Baada ya Dr. Slaa kufunua nyongeza; Sheria ya "mbwembwe" ni batili?


Mawazo yako ni mazuri lakini yameingia doa........... kiswahili cha kingumbaru...
.
 

Kuna wakati nilisema kuwa Dr Slaa ni kati ya watu watatu katika nchi hii wanaohitaji kupewa tuzo ya heshima. Huyu mtu anajali na kuipenda sana nchi yetu. Ukiangalia kwa ukaribu utagundua kuwa anaongoza nchi hii, ndiyo kama rais.
 

Mkuu kuna baadhi ya watanzania Kikwete yeye ni malaika wakati wote, hakosei. Hata yeye hataki kuonekana kama huwa anakosea. Mimi naamini kuwa kipengele kiliingizwa makusudi, tumshukuru Dr. Slaa aliyeweka nchi katika moyo wake, anaiongoza nchi hii, ndiyo kama rais wetu.

Kipengele hiki kina uhusiano na juhudi zilizokwishaanza za kuzuia wanachama wa CCM kumkabili JK kwenye uchaguzi. Nadhani pia Dr. Slaa anaonekana ni tishio kwenye uchaguzi ujao. Sasa hapo rais ni yupi, anayesaini bila kusoma sheria, au anayefanya kazi kama rais kuhakikisha kuwa nchi inaendeshwa kwa misingi ya sheria za haki? Tumpe haki yake Dr Slaa anayositahili kuiongoza nchi hii octoba 2010.
 
Kwa nini asaini kitu asichokijua
 

Type ya watu kama nyie ndiyo aina ya wasidizi alionao Mkulu wanamwambia mambo poa tu mzee kanyaga twende, sasa mfano Kabuche1077 na FairPlayer wawe washauri wa rais kwa mambo ya bunge na katiba na wanashauri hivi wanavyosema na mkulu anawaamini taifa litegemee nini
 
Hivi, kuna ugumu gani kwa Mh Kikwete kuchukua msimamo wa kutovumilia utendaji usioridhisha? Ingekuwa ni mtu mdogo kwenye ofisi ya umma kafanya kakosa kadogo angeshatimuliwa tena kwa mbwembwe!!

Kinachohitajika hapa ni yeye kuchukua hatua juu ya mzembe MMOJA TU kati ya hao wengi wanaomzunguka na wengine watashika adabu.

Yaani napata hisia ya kumtingisha, labda kalala ataamka!!
 
Dr. Slaa yuko sahii hapa, hawa wakuu wamefanya makosa, hakuna haja ya ku SPIN, badala yake ni kukubali makosa na kurekebisha hiyo sheria. Kikubwa zaidi ni kujifunza ili makosa kama hayo yasifanyike tena huko mbeleni. Ndio maana wenzetu walioendelea, huunda tume ili kugundua kwanini makosa yamefanyika na kisha kuziba mianya ili yasifanyike tena.

Inaudhi unapoona watu wanajaribu ku SPIN hata pale walipokosea, why? Kila mtu anakosea na muhimu ni kujifunza ili kuepuka makosa kama hayo.

 
Wasaidizi wanamtesa sana Rais wetu......timuatimua wote unipe mimi unikulu hapo ikulu!!!!
 
Kwa uzembe wa ofisi yake mara kwa mara unaofanywa na wasaidizi aliowateua yeye mwenyewe na kushindwa kuwawajibisha, angefanya jambo moja muhimu ili akumbukwe kama shujaa. ASIJIUZULU ILA ATANGAZE KWA MBWEMBWE KUBWA KWAMBA OCTOBER 2010 HATAGOMBEA TENA KITI HICHO KWA VILE KIMEMSHINDA
 
Huyu bwana hajafura lolote wala nini, he is an artist and comedian just like others. Who knows may be he's the one who ordered them to be inserted!
 
