Baada ya chama cha ACT Wazalendo kuamua kuwa chawa wa Samia kimepoteza mvuto kwa wananchi

Baada ya chama cha ACT Wazalendo kuamua kuwa chawa wa Samia kimepoteza mvuto kwa wananchi

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
15,101
Reaction score
56,054
Baada ya Ujio wa Samia Suluhu Hassan kuwa rais wa Tanzania, kiongozi mkuu wa ACT wazalendo ndugu Zitto Kabwe akautangazia umma kuwa tusimtegemee kuikosoa serikali ya Samia kama tulivyozoea kumuona akikosoa serikali zilizopita(Hasa serikali ya Magufuli).

Na kweli ndugu Zitto ameacha kabisa kuikosoa serikali ya Samia, hakukosoa wakati serikali ya Samia ikiwaswaga Wamachinga utadhani wahamiaji haramu nchini, Hakusimama kutoa chembe ya kauli wakati wamasai wanafurushwa kibabe huko loliondo, Hukumsikia kwa nguvu kubwa akikosoa upandaji wa kutisha wa bei za bidhaa za vyakula uliotokana na mismanagement ya uchumi, Siku hizi anatetea upandaji wa deni la Taifa kuwa si wa kutisha wakati ni miaka michache kipindi cha Magufuli alikuwa akipiga kengele ya tahadhari juu ya kupanda kwa deni la Taifa.

Leo ACT wazalendo kimekuwa mtetezi wa upande mmoja wa muungano. Kule Zanzibar angalau kinatetea mambo ya Wazanzibar, lakini huku Tanganyika, huoni viongozi wake hata wa huku Tanganyika wakizungumza na kuwasemea Watanganyika juu ya mambo wanayoyalalamikia katika muungano. Ni rahisi sana kumsikia Zitto Kabwe hadi kiongozi mdogo kama Abdu Nondo wakiwa very articulate kuelezea namna Zanzibar inavyoumizwa na Tanganyika, lakini hutawahi hata siku moja kuwasikia wakisemea namna Watanganyika wanavyoumizwa na huu muungano. Na mambo yapo ambayo Watanganyika wanalaumu, kwa mfano muungano unamfanya Mzanzibar awatawale watanganyika hata kwa mambo yale yasiyo ya muungano, lakini kwa kule Zanzibar, mambo yao yasiyo ya muungano anatawala mzanzibar mwenzao!

Kwa hiyo kimsingi, Chama cha ACT Wazalendo kimeamua kuwa chawa wa Samia. Ila kwa kufanya hivyo, chama kimekosa mvuto huku Tanganyika, Wengine wanakiita CCM B.

Ili Viongozi wakuu wa chama hicho wazuge kuwa bado wanasimamis masuala ya wananchi, eti wakaunda wizara "vivuli" , wakadai eti "wanagroom vijana", wakadai eti "chama ni taasisi na siyo Zitto". Lengo la kufanya hivyo ni kuwafanya viongozi wakubwa haswa Zitto wasiiconfront directly serikali ya Samia. Unaweza kujiuliza kuwa kwani kipindi cha Magufuli wakati Zitto anamkosoa chama kilikuwa ni yeye na siyo Taasisi?

Ni dharau kubwa kwetu sisi wananchi, kuona Chama kinamtuma mjumbe mdogo tu kuzugazuga kuongea maneno mawili matatu ya mambo mazito ya kitaifa wakati mambo hayo yalipaswa kyzungumzwa na kiongozi mkuu wa chama!.

Mimi naona kama Kiongozi mkuu wa chama hicho ndugu Kabwe hawezi kumkosoa Samia kwa energy, zeal na determination basi akae pembeni mapema tu kabla ya mwaka 2024. Maana kwa style yake hii anakwamisha hicho chama kukua hasa Tanganyika.

Kama Zitto anampenda sana Samia, na anahisi akimkosoa ataumiza hisia zake basi akanywe naye chai aachane na uongozi wa chama. Siasa ni kukusoa, na siyo kulembalemba na kuoneana aibu!
 
Lazima awapambanie wazenji mana ndio silaha pekee aliyo nayo,wasipo muunga mkono wa zenji na kujitoa kwenye chama chake hakika atarudi kigoma kesho kuendeleza fani yake ya uganga wa kienyeji.
 
Ila CHADEMA naona mnateseka sana na ACT na hivyo kutwa mnakipaka matope, lin Zito kasema hawezi kumkosoa Samia, ACT kwa sasa wanapigania bima ya afya kwa wote iunganishwe na mfuko wa hifadhi ya jamii na wanakosoa mpango wa serikali wa bima ya afya kwa wote.
Nitajie kiongozi mkubwa wa CHADEMA alieponda muungano hadharani,
 
Tanganyika ndio inayoinyonya Zanzibar kwenye huu Muungano, Ila wananchi wakawaida waliowengine wanashindwa kufahamu hilo.

Ni lini Lisu au Mbowe wamelalamika kuwa Watanganyika wanayonywa? kwanini Unamsema Zitto tu
 
Tukiweka UNAFIKI, UZANDIKI, HILA na ROHO MBAYA YA KISHETANI dhidi ya Zitto pembeni, kuna chama cha upinzani kwa sasa ambacho si chawa wa mama?!!!!! Tuwe tu wakweli angalau kwa dakika 1.

Nje ya mada; HIVI ZITTO ALIIFANYA NINI HASWA CHADEMA?!!!!!!! MBONA WAMETOKA WENGI, TENA WENGINE WAKATI MUHIMU WA UCHAGUZI NA NI HIVI KARIBUNI ZAIDI KULIKO, LAKINI HAWASAKAMWI (KUANDAMWA) KAMA ZITTO?!!!!!!!!! Kuna kitu hapa!!!!!
 
Back
Top Bottom