Baada ya IGA ya DPW na Bandari zetu, licha ya mapungufu, HGA yake inakuja. Ombi kwa Serikali yetu sikivu, tunaomba Maximum Transparency kwenye HGA

Tukiasili akili za mbuni za kuzika kichwa mchangani kwa matumaini kuwa tufani itapita tu, donda lililosababishwa na huu mkataba kwa taifa halitakaa lipone.

Mnawadunisha sana Watanzania.
 
Usikivu wa serikali upo wapi sasa kama watu wamepiga kelele kwenye mapungufu ya IGA hadi sauti zimekauka huku hata nukta tu haijahamishwa?
Ahadi ni deni!, PM Majaliwa alitoa solid promise hoja zitazingatiwa kwenye HGA, ndio maana nimeshauri HGA iwe wazi.
Kama hamuwaondolei kinga ya mashtaka hawa viongozi wenu,wataendelea kuwadharau hadi kiama!
Sii kweli!.
P
 
Kama kweli itakuwa ni kampuni yenye mitambo ya kisasa, zungumzia watu wangapi watapoteza ajira hapo bandarini, na sio idadi ya ajira.
Hakuna atakapoteza ajira!. Kwa kuanzia wanaleta semi 2000!.
P
 

Mwandishi Mkuu wa habari za kiuchunguzi.

Kuna hii HGA kati ya serikali wa wawekezaji wanaopromote upinde.

Tunaweza kuupata mkataba huu ili tuujadili....
Manake wapambanaji wamekomaa kuwapiga Dpw na kuwakingia kifua wanaupinde.
 
Sasa wewe mwenyewe unawasiwasi wa openess ya hizo HGA unategemea nini bwana P ??!
Ndio essence ya bandiko hili kuiomba serikali yetu sikivu itusikilize, Watanzania tunataka kuziona hizo HGA ili tujiridhishe maoni yetu kuhusu mapungufu ya IGA, yamezingatiwa kwenye HGA.
P
 
Hofu zetu zimejibiwa na wanasheria wa serikali kwa kina na kwa hoja zenye kueleweka, kama wanasheria wakati wanatoa ufafanuzi wa kina kwenye TV sisi tunaangalia channel za nyimbo mpya za Diamond na Zuchu, basi hayo ni matatizo yetu binafsi.
 
Mwandishi Mkuu wa habari za kiuchunguzi.
Ndugu yangu Mohamed Abubakar , kwanza mimi sio mwandishi Mkuu wa habari za uchunguzi, mimi ni mwandishi wa kawaida wa habari za kawaida nikiandika kwa kujitegemea kwa kujitolea
Kuna hii HGA kati ya serikali wa wawekezaji wanaopromote upinde.
Sijabahatika kuiona
Tunaweza mkataba huu ili tuujadili....
Manake wapambanaji wamekomaa kuwapiga Dpw na kuwakingia kifua wanaupinde.
Duh...!.
P
 
Ujinga ni kushindwa kuona kwamba hapo bandarini panachangia sana bei za bidhaa kupanda na kufanya maisha mtaani yakawa magumu.

Ujinga ni kuendelea kudhani kuwa njia za kizamani za utatuzi wa matatizo zinaweza kusaidia wakati dunia ya sasa imeshabadilika na haina tena muda wa kukusubiri ujipange, ujinga ni kuishi na mitazamo ya kizamani katika dunia mpya.

Ukielewa namna DPW atakavyokwenda kuiondoa hiyo foleni ya meli na ukaelewa kuwa hatua hiyo inakwenda kugusa uchumi kwa mapana yake naamini hutakuwa na mitizamo uliyonayo hivi sasa.

Maaskofu walipewa shule pana ya IGA siku walipofanya mkutano na wanasheria wa serikali, baadhi yao wana mitazamo ya kijamaa ya sisi wenyewe wazalendo kushika njia kuu za uchumi, ni mitazamo ile ile ya hayati Julius Nyerere lakini dunia ya sasa imeshabadilika kwa kiasi kikubwa.

