi wala hauna ulazima wa kujieleza mambo yanapokwenda mrama sawa na watumishi wa umma na wana taaluma. Tokana na ubovu huu wa kimfumo, hata vijana wetu siku hizi hawana motisha wa kusoma. Badala yake wanaona usanii, siasa, uhubiri na mambo kama hayo ni muhimu kwa vile vinawaingizia fedha kuliko usomi.

Eneo jingine linaloweza kutozwa kodi kubwa ni masuala yote ya starehe. Kwa mfano, mabaa, kumbi za muziki, wanamuziki na wasanii kwa ujumla, wanapaswa kutozwa kodi ya kutosha kwa vile huduma zao ni za upili na siyo za kwanza kwa maisha ya binadamu. Ili nisionekane nawakandamiza baadhi ya watu wetu, inakuwaje, mfano, mwanamuziki awe na fedha nyingi kuliko daktari au mtunzi wa vitabu ya kiada kama siyo mfumo mbovu wa kuangalia nini tunataka kama binadamu na taifa? Katika hali ile ile, inakuwaje mazao ya mkulima yawe na bei ya chini kuliko hata muziki ambao hauliwi wala kuhitajika sawa na chakula? Jibu ni ni wazi kuwa tulirithi mfumo wa kijambazi na kikoloni ambapo watu wachache wananeemeka kwa mgongo wa maskini walio wengi. Kimsingi, mfumo huu hauna tofauti na mfumo wa sasa ambapo mtu anaamka asubuhi na kuanzisha kanisa lake na kuanza kuwanyonya maskini na wajinga waliokata tamaa na kulala tajiri bila hata kutozwa kodi huku serikali ikiangalia na kulalamika haina vyanzo vya kupanulia wigo wa kodi kwa ajili ya mapato ya serikali. Hii ndiyo siri ya utitiri wa makanisa kila sehemu kwa vile ni biashara inayoingiza fedha nyingi bila kukatwa kodi sawa na siasa.

Japo binadamu anahitaji huduma za kiroho na kisiasa, si kwa ulazima sawa na huduma kama afya, elimu, chakula, mavazi, maji na hata uzoaji taka mijini ambavyo umuhimu wake ni wa kwanza na wajuu kuliko miziki, maigizo, nyimbo, mpira, siasa, dini na mengine kama hayo.

Naomba niwasilishe kwa kutoa mchango wangu wa namna ya kupanua wigo wa mapato kwa kuangalia mambo ambayo hatukuyaona au kuyarekebisha kama tulivyoachiwa na wakoloni nasi tukayashikilia na kuyaendeleza hata baada ya kupata uhuru. Mfano mdogo, hapa Kanada, mambo yasiyo ya ulazima wa kwanza katika maisha ya binadamu yanatozwa kodi ya juu kiasi cha kutisha ili kupata fedha ya kugharimia huduma za msingi na siyo za upili. Mfano, wabunge hapa wanajiendesha. Hakuna serikali kuwalipia fedha za madereva, wasaidizi na mengine kama hayo. Hivi tukiondoa madereva wa wakuu wa idara, mawaziri, wabunge, makatibu wakuu wa wizara, makatibu wakuu wasaidizi, manaibu wa mawaziri, wakuu wa wilaya na mikoa, wakurugenzi wa kada mbali mbali na wengine wengi wanaoweza kujiendeshea magari yao tutaokoa mabilioni mangapi? Je hao madereva na wasaidizi wengine wadogo wanahitajika?

Hakuna haja ya kulalamika wala kuwabana walalahoi bure. Hivi ni vyanzo vikubwa na vizuri vya mapato. Basi waheshimiwa wabunge waonyeshe mfano kwa kuanza kubana matumizi yao na kutozwa kodi ili umma ufuatie.
 
