Salamu wakuu,poleni na majukumu ya hapa na pale
Siku chache zilizopita baba mwenye nyumba alikuwa amenibana kweli kuhusu kulipa kodi ya nyumba ,yaani kabla ya tarehe 20 alikuwa kila mara ananipigia sim nilipe kodi ila nikawa namwambia anipe muda mwisho wa mwezi
Ila bado akawa hatulii ,hakubali ,akidai kuna kazi hiyo hela inataka ikafanye,baadae nikaamua kupiga kimya nikawa siongei kuhusu hiyo hela
Jana nikawa nimepata hiyo hela nikaenda kuilipa kwenye akaunt yake bank na kumpelekea risit ya malipo
Leo nimekaa zangu napumzika nashtuka SMS inaingia kuangalia imethibitishwa sh million 1,500000 kutoka kwa huyo mzee,nikashtuka au alikuwa amekosea,nikampigia sim kumuuliza,amesema "Ndiyo mama nimekutumia unitunzie hiyo hela"
Bado najiuliza hili tukio sipati picha,iweje Mimi nimtunzie hela na huku ana akaunt na sim zenye akaunt?
Kama ananitaka mbona hajawahi kuonyesha hata dalili na mbona mtu mzima sana halafu mbaba mwenye heshma zake hapa mjini,mcha mungu!
Mbona alikuwa amenibana kuhusu hela ya kodi,kwenda kufanya shughuli zake nimelipa laki 7 lakini ananitumia million moja na nusu eti nimtunzie?
Mbona hajawahi kunipa hela nimtunzie iweje sasa?
Msaada,nipo njia panda