Ni mwendo wa teknolojia na kuzimiliki ni bei ghali pia uendeshaji wake unahitaji nidhamu kubwa.
 
Umeulizwa kuhusu Djibouti. Mbona hayo maendeleo hayapo?. Pia wapo Rwanda mbona hayo mabadiliki hayapo?. Unamtumia nchi za ulaya ambapo makubaliano yao ni tofauti na haya ya kwetu. Kasome mkataba wa Sweden na DP World.
Ni vigumu kuongelea Djibouti kwani hujui uendeshaji wao mzima wa serikali upo vipi, je walijipanga vipi kwenye masuala ya kisheria mpaka kufikia kusaini mikataba? Djibouti hawakujipanga sisi tumejipanga vizuri sana.
 
maneno yakinafiki Zaidi kwa wakati huu ni selikari sikivu na Bunge tukufu
 
Sijajua km unasali au la Ila naomba ufute neno ili "TUKUFU"
Bonge lire la Tanzania sio TUKUFU, pili na serikali sio TUKUFU.
Km we unasali kwel utanielewa vizur
 
Mkuu, naomba nizungumze kidogo kwenye kile unachokiita jambo la kisheria. Kwa kawaida kwenye nchi zilizo na mfumo wa utawala kama wa kwetu, kinachofanyika ktk hii mihimili mitatu ni ubatili mtupu. Ni kwa bahati mbaya wanayoyafanya haya ni wasomi wakubwa tena wa sheria ambao nadharia ya "checks and balance" wanaijua vizuri.

Pamoja na kutunga sheria, bunge letu limeacha kazi yake ya msingi ya kushahuri na kuisimamia serikali na badala yake serikali ndiyo inalipangia na kulisimamia Bunge. Kinachoendelea kwasasa ni mfumo wa kifalme (madhara ya kuwa na chama kimoja kilichovimbewa). Kazi ya mhimili wa mahakama pamoja na mambo mengine ni kutafasili Sheria.

Sasa bwana Mayalla, unaponiambia serikali ilikosea kwenye IGA kati yake na DPW alafu ile mihimili mingine nayo ikabariki makosa hayo kwa kile unachokiita mhimili mmoja hauwezi kuingilia mwingine, nakuwa sikuelewi!! Hii mihimili kwa hapa kwetu ni kama "organised criminal group" linalotafuna nchi yetu kwa kulindana. Bunge limekuwa rubber stamp ya kubariki makosa yanayofanywa na serikali. Hii ya kuitana kwenye party caucus kabla ya bunge kupisha jambo lolote lenye maslahi ya nchi, kunalinyima uwezo bunge letu kusimama kama mhimili unaowajibika kwa wananchi badala yake linawajibika kwa CCM na serikali yake. Ni bunge dhaifu zaidi ya bunge dhaifu alilolizodoa Prof. Assad!!

Nije kwenye HGA unazotaka ziwekwe wazi!! Najua ni matamanio yako na ndiyo sababu umetoa ushauri. Ukweli ni kwamba ni ushauri ambao kamwe hautakaa utekelezwe. Sababu ni nyingi hapa nakupa chache. Kwanza, moja ya masharti ya Mwarabu kwenye IGA iliyosainiwa na Serikali yetu ni kutokuweka wazi mikataba midogomidogo ya utekelezaji (HGAs). Pili, Sheria za kulinda raslimali za nchi za mwaka 2017, zinaitaka serikali kutisha Bungeni mikataba yote inayoingiwa na wageni kwenye raslimali zetu. Sasa shida iko hapa: Tangu SSH aingie madarakani, nadhani ni huu mkataba mmoja tu wa bandari ambao umepitishwa Bungeni tena kwa maelekezo. Unadhani hizo HGA watakuonyesha? Kama Serikali imeamua kuvunja Sheria kutopeleka mikataba mingine, je, hii ambayo sheria inaweka wazi kuwa iwe siri??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…