Baa Sinza zinaendelea kutokomea, Tabata kapokea kijiti kwa fujo

Acha tu
C Park Matema na Ben, ilikuwa unavuka tu barabara.
Tukitoka hapo tunakutana PapiChulo.

Hv unakumbuka Ben Pub na ule mlango wa tinted?
Unajua bado hakujakucha, ukifungua mlango tu, saa 4 asubuhi ... nachoka hoi🥴😙😙
Mimi nikifululiza kukesha bar lazima malaria inigonge hivyo saa mbili tu nishaondoka.
 
H
Ilishawahi kunitokea hapo ben pub. Unakula starehe unajisahau unatoka nje unakuta jua kali watu wanaendelea na shughuli zao.
Papii chulo nayo mwendo ilishaumaliza ila kuna mbadala las carinyo.
Hawa wamiliki wa hizi night clubs,pub etc nadhani wana dawa ukiingia wazo la kuondoka linatoka kabisa, kuna mmoja ipo maeneo ya home ukienda na pesa lazima uimalize hats kama ulijipangie budget kwamba utatumia kiasi kadhaa utajikuta unawanunulia watu, wahudumu hadi hivyo pesa ikate ndo akili zinakurudia na kuona kama umetumia pesa nje ya budget na unnecessary offers
 
Maeneo yangu hayo, kuanzia manyanya mpaka morocco nlikuwaga nakaa sana hapo ben
 
Pole kwa bar-fever, saa 2 usiku unatoka bar?
Mie saa 2 ndio naanza kutafuta nguo ya kuvaa.
Tumetofautiana mkuu
Yap naogopa sana mbu hata nyumbani ikifika saa tatu Niko ndani ya net, malaria na typhoid ndo magonjwa ninayoyaogopa nakunywa maji ya kuchemsha au ya chupa tu zaidi ya miaka 25, pia mbu hata akiingia kwenye net lazima nishtuke usingizini na nimtoe ndo nilale.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…