PreGE2025 Baada ya Jaji Mkuu Mstaafu wa Kenya Willy Mutunga kushikiliwa Uwanja wa Ndege Dar, Jaji Mkuu mwingine mstaafu David Maraga afanikiwa kupenya Kisutu

PreGE2025 Baada ya Jaji Mkuu Mstaafu wa Kenya Willy Mutunga kushikiliwa Uwanja wa Ndege Dar, Jaji Mkuu mwingine mstaafu David Maraga afanikiwa kupenya Kisutu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Naona wameamua kumpa promo bila wao kujua,haya maisha nyie.
 
Ifike mahali uone aibu na uache kutudanganya uliwahi kuona Kenya cheo cha Chief Justice kinatolewa kama teuzi za mwenyekiti wa CCM?

Hivi huna habari Kenya cheo cha Jaji mkuu hutangazwa na mawakili wanaokidhi vigezo hutuma maombi.

Raundi inayofuata kuna kamati ya maadili ya mahakama huwafanyia mchujo [vetting] ndio huidhinishwa na mamlaka iitwayo Judicial Service Commission ambayo ndio husimamia mchakato huu.

Kwa Tanzania hayo yote umewahi kusikia wapi tangazo la kuomba kuwa jaji mkuu ?

Si mwenyekiti wa CCM akishaletewa jina anadondosha saini yake na imetoka hivyo.

Willy Mutunga kasoma hapo UDSM kwa taarifa yako anaijua Tanzania vizuri tu na anashangaa miaka ile wamemkimbia dikteta Moi Tanzania ilikuwa sehemu salama kwao ila sasa anashangaa Tanzania ya 2025 inaishi maisha waliyoishi kipindi cha Moi 1980's .

Hiyo ilikua ni safari ya kibinafsi sio ya kikazi na shirikisho la Afrika mashariki linatoa freedom of movement hivyo wao wamesafiri kibinafsi kuja tufuatilia kesi hawajalipiwa nauli na LSK na sheria inawaruhusu wapewe visa on arrival sasa nyie mmewauzia na sababu hamtoi nani wa kutiliwa shaka.

Kwamba Willy Mutunga amekuja kumpindua Samia?

Nakuwekea hapa na tangazo la maombi ya kuomba kuteuliwa kuja jaji mkuu wa Kenya usitudanganye eti wanapeana tu.

Sasa Tanzania uliwahi kuona tangazo kama hili?
View attachment 3338882
Umemvua nguo huyo ndugu chawa, maana anajiandikia tu bila kuwa na maarifa ya kile anachokiandika.
 
Baada ya Jaji Mkuu Mstaafu wa Kenya Willy Mutunga kushikiliwa Uwanja wa Ndege Dar majira ya saa 9 alfajiri alipowasili nchini kufuatilia kesi ya Tundu Lissu, Jaji Mkuu mwingine mstaafu wa nchi hiyo David Maraga, amefanikiwa kutinga Kisutu.View attachment 3338717
Pia soma Pre GE2025 - DSM - Kesi ya Lissu: Jaji Mkuu Mstaafu wa Kenya Willy Mutunga ashikiliwa uwanja wa Nyerere. Polisi waonekana Kisutu
Huyo hakutinga kinyemela. Alifuata protocol zote zakuomba kuja kujifunza kwetu namna tunavyodumisha amani na kuzingatia utawala wa sheria. Yeye si mwanaharakati kama huyo Karua na wenzake. Hivyo yeye alirusiwa kuja kwetu kujifunza. Yeye ni rafiki yetu tangia akiwa Chief Justice huko Kenya alipompa ushindi rafiki yetu Raila Odinga
 
Mimi nashangaa kijana mwenzangu mwenye ufahamu na hofu ya Mungu anaona kinachofanywa na ccm ni sahihi
Jamani tuache uchawa
Hebu fikiria walitaka kumuua lissu na. Kabla ya kupewa haki yake wanataka tena kumnyonga
 
