Baada ya Aweso kutumbua watendaji kwa madudu ya maji Dar, CCM itumbue pia watendaji wake kwa kushindwa kuisimamia Serikali maeneo husika

Baada ya Aweso kutumbua watendaji kwa madudu ya maji Dar, CCM itumbue pia watendaji wake kwa kushindwa kuisimamia Serikali maeneo husika

The Phylosopher

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2015
Posts
1,968
Reaction score
2,957
Kwa uelewa wangu ni kwamba chama kinachotawala kimeomba na kupewa ridhaa ya kuisimamia Serikali ili itoe huduma stahiki kwa niaba ya wananchi walioichagua.

Kwa maelezo ya waziri inaonekana matenki yapo na maji yapo ila watendaji wa serikali kwa makusudi hawakupeleka maji kwenye hayo matenki alafu sisi wakazi wa goba kinyerezi MBEZI kibamba nk tukaanza kukosa huduma ya maji ambayo kodi zetu zimejenga miundombinu.

Swali langu najiuliza hao watendaji wa CCM wenye wajibu wa kuisimamia Serikali maeneo husika walikuwa wapi!? Je haiwezi kuwa pia wao ni wanufaika wa shida ya maji ambayo tumeipitia sote!?

Ni kwa nini nao wasichukuliwe hatua kwa kulea huu upumbavu!?

Bila kuwaadhibu watendaji wa CCM haya mauzauza hayataisha.
 
Hakuna alichotumbua zaidi ya kushindwana kwenye rushwa, DAWASA wanapokea rushwa lakini yeye haimfikii
 
Malori Yanayouza Maji Mtaani Ni Mali Za Hao Watumishi
 
Kwa uelewa wangu ni kwamba chama kinachotawala kinameomba na kupewa ridhaa ya kuisimamia serikali ili itoe huduma stahiki kwa niaba ya wananchi walioichagua.

Kwa maelezo ya waziri inaonekana matenki yapo na maji yapo ila watendaji wa serikali kwa makusudi hawakupeleka maji kwenye hayo matenki alafu sisi wakazi wa goba kinyerezi MBEZI kibamba nk tukaanza kukosa huduma ya maji ambayo kodi zetu zimejenga miundombinu.

Swali langu najiuliza hao watendaji wa ccm wenye wajibu wa kuisimamia serikali maeneo husika walikuwa wapi!? Je haiwezi kuwa pia wao ni wanufaika wa shida ya maji ambayo tumeipitia sote!?

Ni kwa nini nao wasichukuliwe hatua kwa kulea huu upumbavu!?

Bila kuwaadhibu watendaji wa ccm haya mauzauza hayataisha.
Wana mnyororo wao usio na thamani
 
Back
Top Bottom