Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,101
- 56,054
Na msukuma...We kweli mnyonge na maskini....
moja ya dalili ya kuwepo kwa biashara haramu ya unga ni utitiri wa mikutano ya injili ikifanywa na watu wasiokuwa na haiba wala karama ya kuwa wachungaji wala watumishi wa Mungu. dalili zimeanza kuonekana.
mikutano hiyo huambatana na safari za kuenda nje zisizoeleweka malengo yake. pia hutokea kuingia kwa wageni wengi kuwasili nchini kwa kivuli cha kufanya matamasha ya 'injili'.
safari za wasanii wetu na wa nje kutoka na kuingia nchini pia hushamiri.
wakati huohuo mtaani visa vya matumizi ya dawa za kulevya hushamiri. ulaji wa 'bata' kwa watu wasioeleweka wanafanya kazi gani kwa kipato kipi huongezeka.
kipindi cha dokta magufuli uovu huu ulidhibitiwa sana. China adhabu ya biashara hii ni kifo tu maana ukiwa na taifa la mateja kama nchi huwezi kupiga hatua kimaendeleo. China hayupo tayari kuona anazidiwa na Marekani kiuchumi ndo maana anailinda nguvukazi ya nchi yake kwa kutoa adhabu kali kwa walanguzi wa dawa za kulevya na wahujumu-uchumi wote bila kuangalia ni nani?
enzi za dr. magufuli dawa za kulevya zilidhibitiwa sana. madalali na walanguzi walikiona cha moto.
sasa tunarudi kulekule.
Mungu aunusuru uzao wetu maana yajayo yanasikitisha.
Pumzika kwa amani Dr. John Pombe Joseph Magufuli.
Huyu atakuwa Mpinga Kristo.Una mawazo ya kishamba sana. Hilo ni jukumu la vyombo vya usimamizi, lakini mikutano ya injili au mihadhara haina uhusiani na hicho unachokisema.
Leta ushahidiKuna ukweli hapo....[emoji382]lords wamejificha kwenye dini na michezo...walikuwa wanaleta mabox ya vitabu vya dini pamoja na madawa...