Baada ya Hayati Magufuli kuombewa Chato, Mwanza nao wanaandaa maombi, binafsi naona haya yanayofanyika baada ya Chato yako kimkakati

Jina langu limeshaandikwa kwenye Kitabu cha uzima cha Mwanakondoo, nimeokoka ndugu, na Mungu yupo moyoni mwangu. nakukaribisha kwa Yesu na wewe uokoke. nina uhakika Mungu yupo moyoni mwangu kwasababu namwona.
Asante Sana, basi endelea kumwomba Mungu {Yesu Kristu} aendelee kukujalia karama ya utambuzi.
 
Itakuwa jamaa wanajua ndio maana wamegauza kanisa kuwa taasisi ya kufanyia laundering criminals (kutakatisha wahalifu)
Lakini sini huyu huyu GWAJI boy alisema anafufua "WAFU" sasa sindio muda muafaka wakuonyesha uwezo wake? Cha ajabu kakaa kimya utadhani si yeye.. Kweli Mungu alisema katika biblia siku za mwisho watakuja mana bii wa uongo!!
 
Asante Sana, basi endelea kumwomba Mungu {Yesu Kristu} aendelee kukujalia karama ya utambuzi.
huwezi kujua hili kwasababu mmemkataa Roho Mtakatifu, mnasema wale wanaompokea na kuomba kwa Roho wamepagawa tu, ninyi hamumtaki. pia hamtaki kuokoka. Ukiokoka na Roho akaingia ndani yako haubashiri kama wewe una Mungu ama la, unashuhudiwa na Mungu mwenyewe. nakuasa kwa mambo ya fuatayo, na wala sio kwamba nakushusha au kukudharau au kukuhukumu, bali ndio ukweli wa Neno la Mungu.

1. kama wewe unajiita Mkristo na haujajazwa Roho, wewe ni mtu wa dini, unaabudu dini, na hauna Mungu. waabuduo halisi ni wale wanaomwabudu Mungu katika Roho na kweli. yaani ukiimba Roho ahusike, ukisali Roho ahusike, ukihubiri Roho ahusike. Roho Mtakatifu ndio awe kiongozi wako kwenye kila kitu.

Warumi 8:9 - 11 INASEMA, 9 Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake. 10 Na Kristo akiwa ndani yenu, mwili wenu umekufa kwa sababu ya dhambi; bali roho yenu i hai, kwa sababu ya haki. 11 Lakini, ikiwa Roho yake yeye aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho wake anayekaa ndani yenu.
Warumi 8: 15 - 17 INASEMA, 15 Kwa kuwa hamkupokea tena roho wa utumwa iletayo hofu; bali mlipokea roho ya kufanywa wana, ambayo kwa hiyo twalia, Aba, yaani, Baba. 16Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu; 17na kama tu watoto, basi, tu warithi; warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja naye ili tupate na kutukuzwa pamoja naye.

kwahiyo ushauri wangu kwako, Okoka, mwombe Mungu akupatie Roho Mtakatifu akuongoze, kwasababu usipokuwa naye huwezi kushinda dhambi, pia, utakuwa si mtoto wa Mungu, kwasababu Mungu hayupo ndani yako. huu ndio ukweli mchungu mlioukataa. na hata hapa utapinga.

na hata ninyi nyote, ukienda kanisa ukaona halihubiri chochote kuhusu ujazo wa Roho Mtakatifu, kimbia, hiyo ni dini, chama tu cha watu kukusanyika ila Roho Mtakatifu hayupo. na kama Roho hayupo manake hakuna atakayewahubiria. Mchungaji akisimama hatakiwi kuongea yeye, Roho Mtakatifu anatakiwa aongee kupitia yeye, yeye anatumiwa tu kama chombo, hayo ndiyo mahubiri yanayookoa, zingine zote ni motivation speeches na vitisho tu na haziokoi. hao wanaohubiri miujiza, maji, vitambaa, mafuta muda wote, bila kuhubiri mafuta ya Roho, ni wa kuwakimbia. binafsi, dhehebu langu la TAG, EAGT au pentecost zote, nikikuta sehemu hawahubiri namna hii, hata siwezi kusali natafuta pengine. siabudu dhehebu, naabudu uwepo wa Mungu.
 
Kifua chako kimehifadhi chuki sana inaonekana

Hayo ni maradhi kama ilivyo UTI na mengine

wahi kwny Clinic ya Maombi na Dua ili upate rehma za Mola wako

kuna watu ukisoma comment zake mbili tatu tu unaona alichohifadhi kifuani
Ndiyo maana magufuli tulimkubali alipo ongea chochote kinywani tulikiona hadi moyoni mwake hakuwa mnafiki wewe maneno yako hayawezi kuonyesha kilichopo moyoni mwako kwa sababu ni mnafiki ...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…