Hii inatoa mwanga kidogo kuona jinsi ambavyo nchi hii inaendeshwa. Ikiwa hivi ndivyo ni sheria ngapi zimeshakuwa doctored namna hii? Mie bado sijaamini na ninasubiri maelezo ya serikali. Fikiria sasa mikataba ya madini, ndo maana inabidi iwe siri!

Haiwezekani kuwa jambo hili (kama kweli limefanyika) lilikuwa limefanyika kwa mara ya kwanza. Sema sasa hivi kuna mtu amejisumbua kuthibitisha kuwa kweli kinachosainiwa ndo kile kile? Na pengine na yeye amepata TIP kutoka kwa watu wanaojua kuwa mambo huwa yanakuwa hivyo! So we know sheria zinatungwa then wale ambao wanahisi kuna kitu ambacho kama wangepekipeleka bungeni kisingepita, wanapata muda wa kukipenyeza, then sheria inatiwa sahihi.

Ingekuwa ni omission ungesema ni typing error, lakini addition? Haiwezekani. Lazima kipengele hiki walishapanga kukitumia mahali. Nchi hii sheria huwa wanatungiwa watu na mazingira fulani tu! Ndo maana sheria nyingi baada ya kutumikia kile ilichotungiwa hubaki bila kutekelezwa na yeyote hata kama zinavunjwa kila siku!
 
Jamani kama kuna mambo ambayo mimi binafsi huwa yananiudhi ni lack of seriousness and censorship on the part of our Accounting officers in the government. Ukienda hata kwenye maonesho yao pale mnazi mmoja au Karimjee documents nyingi hazifanyiwi editing hata kidogo. Sasa kama hilo la cheque kweli wameshindwa kuliona hilo kama siyo uzembe ni nini?
 
Hapa wakuu hakuna kutafuna meno mengi yalishasemwa kuwa hatuna uongozi na hii ni mbaya sana kwani inaonyesha jinsi raisi wetu alivyozungukwa na watu wasiowahaminifu kwake. Yaani wanamfanyia usanii live. Hii ni hatari. Inawezekana kuna mengi yanafanyika jamaa anasign kumbe watu wanatafuna kona. HATUNA UONGOZI KWAKWELI.
 
Kiutaratibu sheria hiyo ni batili na haiwezi kutumika. Nilazima irudiswe bungeni ikafanyiwe marekebisho tena. Ila nachelea kusema itafumbiwa macho.
 
Kwa mtazamo wangu hakuna namna ambavyo ingeweza kutokea kuongezwa kipengele hiki bila kufahamika au kugundulika, kwani raisi makini anazo mbinu zote za kuhakikisha jambo hilo halitokei. Hata kuunda timu maalum ya wabunge kuipitia kuihakiki ingesaidia. Lakini kama mpaka leo ameshindwa kutoa tamko la ni namna gani imetokea na ni nani mhusika aliyeipitia na kumhakikishia iko sawa na anakusudia kuchukua hatua gani, basi huu ni usanii kama walivyosema Wakuu hapo juu!
 
Hongera sana Dkt Kikwete, keep it up!

Siamini macho yangu, Jamani hii nini? ila naye amezidi mno upole,kwanini asiwabadilishe hawa wanaomsaidia,hivi ni kweli alikuwa mwanajeshi au ulikuwa ni usanii?
 
Kuna wakati nilisema kuwa Dr Slaa ni kati ya watu watatu katika nchi hii wanaohitaji kupewa tuzo ya heshima. Huyu mtu anajali na kuipenda sana nchi yetu. Ukiangalia kwa ukaribu utagundua kuwa anaongoza nchi hii, ndiyo kama rais.

Nakubaliana na wewe kwa asilimia zote, maana kama siyo Dr Slaa mambo mengi yalishapita tu hivi hivi, na pia amesaidia kuondoa ile kauli ya yule kiongozi wa Kenya aliyemwambia JKN kuwa anatawala marehemu
 

Kama anashindwa kuwatimua, basi tumtimue yeye
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…