tpaul
Platinum Member
- Feb 3, 2008
- 27,843
- 29,350
Serikali ya CCM haipoi na haijawahi kupoa. Ndivyo unavyoweza kusema. Baada ya serikali kulifuta kanisa la Gwajima kwa kuhoji kuhusu utekaji na mauaji yanayoendelea hapa nchini kila kukicha, kanisa la KKKT nalo limeanza kuleta chokochoko kwa kutetea usawa, haki na uwazi kwenye uchaguzi, kutungwa kwa katiba mpya na kuundwa kwa tume huru ya uchaguzi. Hebu msikilize wewe mwenye askofu huyu wa KKKT jinsi anvyotetea jambo ambalo serikali hailitaki mkuu.
MAONI YANGU
Kwa kuwa serikali inapinga vikali mtu au taasisi yoyote inayoikosoa, sioni ni namna gani kanisa la KKKT litanusurika kufutwa kwa kufanya kitu kilekile ambaco Gwajima alifanya na kupelekea kanisa lake kufutwa. Nina uhakika na imani kuwa serikali yetu tukufu ni sikivu na kwamba italifuta kanisa la KKKT haraka iwezekanavyo, hata kama mwenye kanisa (Askofu Malasusa) ni kada maarufu wa CCM.
Endapo kanisa hili litanusurika kufutwa, basi huyu askofu aliyetetea haki akiwa madhabahuni, huku akifahamu fika kuwa utetezi wa aina hiyo ni masuala ya kisiasa, basi tutarajie askofu huyu kupotezwa huku kanisa likipewa onyo na karipio kali. Stay tunded and informed.