Tatu, wabunge wetu ni wengi kuliko idadi inayohitajika kulingana na uwezo wetu wa kiuchumi kama taifa. Kimsingi, majimbo yetu mengi yameanzishwa kisiasa na si kiuchumi wala kiuhalisia. Hata baadhi ya mikoa nayo kadhalika imeanzishwa kisiasa hasa tukizingatia kuwa tokana na kuwa na miundo mbinu mizuri kwa sasa, tuna haja ya kuipunguza. Hivyo, sehemu nyingine ya kupanua wigo wa mapato ya serikali ni kubana matumizi ambapo mojawapo ya njia inanaweza kuwa kupunguza majimbo ya uchaguzi. Mfano, ukiangalia wabunge watokao visiwani na idadi ya watu wanaowakilisha, unashangaa mantiki ya jumla ya kufanya hivi. Katiba ya Tanzania inatamka wazi kuwa watanzania wote ni sawa. Je ni usawa gani iwapo wabunge mfano, toka Visiwani wanawakilisha idadi ndogo ya wapiga kura na wananchi wakati watokao Bara wanawakilisha idadi kubwa? Lazima tukiri. Hapa kuna tatizo la kimfumo ambalo lisiposhughulikiwa, linaweza kuleta malalamiko baadaye.
Kuna mtu alisema hilo Bunge ni genge la wezi waliokubuhu, hebu tazama kwanini wanaikataa katiba mpya kama si kwakuwa imekosoa mfumo tulio nao hivi sasa?
 
Kuna baadhi ya masuala yakigusiwa nahisi vinyweleo vinanisisimka. Miongoni mwayo ni suala la mfumo wetu wa elimu na hili la mishahara na marupurupu ya viongozi wa umma na wale wa kisiasa.

Uwiano wa maisha katika mambo ya msingi nchini kwetu unatia kichefuchefu. Umbali uliopo ni mkubwa Sana na hausababishwi na Elimu au ujuzi bali nafasi.

NITAFAFANUA
Shule ya Msingi Bunge (mfano) inawalimu 50 ambapo idadi ya wanafunzi kuanzia darasa la 1 -7 ni 300.

Shule ya Msingi Vingunguti A inawalimu 5 na ina jumla ya wanafunzi 1,200. Mikoani tusiende kwakua hali inatisha sana uwiano umeshuka hadi kufikia walimu 3 kwa wanafunzi 800. Si dhani kama unaweza ukamuhukumu mwanafunzi akimaliza darasa la Saba na hajui kuandika jina lake vizuri achilia mbali la aliyemleta duniani!

Ukienda kwenye Afya, Maji, makazi ni haki ya kutisha.

TATIZO
Waliowahi kuwa na madaraka waliamua kujilimbikizia mali na wakaona haitoshi wakajilimbikizia posho na marupurupu pia! Na kama haitoshi wakaamua kuyafanya yakudumu hadi vifo vyao.

MFANO
Mtumishi wa umma wa kawaida Graduate analipwa takehome ya 750,000/- alafu Mbunge analipwa 130,000/ posho ya kupiga meza na usafiri na mafuta na bima ya afya na muda wake ukiisha anakabidhiwa marupurupu yasiyo na kodi yoyote.

Mwalimu wa shule ya Msingi alipwe 250,000/- take home ajigharamie usafiri, makazi, chakula.

Hizi hesabu zinanishinda kukokotoa. Alafu Mbunge huyo anataka iwepo kodi ya UZALENDO.

HAKIKA ALIYESHIBA HAMJUI MWENYE NJAA...
 
Kodi ya uzalendo...?! Sheria za Kodi zinasemaje...
Hata ngoma ya kuanza kujenga bandari ya Bagamoyo amepewa Azan Zungu aipige kwa kuamini kwamba ndiye mawazo sahihi yanayochukuliwa na utawala huu kwamba yanafaa. Si muda mrefu ujenzi unaanza kwa ujasiri.

The rats are dominating the house in the absence of the cat.........................
 
Nawasalimu kwa jina la CCM

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza ni kwamba nasisitiza hakuna hoja inayotamkwa bungeni kwa bahati mbaya. Mbunge akisimama na kuanza kuzungumza tukubali kwamba tayari ilishapangwa na kufikiriwa. Hakuna bahati mbaya wala nini. Tusikimbilie kumbeza mbunge na kumwita kilaza au ana roho mbaya.

