Baada ya Januari 20 kupita, TCRA yasema itakuwa inazima laini za simu zisizosajiliwa kwa alama za vidole kwa awamu

Baada ya Januari 20 kupita, TCRA yasema itakuwa inazima laini za simu zisizosajiliwa kwa alama za vidole kwa awamu

Tangu lini utawala huu ukafuata sheria ndg?
Kuja jambo ambalo serikali imekosea.

Sheria ya mawasiliano ya mwaka 1997 hailazimishi mmiliki wa laini ya simu kusajili kwa kitambulisho cha taifa tuu bali inaruhusu kutukia vitambulisho vitano.

Hivyo serikali ilitakiwa kwanza kuhuisha sheria kabla ya kuja na katazo hili.

Ukiwauliza wametumia sheria ipi hawana jibu?



Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shukran ya usumbufu usio na sababu? Hizo line tulisajili kwa kutumia vitambulisho vya kura vyenye finger print. Na utaratibu/sheria inatambua kitambulisho cha kura, driving licence nk kama vitambulisho halali kwa usajili wa line za simu, hii ya kulazimisha kitambulisho cha NIDA tu inatoka wapi? Kibaya zaidi tatizo liko huko huko NIDA. Mimi nilijiandikisha NIDA mwaka jana mwezi wa tatu, mpaka leo sina nakala ya kitambulisho zaidi ya namba, sasa hapo shukran ya nini?
Kuwa mvumilivu serikali yetu sikivu haiongozwi na malaika
 
Habarini ndugu zangu wa JF, naomba kujua ni kweli ambao hawajajisajili kwa alama za vidole laini zao zimefungwa au ilikuwa siasa tu kama tulivyozoea miaka yote matamko?

Naomba kujua maana naona shughuli zinaendelea kama kawaida au muda umeongezwa tena?
Toka lini walitimiza wanallosema?
Kwanza bado sheria haijabadilishwa kusema ni kitambulisho cha uraia..

Ni ubabe na janja janja ya awamu hii. Jeuri ya kuzima simu hawana.. Watashitakiwa na kulipa fidia kubwa sana.
 
.
Screenshot_20200121-180927.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimepata hoja hapa... watanikoma!
Kuja jambo ambalo serikali imekosea.

Sheria ya mawasiliano ya mwaka 1997 hailazimishi mmiliki wa laini ya simu kusajili kwa kitambulisho cha taifa tuu bali inaruhusu kutukia vitambulisho vitano.

Hivyo serikali ilitakiwa kwanza kuhuisha sheria kabla ya kuja na katazo hili.

Ukiwauliza wametumia sheria ipi hawana jibu?



Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TCRA ni regulator. TCRA anazima kwa kutoa amri kwa service provider na service provider hana ubavu wa kukataa amri ya TCRA. Inawezekana internally service provider hajapewa hiyo amri bado. Ni busara tu imetumika kutofunga sababu ya matatizo ya masuala ya namba. Percentage kubwa hawajasajili line.
 
Lain za simu zinazosemwa ni takribani milion 48 hizo ni laini za simu sio wamiliki wa hizo laini.
uichukulia kwa uchache wastani kila mtu mmoja ana lain 2 wapo wenye lain 3 au 4..sasa hiyo million 48 ukigawa kwa 2 unapata wamilki milion 24 sio kwamba katika watanzania milion 50 wote wanamili lain za simu
Hesabu zingine ni kanyaboya tu.
Tutofautishe wingi wa lain za simu na wamiliki wa lain za simu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Line haziwezi kufungwa sababu vitambulisho vinavyotambulika kisheria vya kisajilia line ni 4 navyo ni 1. National ID 2. Zanzibar Residents ID 3. Voters ID na 4. Pasaport mtandao utakao fungia line yako unaweza kuushitaki mahakamani na ukakulipa fidia za aina yoyote kutokana na usumbufu waliokuletea wakati wanazima line
 
Back
Top Bottom