Baada ya IGA ya DPW na Bandari zetu, licha ya mapungufu, HGA yake inakuja. Ombi kwa Serikali yetu sikivu, tunaomba Maximum Transparency kwenye HGA

Baada ya IGA ya DPW na Bandari zetu, licha ya mapungufu, HGA yake inakuja. Ombi kwa Serikali yetu sikivu, tunaomba Maximum Transparency kwenye HGA

Hakuna atakapoteza ajira!. Kwa kuanzia wanaleta semi 2000!.
P
Hizi porojo zako pia tulizosikia wakati wa ule utapeli wa fursa za bomba la gas. Wengine tukajichanganya hadi kununua viwanja huko Mtwara, leo hii muulize hata Ridhiwani ama mama Salma Kikwete kama wana hata vibanda vya mpesa kule.
 
Mkuu, naomba nizungumze kidogo kwenye kile unachokiita jambo la kisheria. Kwa kawaida kwenye nchi zilizo na mfumo wa utawala kama wa kwetu, kinachofanyika ktk hii mihimili mitatu ni ubatili mtupu. Ni kwa bahati mbaya wanayoyafanya haya ni wasomi wakubwa tena wa sheria ambao nadharia ya "checks and balance" wanaijua vizuri.
Mkuu mbussi , naunga mkono objectivity yako, usemayo ni kweli kabisa ile the doctrine of separation of powers, checks and balance haipo kabisa kwenye nchi yetu!. Hili niliwahi kulizungumza humu kuhusu Bunge kujipendekeza kwa serikali, Mahakama nayo kuligwaya Bunge na kujipendekeza kwa serikali Nani Zaidi Kati ya Bunge na Mahakama?!. The Doctrine of "Separation of Powers" Nothing, Just a Myth!
Pamoja na kutunga sheria, bunge letu limeacha kazi yake ya msingi ya kushahuri na kuisimamia serikali na badala yake serikali ndiyo inalipangia na kulisimamia Bunge. Kinachoendelea kwasasa ni mfumo wa kifalme (madhara ya kuwa na chama kimoja kilichovimbewa). Kazi ya mhimili wa mahakama pamoja na mambo mengine ni kutafasili Sheria.
Naunga mkono hoja, Bunge halitimizi wajibu wake kikamilifu, Mahakama haitimizi wajibu wake kikamilifu na serikali haiwajibiki kikamilifu kwasababu there is no one to check it out!.
Sasa bwana Mayalla, unaponiambia serikali ilikosea kwenye IGA kati yake na DPW alafu ile mihimili mingine nayo ikabariki makosa hayo kwa kile unachokiita mhimili mmoja hauwezi kuingilia mwingine, nakuwa sikuelewi!!
Lazima utaelewa tuu with time!
Hii mihimili kwa hapa kwetu ni kama "organised criminal group" linalotafuna nchi yetu kwa kulindana. Bunge limekuwa rubber stamp ya kubariki makosa yanayofanywa na serikali. Hii ya kuitana kwenye party caucus kabla ya bunge kupisha jambo lolote lenye maslahi ya nchi, kunalinyima uwezo bunge letu kusimama kama mhimili unaowajibika kwa wananchi badala yake linawajibika kwa CCM na serikali yake. Ni bunge dhaifu zaidi ya bunge dhaifu alilolizodoa Prof. Assad!!
Ni kweli kabisa, dawa pekee ya kulitibu hili Bunge la namna hii ni kulizomea from time to time kama hivi
Nije kwenye HGA unazotaka ziwekwe wazi!! Najua ni matamanio yako na ndiyo sababu umetoa ushauri. Ukweli ni kwamba ni ushauri ambao kamwe hautakaa utekelezwe. Sababu ni nyingi hapa nakupa chache. Kwanza, moja ya masharti ya Mwarabu kwenye IGA iliyosainiwa na Serikali yetu ni kutokuweka wazi mikataba midogomidogo ya utekelezaji (HGAs).
Maadam IGA ni barua tuu ya posa, anayechumbia hawezi kutupangia, sisi wenye binti Bandari ndio tunapanga mahari na kupanga masharti na sio kupangiwa!, hivyo bado HGA inaweza kuwa nzuri!
Pili, Sheria za kulinda raslimali za nchi za mwaka 2017, zinaitaka serikali kupitisha Bungeni mikataba yote inayoingiwa na wageni kwenye raslimali zetu. Sasa shida iko hapa: Tangu SSH aingie madarakani, nadhani ni huu mkataba mmoja tu wa bandari ambao umepitishwa Bungeni tena kwa maelekezo.
No sio hii IGA moja tuu imeingia Bungeni hata IGA ya mradi wa LNG imepita Bungeni na kuridhiwa, HGA ya LNG bado!, unaweza kushangaa HGA ya DPW na Bandari zetu ikatoka kabla ya HGA ya LNG haijatoka!.
Unadhani hizo HGA watakuonyesha? Kama Serikali imeamua kuvunja Sheria kutopeleka mikataba mingine, je, hii ambayo sheria inaweka wazi kuwa iwe siri??
Serikali, Bunge na Mahakama vinatufanya kama Watanzania ni ndondocha!, kwasababu wanaamini no one can do anything!, but... naomba nisimalizie...!
P
 
Let it come, Tanzania ina wenyewe na wenyewe ni CCM.
Mkuu elvischirwa , this is the notion iliyopo kwa waliowengi wakiwemo CCM kuamini kuwa Tanzania ina wenyewe na wenyewe ni CCM!. This is a wrong notion, ni kweli Tanzania ina wenyewe ila wenyewe sio CCM!, wenyewe ni Watanzania, CCM ni inclusive, ila it's very unfortunately wenyewe wenye Tanzania yao, hawajitambui, hawajijui kuwa wao ndio wenye Tanzania yao, ndio wenye serikali, Bunge na Mahakama, ili kuwawezesha Watanzania kujitambua ni kuwaelimisha kuhusu katiba, sheria, haki na wajibu.
P
 
