Baada ya IGA ya DPW na Bandari zetu, licha ya mapungufu, HGA yake inakuja. Ombi kwa Serikali yetu sikivu, tunaomba Maximum Transparency kwenye HGA

Kwamba wataleta magari ya mizigo zaidi ya 2000 kwa ajili ya ku supply cargo yote inayopita bandarini,, swali madereva na matingo watakuwa waarabu au watanzania,,?
na mnafikiria vipi wamiliki wa magari ya mizigo wa kitanzania watakaokuwa wameathiriwa na jambo hili,, kuna watu wanaenda kupoteza mikate ya kila siku mjue hilo,, yasije yakaanza kama yale ya wazulu kule Africa kusini dhidi ya waafrica wenzao walioenda kujitafuta kule,,
 
Hakuna kinachobadilika kwenye HGA kutakuwa na mikataba ya utekelezaji yenye ukomo lakini sababu HGA inafuata kile kilichoandikwa kwenye IGA inasema mkataba utaisha pale shughuli za bahari zitakapoisha

DPW watawarudia tena serikali kusaini mkataba mwingine kipindi cha muda wa miaka kadhaa ili kufikia malengo mengine

Sasa hichi ndio ccm ndio wanatuambia ccm tusubiri HGA
 
Ni nchi yetu pekee ambayo masuala ya IGA na HGA yanaongelewa kama vile matokeo ya mechi za Simba na Yanga, hakuna sehemu nyingine duniani penye mijadala kwenye masuala nyeti na ya kiserikali kama haya.

Tumecheza na elimu kwa muda mrefu na huu uholela wa kujadili mikataba ambayo ni nyaraka za serikali kama vile ni karatasi tu, ni matokeo ya hiyo michezo ya hatari kwenye sekta nzima ya elimu.

Mikataba ipo mingi na inakuja mingi kila kukicha. Cha muhimu ni hao wenye dhamana ya kuihodhi huko serikalini kuwa watiifu na waaminifu kwa mamlaka zinazowaajiri. Kwa maana hata kuuvujisha mkataba ni matokeo pia ya kucheza na elimu kwa mapana yake.

Tufike mahali pa kuwa na mipaka ya masuala ya masikhara na yale yenye kuhitaji umakini.
 
Kaka Paskali,
Mimi naganda hapo kwenye sehemu ya heading ya bandiko lako., NANUKUU... "licha ya mapungufu" ... MWISHO WA KUNUKUU..!! na baadhi ya maeneo kwenye bandiko lako.

Hayo maneno niliyoyanukuu, yananipa taarifa kwamba hata wewe unaona TEC wapo 100% sahihi kwa waliyoyasema kwenye tamko lao kuhusu DPW. Na kwa namna moja au nyingine, wamekufanya uone mapungufu yaliyoko. Sasa, nina maswali haya kwako na kwa wengine wenye mtazamo kama wako;

1. Kwanini unadhani IGA iendelee huku mkataba una mapungufu??

2. HGA yake unayoizungumzia, unadhani itaondoa mapungufu yanayotajwa?

3. Hivi HGA huwa haifuati IGA imesema nini? Hapa naomba kuelimishwa ni kwa namna gani HGA inaweza ikaongea kinyume na IGA.

4. Unadhani transparency itaondoa mapungufu?? Kwani hawawezi weka transarency huku mapunguvu yakiongezeka? Unadhani mapungufu yametokana na kutokuwa wawazi?

5. Kwa kutumia hiyo hiyo kawaida ya HGA, kuwa huwa ni confidential, unadhani wataweka wazi yatakayokuwemo kwenye HGA? Nini kitawalazimisha kuweka wazi wakati kawaida yake ni USIRI? Wasipokuwa OPEN what will be the next step?. Huoni kwamba unataka tucheze kamari au pata potea?

6. Kwenye content yako, kuna maelezo haya, nanukuu .."Wale wote mlioipinga hii IGA kwa hoja za kisheria, hoja zenu zote zitakuwa zimezingatiwa kwenye HGA.".. Mwisho wa kunukuu. Nini kinakufanya uamini hicho ulichokiandika? Wasipozingatia je?

7. Nanukuu swali lako... "The issue ni moja tu, jee HGA ya DPW na Bandari zetu itakuwa open kama hii IGA?." .. Mwisho wa kunukuu. Huoni kwamba swali lako lina-contract nilichokinukuu kwenye item 6. hapo juu? Huoni kwamba, swali hili linaturudisha pale pale kwenye mashaka tuliyonayo juu ya mapungufu ya IGA?

Kaka Paskali, naheshimu sana uelewa wako kwenye mambo mbalimbali. Binafsi nimekuuliza maswali kadhaa kwenye posts zako mbalimbali. Yapo uliyoyakwepa na hujawahi kuyajibu hadi sasa, kwa ahadi kwamba utarudi na majibu, lakini hujarudi. KWA MASWALI HAYA NITAKUWA KINGÁNGÁNIZI KWAKO KAKA, ILI UJIBU KILA MOJA KWA UFASAHA.

Ngali K.
 
Huoni tunavyoshitakiwa nje na kulipa pesa nyingi?
 
Naunga mkono hoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…