Baada ya Januari 20 kupita, TCRA yasema itakuwa inazima laini za simu zisizosajiliwa kwa alama za vidole kwa awamu

Tangu lini utawala huu ukafuata sheria ndg?
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuwa mvumilivu serikali yetu sikivu haiongozwi na malaika
 
Toka lini walitimiza wanallosema?
Kwanza bado sheria haijabadilishwa kusema ni kitambulisho cha uraia..

Ni ubabe na janja janja ya awamu hii. Jeuri ya kuzima simu hawana.. Watashitakiwa na kulipa fidia kubwa sana.
 
Nimepata hoja hapa... watanikoma!
Sent using Jamii Forums mobile app
 
TCRA ni regulator. TCRA anazima kwa kutoa amri kwa service provider na service provider hana ubavu wa kukataa amri ya TCRA. Inawezekana internally service provider hajapewa hiyo amri bado. Ni busara tu imetumika kutofunga sababu ya matatizo ya masuala ya namba. Percentage kubwa hawajasajili line.
 
Lain za simu zinazosemwa ni takribani milion 48 hizo ni laini za simu sio wamiliki wa hizo laini.
uichukulia kwa uchache wastani kila mtu mmoja ana lain 2 wapo wenye lain 3 au 4..sasa hiyo million 48 ukigawa kwa 2 unapata wamilki milion 24 sio kwamba katika watanzania milion 50 wote wanamili lain za simu
Hesabu zingine ni kanyaboya tu.
Tutofautishe wingi wa lain za simu na wamiliki wa lain za simu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Line haziwezi kufungwa sababu vitambulisho vinavyotambulika kisheria vya kisajilia line ni 4 navyo ni 1. National ID 2. Zanzibar Residents ID 3. Voters ID na 4. Pasaport mtandao utakao fungia line yako unaweza kuushitaki mahakamani na ukakulipa fidia za aina yoyote kutokana na usumbufu waliokuletea wakati wanazima line
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…