Baada ya IGA ya DPW na Bandari zetu, licha ya mapungufu, HGA yake inakuja. Ombi kwa Serikali yetu sikivu, tunaomba Maximum Transparency kwenye HGA

Hatuoni hizi taratibu na urasimu wake kama zinachelewesha uchumi wetu kwa ujumla, hatuwezi kuona hilo suala kwa sababu wengi wetu sio wadau wa moja kwa moja wa biashara za bandari.
Uadilifu tu ila taratibu zipo sawa kabisa ila uadilifu wetu ndiyo huu tunachukuliwa wanaenda kutupa semina sijui wanatulipia hotel then wanakupa malaptop unarudi hapa meno 34 yote nje then kesho unaletewa mkataba unasain tu wala husomi sababu jana alikufanyia ukarimu!
 
Kuna mtu umeongea nae leo amekuhakikishia hilo?. Hivyo umeona uwahi kuleta. Huu mkata utatupwa, utaipasua CCM
Watanzania ni wazito sana kuelewa, kunapotolewa tuhuma, ukiona watuhumiwa wamenyamaza kimya, ujue ni admission of guilty!, tangu TEC wametoa waraka, umemsikia kiongozi yeyote wa serikali yetu akijibu kitu?. Maana yake mapungufu na madhaifu yote ya IGA ni ya kweli, lakini kwa vile IGA sio mkataba ni barua tuu ya posa, Mwenye dada hakosi shemeji, IGA ni posa tu. Je, tuendelee kupiga kelele kuzozania posa, au tutulie tupange Mahari ya maana kwenye HGA? HGA ndio mahari, tutapanga mahari nzuri ya binti yetu.
P
 
Mayalla siku hizi anatukosea heshima sana humu ndani, anadhani anacheza na watoto wadogo wa nursery.
Owa
Kwa hiyo wewe shida yako ni posa! Mtauza watoto aisee.
 
Mwarabu anakuja kuwekeza huku likiwa ni suala la kimkakati sio la kukurupuka hata kidogo. Alijipanga miaka na miaka kwenye masuala ya biashara za usafiri wa kwenye maji.

Anazo meli 400 sio kampuni ndogo ni kubwa sana. Pia anamiliki migodi huko DRC na Congo. Mmarekani kampiga vita mpaka kachoka, jamaa anazidi kutanua wigo wa biashara zake.
 
Unaombaje maximum transparency kwenye HGA wakati governing IGA ina kipengele cha usiri na hata ulivyoiona IGA ni kwa njia za panya tu imevujishwa?
 
Tunataka tujue wanachukua Bandari kwa muda gani na serikali yetu itapata kiasi gani.
Hii utaijua kwenye HGA, ila mikataba ya kihivi ni long lease ya kuanzia 10 years ili ku guarantee the return of investment.
Pia tunataka tujue wataajiri Watanzania wangapi?
Wataajiri Watanzania wengi, ila pia watakuja wageni wengi kwasababu ya modernity na state of art highly sophisticated robotic technology ambayo sisi Watanzania hatuna. Wafaidika wakuu wa kwanza wa ajira mpya ni madereva wa semi trelas, wanaleta malori ya container 2,000 kubebea containers zao kutoka Dar port hadi dry port yao ya Kigali.
P
 
Unaombaje maximum transparency kwenye HGA wakati governing IGA ina kipengele cha usiri na hata ulivyoiona IGA ni kwa njia za panya tu imevujishwa?
As long as the cat is out of the basket, there is nothing to hide!, public interest supersedes confidentiality clause.
P
 
mark my words ndo utajua ukuu wa kanisa.Muda utaongea
Kanisa litabakia likishangaa, kwani mwekezaji atakuja na kupokelewa na biashara zitaanza kama kawaida.

Vigezo vya uzawa kumiliki biashara vinavyotumiwa na maaskofu ni kama vimechelewa kusikika, ni masuala ya kiuchumi tena ule wa kisasa.

Wazalendo wa kitanzania wanao uwezo wa kufunga mitambo ya kisasa na kuendesha magati kumi na mbili ya TPA inayohudumia nchi nane zinazotuzunguka?. kuongea ni kazi nyepesi sana kuliko kutenda.
 
As long as the cat is out of the basket, there is nothing to hide!, public interest supersedes confidentiality clause.
P
But is the cat really out of the basket? Serikali hata haijatoa IGA na ikiamua inaweza kuwakamata wote mnaoijadili kwa kuwaambia mnajadili nyara za siri za serikali bila kibali wala uhalali.
 
DP waliwekeza Djibouti mbona haina hayo maendeleo kama Dubai?
 
Mawazo ya kijinga kama haya ndo nyinyi mnapotosha bi tozo mpaka mnataka kuipasua nchi!
 
Mkuu sina hakika kama tutaambiwa cho chote! Maana Mama ameshasema ataendelea kukaa kimya! Sasa akikaa kimya kuna cho chote tunatarajia kuambiwa?
 
Yaani mnajisifu kuwa mnaenda kujenga nyumba nje ya Msingi?
 
Kuwepo na transparency kwenye mkataba ambao hukushirikishwa wakati wa utiaji saini?
Sio lazima kumshirikisha kila mtu kwenye kila kitu, kuna mikataba inayohitaji ushirikishwaji umma, na kuna mikataba ni internal affairs, sheria yetu ya rasilimali za taifa iko very clear, hakuna usiri kwenye rasilimali za taifa!.
Sasa hivi utetezi uko wazi kuwa hilo suala linapingwa kwakuwa ni la muisilamu.
Wote wanaopinga IGA ya DPW na Bandari zetu kwa hoja za udini ni muflis!, ni watu waliofilisika!.
P
 
Uncle bandari kumepoa wafanyakazi hawaelewi, lakini ukweli ndio huo
Sii kweli, kwasababu since day one, wafanyakazi wameelezwa no one will lose his/her job!, sasa wasiwasi wa nini?.
Mama hana nia ya kujinasua kwakua alipojiingiza akisimama mchale akikaa mchale ila atatupuuza Watanzania kwakua anajua sisi ni debe tupu tuu hatuna madhara wala hatujielewi....
Kwani ni uongo?. Hii IGA ya DPW na Bandari zetu, imetusaidia kwa mengi
HGA itaendelea kua siri kama ilivyo siku zote na pia hakutakua na mkataba uki vuja tena kwa serikali hii ya awamu ya 6
Duh...!.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…