Baada ya hiki nini kitafuata

Baada ya hiki nini kitafuata

Salamu wakuu,poleni na majukumu ya hapa na pale

Siku chache zilizopita baba mwenye nyumba alikuwa amenibana kweli kuhusu kulipa kodi ya nyumba ,yaani kabla ya tarehe 20 alikuwa kila mara ananipigia sim nilipe kodi ila nikawa namwambia anipe muda mwisho wa mwezi

Ila bado akawa hatulii ,hakubali ,akidai kuna kazi hiyo hela inataka ikafanye,baadae nikaamua kupiga kimya nikawa siongei kuhusu hiyo hela

Jana nikawa nimepata hiyo hela nikaenda kuilipa kwenye akaunt yake bank na kumpelekea risit ya malipo

Leo nimekaa zangu napumzika nashtuka SMS inaingia kuangalia imethibitishwa sh million 1,500000 kutoka kwa huyo mzee,nikashtuka au alikuwa amekosea,nikampigia sim kumuuliza,amesema "Ndiyo mama nimekutumia unitunzie hiyo hela"

Bado najiuliza hili tukio sipati picha,iweje Mimi nimtunzie hela na huku ana akaunt na sim zenye akaunt?

Kama ananitaka mbona hajawahi kuonyesha hata dalili na mbona mtu mzima sana halafu mbaba mwenye heshma zake hapa mjini,mcha mungu!

Mbona alikuwa amenibana kuhusu hela ya kodi,kwenda kufanya shughuli zake nimelipa laki 7 lakini ananitumia million moja na nusu eti nimtunzie?

Mbona hajawahi kunipa hela nimtunzie iweje sasa?

Msaada,nipo njia panda

Nitumie mm hyo hela niiweke usieje kuitumia.
 
Umri wake na heshma yake hapa mjini Loh!
Umri ni namba tu heshima ni malipo mazuri kwa kumkubalia umpe hiyo neema. Akija muulize anataka mara ngapi hiyo iwe ndo bagain price yako. Mzee umfumbie macho aje kimya kimyaaa
 
Hapoo Chukuaa pesaa mwambie na shemu nae akupee hela ya Kodi Jumlaa utakuwa Kama na Mil 3 funguaa biashraa achaa kuzubaa
 
Mleta mada naona umekuja na style ya kipekee ya kujijengea profile hapa jf,


Wakubwa tumeshakuelewa!
 
Heshima ya mpangaji wa kike hujengwa na mkwaju wa baba mwenye nyumba
Mmuuh! Nawe ukiwa na nyumba ya kupangisha kumbe wadada watapata tabu eeh!
 
Back
Top Bottom