Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Muda mrefu ilielezwa kuwa Gaza ndio gereza kubwa la wazi duniani lililowafungia watu karibu milioni 2.5
Baada ya hilo mshauri wa mambo ya nje wa jumuiya ya Ulaya,Joseph Borell amesema eneo hilo pia linapaswa kuitwa ni kaburi la sheria walizojiwekea binadamu.
Uchaguzi wake wa jina hilo bila shaka umekuja baada ya kuona mengi ambayo yamekuwa yakiendelea kinyume na yalivyo kwenye makaratasi.
Na sijui ni nani tena atakayetoka nchi za Ulaya na Marekani kwenda nchi nyengine kuhimiza utawala bora na utawala wa kisheria pamoja na demokrasia.
Mimi binafsi namuongezea kuwa Gaza ni kaburi pia la ubinadamu.
1. Hukumu ya ICJ iliyotolewa baada ya mashtaka ya Afrika kusini yamepuuzwa na hakuna aliyehoji
2. IDF wanapiga makazi ya watu kwa nguvu zote na kuua watu bila sababu na hakuna anayeizuia
3. Israel imezuia chakula kisiingie Gaza mbele ya macho ya walimwengu na wameshindwa kutumia nguvu kupitisha chakula hicho kama ilivyopendekezwa na SA.
4. Kawaida binadamu ukimshambulia mama au ndugu zake huwa mkali na lazima atatumia kila silaha aliyonayo kupigana na adui huyo.Kwa upande wa Gaza wanapigwa na kugaragazwa mbele ya macho yao lakini wao wanaendelea kula pilau zao.