Niko tabata kitambo tangu 1983 kipindi hicho baa ni mbili tu,Hai bar ya mzee mushi na camp bar ya mzee mmari.kwa nini nasema tabata ililenga watu wa kipato cha kati?serikali ya nyerere ilichagua tabata kuwa makazi ya watumishi wake,ngoja nikutajie mashirika na taasisi za umma zenye kota zao tabata,tunaanza na nssf opposite na aroma,kuna azimio,hizi ni za ccm,kuna,tazara,polisi,masoko,bima ,nnsf tena,karibu na kristo mfalme,tazara tena maeneo ya liwiti,sigara,chuo cha veta chang'ombe,ladwa,NHC mawenzi .ongeza zingine,sasa eneo kama hilo huwezi kuliita la masikini,mimi nimekulia tabata bima zile kota zilizonunuliwa na mama rwakatare,karibu na 40 40 tangu miaka ya 80 watoto wa mle tulikuwa wa kishua NIC lilikuwa shirika kubwa.
Kuhusu matumbi hata msasani na mikocheni kuna mitaa ya uswazi kuliko hiyo matumbi.
Nimesoma uzi wako unaonekana na wewe ni mkongwe tabata ila iangalie tabata katika angle hiyo.umemaluza tabata primary 2002 mimi 1992 hizo bar ulizotaja hazikuwepo,jengo la Aroma linajengwa naliona