GSM ndiyo wamesimamia huu Mchakato mzima. GSM hawa hawa ndiyo kwa 99% wanaendesha 'Operations' zote za Yanga SC na cha Kushangaza tena Mmoja wa Watendaji Wakuu wa GSM Injinia Hersi Said nae amechukua Fomu Kugombea Urais Yanga SC.
Je, kwa Kitendo hiki ( hatua hii ) ya Injinia Hersi Said nae kuingiwa na Tamaa ya Kuutaka Urais kutakuwa na Uchaguzi wa Uhuru na Haki kwa wana Yanga SC wote?
Je, mfano ikitokea Injinia Hersi Said akaukosa huo ( huu ) Urais ndani ya Yanga SC hawezi akaishawishi GSM iachane na Kuidhamini Yanga SC na Yanga SC warudi tena katika zile zama zao walizozizoea za Umasikini, Shida, Taabu na kutembeza Bakuli huku wakichapana Bakora?
Hata hivyo wenye Akili Kubwa tulishajua tu tokea zamani kuwa GSM ilikuwa inamuandaa Injinia Hersi Said kuja kuwa Kiongozi wa Yanga SC na ndiyo maana ikaanza Kwanza kwa 'Kuwalainisha' Kifikra na Kimtizamo wana Yanga SC wote duniani ambao ukitaka Ugombane nao Wewe iseme GSM au Injinia Hersi Said kwani Kwao huyu Injinia Hersi na Gharib wameshawageuza kuwa ni Mungu na Kimbilio Kuu la Kiuchumi kwa wana Yanga SC 'Njaa Njaa' wengi waliopo Tanzania.
'Mission Accomplished' tu kwa GSM.