Baa za Tabata na maeneo yake ya kula bata

Baa za Tabata na maeneo yake ya kula bata

Niko tabata kitambo tangu 1983 kipindi hicho baa ni mbili tu,Hai bar ya mzee mushi na camp bar ya mzee mmari.kwa nini nasema tabata ililenga watu wa kipato cha kati?serikali ya nyerere ilichagua tabata kuwa makazi ya watumishi wake,ngoja nikutajie mashirika na taasisi za umma zenye kota zao tabata,tunaanza na nssf opposite na aroma,kuna azimio,hizi ni za ccm,kuna,tazara,polisi,masoko,bima ,nnsf tena,karibu na kristo mfalme,tazara tena maeneo ya liwiti,sigara,chuo cha veta chang'ombe,ladwa,NHC mawenzi .ongeza zingine,sasa eneo kama hilo huwezi kuliita la masikini,mimi nimekulia tabata bima zile kota zilizonunuliwa na mama rwakatare,karibu na 40 40 tangu miaka ya 80 watoto wa mle tulikuwa wa kishua NIC lilikuwa shirika kubwa.
Kuhusu matumbi hata msasani na mikocheni kuna mitaa ya uswazi kuliko hiyo matumbi.
Nimesoma uzi wako unaonekana na wewe ni mkongwe tabata ila iangalie tabata katika angle hiyo.umemaluza tabata primary 2002 mimi 1992 hizo bar ulizotaja hazikuwepo,jengo la Aroma linajengwa naliona
Daah kweli wewe ni mkongwe wa Tabata
 
Ukitoka Twist unasogea mbele Kuna Mr Wine ilipokua kitambaa Cheupe zamani, ukisogea shell kushoto Kuna Mazembe Park usiombee mademu hapo wanakunywa Henken na Windhoek tu! Tuache hapo segerea mwisho utakutana Na kingdom wahudumu ni kama wamevaa vichupi 24/7, hapo utakutana na Ale Bush na Fantasy, endea Kinyerezi Kabla ya Round about utakutana na Big Boys na hapo ukielekea Airport Kuna Darajani 24/7 halali na haamki mtu! Tabata sio Poa nimesahau Kaites lounge Baada ya KP
Hujaitaja Nderingo ipo Sanene hapo ni full toto'z
 
Hujaitaja Nderingo ipo Sanene hapo ni full toto'z
Nderingo kuanzia kaunta wahudumu meneja (kina asenga na Babu juma) mpaka wateja ni wazee hakuna totoz never! Uzuri wa nderingo haivumi na haifi Ila supu ni 24/7 tena yenye ubora wa hali ya Juu! Leo Niko Kimara Korogwe (white house baa kongwe zaidi ukanda huu ukiuacha Ruaha galaxy- hapa ni mdudu wa kuchoma huwezi pata huu popote!
Labda safari bar ya Mbezi mwisho! Safari resort sijawahi kuingia
 
Nderingo aka Peace of Mind pale hapatajwi sana kwa sababu ni kwa wazee. Wazee wastaafu na wanaokaribia kustaafu. Ndio maana ukiangalia hata parking yake utakuta ni Prado, Hilux, Rav4 Old, hakuna alteza wala subaru.
 
Leo pembeni ya Kaites Kuna Uzinduzi mkubwa Nyama choma ni free kazi yako ni kukata mayi mana nguvu ya mamba kumayi! Ni FEDO PUB! Jamhuri ya Tabata sio paziri! Ukifika KWETU PAZURI YA ZAMANI MBELE KIDOGO KISHOTO UTAONA MAPAMBO YA KRISMASS NA RED KAPET! Picha hakuna! Mimi sio cameraman
 
Niko hapa now mkuu
 
Back
Top Bottom