Baada ya IGA ya DPW na Bandari zetu, licha ya mapungufu, HGA yake inakuja. Ombi kwa Serikali yetu sikivu, tunaomba Maximum Transparency kwenye HGA

mawazo ya kijinga kama haya ndo nyinyi mnapotosha bi tozo mpaka mnataka kuipasua nchi!
Mawazo ya kijinga ni yale ya kuandika waraka kupinga uwekezaji mkubwa wenye kuja kuinua uchumi wa nchi.

Mlipoambiwa nchi inafunguliwa ndio hivi sasa, sasa ujinga ulivyowajaa mnakuja na hoja za siri za uislam wa mwekezaji.

Kawekeza Uingereza, USA kote huko kuna wakristo wanaojielewa kuliko sisi tuliojaa roho mbaya na uchoyo mwingi wa kijamaa.
 
No hatijisifu, bali nyumba ikijengwa kwenye msingi mbovu, ili isivunjike, inawekewa reinforcements.
P
Natamani nijibu hii, ila najizuia sababu ya heshima yangu kubwa niliyo nayo kwako.
The Boss na na wewe Pascal Mayalla mmeweza sana kuni block maana mmenisababishia kujizuia sana juu yenu sababu ya appreciation niliyo mayo juu yenu kwa historia ya humu JF.
You know. We Italians value a lot about back ground.
 
Na hii ndiyo kazi ya ujasusi wa kiuchimi.Asante kwa elimu hii mkuu.
 
Angalau Paskali safari hii umeandika vizuri kwa hekima. Hongera.
 
Naunga mkono hoja, na tuko Wakatoliki wengi tuu hatuungi mkono waraka wa viongozi wetu wa kanisa Katoliki.
P
 
Wanabodi,

Kama kawaida yangu ya kuwaletea trends mbalimbali, leo naomba niwaletee hii trends za kinachoendelea kwenye hii issue.

Baada ya IGA ya DPW na Bandari Zetu, HGA yake iko njiani inakuja...
Sitaki kukosoa mawazo yako ndugu Mayala, lakini angalizo tu. Mara nyingi umekuwa ukijadili swala hili la bandari kichawachawa sana badala ya kuwa mkweli kama mwanasheria. Kabla ya yote, unapodai HGA ziwekwe wazi, hujasoma itajio la IGA yenyewe kwamba HGA zote ziwe siri? Unaposema serikali na Bunge lako tukufu pamoja na Mahakama zimepitisha jambo hili bila mhimili mmoja kuingilia mwingine, una uhakika?

Tuwe wakweli hii mihimili, mmoja umemeza mihimili mingine, wote ni mashahidi kwa matukio mengi likiwemo ili la bandari, labda tuwe wanafiki na kuanza kuombana ushahidi. Kwasababu bandiko hili hapa chini linaeleza mambo mengi, nakuomba ulisome angalau litakupa picha halisi. By the way, IGA ilipaswa kufuata Sheria zetu, au sisi kubadili Sheria zetu kufuata matakwa ya mkaba wa Waarabu kama ambavyo bunge lako na serikali yako tukufu hiko mbioni kufanya?

1. Preamble

Dear Jakaya Mrisho Kikwete,
The Former President of the United Republic of Tanzania,

The convergence point of hopes and fears of the citizenry in each and every nation-state is land, the natural resources embedded in the land and the land-borne artificial infrastructures.

The said... A Letter to Jakaya Kikwete concerning a threat of 'Arab Settler Colonialism' through the instrumentality of Tanzania-Dubai Treaty
 
Umehongwa au akili huna?
 
Mpaka muishushe hii picha kutoka Dubai.
 
Toka lini hga zikawa wazi Kwa wananchi.
 
Punguza uongo. Mbona JPM alipigwa nyaraka mbili ya TEC na KKKT na maisha yakasonga?.
 
Kusomea mikataba ni Jambo moja na kuandika mikataba ni Jambo jingine. Ndio maana Rais aliwapa makavu waandika mikataba kutoka serikalini.
 
Kwa hivyo unakiri kwamba Tanzania haiwezi kusimamia na kuendesha bandari zake mpaka mwarabu aje. Kwa akili hizi ndio maana tumeporomoka kwenye uchumi wa kati.
 
