MWALLA
JF-Expert Member
- Dec 12, 2006
- 16,952
- 10,513
VIPI LEO? ... UTATII SHERIA BILA SHURUTI?Ni dhahiri ndugu Makonda katika utekelezaji wa majukumu yake kama Mwenyekiti wa ulinzi na usalama jijini Dar, kachoma kisu kwenye Mfupa.
Chadema bila kukaa chini na kutafakari jinsi ya kukabiliana na tatizo hilo kwa kuondoa uchafu ndani ya chama,wameamua kukumbatia uchafu kwa kupambana na Makonda.
Ajizi nyumba ya njaa,Makonda ageuka ajenda Kuu ya upinzani mtaani,mahakamani na bungeni.Ni hatari kubwa sana kwa Chadema kumgeuza Makonda hoja Kuu ya kisiasa.