GE2025 Baada ya Kesi ya Lissu kuahirishwa hadi Septemba 9, 2025, raia wameanza kuimba 'Rais!…Rais!…. Rais!'

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Maneno ya Rais Rais kuimbwa sio mageni maskioni mwa watu Rais ni Mama Samia hizo nyingine ni blaa blaaa nachoomba kama Mtanzania Lissu awe huru aendelee na majukumu yake
Unakataa ukweli, au! Unafikiri Lissu ni Rais wa viti maalum, au figure head wa kundi haram la wahuni!
 
R
Kesi ya uhaini dhidi ya Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu imeahirishwa hadi kesho Septemba 9, 2025 baada ya kuomba muda zaidi kupitia nyaraka za committal proceedings.

Lissu aliwasilisha hoja kuwa nyaraka alizopewa akiwa gerezani zinatofautiana na zile alizokabidhiwa leo na Mahakama Kuu, akidai tofauti hizo zinaashiria “doctoring” na huenda ni kosa la jinai.

Kutokana na uzito wa madai hayo, aliomba muda wa usiku mzima kuzisoma nyaraka hizo kwa kina na kujiandaa na hoja zake. Ombi hilo limekubaliwa na Mahakama Kuu chini ya Jaji Dunstan Nduguru.

Kesi itaendelea kesho, ambapo Lissu anatarajiwa kuendeleza pingamizi lake kuhusu mamlaka (jurisdiction) ya Mahakama Kuu.

Labda rais wa jela

USSR
 
Maneno ya Rais Rais kuimbwa sio mageni maskioni mwa watu Rais ni Mama Samia hizo nyingine ni blaa blaaa nachoomba kama Mtanzania Lissu awe huru aendelee na majukumu yake
Huo urais Samia aliununua duka gani mkuu 'boaz'. Kwenye duka hilo ni yeye pekee mwenye uwezo wa kuununua u-rais?
 
Tanganyika inamuhitaji Lissu zaidi kwa sasa kuliko yeye anavyoihitaji.

Tutapata Tanganyika bora pamoja na uboreshaji wa muungano wetu na Wazanzibari.
Samahani; lakini naona unayo matarajio hewa.
Haiwezekani pakawepo Tanganyika, halafu muungano na Zanzibar uendelee kuwepo.

Siku Tanganyika ikirudi kwenye uhai wake (jambo ambalo wengi tunalisubiri), hapo ndipo Zanzibar itaanza rasmi kujiondoa ndani ya muungano.
 
Lissu aliwasilisha hoja kuwa nyaraka alizopewa akiwa gerezani zinatofautiana na zile alizokabidhiwa leo na Mahakama Kuu, akidai tofauti hizo zinaashiria “doctoring” na huenda ni kosa la jinai.
Kuhusu Lissu kesi hii ilitakiwa iishe ndani ya wiki ile ile. Ila kwa kuwa wameamua kutamba nayo Hata miaka 10 sawa tu at the end He is the Victor.
 
Maneno ya Rais Rais kuimbwa sio mageni maskioni mwa watu Rais ni Mama Samia hizo nyingine ni blaa blaaa nachoomba kama Mtanzania Lissu awe huru aendelee na majukumu yake
Sahihi kabisa,lakini wanaoimba rais wasitekwe ama kudhuriwa kwa namna yoyote.
 
Rais wa Tanzania Tundu Lissu Mungu akulinde wanakuogopa ndio maana wanakufunga ila watashindwa tu maana Mungu wetu ni mkuu kuliko wote

Amina.

Nami naongezea:

Ee Mungu wetu mkuu, wewe wajua namna watawala wa nchi hii wanavyodhulumu haki za wanadamu wenzao, wakiamini wana mamlaka yasiyo na ukomo. Baba tunaomba mkono wako wenye nguvu ukawanyong'onyeshe, ukawashushe mpaka chini kabisa, ili wajue kuwa juu ya chochote upo wewe Mungu wetu mwenye mamlaka na uweza usio na mipaka.

Mungu wetu wa huruma, kwaajili ya Tundu Lisu, tunaomba kama ulivyomlinda dhidi ya risasi zaidi ya 30 zilizoelekezwa kwake, ukamwokoe na kumjalia ushindi mkuu dhidi ya hawa wadhulumaji wa haki zake. Mungu wetu tunaomba, kwa kila uovu waliomtendea, kwa wakati ulio sahihi ukawarudie wenyewe na izazi vyai, kwa mara 3 zaidi. Bwana mapenzi yako yatimizwe.
 
Back
Top Bottom