Wamewekeza pia Amsterdam, London, Southampton na bandari nyingine nyingi za mataifa yenye watu wanaojielewa.
Umeulizwa kuhusu Djibouti. Mbona hayo maendeleo hayapo?. Pia wapo Rwanda mbona hayo mabadiliki hayapo?. Unamtumia nchi za ulaya ambapo makubaliano yao ni tofauti na haya ya kwetu. Kasome mkataba wa Sweden na DP World.
 
Na wewe nawe punguza uongo. TEC wamepinga vifungu vya mkataba. Ndio maana wamekuwa specific kwamba wanapinga mkataba wa bandari na sio uwekezaji.

Halafu ujinga ni kwamba umeshindwa kuinua uchumi wako unategemea mwarabu aje akusaidie kuinua uchumi wako.
 
Chuki za kidini unazo wewe mnafiki. Wananchi wameonesha hofu wewe unadai ni chuki za kidini. Wananchi wakae kimya?. Baadala ya kujisimamia kiuchumi, tunataka mjomba kutoka nje ndio aje atusaidie kiuchumi. Kwa maana nyingine tunajitukana kwamba sisi ni bogus.
 
Naunga mkono hoja, na tuko Wakatoliki wengi tuu hatuungi mkono waraka wa viongozi wetu wa kanisa Katoliki.
P
Punguza unafiki jiongelee mwenyewe. Wewe hata JPM alikuita ni mtu wa njaa. Na ni kweli upo tayari kuongea uongo upate chakula. Very ashaming.
 
Umeulizwa kuhusu Djibouti. Mbona hayo maendeleo hayapo?. Pia wapo Rwanda mbona hayo mabadiliki hayapo?. Unamtumia nchi za ulaya ambapo makubaliano yao ni tofauti na haya ya kwetu. Kasome mkataba wa Sweden na DP World.

Akikujibu nitag
 
Sitaki kukosoa mawazo yako ndugu Mayala, lakini angalizo tu. Mara nyingi umekuwa ukijadili swala hili la bandari kichawachawa sana badala ya kuwa mkweli kama mwanasheria.
Mkuu mbussi , naomba kuheshimu maoni yako, kabla Bunge letu Tukufu halijaridhia hii IGA nilitoa ushauri huu Wabunge Wetu, Macho ya Watanzania Wote Leo ni Kwenu!. Maslahi ya Taifa Mbele!. Tuwaogope Kama Ukoma Muflis Hawa!, Kama Huwezi, ni Lazima Usaidiwe Tuu! jee kwenye ushauri huo kuna uchawa?

Baada ya Bunge letu Tukufu kuridhia IGA hivyo hivyo ilivyo na makandolando yake bila any reservations, ile Jumamosi ya tarehe 10 June, 2023, tarehe 11 June, 2023 mimi ndio mtu wa kwanza nilipandisha bandiko hili Japo Bunge Limeridhia, DPW Kuendesha Bandari Zetu, ni Makubaliano Tu, Tukithibisha Kuna Matatizo, Tunarekebisha Mkataba wa HGA, Kazi Nzuri Iendelee! ambalo ndio blue print ya ukosoaji wa mkataba wa IGA na Bandari zetu, wengine wote waliokosoa walipita mule mule!. Angalia bandiko hilo jee kuna uchawa?
Kabla ya yote, unapodai HGA ziwekwe wazi, hujasoma itajio la IGA yenyewe kwamba HGA zote ziwe siri? Unaposema serikali na Bunge lako tukufu pamoja na Mahakama zimepitisha jambo hili bila mhimili mmoja kuingilia mwingine, una uhakika?
Hili ni jambo technical la kisheria, Tanzania tuna sheria ya rasilimali za taifa inayozuia migogoro kutatuliwa nje ya nchi, hivyo serikali yetu haikupaswa kuingia ile IGA kabla ya kwanza kubadili sheria zetu!. Serikali imesaini mkataba au makubaliano batili ya hii IGA ya DPW na Bandari zetu, Bunge letu Tukufu likaridhia hii IGA batili hivyo hivyo na ubatili wake, ni Bunge kutoiingilia serikali. Mahakama nayo ikauona ubatili huo na kuamua in favour of IGA ili kutoliingilia Bunge letu Tukufu!.

Hoja yangu ya HGA kuwekwa wazi ni for public interest. Japo HGA huwa ni confidential lakini kufuatia kelele nyingi kuhusu hii IGA, then HGA iwekwe wazi.

P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…