Baada ya Januari 20 kupita, TCRA yasema itakuwa inazima laini za simu zisizosajiliwa kwa alama za vidole kwa awamu

Baada ya Januari 20 kupita, TCRA yasema itakuwa inazima laini za simu zisizosajiliwa kwa alama za vidole kwa awamu

Habarini ndugu zangu wa Jf , naomba kujua nikweli ambao hawajajisajiri kwa alama za vidole ,laini zao zimefungwa au ilikuwa siasa tu kama tulivyozoea miaka yote matamko ? Naomba kujua maana naona shughuli zinaendelea kama kawaida au muda umeongezwa tena?
Kumetokea ugomvi kati ya NIDA na TCRA NIDA wanalalamika kuwa kwanini TCRA wanasajili simu kwa vitambulisho vyao (NIDA) ?
Eti kuwa TCRA wanawagombanisha na wananchi kwa kuwasingizia NIDA watafunga laini za simu.NIDA wamesema hawahusiki na mambo ya kuzima wala kuwasha simu.TCRA kama wanaona kutengeneza vitambulisho ni kazi rahisi kwanini wasitengeneze vya kwao kwa ajili ya kusajilia simu?
 
Kuna watu wameandika mambo mengi sana kwanini TCRA hawaja zima line za simu mara moja.

Wengine wamekuja na mawazo kwamba TCRA hawana technologia ya kuzima simu.

Wengine eti zoezi la kuzima limezuiliwa kiana.

Ukweli ndio huu.

1. Ni kweli TCRA wanazima simu. Hawana utani.

2. Wanao zima laini za simu sio TCRA , bali ni makampuni ya simu ,a mkononi kwa meelekezo ya TCRA.

3. Kuzima kwa awamu ni kutikana na kwamba NIDA hawana uwezo wa kuwapa vitambulisho watu wote watakao fungiwa laini za simu kwa simu moja kama watu wote wakiamua kwenda nida kudai namba zao.

4. Kuondoa taharuki katika jamii.

5. Kupunguza tension kati ya serikali na wenye simu.

6. Kuwapa nafasi wananchi kutafuta vitambulisho na kusajili laini zao.

Hivyo swala la kuzima kwa awamu limepangwa na lipo kimkakati.

Nawasilisha.

Tabutupu

Nyaishozi, Kagera.

Sent using Jamii Forums mobile app
Tunamlaumu tu ila sometimes Trump hakukosea. Alikua na point.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Halotel hawajanifungia line yangu. Sijui kwa nini wakati sikujindikisha?
 
Kumetokea ugomvi kati ya NIDA na TCRA NIDA wanalalamika kuwa kwanini TCRA wanasajili simu kwa vitambulisho vyao (NIDA) ?
Eti kuwa TCRA wanawagombanisha na wananchi kwa kuwasingizia NIDA watafunga laini za simu.NIDA wamesema hawahusiki na mambo ya kuzima wala kuwasha simu.TCRA kama wanaona kutengeneza vitambulisho ni kazi rahisi kwanini wasitengeneze vya kwao kwa ajili ya kusajilia simu?
Mkuu ya kweli haya?
 
Back
Top Bottom