Nawaagiza idara ya uhamiaji iangalie uhalali wake wa kuwepo nchini ikiwa karuka kipengele hata kimoja akamatwe mara moja na afungiwe mahabusu moja na Lissu
 
Naweza kukubaliana na baadhi ya hoja żako. Lakini kusema Mh Lisu anapata umaarufu overnight, ni kiashiria kuwa humfahamu vizuri wala hujui historia yake. Vinginevyo tupate tafsiri ya neno overnight
Uko sahihi. Lissu amekuwa mpambanaji toka mwanzo. Nilichomaanisha kwa aarufu wa overnight ni:
1. Ingawa toka mwanzo alikuwa mpambanaji hakuwahi kupata attention hii anayopata sasa ( jaribu kukumbuka enzi za Kikwete)...na hakuwahi kupaishwa hivi siku zile.
2. No reform no election ilikuwa confined ndani ya nchi(labda na mabalozi wa nchi zingine km ilivyosemekana) Lakini kwa kumweka ndani na kujaribu kuzuia asipate haki zake za kisheria tunamtangaza zaidi kuliko alivyokuwa anajitangaza alipokuwa huru uraiani. No reform no election inatangazwa nje ya mipaka ya Tanzania zaidi sasa na kazi hii inafanywa zaidi sio na Lissu au chadema bali na kitendo Cha kumshikilia.
3. Tuwe wakweli. Lissu ni mpambanaji wa enzi na enzi Lakini amepata umaarufu zaidi baada ya shambulio lile la Dodoma na anayofanyiwa sasa ndio kabisa yanamfanya aonekane shujaa. Sijui wanaomshikikia wanawaza nini na end game yao ni nini. Ni AJABU kuwa Kuna watu wanawaza kuwa mbinu hizi zitafanikiwa kumnyamazisha Lissu milele. Well, wanaweza kumnyamazisha Lissu huyu (Tundu Lissu) Lakini punde watajitokeza Lissu wengine tena imara zaidi kuliko huyu wa sasa.
 
mhalifu yeyote lazima ashikiliwe bila kujali historia yake ya huko nyuma. Wanaompa kiburi watamzika muda si mrefu.
 
Mnaonekana hamjui kitu chochote kile kuhusiana na masuala haya ya Uhamiaji wa Kimataifa, unapaswa uelewe tofaufi iliyopo Kati ya: - Visa Revocation and Denied Entry. Hivi ni vitu viwili tofaufi kabisa, wala siyo kitu kimoja.
Toa darasa tafadhari na mfano ukiwa hiyo post ya US na mwingine ukiwa wa TZ, Angola na Uganda
 
Hawa watu sijui wanawaza nini. Wameamua kumpanTundu Lissu umaarufu over night!!! Sasa kesi hii inafahamika nje ya mipaka yetu. Sasa Lissu anazidi kujulikana said na no election no reform inavuka mipaka ya taifa letu. Kilikuwa na sababu ya yote haya? Kilikuwa na sababu gani ya kumkamata na kumpaisha Lissu kwa kiwango hiki? Kuna sababu Gani ya kuendelea kumshukilia?
Ni kweli kumuachia kwa kuifiluta kesi hii itawachora mno waliomkamata Lakini kuendelea kumshukilia (ambako lazima TU watamuachilia baadaye) ni kuendelea kuharibi zaidi kitaifa na kimataifa. Lissu aachiliwe TU aendelee na siasa sake na nreforms zifanyike, uchaguzi uwe huru na aliyepangiwa na Mungu kushinda ashinde kwa haki. Km Lissu alipangiwa kuwa rais wa nchi hii hakuna wa kuweza kuzuia hilo. Km hakupangiwa hawezi Kuja kuwa rais wetu. Tuache haya tunayofanya sasa kwa sbb yanaharibu zaidi kuliko kujenga
Neno la kuponya
 
Back
Top Bottom