Mapand
Senior Member
- Nov 9, 2022
- 134
- 202
Habari wakuu? Natumaini wengi wetu tumeona taarifa juu ya serikali ya Kenya kupeleka askari wake kwaajili ya kupambana na waasi wa M23 pamoja na vikundi vingine pale mashariki mwa jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo ambapo askari hao wamepelekwa kama askari wa jumuiya ya Afrika mashariki ukiachana na wale walio chini ya Umoja wa mataifa.
Ifahamike kwamba askari wa kenya waliopelekwa leo licha ya kwamba ni makubaliano baina ya nchi za EAC lakini muhimu zaidi wamepelekwa kwa makubaliano kati ya Tshekedi na Uhuru kabla hajastaafu.
sasa swali langu ni je,Rwanda na Uganda zitakubali kutoa askari wake zikihitajika na jumuiya ya Afrika ya mashariki kusaidia kupambana na waasi waliopo DRC?
Nimeuliza swali hili kwasababu DRC imekuwa ikiishutum Rwanda kufadhili vikundi vya waasi vilivyopo mashariki mwa DRC.Pia kwa mbaali ni kama Drc wanataka kuijumuisha Uganda kama nchi inayounga mkono shutuma inazodaiwa Rwanda anazifanya dhidi yake(DRC).
Na mwisho,kama Rwanda na Uganda hawatapeleka askari wao kule DRC je,jumuiya ya kimataifa na Dunia kwa ujumla ijue kwamba nchi hizi mbili zinashirikiana kuihujum DRC?