Baada ya HIMARS, Mfumo wa Phoenix Ghost Drone unaopelekwa Ukraine Utamfanya Putin aitishe Vikao zaidi Kremlin

Baada ya HIMARS, Mfumo wa Phoenix Ghost Drone unaopelekwa Ukraine Utamfanya Putin aitishe Vikao zaidi Kremlin

Annunaki

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2021
Posts
2,042
Reaction score
3,674
Mambo yanazidi kuwa magumu na kama nilivyokwisha kusema kwamba Putin kashapoteza Dira ya vita Duniani: Vita ya Ukraine, Putin amepoteza Dira, mpaka sasa haelewi afanyeje kumaliza vita aliyoianzisha.

Kwa sasa Ukraine inazidi kupata nguvu ya hali ya juu tofauti na mwanzo kabisa, kwa sasa Ukraine imeanza Kupokea silaha za kisasa zaidi ambazo anazidi kuzitumia ipasavyo na mpaka sasa Russia ameshindwa kusonga mbele Donbas & Kherson mara baada ya Ukraine kuanza kutumia HIMARS hali iliyomfanya Putin kuhitisha kikao cha dharula Kremlin.

Baada ya HIMARS, Ukraine inaenda kuanza kutumia Mfumo wa Phoenix Ghost Drone kupambana na Russia.

Mbaya Zaidi Putin kaenda kuomba Silaha Iran & Syria, hali inayoonyesha kwa sasa Russia imeanza kupungukiwa na silaha za kivita.

Je, mfumo wa Phoenix Ghost Drone unaopelekwa Ukraine ni nini?
Phoenix Ghost ni aina ya silaha zinazotembea kumaanisha kwamba husalia angani kwa muda mrefu kabla ya kupata shabaha.

Marekani inatuma zaidi ya ndege 500 za Phoenix Ghost kwenda Ukraine kama sehemu ya kifurushi chake cha dola milioni 270 ambazo Idara ya Ulinzi ya Marekani ilitangaza Ijumaa.

Tovuti ya Defense Express ilinukuu taarifa zilizotolewa na mshauri wa ofisi ya Rais wa Ukraine, Oleksii Arestovysch, ambaye alielezea ndege isiyo na rubani ya Phoenix Ghost kama "wijeti nzuri."

Ndege isiyo na rubani hutoshea ndani ya mkoba na inaweza kuning'inia hewani kwa saa sita. Ina mwongozo wa ‘infrared’, kumaanisha kuwa inaweza kufanya kazi usiku na kuharibu shabaha za silaha za wastani.

"Mia tano na themanini ya vitengo kama hivyo ni sawa na malengo 350 yaliyoharibiwa kwa nyuma," alisema.

Kulingana na Defence News, Phoenix Ghost, ambayo ilitengenezwa na Marekani mahususi kwa matumizi nchini Ukraine, inafanya kazi kwa njia sawa na AeroVironment Switchblade.

Kama vile Switchblade, ndege isiyo na rubani ya Phoenix Ghost ni aina ya silaha inayoteleza, kumaanisha kwamba inasalia hewani kwa muda mrefu kabla ya kupata shabaha.

Uwezo wa Phoenix Ghost
Tangazo la Biden la msaada wa kijeshi ni la 16 kutoka kwa orodha ya idara ya Ulinzi DoD kwa Ukraine ambayo Utawala wa Biden umeidhinisha tangu Agosti 2021," Idara ya Ulinzi ilisema katika taarifa yake Ijumaa.

Silaha hiyo ilundwa na Aevex Aerospace huko California, Phoenix Ghost inafaa dhidi ya magari ya kivita ya wastani, Politico ilimtaja mjumbe mstaafu wa bodi ya Aevex Lt. Jenerali David Deptula akisema.

Phoenix Ghost ina uwezo wa kuruka wima, inaweza kufuatilia lengo kwa hadi saa sita na inaweza kufanya kazi usiku kwa kutumia vitambuzi vya infrared, Deptula aliiambia Politico.

Ingawa Switchblade inaweza kuruka kwa chini ya saa moja pekee, Phoenix Ghost inaweza kusalia angani kwa muda mrefu zaidi.

