Mrs Gudman
JF-Expert Member
- Jul 3, 2015
- 613
- 1,297
Habari Wana Jamii Forum
Nianze Kwa historia kidogo ,
Takribani miaka minne iliyopita nilikuwa napitia vipindi vigumu sana Kwa sababu nilimpoteza mwenzangu, malezi na majukumu kuniwia mengi
Kutoka kwenye hali ya kutokujishughulisha kivile (kama mjuavyo wadada wamama wa Kiafrika ukiwa na mwanaume kuna majukumu automatically anayasimamia yeye na wewe Kuna majukumu Yako) mpaka kwenye hali ambayo Kila kitu kinakuangalia alafu Wakati huo huo nilikuwa nalea ,alafu Wakati huo huo nilikuwa nasimamia miradi yangu na kazi pia nilijikuta nafanya mambo makubwa peke yangu ambayo sikuwahi kufanya before bila msaada wa mtu wa karibu.
Imagine naenda Kazini ,natoka Kazini naenda Biasharani ,natoka Biasharani naenda site nikifika site nasikiliza matatizo mara nimeibiwa mara Sijui kitu gani kimeisha (Wakati mwingine nimeishiwa) nikitoka naenda nyumbani mara mtoto anaumwa mara Sijui kimepanda kimeshuka ,nikajikuta Nina tumia akili yangu kupita kiasi kitu ambacho sikuzoea hapo mwanzo .
Ule Wakati ulipita salama maumivu yakaisha, shughuli zangu zikaenda vizuri lakini nimebaki na tatizo, tatizo lenyewe ni kusahau.
Mimi Nina mdada wa miaka 31 lakini naweza kukutana na mtu ambaye tunafahamiana na nikamsahau completely, naelewa kabisa huyu si mgeni machoni pangu ila nashindwa kumkumbuka jina mpaka nimuulize (siyo wote ila ishatokea Kwa watu wanne)
Napoteza vitu mfano flash, funguo, Hela, nikiwa na Hela ndogo ndogo sikumbuki nilipoweka na mara nyingine zinapotea au kuja kuzikuta siku nyingine.
Sifanyi kazi zangu kwa ufanisi kama mwanzo, mara nyingi kazi zangu zinakuwa na dosari kitu ambacho naonekana nimekuwa mzembe while najijuwa kabisa Mimi siyo mzembe, siyo mvivu Wala nini.
Hayo ni machache tu, naombeni nijue nifanyeje kurudi katika hali yangu ya mwanzo.