Mkuu elvischirwa , this is the notion iliyopo kwa waliowengi wakiwemo CCM kuamini kuwa Tanzania ina wenyewe na wenyewe ni CCM!. This is a wrong notion, ni kweli Tanzania ina wenyewe ila wenyewe sio CCM!, wenyewe ni Watanzania, CCM ni inclusive, ila it's very unfortunately wenyewe wenye Tanzania yao, hawajitambui, hawajijui kuwa wao ndio wenye Tanzania yao, ndio wenye serikali, Bunge na Mahakama, ili kuwawezesha Watanzania kujitambua ni kuwaelimisha kuhusu katiba, sheria, haki na wajibu.
P
Ohoo! Hii mambo ya darasa utabaki peke yako, labda wawemo na akina Daimondi.
Katika Afrika Mashariki na Kati watanzani tuko nyuma sana kwenye kupenda haki zetu, tunamuachia Mungu au mungu japo wote hawatusikilizi.
 
Mawazo ya kijinga ni yale ya kuandika waraka kupinga uwekezaji mkubwa wenye kuja kuinua uchumi wa nchi.

Mlipoambiwa nchi inafunguliwa ndio hivi sasa, sasa ujinga ulivyowajaa mnakuja na hoja za siri za uislam wa mwekezaji.

Kawekeza Uingereza, USA kote huko kuna wakristo wanaojielewa kuliko sisi tuliojaa roho mbaya na uchoyo mwingi wa kijamaa.
mikataba waliyoingia nchi hizo sawa na huu wa kimangungo wa bi.tozo?
 
Maamuzi magumu hupigwa vita siku zote. Mnasema anataka kuuza nchi lakini hamna uwezo wa kuonyesha risiti za mauzo zipo vipi, hamna uwezo wowote wa kuweka hadharani ushahidi wa hicho mnachokisema zaidi ya kuwa ni chuki za kidini zenye ubaguzi ndani yake.
nyie mliofilisika kimawazo ndo mnaleta masuala ya kidini.TEC wanatoa WARAKA miaka yote haijalishi rais ni muislam au ni mkristo.

kwanini waraka wa sasa wa TEC muone wa kidini?
 
Usituchoshe na wewe. Hatuutaki mkataba na DPW. Kuhonga tu watu kumemuondolea uhalali. Hatutaki
Watanzania tujifunze kitu kinachoitwa managing diversity, kuna watu wengi tuu wameikubali DPW na Bandari zetu, ila tatizo ni IGA na sio DPW!, msianze kujimilikisha watu kujiita hatuutaki mkataba wa DPW, jifunze kuwavumilia wanaoutaka mkataba wa DPW na Bandari zetu!.
P
 
Wanabodi,

Kama kawaida yangu ya kuwaletea trends mbalimbali, leo naomba niwaletee hii trends za kinachoendelea kwenye hii issue.

Baada ya IGA ya DPW na Bandari Zetu, HGA yake iko njiani inakuja!

Naomba kukiri nimekuwa inspired kupandisha bandiko hili kwa bandiko la mwana JF huyu. Wananchi tupige kura kulimaliza hili sakata la Dp world

Mkuu utukufu mwanjisi , baada ya IGA ya DPW na Bandari zetu kusainiwa na Mhimili wa serikali yetu Tukufu, licha ya kuwa na mapungufu lukuki ya kisheria, ikiwemo illegality on the capacity of Dubai to contract an international Treaty, ikapelekwa Bungeni na kuridhiwa na Mhimili wa Bunge letu Tukufu, hivyo hivyo ilivyo without any reservations, na Mhimiliwa Mahakama ukatoa baraka zake za the Separation of Powers, bila Checks and Balance, ya kutoliingilia Bunge, kinachoendelea sasa ni maandalizi tuu ya HGA.

Kwa kawaida HGA zinakuwaga ni confidential, lakini kufuatia sintofahamu nyingi za hii IGA, tuiombe serikali yetu Tukufu, kufanya a maximum transparency kwenye hii HGA ya DPW na Bandari zetu, isiwe confidential as it used to be, iwe open ili wale wote waliopinga IGA kwa hoja za kisheria, waridhishwe kuwa hoja hizo zimezingatiwa kwenye HGA.

The chronology of events ni
1. Kikao kijacho cha Bunge, kitaibadili ile sheria ya Magufuli ya ulinzi wa Rasilimali za Taifa, ili to accommodate HGA ya DPW na Bandari.

Hizi HGA usually takes time, mfano mpaka sasa HGA ya mradi wa gesi wa LNG bado haijasainiwa, ila mnaweza kushangaa HGA ya DPW na Bandari zetu ikatoka fasta.

Wale wote mlioipinga hii IGA kwa hoja za kisheria, Waziri Mkuu wetu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, alituahidi hoja zenu zote zenye mashiko, zitakuwa zimezingatiwa na kuwa accommodated kwenye HGA.

The issue ni moja tu, jee HGA ya DPW na Bandari zetu itakuwa open kama hii IGA?.

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali
Wewe ni kada wa CCM tunakufahamu! Hatuitaki hata hiyo IGA
 
Watanzania tujifunze kitu kinachoitwa managing diversity, kuna watu wengi tuu wameikubali DPW na Bandari zetu, ila tatizo ni IGA na sio DPW!, msianze kujimilikisha watu kujiita hatuutaki mkataba wa DPW, jifunze kuwavumilia wanaoutaka mkataba wa DPW na Bandari zetu!.
P
Pascal msikilize huyu jamaa wa huko South
 
Back
Top Bottom