"What is the Phoenix Ghost Drone that is set to be used in Ukraine? - The Jerusalem Post" What is the Phoenix Ghost Drone that is set to be used in Ukraine?

switchblade300-aerovironment.jpg
b7ffdc51a402c5bc43937b1039cd6c04.jpg
maxresdefault.jpg
 
Bongo zozo bana wewe jiulize jambo dogo tu kwanini mmoja anampiga mwenzake alafu mwenzie analia badala ya kushambulia ngome ya mwenzake utapata jibu
Kulia nako ni njia ya kupambana na adui. Unaweza kujifinya uanalia ili adui akuonee huruma aache kukushambulia kwa ngumi, ili akashaacha akizani ameshinda, wewe unanyanyua silaha yeyote iliyoko mbele Yako then bila yeye kujua unabamiza, adui huyo chali chini damu zinavuja tu, kujitetea hawezi tena, unachukua ushindi kiulaini [emoji16]

Kwahiyo Siyo kila kulia ni kushindwa, sometimes kulia ni maumivu unayokumbana nayo wakati wa mapambano na hili ushinde lazima upate maumivu pia.
 
Waulize watu wanaoishi nchi za EU zinazotegemea mafuta na gas Russia ndio watakwambia mziki wa inflation ni shida hasa kwa watu wa low income.

Ikifika winter hakuna suluhisho la inflation kuwasha hitting iwe anasa majumbani watu wataingia kitaa hiyo vita isiwe tabu kwenye maisha yao.

Vita sasa inaanza kuwa adhabu kwa raia wa West Europe wanasiasa wanaleta ukaidi tu lakini uwezi pambana na mtu mwenye nishati unayoitegemea wameshashindwa psychological war tayari wanaona aibu kukiri ikifika November awatakuwa na namna zaidi ya kumpigia magoti Russia vinginevyo wapambane na hasira za wananchi wao.
 
Super Power wa kuchonga kutimuliwa mji wa Kherson muda wowote baada daraja muhimu kulipuliwa na Himars
Ukraine's campaign to retake the occupied Kherson region is "gathering pace", Western military sources say.

A key bridge into the city of Kherson is now out of action after Ukrainian forces struck it with long-range rockets supplied by the US.

UK defence officials say the city is now "virtually cut off from other occupied territories"
 
Waulize watu wanaoishi nchi za EU zinazotegemea mafuta na gas Russia ndio watakwambia mziki wa inflation ni shida hasa kwa watu wa low income...
Hakuna mtu wa kumpigia magoti Putin, ni kichaa na tahira pekee anayeweza kufanya hivyo. Ni lazima kiunzi cha mafuta ya Urusi kirukwe kwa ajili ya usalama wa EU kwa miaka ijayo.
 
Super Power wa kuchonga kutimuliwa mji wa Kherson muda wowote baada daraja muhimu kulipuliwa na Himars
Ukraine's campaign to retake the occupied Kherson region is "gathering pace", Western military sources say.
A key bridge into the city of Kherson is now out of action after Ukrainian forces struck it with long-range rockets supplied by the US.
UK defence officials say the city is now "virtually cut off from other occupied territories"
Putin itambidi aongeze safari za vikao Kremlin, hizi silaha zinaenda kuanza kubadilisha kila kitu kwenye ulingo
 
Uyu popoma wa Pro nato anafikiri russia hii vita anataka iishe leo? angetaka ivyo mapema kabisa angeshamaliza kazi ukraine amefanya makusudi ili tuone uerope kuwa si chochote kama walivyokuwa wanatuaminisha kuwa ni watu smart,magenius etc
Hakuna cha kutaka, amekutana na kisiki cha mbabe wa Vita Marekani.
 
Hakuna mtu wa kumpigia magoti Putin, ni kichaa na tahira pekee anayeweza kufanya hivyo. Ni lazima kiunzi cha mafuta ya Urusi kirukwe kwa ajili ya usalama wa EU kwa miaka ijayo.
Hakuna mtu wa kumpigia magoti Putin, ni kichaa na tahira pekee anayeweza kufanya hivyo. Ni lazima kiunzi cha mafuta ya Urusi kirukwe kwa ajili ya usalama wa EU kwa miaka ijayo.

Hiyo inakwambia athari zake McDonalds awajapandisha bei ya bidhaa zao kwa miaka 14.

Waulize watu wanaoishi huko bei za vyakula sasa supermarkets.

Hao waingereza walau wana security of supply lakini awawezi kukwepa bei ya soko Russia akipunguza hasa winter, hao wengine ndio dependent na Russia kuanzia 90% to 40% kama unajua millions of cubic wanazotumia na ugumu wa kufidia hiyo supply in terms of shipping usingeongea.

Like I said subiri November wasipokubali yaishe basi wawe tayari na mziki wa wananchi wao; hivi tunavyoongea U.K. kuna mgomo wa railway kisa cost of living.

Sasa huko kwingine wanapotegemea Russia ndio kabisa ata Italy kumbe mzozo wao Russia politics pia zina changia. Chama chenye viti vingi kwenye bunge na senate (five star party) asilimia kubwa ya viongozi wake awaungi mkono tena vita.
 
Back
Top Bottom