Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Kesi ya uhaini dhidi ya Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu imeahirishwa hadi kesho Septemba 9, 2025 baada ya kuomba muda zaidi kupitia nyaraka za committal proceedings.
Lissu aliwasilisha hoja kuwa nyaraka alizopewa akiwa gerezani zinatofautiana na zile alizokabidhiwa leo na Mahakama Kuu, akidai tofauti hizo zinaashiria “doctoring” na huenda ni kosa la jinai.
Kutokana na uzito wa madai hayo, aliomba muda wa usiku mzima kuzisoma nyaraka hizo kwa kina na kujiandaa na hoja zake. Ombi hilo limekubaliwa na Mahakama Kuu chini ya Jaji Dunstan Nduguru.
Kesi itaendelea kesho, ambapo Lissu anatarajiwa kuendeleza pingamizi lake kuhusu mamlaka (jurisdiction) ya Mahakama Kuu.