Baada ya hayati Magufuli kufariki 'mikutano ya injili' imeanza

Baada ya hayati Magufuli kufariki 'mikutano ya injili' imeanza

Kikwete ameawahi kuwaambia Maaskofu kuwa miongoni mwao kuna wafanyabiashara ya Ngada, wakammaindi, wakamsema, wengine wakasema awataje majina, wengine wakaagiza apuuzwe!

May be kuna mchezo mchafu wa watu kutumia dini kupenyeza haya madawa
 
Tutaona tena vijana wakiwa arosto,,piga miayo na kudondosha mimate ovyo... Kuna fursa hapo...naanzisha sober house
 
Ccm kama chama ni wezi wa kura na hawatakaa waache, ila shetani yeye alikuwa kwenye advance level ya wizi, yeye alikuwa ananajisi chaguzi, yaani ni zaidi ya wizi, maana yeye alikuwa anaagiza mauji, kuacha watu na vilema, kuteka, unyama na ukatili wa wazi.
 
moja ya dalili ya kuwepo kwa biashara haramu ya unga ni utitiri wa mikutano ya injili ikifanywa na watu wasiokuwa na haiba wala karama ya kuwa wachungaji wala watumishi wa Mungu. dalili zimeanza kuonekana.

mikutano hiyo huambatana na safari za kuenda nje zisizoeleweka malengo yake. pia hutokea kuingia kwa wageni wengi kuwasili nchini kwa kivuli cha kufanya matamasha ya 'injili'.

safari za wasanii wetu na wa nje kutoka na kuingia nchini pia hushamiri.

wakati huohuo mtaani visa vya matumizi ya dawa za kulevya hushamiri. ulaji wa 'bata' kwa watu wasioeleweka wanafanya kazi gani kwa kipato kipi huongezeka.

kipindi cha dokta magufuli uovu huu ulidhibitiwa sana. China adhabu ya biashara hii ni kifo tu maana ukiwa na taifa la mateja kama nchi huwezi kupiga hatua kimaendeleo. China hayupo tayari kuona anazidiwa na Marekani kiuchumi ndo maana anailinda nguvukazi ya nchi yake kwa kutoa adhabu kali kwa walanguzi wa dawa za kulevya na wahujumu-uchumi wote bila kuangalia ni nani?

enzi za dr. magufuli dawa za kulevya zilidhibitiwa sana. madalali na walanguzi walikiona cha moto.

sasa tunarudi kulekule.

Mungu aunusuru uzao wetu maana yajayo yanasikitisha.

Pumzika kwa amani Dr. John Pombe Joseph Magufuli.

Mkuu inchaji salam. Tafadhali unatakiwa (sio kuombwa) kuthibitisha hii kauli yako " moja ya dalili ya kuwepo kwa biashara haramu ya unga ni utitiri wa mikutano ya injili". MOD naomba muangalie sheria zetu muone kama alichoandika inchaji kinaruhusiwa AU apewe BAN ya miezi kadhaa.

Nawasilisha
 
Back
Top Bottom