Majuzi hapa alisimama mbunge Zungu na kutaka tukatwe tsh 50 kila siku kwenye simu zetu ili kulipa kodi ya uzalendo. Siku kadhaa baadae tumeona Waziri wa fedha akija na kodi za kwenye miamala ya fedha na muda wa maongezi kwamba ni kodi za uzalendo. Kumbe Zungu alikuwa anatuandaa tu kisaikolojia kwa kile kilichokuwa kinaenda kutokea. Hii kodi ya uzalendo ni kodi ya kichwa iliyoboreshwa. Na ni zaidi ya kodi ya kichwa kwasababu hii watalipa hata watoto wadogo tofauti na ile ya kichwa.

Nyakati fulani katika haya maisha ya dhambi aliwahi kuniambia kitu msichana mmoja kwamba kamwe serikali haijawahi kusamehe wala kufuta kodi yoyote. Kinachofanyika ni kodi hii kuhamishwa hapa na kupelekwa pale. Hii serikali yetu imefanya ubunifu wa kuondoa TASKFORCE kwenye kukusanya kodi lakini ni kwamba watu wote tupende tusipende lazima tulipe kodi. Hii haina kukwepa. Utaamua umeze au uteme.

Binafsi najua kuna kibano kikali kinakuja kwasababu ya hii miradi mikubwa kama SGR, bwawa la umeme nk. Pia waziri kasema barabara zitazidi kujengwa kwa kupitia "kodi ya uzalendo".... naisihi sana serikali ya CCM itumie vizuri hela zitakazopatikana kufanya mambo waliyotuahidi yatafanyika kupitia hii kodi ya uzalendo. Yale mambo ya kusikia maafisa flani wamefakamia bilioni kadhaa kifisadi hayatavumilika.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
 
Nawasalimu kwa jina la CCM

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza ni kwamba nasisitiza hakuna hoja inayotamkwa bungeni kwa bahati mbaya. Mbunge akisimama na kuanza kuzungumza tukubali kwamba tayari ilishapangwa na kufikiriwa. Hakuna bahati mbaya wala nini. Tusikimbilie kumbeza mbunge na kumwita kilaza au ana roho mbaya.

Majuzi hapa alisimama mbunge Zungu na kutaka tukatwe tsh 50 kila siku kwenye simu zetu ili kulipa kodi ya uzalendo. Siku kadhaa baadae tumeona Waziri wa fedha akija na kodi za kwenye miamala ya fedha na muda wa maongezi kwamba ni kodi za uzalendo. Kumbe Zungu alikuwa anatuandaa tu kisaikolojia kwa kile kilichokuwa kinaenda kutokea. Hii kodi ya uzalendo ni kodi ya kichwa iliyoboreshwa. Na ni zaidi ya kodi ya kichwa kwasababu hii watalipa hata watoto wadogo tofauti na ile ya kichwa.

Nyakati fulani katika haya maisha ya dhambi aliwahi kuniambia kitu msichana mmoja kwamba kamwe serikali haijawahi kusamehe wala kufuta kodi yoyote. Kinachofanyika ni kodi hii kuhamishwa hapa na kupelekwa pale. Hii serikali yetu imefanya ubunifu wa kuondoa TASKFORCE kwenye kukusanya kodi lakini ni kwamba watu wote tupende tusipende lazima tulipe kodi. Hii haina kukwepa. Utaamua umeze au uteme.

Binafsi najua kuna kibano kikali kinakuja kwasababu ya hii miradi mikubwa kama SGR, bwawa la umeme nk. Pia waziri kasema barabara zitazidi kujengwa kwa kupitia "kodi ya uzalendo".... naisihi sana serikali ya CCM itumie vizuri hela zitakazopatikana kufanya mambo waliyotuahidi yatafanyika kupitia hii kodi ya uzalendo. Yale mambo ya kusikia maafisa flani wamefakamia bilioni kadhaa kifisadi hayatavumilika.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
Sasa ni yapimaoni kuhusu kodi yako hiyo pendwa.
 
Back
Top Bottom